Baada ya miaka 35 kundi la ABBA linarudi tena dah!

don88

Member
Jan 22, 2013
53
84
KWa wale vijana wenzangu wa zamani wanaweza kushangaa kidogo kama kweli kundi hili lililowahi kutamba sana miaka 35 iliyopita na vibao kibao kama vile Chiquitita, Money Money na nyingine kibao.

Habari ikufikie kuwa kundi hili lenye vichwa hatari kama vile Bjorn Ulvaeus, Benny Andersson, Agnetha Faltskog na Anni-Frid Lyngstad limeamua kuungana tena na kurudisha kiu kwa siye vijana wa zamani ambapo tayari limeingia studio na kutengeneza nyimbo mbili za kuanzia moja wapo ni I Still Have Faith In You.

Karibuni tena ABBA, tulizoea kusikia nyimbo zenu sikukuu za Krismasi tu!

ABBA return after 35 years with two new songs
 
Attachments

  • Collected-CD2-cover.jpg
    Collected-CD2-cover.jpg
    89.5 KB · Views: 60
  • f8e476ae-4a41-11e8-85b3-af25d27017e0_1280x720_052015.jpg
    f8e476ae-4a41-11e8-85b3-af25d27017e0_1280x720_052015.jpg
    64 KB · Views: 57
Nilisikia hizi habari mahali nikafurahi sana kusikia kama bado wanafikiria muziki.

Hawa nilikuwa nawafananisha sana na wale Boney M.

Ni bahati mbaya sana sidhani kama kizazi hiki wanaweza kujua utamu wa muziki halisi uliokuwa unafanywa na haya makundi.

Ila kwa Boney M wao walishapoteza member mmoja, yule wa kiume....hata wakirudi tutakosa zile flavour zao.
 
Kwa hawa wananikosha sana tena wapo wote, walikuwa na sauti flani hivi kama za kitototo
 
Alafu nilikuja kugundua baadae sana kuwa Boney M ni (waswahili) na ABBA ni Wazungu (swedish)....mwanzo nilijuaga makundi yote ni ya Wazungu.
 
KWa wale vijana wenzangu wa zamani wanaweza kushangaa kidogo kama kweli kundi hili lililowahi kutamba sana miaka 35 iliyopita na vibao kibao kama vile Chiquitita, Money Money na nyingine kibao.

Habari ikufikie kuwa kundi hili lenye vichwa hatari kama vile Bjorn Ulvaeus, Benny Andersson, Agnetha Faltskog na Anni-Frid Lyngstad limeamua kuungana tena na kurudisha kiu kwa siye vijana wa zamani ambapo tayari limeingia studio na kutengeneza nyimbo mbili za kuanzia moja wapo ni I Still Have Faith In You.

Karibuni tena ABBA, tulizoea kusikia nyimbo zenu sikukuu za Krismasi tu!

ABBA return after 35 years with two new songs
nimeipenda hii taarifa mkuu...tunawasubiri kwa hamu kubwa!!!
 
Back
Top Bottom