Baada ya mume wangu kuninyima unyumba kwa miez 8,Nimegundua anamwanamke kazaa naye

nyumba kubwa nakukabidhi huyu dada najua kwako atakuwa mikono salama kabisa kumtoa hapo alipo kihisia,please!
 
Last edited by a moderator:
The Boss rafiki yangu i beg to differ with yu!huyu dada anazidi kujiumiza kwenye hii ndoa last time nilimwambia kuna wakati tunajitoa mno sadaka kwenye ndoa amabzo wakti mwingine wala they don worth it.\


nakubaliana na wewe
na mimi last time nilimwambia pia atazame life yake
so sisemi asimuache for now
ninachosema atazame namna ya kumsaidia baada ya kujiweka pembeni
kwanza ajitoe ili apate nafuu
pili atazame namna ya kumsaidia mwenzie...

usisahau na yeye keshasema anamuonea huruma mwenzie
so kwenye huruma,kuna upendo still....
na upendo ni kumsaidia mtu sio?
 
But huyu mume ni kama 'kalogwa' vile
kumuacha tu badala ya kumsaidia?
si mke ni wa shida na raha?



la hasha The Boss, mume hajarogwa bali:-
1. Mume hana maamuzi ya maisha yake, either hajakomaa kiakili, or ni mama's boy, au ni aina ya mume asojua jukumu lake, hajui ndoa ni yeye na mkewe ameruhusu familia iwe na maamuzi juu ya ndoa

2. Mume alioa ili apate mtu wa kutunza wazee wake? Baada ya mke kugoma amegundua hana matumizi ya mke huyu

3. Familia ya mume, inawakilisha familia nyingi za kiafrica, wanadhani ukoo mzima umeoa, wanataka kufanya maamuzi kwenye nyumba isiyowahusu, na kuyokana na mume kuwa 'dhaifu ' kimaamuzi ndo maana imeyumba

4. Mume hana mapenzi tena na mke, na ukizingatiwa ni bendera fuata upepo, kaanza mapenzi hukooooooo nje, yupo happy na anaona mke anamkera, huko nje anapata kila kitu na ukizingatia hana hisia na mke unategemea nini?

Sasa basi mume keshashikwa na wajanja wa mjini.....

Too bad mke hataki kukubali ukweli, hataki kukubali kuwa mapenzi yameisha na mapenzi hayalazimishwi.....mbaya zaidi mke anaogopa kuanza upya.......au ana mayumaini ipo siku mume atajirudi, mwenzie ale gudtime yeye asubirie mume kujirudi? Akijirudi uzeeni je? Ndo atakuwa kapoteza miaka chungu nzima bila sababu? Kwa nini mtu ujifrustrate? Wanaume wameisha duniani?

Mateso mengine yakujitakia
 
Last edited by a moderator:
Dada anza mbele. Mumeo kwenda kuzaa na mwanamke wamepishana miaka 8 jua kakuchoka kupita maelezo. Hivi ni kuulize swali!!! Huyu mwanaume angekufa leo si ungebaki mjane? Sasa ungeishi je? Assume wewe ni mjane and move on!! Washirikishe ndugu zako kama huna kazi na wao wana ka uwezo kidogo wakuwezeshe uanze maisha mapya!! Mumeo atakuletea UKIMWI kama huna hadi sasa!! Achana na wanaume vicheche hana maadili kabisa.
 
nakubaliana na wewe
na mimi last time nilimwambia pia atazame life yake
so sisemi asimuache for now
ninachosema atazame namna ya kumsaidia baada ya kujiweka pembeni
kwanza ajitoe ili apate nafuu
pili atazame namna ya kumsaidia mwenzie...

usisahau na yeye keshasema anamuonea huruma mwenzie
so kwenye huruma,kuna upendo still....
na upendo ni kumsaidia mtu sio?
kwa kweli ili aweze kumsaidia ni sharti atoke hapo
yani ni lazima ajitoe kweny hiyo ndoa atafute hewa ya kimahusiano ili aweze kuja kupigania ndoa yake tena (kama bado atajiona anaiihitaji baada ya hap)
sio siri haya ni mateso dada zako wanitese,mamako anitese,wewe unitese,no dushelele mieze 8,bado nigundue una mwanamke na mtoto nje bado kuna ndoa hapo jamani!moyo huu huu ulioumbwa kwa nyama huu huu kweli!hapana!
nayapenda sana mapenzi lakini siyapi nafasi ya kunitesa kiasi hiki!
 
Lol! Shida zingine za kuendekeza aisee. Si tutauana kwa presha na ukimwi? Hivi mkeo akifanya hivi utamsamehe kwa shida na raha? Nkuki kwa nguruwe aisee. . .
Weeh lonely heart, hebu anzisha uzi utafutw kidumu humu wakati tunajadili hoja.
But huyu mume ni kama 'kalogwa' vile
kumuacha tu badala ya kumsaidia?
si mke ni wa shida na raha?
 
huwezi kujitegemea hata kidogo?
Huwezi kulea watoto 2 tu?

Anyway, sijui viatu vyako
 
mi sielewi jamani nani kasema kuolewa ni kupoteza uwezo wa kufikiri
nani kasema kuolewa ni kupoteza uwezo wa kujiamini
anayewadanganya nani kuwa kuolewa kunakwenda sawa na kushindwa kujisimami kihisia na kimwili
watu wa aina yako Lonely heart ndo mnafanya ndoa zionekane ni za mateso sana!
mwanaume anakutenda kiasi hiki
SIMAMA PIGANIA FURAHA YAKO
NYANYUKA TETEA MAISHA YAKO
PIGANA KULINDA USTAWI WA WATOTO WAKO
LINDA HADHI YAKO KAMA KIUMBE KATIKA UPEKEE WAKO
TEGEMEZA AKILI YAKO NA KUYAKABILI MAISHA
ONGEZA UKARIBU NA MUUMBA WAKO
 
Last edited by a moderator:
Sawa dada unavumilia kwa ajili ya wanao labda ukifa sa hvi kwa magonjwa ya moyo au pressure wanao watakula nyama yako,tafadhali dada angu kaanze maisha yako Mungu atakusaidia yataenda 2 vyema,usijiue watoto wako watateseka zaidi na zaidi fight to live for them by avoiding stupid stresses,nakupenda ila ungekuwa dada yangu ningekuja kukutoa huko kwa mumeo na ukirudi huko nafuta udada,give them space the world has so much to teach cruel people like these,eti huna ndugu?nije niwe dada ako wa muda?
 
nakubaliana na wewe na mimi last time nilimwambia pia atazame life yake so sisemi asimuache for now ninachosema atazame namna ya kumsaidia baada ya kujiweka pembeni kwanza ajitoe ili apate nafuu pili atazame namna ya kumsaidia mwenzie... usisahau na yeye keshasema anamuonea huruma mwenzie so kwenye huruma,kuna upendo still.... na upendo ni kumsaidia mtu sio?
nimejiweka pembeni kabisa,Sitaki anisogelee kwani sina uhakika na afya yake,Na ninaendelea kutafuta jins ya kumsaidia kwani all in all ni mzazi mwenzangu,Na pia lazma nihakikishe mali zote nilizochuma naye zinabaki mikononi mwa wanangu.
 
Roho ya kupenda haina kigugumizi.

Kaa ukijua kuwa:

1. Hakupendi wala hakutaki TENA
2. Ukoo mzima umekuchoka
3. Inaelekea wewe ndo una tatizo SI RAHISI mume kukuhama miezi 8+ ndugu wachache wangekutetea
4.Mapenzi hayana cha umri wala nini, mwenzio amekupiku. Baada ya kuzaa watoto 4 amefunzwa na dunia hivyo anajua kuhandle familia.
5. Familia ni zaidi ya mumeo na watoto wako

6. Kila kitu kina sababu; ondoka wala usigeuke nyuma
7. Mlango ukifungwa, dirisha hufunguliwa......sepa fasta huna chako uspoteze muda dudu jeusi kafungua mlango
8. Nyumba yenu imejaa nyufa. Nyufa hutokea kwa sababu!......


ILI MWANGA UPENYE.....

UPO HAPO DADA????????????????????????????????
 
nimejiweka pembeni kabisa,Sitaki anisogelee kwani sina uhakika na afya yake,Na ninaendelea kutafuta jins ya kumsaidia kwani all in all ni mzazi mwenzangu,Na pia lazma nihakikishe mali zote nilizochuma naye zinabaki mikononi mwa wanangu.


usifikirie mali kwa sasa
ukijipanga waweza chuma zako upyaaa...
 
nimejiweka pembeni kabisa,Sitaki anisogelee kwani sina uhakika na afya yake,Na ninaendelea kutafuta jins ya kumsaidia kwani all in all ni mzazi mwenzangu,Na pia lazma nihakikishe mali zote nilizochuma naye zinabaki mikononi mwa wanangu.
kwa aina ya mume uliyenyae nina hofu kuwa haya maazimio yako hayatafanikiwa!
 
Kama nilivyowah kuwaeleza manyanyaso toka kwa mama mkwe na mawifi baada ya kukataa wasinitawale,Na hatimaye mume wangu akajiunga nao na kuninyanyasa nilipokua mjamzito na kunisababishia matatizo makubwa na kunipelekea kujifungua mtoto (boy)wa miez 7...na baada ya kujifungua mume wangu akahama chumba na kuninyima unyumba, nimefanya utafiti na kugundua MUME WANGU ANA MWANAMKE ALIYEZAA NAYE MTOTO(girl 1yr) na mwanamke huyo amemzidi mume wangu miaka 8 na anajumla ya watoto 4 kila mtoto na baba yake.na taarifa za kusikitisha ni kwamba mawifi zangu wanamshawishi mume wangu afumge naye ndoa ili wanikomoe. Namuonea huruma sana mume wangu,mimi na watoto wangu.Naombeni ushauri
Please leave as soon as possible Kama human kazi nu inbox Nitakuajiri .usinyanyasike na mwanaume duh pole sana .na Kama huna pa kwenda nitakutafutia pa kuka.yaani machozi ya nanitoka duh .dada HIV uOndoke mambo ya
 
usifikirie mali kwa sasa
ukijipanga waweza chuma zako upyaaa...

sijui kwanini hili la mali huwa linatutoa sana roho wanawake ndoa inapofikia hatua hii!
wengi huwa tunasahau kuwa kwa hatua ilipofika kwa hiyo ndoa tayari huyo mwanaume ameshatunyang'anya zaidi ya mali
KUJITAMBUA!
na hakika hili ukilikosa hata uwe na mali kiasi gani huwa haziwezi kutusaidia
mali zitawafaa vipi watoto ambao wanakua katika familia iliyojaa udhalimu?
mali zitawafaa vipi watoto waliolelewa na mama aliye na low self esteem?
mali zitawafaa nini watoto waliozungukwa na ndugu wa baba wanaomuongelea na kumtusi mama yao?
 
Back
Top Bottom