KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,591
- 4,604
Siku Daktari wa Sheria na Spika wa bunge Mhe.Tulia aliposema CCM haitoacha dola kamwe , kwa mara ya kwanza nilishtuka lakini baada ya kujiridhisha na hotuba nzima, nakiri kusema nukuu ya kipande hicho kinatumika kupotosha.
Siku zote natumia kanuni ya Thomaso, kujiridhisha kwa kuona na baada ya hapo nafanya uamuzi na ninachagua upande ulio sahihi. Kwa kauli ya Mhe.Dkt. Tulia huo ndio upande ninaochagua kwamba CCM haitaacha dola kamwe.
Ukimsiliza Spika Tulia katikati ya mistari unaona msingi wa hoja ya Spika umesimamia kwenye utendaji, usimamizi na utekelezaji wa miradi unaofanywa na Serikali ya CCM na matokeo yake. Kimsingi dola ni Wananchi, kama Wananchi wanaona utendaji mzuri, usimamizi wa hali ya juu na utekelezaji wa miradi sidhani kama hawataichagua CCM. Spika Tulia ni mkuu wa muhimili unaousimamia serikali na lolote analoongea ni kweli tupu.
Haya ni kwa utangulizi wa mada yangu kulingana na kichwa Cha mada. Baada ya kuruhusiwa mikutano ya hadhara, nimekuwa ni msikilizaji mzuri wa hoja za upinzani kwa kuwa sasa ni muda wa siasa za hoja. Kuna baadhi ya hoja nakubaliana na wapinzani lakini kwa nyingine hususani anazotoa Tundu Lissu zinaniachia maswali zaidi.
Siku za nyuma nilikuwa na imani kuwa miaka 50-100 ijayo upinzani ukipambana na kuamiwa na watanzania wanaweza kushika dola lakini kauli ya Tundu Lissu ya ukomo wa madaraka ni anasa imenifnaya nipoteze Imani.
Ukomo wa madaraka unawekwa kwa lengo la kuimarisha demokrasia na siasa safi. CCM Cha Mapinduzi toka uongozi wa Mwalimu mpaka sasa viongozi wote wanakuzwa na kulelewa katika Imani ya ukomo wa Madaraka. Uongozi wa Mwalimu ulikuwa na ukomo na ninaamini uongozi wa Rais Samia utakuwa na ukomo pia.
Kitendo cha kiongozi mwandamizi wa chama kuona ukomo wa madaraka sio mzuri ni jambo la kushangaza sana na kitendo hicho kina lengo baya. Kwamba kesho wakipewa dola ,kwa sababu waliondoa kipengele hicho kwenye Chama bila kelele kupigwa si wataamua kukiondoa kwenye katiba ya nchi na tukatawaliwa kifalme?
Yaani Tanzania iwe na utawala na mtawala asiye na ukomo wa madaraka hapa nasimama na wote wenye mtazamo wa CCM kuongoza milele.
Tusimhukumu Dkt.Tulia kwa kauli yake kabla ya kuukunjua upinzani tujue lengo lao la kutengeneza katiba za kifalme kwenye utawala wa kidemokrasia.