Baada ya kusikia vitu kama mchanga unamwaga batini usiku wa manane nimetoka nje kuangalia ila sioni kitu, nini tatizo?

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Nipo mkoani kikazi kuna ki apartment nimelipia mimi na mwenzangu mwezi japo kazi ni ya wiki 2 tu,

tumeishi wiki moja bila tatizo ila kuanzia usiku wa juzi kulikuwa na shida, ni kama kuna ndoo iliyojazwa mchanga inamwagwa juu ya bati.

Siku ya juzi nilidhani labda ni ndege au mnyama sikuzingatia sana japo mwenzangu alikuwa anaweweseka sana kusema ni wachawi, mi wala sikujali.

Siku ya jana hali ilikuwa kawaida tu ila mwenzangu alianza kulala bila kuzima taa, nikabaki namshangaa.

Sasa na leo hali imejirudia kama ya juzi nilitoka nje kuangalia batini ila sikuona chochote, nikapotezea nikarudi kuchapa usingizi huku mwenzangu akiwa amepaniki usingizi wake umekata, ghafla tena hali ikajirudia nilitoka nje kama mshale nikiwa nimebeba kurunzi kumulika batini lakini sikuona chochote

Naombeni ushauri maana sielewi, mwenzangu ndio yupo hoi kabisa nahisi tanesco wakikata umeme atazimia.
 
ndrungu zango,

apo apartment si kuna mti apo ambao matawi yake yanakaribia kugusa bati?🐒

maana yake kukiwa na upepo hayo matawi yananesa hadi kugusa bati ndio mnaskia kama kumwagwa mchanga means ayo matawi yanakua kama yanafagia bati 🐒

kwahivyo msiogope wala kua na Imani potofu 🐒

By the way,
mchawi mwenyewe muoga kichizi ndio maana anafanya kazi zake usiku gizani🐒
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom