Baada ya kuniumiza, amerudi anataka turudiane

Mwambie akupeleke tena dubai mkirudi tu leta uzi tena tutachangia
 
Uyo mwanaume anataka sex tu, ndo maana karudi kwako
 
Ukirudi umekwisha hizo dubai, mombasa, gongo la mboto sahau kamatia hapohapo
 
sasa kama umeshafanya maamuzi ya kuachana na Uliyenae, hili suala amerudi kwa kasi na kutaka kuiharibu furaha yako limetoka wapi?
 
Hekima na busara za mwanadamu ni kujifunza kutokana na makosa......kwa kuwa hakuna mwanadamu mkamilifu hivyo kukosea ni sehemu muhimu ya kujifunza.......ni kama mtu aliyejikwaa na kisiki katika njia hiyo hiyo moja zaidi ya mara moja huyo ni mpumbavu na mpuuzi.....

Maisha yetu ni mafupi sana...hivyo hatuna budi kuutumia muda wetu mchache uliopo kuyafurahia maisha.....uelekeze moyo wako na mwili wako kwenye furaha....inunue furaha yako kwa gharama yoyote ile....na ujitahidi kuliepuka jambo linalokunyima raha kwa gharama yoyote ile.....
 
Niliwahi leta thread hapa kuhusiana na experience yangu ya kuwa baby mama.
Ofcourse niliumia sana kwa yaliyo tokea,ila sikuwa na budi kumove on.Doctor wangu alinisaidia sana kisaikolojia,Mungu ambariki.

Sikuwahi mnyima kuja mwona mwanaye kila alipojisikia.Na still simnyimi kumwona mwanaye kwani ni damu yake.Baada ya muda kupita na counselling za kutosha,nilifanikiwa mwondoa moyoni na mawazoni mwangu.Doctor wangu alinisaidia kuyaona maisha katika mwanga mpana,hadi kupelekea kuja kumkubali mwanaume mwingine aliye kuwa ananipenda kabla hata sijapatwa na mkasa wa kuwa baby mama.Jamaa alinipenda na still ananipenda sana,na ndio niko naye sasa kimapenzi.

Anampenda sana mwanangu na wametokea kuelewana sana tumekuwa tukispend week ends pamoja kama family.Tumesafiri sehemu mbalimbali pamoja na mwanangu kama Zanzibar, Mombasa na Dubai.

Tatizo ni kama mwezi baba wa mtoto wangu ameanza kurudi kwa kasi kwangu,akitaka turudiane tuanzishe family na mwanetu.Anadai hataki mwanae alelewe na mwanaume mwingine.

Nimechunguza nikagundua yule mwanamke alokwenda mtambulisha kwao wameachana,sababu hasa sizijui.Namshangaa kurudi na kutaka kuniharibia furaha yangu niliyoipata baada ya kuumia sana.

Wanaume kuweni na msimamo,msipende haribu furaha za wanawake.Ni kweli nilimpenda sana ila aliniumiza sana,sasa kwanini anione nimerudi kwenye furaha yangu atake kuiharibu.Huyu niliye naye kwa sasa nampenda sana na sina mpango wa kuachana naye.Mwanao atabaki kuwa mwanao,live with it man.
Majuto mjukuu
Busara itumike hapo
 
Ndivyo walivyo baadhi yao wanategemea wakishakuacha kwa kiburi utakua katika msiba wa moyo siku zote.

Wanapoona hali tofauti wanajirudisha. Usilogwe ukarudi endelea ku enjoy na new hubby wako
 
dada kuchangua furaha yo moyo wako ni wewe mwenyewe...fata moyo wako kama umuhitaji mwambie mapema kwamba uhusiano uliopo ni kwa jili ya mtoto na si mengine.
 
Niliwahi leta thread hapa kuhusiana na experience yangu ya kuwa baby mama.
Ofcourse niliumia sana kwa yaliyo tokea,ila sikuwa na budi kumove on.Doctor wangu alinisaidia sana kisaikolojia,Mungu ambariki.

Sikuwahi mnyima kuja mwona mwanaye kila alipojisikia.Na still simnyimi kumwona mwanaye kwani ni damu yake.Baada ya muda kupita na counselling za kutosha,nilifanikiwa mwondoa moyoni na mawazoni mwangu.Doctor wangu alinisaidia kuyaona maisha katika mwanga mpana,hadi kupelekea kuja kumkubali mwanaume mwingine aliye kuwa ananipenda kabla hata sijapatwa na mkasa wa kuwa baby mama.Jamaa alinipenda na still ananipenda sana,na ndio niko naye sasa kimapenzi.

Anampenda sana mwanangu na wametokea kuelewana sana tumekuwa tukispend week ends pamoja kama family.Tumesafiri sehemu mbalimbali pamoja na mwanangu kama Zanzibar, Mombasa na Dubai.

Tatizo ni kama mwezi baba wa mtoto wangu ameanza kurudi kwa kasi kwangu,akitaka turudiane tuanzishe family na mwanetu.Anadai hataki mwanae alelewe na mwanaume mwingine.

Nimechunguza nikagundua yule mwanamke alokwenda mtambulisha kwao wameachana,sababu hasa sizijui.Namshangaa kurudi na kutaka kuniharibia furaha yangu niliyoipata baada ya kuumia sana.

Wanaume kuweni na msimamo,msipende haribu furaha za wanawake.Ni kweli nilimpenda sana ila aliniumiza sana,sasa kwanini anione nimerudi kwenye furaha yangu atake kuiharibu.Huyu niliye naye kwa sasa nampenda sana na sina mpango wa kuachana naye.Mwanao atabaki kuwa mwanao,live with it man.
"Hii ni Taarifa au maombi ya ushauri mkuu?"
 
last time nilikwambia huyo mwanaume atarudi na atakugonga.ukapuuza nilichosema.naona umeamua kukiri kijanja. tueleze kuwa amekugalagaza tena.kama humtaki mngemalizana hukohuko huo mrejesho hauko sawa kwakuwa umempa nafasi ya kuja kwako pamoja na ubazazi alioufanya.pia unafuatilia maisha yake!
 
Back
Top Bottom