Baada ya Mazishi ya Hayati Magufuli tuambiwe ni kiasi gani cha pesa kilichotumika kwenye shughuli nzima

Naja naja

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
747
1,452
Kwa jinsi hii shughuli ya msiba inavyoendeshwa inaonyesha wazi kuna mabilioni ya fedha yanapotea kwa kutumia mgongo wa kumzika kiheshima Rais Magufuli.

Kuna wengine bila shaka wanatumia fursa hii kupiga pesa, pesa ambazo kwa namna moja au nyingine zingesaidia mambo mengi mno MF madawa hospitalini, upanuzi wa barabara, mikopo kwa wanafunzi, mishahara nk.

Mh rais Magufuli enzi za uhai wake miongoni mwa vitu ambavyo alikuwa havipendi ni matumizi yasiyo ya lazima ya pesa ndio maana alikuwa mstari wa mbele kwenye kubana matumizi.

Hivyo basi si mbaya tukajua ni kiasi gani cha pesa kilichotumika kwenye mazishi yake.
 
Hataki apewe yeye, anataka mama yake kule kijijini kwa apelekewe nazo maji ya bomba.
Wakikwambia wewe utafaidi nini? Wasipozitumia msibani unadhani utapewa wewe?
Watu wote viongozi walokufaga ushawahi kuuliza gharama walizotumia msibani? Au kisa magufuli?
Hivi ni chuki au ni nini? Kwahiyo ulitaka raisi wa nchi azikwe kienyeji enyeji? Ishiiiiiiiy.
 
Kwenye misiba mitaani ni kiasi gani cha pesa huwa kinatumika? Kusema kwamba hela zingetumika kwenye mashule au hospitali ni sawa na Yesu alivyowajibu waliokuwa wakihoji mama aliyemuosha miguu na kumpaka manukato ya gharama. Kuna waliosema mafuta hayo yangeweza kuuzwa na fedha zinazopatikana zikapewa maskini.

Yesu alijua kutaja maskini ni kisingizio tu na si kwamba kweli wanawafikiria hao maskini. Akawaambia maskini mnao kila leo.

Sikatai kwamba kuna 'wajanja' ambao wanaweza kuwa wanautumia msiba kujinufaisha wenyewe. Hoja ni kwamba dhamira ya mpangilio wa maombolezo ni ipi? Hao wanaojinufaisha wakibainika mkondo wa sheria uingilie kati.

Hatuwezi kuacha kufanya mema tunayoyafikiria kwa kuogopa kutakuwepo wapotoshaji wa kujinufaisha wenyewe.
 
Back
Top Bottom