Baada ya Mdau wa Jamii Forums kulalamika, Serikali yaanza kuboresho ya Barabara ya Goba - Mpakani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Siku chache baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai kuwa Barabara ya Goba - Mpakani, Dar Es Salaam ni mbovu na inawagharimu watumiaji hasa wakati wa Mvua, Serikali imechukua hatua ya kuanza maboresho.

Mdau alidai kuwa barabara hiyo haichongwi mara kwa mara na ina madimbwi mengi hivyo hata gharama za usafiri zimekuwa zikipandishwa kiholela.

Leo Mei 10, 2023 watendaji wameonekana wakichonga barabara hiyo kwa lengo la kuiweka sawa.

photo_2023-05-10_12-59-29.jpg

photo_2023-05-10_12-59-29 (2).jpg

photo_2023-05-10_12-59-28.jpg



Soma >> Serikali isikie kilio cha Barabara ya Goba Mpakani, ruti zinabadilishwa, wanapandisha nauli kiholela
 
Dar pamoja na kutoa mapato mengi ila barabara nyingi ni hatari aisee.
 
Huwa nashindwa kuwaelewa hawa watendaji wa manispaa/halmashauri yaani wanamiliki Vijiko/Grader/Scania Mende/Mashimo ya vifusi lakini wanashindwa kuchonga barabara.
 
Dah afadhali
Kwenye lile daraja wakati wa mvua ni tatizo haswa
 
Back
Top Bottom