Baada ya kupigiwa simu jana, nina maswali 3 kwa wapinzani wa UKAWA ndani ya CHADEMA na CUF

Wadau,
Jana nilipigiwa simu na mtu ambaye ninamfahamu kidogo kama mwanachadema kwani tuliwahi kuonana mara moja tukaongea naye kwa muda mrefu maeneo ya ukonga Dsm. Jana alinipigia simu na kunipongeza kwa makala yangu JF na facebook. Baada ya pongezi nyingi kuliko kawaida akanisihi kuwa sisi wazalendo wa kweli ndani ya Chadema tukae kwa umakini na tujadili kwa undani hatima ya chadema yetu ndani ya ukawa.

Baada ya kuongea naye kwa muda mrefu kwenye simu akiwa na umakini wa hali ya juu sana na akionekana kama mtu mwenye kuipenda sana chadema kuliko viongozi wa juu wa chadema, alinisihi nikutane naye kwenye hoteli Ubungo Plaza kwa chakula cha mchana ili tujadili hatima ya Chama chetu. Nilimkatalia.

Hata hivyo, nina maswali matatu kwa wapinzani wa UKAWA ndani ya chadema na CUF.
Mosi, Ni kwa nini wanaopinga ukawa kwa nguvu ni watu wenye matatizo ndani ya vyama vyao kama Yona aliyekanwa uongozi halali wa chadema Temeke kuwa siyo mwenyekiti?? Fuatilia wapinzani wote wa ukawa JF, Utaliona hilo.

Pili, kwa nini taarifa zao au propaganda zao zinatoka zaidi kwenye magazeti yanyomilikiwa na ccm moja kwa moja au makada wa ccm ? Na kwa nini mara nyingi huwa wanaficha vyanzo vya habari zao? (Juliana shonza mwanaccm aliyeasi chadema, ndo ameleta taarifa hapa JF ya mjumbe wa Baraza kuu cuf kujiuzulu)

Tatu, gharama ya kunikaribisha kwenye chakula cha mchana ubungo Plaza kujadili mambo haya inatoka kwa nani na kwa maslahi ya nani?? Au mhusika anagaenda gani zaidi?? Mtu huyu kwa kumwangalia tu kwa macho ya kawaida, siyo mtu wa kunikaribisha chakula cha mchana ubungo Plaza. Na kwa nini ubungo Plaza, mbona mara ya kwanza tulipoonana tulikaa masaa mawili na tukaishia kunywa maji na soda tu tena kwenye mgahawa wa kawaida.
NB; Kilichonishtua zaidi ni pale nilipomshauri kuwa awasilishe hofu yake kwa viongozi wa juu lakini hakutaka hilo, badala yake aonnane na mimi ili tujadili hatima ya chadema yetu sisi wazalendo wa chadema.

Ni maswali ninayojiuliza, wahenga wanasema hakuna swali la kijinga ila kuna jibu la kijinga.

Baada ya kumsikiliza ushauri wa akili yake niliuchanganya na akili yangu, nikajiambia mwenyewe, sidanganyiki.

Nawasilisha.

ukawa imevuruga mpango wa ccm na act ,maana walipanga kudhoofisha nguvu ya chadema kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao.maana act kwa kutumiwa na ccm waliandaa mamluki wengi kutoka ccm na zitto masalia kukwamisha jitihada za watanzania kupitia chadema iliwasiiondoe ccm madarakani.kitendo cha chadema kuungana na cuf pamoja na nccr ni pigo kubwa sana kwao ina maana kama ni hujuma wavihujumu vyama vyote vitatu kitu ambacho hakiwezekani.kwa hiyo hizo kauli zote za kusema ukwa yapingwa kila kona ya nchi au wanachadema wazalendo ni matokeo ya maumivu ya kushindwa. Na bado tutasikia mengi zaidi ya haya.
 
Wadau,
Jana nilipigiwa simu na mtu ambaye ninamfahamu kidogo kama mwanachadema kwani tuliwahi kuonana mara moja tukaongea naye kwa muda mrefu maeneo ya ukonga Dsm. Jana alinipigia simu na kunipongeza kwa makala yangu JF na facebook. Baada ya pongezi nyingi kuliko kawaida akanisihi kuwa sisi wazalendo wa kweli ndani ya Chadema tukae kwa umakini na tujadili kwa undani hatima ya chadema yetu ndani ya ukawa.

Jibu ni rahisi kazi waliyopewa ya kuzamisha Upinzani iko hatarini -UMOJA NI NGUVU HAPO UPO!

Mkuu natumai taarifa ya mapandikizi/wasaliti kama hawa lazima ifike makao makuu ya Chama .
Na kama Chama hakina mfumo wa kuwachunguza viongozi na wanachama wake basi ningeshauri chama kuanzia sasa kila kona ya Nchi hii iwe na Mashushu wakufuatilia wanachama na hasa Viongozi wa Ngazi yoyote na taarifa ziwe zinafika Makao makuu.

Au makao makuu kiwe na timu ndogo kupitia idara ya Ulinzi na Usalama kufanya kazi hii ya kufuatilia Mienendo ya wanachama na hasa Viongozi.Mfumo huu utasaidia kuondokana na Viongozi wasaliti mapema zaidi kabla hawajasababisha usumbufu na maradha/migogoro ndani ya taasisi.

Bila kufanya hivyo safari ya mafanikio ya kuwakwamua watanzania kifikra na kiuamuzi na hatimaye kiuchumi itangumu na itachukua muda.

NB; Kwa kutangaza vita hiyo umekaribisha Changamotto ambayo Imani yako ya Fiti Mwiko/Sidanganyi iko kwenye Majaribu na ni vizuri ukajiandae/jipange.

Mkuu,
We have an excellent security system au usalama wa chama. La sivyo, sasa hivi tungeshasambaratika siku nyingi sana. Unakumbuka makakati wa LWAKATARE????
 
Wadau,
Jana nilipigiwa simu na mtu ambaye ninamfahamu kidogo kama mwanachadema kwani tuliwahi kuonana mara moja tukaongea naye kwa muda mrefu maeneo ya ukonga Dsm. Jana alinipigia simu na kunipongeza kwa makala yangu JF na facebook. Baada ya pongezi nyingi kuliko kawaida akanisihi kuwa sisi wazalendo wa kweli ndani ya Chadema tukae kwa umakini na tujadili kwa undani hatima ya chadema yetu ndani ya ukawa.

Baada ya kuongea naye kwa muda mrefu kwenye simu akiwa na umakini wa hali ya juu sana na akionekana kama mtu mwenye kuipenda sana chadema kuliko viongozi wa juu wa chadema, alinisihi nikutane naye kwenye hoteli Ubungo Plaza kwa chakula cha mchana ili tujadili hatima ya Chama chetu. Nilimkatalia.

Hata hivyo, nina maswali matatu kwa wapinzani wa UKAWA ndani ya chadema na CUF.
Mosi, Ni kwa nini wanaopinga ukawa kwa nguvu ni watu wenye matatizo ndani ya vyama vyao kama Yona aliyekanwa uongozi halali wa chadema Temeke kuwa siyo mwenyekiti?? Fuatilia wapinzani wote wa ukawa JF, Utaliona hilo.

Pili, kwa nini taarifa zao au propaganda zao zinatoka zaidi kwenye magazeti yanyomilikiwa na ccm moja kwa moja au makada wa ccm ? Na kwa nini mara nyingi huwa wanaficha vyanzo vya habari zao? (Juliana shonza mwanaccm aliyeasi chadema, ndo ameleta taarifa hapa JF ya mjumbe wa Baraza kuu cuf kujiuzulu)

Tatu, gharama ya kunikaribisha kwenye chakula cha mchana ubungo Plaza kujadili mambo haya inatoka kwa nani na kwa maslahi ya nani?? Au mhusika anagaenda gani zaidi?? Mtu huyu kwa kumwangalia tu kwa macho ya kawaida, siyo mtu wa kunikaribisha chakula cha mchana ubungo Plaza. Na kwa nini ubungo Plaza, mbona mara ya kwanza tulipoonana tulikaa masaa mawili na tukaishia kunywa maji na soda tu tena kwenye mgahawa wa kawaida.
NB; Kilichonishtua zaidi ni pale nilipomshauri kuwa awasilishe hofu yake kwa viongozi wa juu lakini hakutaka hilo, badala yake aonnane na mimi ili tujadili hatima ya chadema yetu sisi wazalendo wa chadema.

Ni maswali ninayojiuliza, wahenga wanasema hakuna swali la kijinga ila kuna jibu la kijinga.

Baada ya kumsikiliza ushauri wa akili yake niliuchanganya na akili yangu, nikajiambia mwenyewe, sidanganyiki.

Nawasilisha.

Mjumbe wa halmashauri kuu unaonekana unahoja tusaidie HAPA
Ni nini kanuni za msingi za makubaliano na ushirikiano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)? Ni haja ya kuwa na Serikali ya Tanganyika na ile ya Zanzibar ndani ya Muungano? Ni kutaka kuiondoa CCM madarakani? Ni kutaka kuiongoza Tanzania? Ni kupigania Serikali Tatu? Je, vyama hivi vinakubaliana kwa kiasi gani katika sera zao nyingine? Uongozi wa UKAWA na utendaji wake unaongozwa na makubaliano gani? Binafsi sikumbuki kuona viongozi hawa wakikaa chini kuwekeana saini ya makubaliano ya ushirikiano (Cooperation Accord or Memorandum of Understanding). Ni sahihi kushirikiana bila ya makubaliano ya ushirikiano yenye kuvifunga vyama vyote sawa?​

Mwisho wa ukawa ni pale posho za bunge la. Katiba zitakapokata kila mtu atabeba mzigo wake can't wait watakavuoanza kusutana na kutiana masingi itakuwa bonge la muvi stay tuned
 
Chama cha mashetani (ccm) kimepenyeza makuwadi wake wengi katika vyama vya upinzani vyenye nguvu.

Ninajua kuna diwani wa cuf pale mji kasoro bahari, ni mamluki wa ccm.

Ila UKAWA kiboko yao. Mashetani watashika tu adabu.
 
Tumeushtukia ukawa - lipumba

Hahahaha, weka source basi mbona unakimbia mapema, hizo mbinu za divide and rule zimepitwa na wakati, jadilini rasimu iliyoletwa na tume ya Warioba ili ukawa isiwepo, otherwise nyie na magazeti yenu uchwara mnajitekenya na kucheka.
 
Mjumbe wa halmashauri kuu unaonekana unahoja tusaidie HAPA
Ni nini kanuni za msingi za makubaliano na ushirikiano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)? Ni haja ya kuwa na Serikali ya Tanganyika na ile ya Zanzibar ndani ya Muungano? Ni kutaka kuiondoa CCM madarakani? Ni kutaka kuiongoza Tanzania? Ni kupigania Serikali Tatu? Je, vyama hivi vinakubaliana kwa kiasi gani katika sera zao nyingine? Uongozi wa UKAWA na utendaji wake unaongozwa na makubaliano gani? Binafsi sikumbuki kuona viongozi hawa wakikaa chini kuwekeana saini ya makubaliano ya ushirikiano (Cooperation Accord or Memorandum of Understanding). Ni sahihi kushirikiana bila ya makubaliano ya ushirikiano yenye kuvifunga vyama vyote sawa?

"KATIBA YA WANANCHI" -RASIMU YA PILI YA KATIBA YENYE MAONI YA WANANCHI.

Bado hujaelewa MOU (Cooperation Accord or Memorandum of Understanding). Makubaliano mkuu si lazima kusainiana.Thamira na kuaminiana ni nguvu kubwa ,maandishi ni maonyesho tu!
 
Dr Slaa alipotaja majina ya mafisadi wakiwepo majina ya Marais aliulizwa waandishi kama haogopi kufa. Yeye alijibu, maji ukishavulia nguo, huna budi kuyaoga. Nina uhakika kuwa kila mtu akiogopa kufa au tukiwa dhaifu mbele ya rushwa nina uhakika ccm wataiuza nchi hii kwa bei ya jumla siku moja. Nina uhakika hilo halitatokea katika kizazi changu.
wewe pia huogopi kufa??? kwanini hukwenda ubungi plaza??
 
Ni lini cuf wameacha kuwa ccm B?
ni lini nccr mageuzi wameacha kuwa tawi la CCM?
haya majina mabaya mabaya ya kuwachafua wenzenu mchana kisha jioni mnawaita marafiki haamaaanshi uroho wa madaraka wa chadema?

Mavi ya kale .... Kumbuka yaliyopita si ndwele .....
 
"KATIBA YA WANANCHI" -RASIMU YA PILI YA KATIBA YENYE MAONI YA WANANCHI.

Bado hujaelewa MOU (Cooperation Accord or Memorandum of Understanding). Makubaliano mkuu si lazima kusainiana.Thamira na kuaminiana ni nguvu kubwa ,maandishi ni maonyesho tu!
kweli kwa makubaliano ya mdomo yanatosha kwenye vitu vya msingi kama hivi tena kwenye vyama ambavyo haviaminiani na vyote vinasera tofauti.tuchukue ndivyo mbona misimamo ya vyama vyao kabla ya kuungana kuhusu muungano ilikua tofauti kunawanaotaka serekali 3 kunawanotaka zanzibar huru pamoja na muungano wa mkataba Je msimamo wa UKAWA baada ya kukubaliana kwa mdomo ni upi?
Ok hoja ya kusimamisha Mgombea mmoja wa urahisi pia ni makubaliano ya mdomo?
 
Kwa hiyo kwa fikra yako mkiandikiana ndiyo kukubaliana! Mkuu Makaratasi si kitu wala si chochote hakuna kinachoweza kushinda dhamira,Imani na matumaini ya kufikia Malengo.Kwa hiyo angalia picha kubwa ya hivi Vyama utagundua kwa nini waungane sasa!
kwa taarifa yako;

Muungano wa Mkataba = Serikali Tatu
Zanzibar Huru = Serikali Tatu .

Wadau,
Jana nilipigiwa simu na mtu ambaye ninamfahamu kidogo kama mwanachadema kwani tuliwahi kuonana mara moja tukaongea naye kwa muda mrefu maeneo ya ukonga Dsm. Jana alinipigia simu na kunipongeza kwa makala yangu JF na facebook. Baada ya pongezi nyingi kuliko kawaida akanisihi kuwa sisi wazalendo wa kweli ndani ya Chadema tukae kwa umakini na tujadili kwa undani hatima ya chadema yetu ndani ya ukawa.

Baada ya kuongea naye kwa muda mrefu kwenye simu akiwa na umakini wa hali ya juu sana na akionekana kama mtu mwenye kuipenda sana chadema kuliko viongozi wa juu wa chadema, alinisihi nikutane naye kwenye hoteli Ubungo Plaza kwa chakula cha mchana ili tujadili hatima ya Chama chetu. Nilimkatalia.

Hata hivyo, nina maswali matatu kwa wapinzani wa UKAWA ndani ya chadema na CUF.
Mosi, Ni kwa nini wanaopinga ukawa kwa nguvu ni watu wenye matatizo ndani ya vyama vyao kama Yona aliyekanwa uongozi halali wa chadema Temeke kuwa siyo mwenyekiti?? Fuatilia wapinzani wote wa ukawa JF, Utaliona hilo.

Pili, kwa nini taarifa zao au propaganda zao zinatoka zaidi kwenye magazeti yanyomilikiwa na ccm moja kwa moja au makada wa ccm ? Na kwa nini mara nyingi huwa wanaficha vyanzo vya habari zao? (Juliana shonza mwanaccm aliyeasi chadema, ndo ameleta taarifa hapa JF ya mjumbe wa Baraza kuu cuf kujiuzulu)

Tatu, gharama ya kunikaribisha kwenye chakula cha mchana ubungo Plaza kujadili mambo haya inatoka kwa nani na kwa maslahi ya nani?? Au mhusika anagaenda gani zaidi?? Mtu huyu kwa kumwangalia tu kwa macho ya kawaida, siyo mtu wa kunikaribisha chakula cha mchana ubungo Plaza. Na kwa nini ubungo Plaza, mbona mara ya kwanza tulipoonana tulikaa masaa mawili na tukaishia kunywa maji na soda tu tena kwenye mgahawa wa kawaida.
NB; Kilichonishtua zaidi ni pale nilipomshauri kuwa awasilishe hofu yake kwa viongozi wa juu lakini hakutaka hilo, badala yake aonnane na mimi ili tujadili hatima ya chadema yetu sisi wazalendo wa chadema.

Ni maswali ninayojiuliza, wahenga wanasema hakuna swali la kijinga ila kuna jibu la kijinga.

Baada ya kumsikiliza ushauri wa akili yake niliuchanganya na akili yangu, nikajiambia mwenyewe, sidanganyiki.

Nawasilisha.

kwani wewe ni nani hapa mjini mkuu?
 
Hongera kwa kulitambua hilo maana sasa hivi jamaa wanawafuata baadhi ya viongozi wa vyama
hivi kuwashawishi juu ya hilo,baada ya mbinu ya kuitumia ACT kudunda nguvu zao wamehamishia UKAWA'
 
Back
Top Bottom