Baada ya Mwananyamala, mengine yaibuka..

Hatuwezi kukimbilia kuwa ana matatizo ya kiafya (kichaa) hadi jopo la Madaktari wa magonjwa ya akili watakapothibitisha.

Kwa vile kasema mwenyewe kuwa aliwahi kuuwa. Polisi inatakiwa kumuhifadhi mahala kwa usalama wake sasa, kisha kuchukuwa maelezo yake kwa kina na kuyachunguza. Ikithibitisha kuwa ana kesi ya kujibu iihusuyo mauaji na kujihusisha na imani za kichawi asogezwe Mahakamani mara moja kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.

Kwamba alitumwa kuuwa akiwa Msukule na Waziri, hilo la (UCHAWI) ni gumu sana kulithibitisha (beyond reasonable doubt) mahakamani. Hata hivyo maelezo hayo nayo yatafanyiwa kazi kwa kina akiulizwa kuonyesha jinsi alivyokuwa anakutana na huyo Waziri na kupewa maelezo na faida aliyokuwa anaipata huyo Waziri katika kuuwa au hata uthibitisho wowote kuwa huyo Waziri anahusika na hayo Mauaji.

Nasikitika kuwa ikishindikana kuoneka kuhusika kwa Waziri, mtajwa hapa, atakabiliwa na kesi nyingine ya kujibu ya slander per se ambayo itaonekana kuwa anakusudia kumchafua Mh. Waziri kwa sababu anazozifahamu yeye.
 
Ili kuwapa nafasi wenye imani mbadala za misukule n.k ni bora kukaanzishwa jukwaa la imani za kichawi and the like
 
Siwapendi hawa watu wanaotoaga shuhuda za kujitungia!
Mungu anawaona lakini.
 
Hivi intelijensia za polisi ziko wapi, huyo inabidi akamatwe kama kweli kaua na amekiri mwenyewe!!!
 
Hivi hii habari kweli inastahili kukaa kwenye jukwaa la jamii intelligence?
 
mambo mengine yamekaa kimaslahi zaidi sina imani sana na waanzilishi wa makanisa na ushuhuda wa waumini wao, vitu vingine vinahitaji ushahidi na sio kuongea tu na kuwachanganya watu, huyo dada amtaje waziri huyo na aeleze waziwazi ni jinsi gani alikua msukule na namna alivyotumika kuuwa watu na sio kutuletea usanii hapa.
 
Ha ha haaaaaaaaaaa ........... Watanzania wanachekesha kweli - nyie mnamshangaa huyo dada na ushuhuda wake na kusema ni mwongo ...................sasa mkiambiwa ukweli kuwa .......................watanzania tumechukuliwa msukule na ccm kupitia ule moshi na moto wa mwenge unaozungushwa bila sababu mtakataa???? Ndio maana tumeonewa weeeeeeeee tumeibiwa weeeee hatuna lolote tunalofanya ............tunabakia kuandika/ku-comment

hivi inaingia akilini kusikia el amechaguliwa bila kupingwa wakati alihusishwa na richmond???? Kama watanzania sio misukule ni nini????????????????????? Great thinkers semeni ukweli!!!!!
 
oooooooooo Jesus!! raboshandaraba sikaya, horiiiiiiiiiiyaaaaaaa mesiyaa!! oooohhhhhhhh!!
 
Kuna mwanadada mmoja alikuwa anatoa ushuhuda Radio Safina, mh kasema makubwa.

kasema kuwa alikuwa amechukuliwa msukule na waziri mmoja na kazi yake usiku ilikuwa kuwanga, kwenda kuzima, kuua na kunywa damu za watu.

Siku moja akiwa katika mizunguko yake, akapita nyumba moja palikuwa panafanyika maombi, ndo akachanganyikiwa akajistukia anakimbia uchi, ndo watu wakasema mchawi mchawi wakampeka kuombewa. Baada ya hapo akakubali kuokoka na kueleza A to Z. Amesema ameua wajawazito, ameuwa hata wale watoto waliofiwa kwenye kumbi za Disco Dar.

Alikuwa anakaa kwenye Jumba la Waziri mmoja Dar. huyo dada anaendaga kwenyekumbi za disco, anakuwa mzuri na wanaume wanampapatikia. Mwanaume akimchukua kwenda kulala nae, huyo mwanaume anapelekwa kuzimu

Nawaambieni kuwa Mungu yupo, na Anaweza kufanya maajabu. Wanadamu tuache dhambi na kusali.

Binti ana psychological problems. Anahitaji therapy na councelling, sio maombi.

Amandla.......
 
Hatuwezi kukimbilia kuwa ana matatizo ya kiafya (kichaa) hadi jopo la Madaktari wa magonjwa ya akili watakapothibitisha.

Kwa vile kasema mwenyewe kuwa aliwahi kuuwa. Polisi inatakiwa kumuhifadhi mahala kwa usalama wake sasa, kisha kuchukuwa maelezo yake kwa kina na kuyachunguza. Ikithibitisha kuwa ana kesi ya kujibu iihusuyo mauaji na kujihusisha na imani za kichawi asogezwe Mahakamani mara moja kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.

Kwamba alitumwa kuuwa akiwa Msukule na Waziri, hilo la (UCHAWI) ni gumu sana kulithibitisha (beyond reasonable doubt) mahakamani. Hata hivyo maelezo hayo nayo yatafanyiwa kazi kwa kina akiulizwa kuonyesha jinsi alivyokuwa anakutana na huyo Waziri na kupewa maelezo na faida aliyokuwa anaipata huyo Waziri katika kuuwa au hata uthibitisho wowote kuwa huyo Waziri anahusika na hayo Mauaji.

Nasikitika kuwa ikishindikana kuoneka kuhusika kwa Waziri, mtajwa hapa, atakabiliwa na kesi nyingine ya kujibu ya slander per se ambayo itaonekana kuwa anakusudia kumchafua Mh. Waziri kwa sababu anazozifahamu yeye.
Mkuu polisi hawawezi kuchunguza mambo ya kishirikina!!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom