Baada ya kumsikia Tundu Lissu juu ya ukomo wa madaraka ni anasa kwa CHADEMA, imani juu ya upinzani imetoweka kabisa. CCM itawale milele

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,589
4,599
Siku Daktari wa Sheria na Spika wa bunge Mhe.Tulia aliposema CCM haitoacha dola kamwe , kwa mara ya kwanza nilishtuka lakini baada ya kujiridhisha na hotuba nzima, nakiri kusema nukuu ya kipande hicho kinatumika kupotosha.

Siku zote natumia kanuni ya Thomaso, kujiridhisha kwa kuona na baada ya hapo nafanya uamuzi na ninachagua upande ulio sahihi. Kwa kauli ya Mhe.Dkt. Tulia huo ndio upande ninaochagua kwamba CCM haitaacha dola kamwe.

Ukimsiliza Spika Tulia katikati ya mistari unaona msingi wa hoja ya Spika umesimamia kwenye utendaji, usimamizi na utekelezaji wa miradi unaofanywa na Serikali ya CCM na matokeo yake. Kimsingi dola ni Wananchi, kama Wananchi wanaona utendaji mzuri, usimamizi wa hali ya juu na utekelezaji wa miradi sidhani kama hawataichagua CCM. Spika Tulia ni mkuu wa muhimili unaousimamia serikali na lolote analoongea ni kweli tupu.

Haya ni kwa utangulizi wa mada yangu kulingana na kichwa Cha mada. Baada ya kuruhusiwa mikutano ya hadhara, nimekuwa ni msikilizaji mzuri wa hoja za upinzani kwa kuwa sasa ni muda wa siasa za hoja. Kuna baadhi ya hoja nakubaliana na wapinzani lakini kwa nyingine hususani anazotoa Tundu Lissu zinaniachia maswali zaidi.

Siku za nyuma nilikuwa na imani kuwa miaka 50-100 ijayo upinzani ukipambana na kuamiwa na watanzania wanaweza kushika dola lakini kauli ya Tundu Lissu ya ukomo wa madaraka ni anasa imenifnaya nipoteze Imani.

Ukomo wa madaraka unawekwa kwa lengo la kuimarisha demokrasia na siasa safi. CCM Cha Mapinduzi toka uongozi wa Mwalimu mpaka sasa viongozi wote wanakuzwa na kulelewa katika Imani ya ukomo wa Madaraka. Uongozi wa Mwalimu ulikuwa na ukomo na ninaamini uongozi wa Rais Samia utakuwa na ukomo pia.

Kitendo cha kiongozi mwandamizi wa chama kuona ukomo wa madaraka sio mzuri ni jambo la kushangaza sana na kitendo hicho kina lengo baya. Kwamba kesho wakipewa dola ,kwa sababu waliondoa kipengele hicho kwenye Chama bila kelele kupigwa si wataamua kukiondoa kwenye katiba ya nchi na tukatawaliwa kifalme?

Yaani Tanzania iwe na utawala na mtawala asiye na ukomo wa madaraka hapa nasimama na wote wenye mtazamo wa CCM kuongoza milele.

Tusimhukumu Dkt.Tulia kwa kauli yake kabla ya kuukunjua upinzani tujue lengo lao la kutengeneza katiba za kifalme kwenye utawala wa kidemokrasia.
 
Ukomo Wa Madaraka ni 'Anasa'...

Kasema Lissu..

Ndo Maana 'Mbowe Kaking'ang'ania Kiti...! ni Mwenyekiti Wa Kudumu.
 
Najua hapa utasema rais anapomaliza vipindi viwili vya uongozi kama katiba ya nchi inavyotaka ndipo mnapobadiliha m/kiti wenu

Sasa mfano mmepoteza uchaguzi na ndani ya miaka ishirini hamkushinda, m/kiti wenu mtambalilisha vipi? Hapa ndipo ninapotaka mnionyeshe ndani ya katiba yenu ya chama kama kweli mna kikomo cha uongozi ndani ya chama lenu
 
Benjamin akiwa M/Kiti CCM,
Mbowe yupo Kama M/kiti

Kikwete akiwa M/Kiti Wa CCM,
Mbowe Yupo Kama M/Kiti

JPM akiwa Kama M/Kiti Wa CCM,
Mbowe yupooo

Na Sasa ni Mama, Mbowe yupooo...!

Ama Hakika Huyu Mwamba ni Ruba...!
 
W
Ccm inajivunia kuwa na wapinzani wapumbavu
Wapinzani si wapumbavu,wamepitia mengi, wamevumilia mengi.
Wanapoanza kujipanga upya kwa nafasi waliopewa na serikali,ya kufanya siasa kwa uhuru zaidi kuliko enzi zile ,tuwaachie waamue mambo yao wenyewe.
Wapo baadhi ya viongozi wa vyama hivyo wamepigwa,wamebakwa,wamefungwa,wamejeruhiwa,wamenyanganywa na kuporwa mali zao kwa sababu ya misimamo yao. Viongozi kama Mbowe, Lissu,wana nafasi muhimu ya kuendeleza mapambano ya kujenga na kuimarisha vyama vyao kwanza.
 
..Lissu alikuwa anazungumzia katiba za vyama vya siasa, haswa vya upinzani hapa Tz.

..Pia alizungumzia changamoto waliyokutana nayo Chadema na kulazimika kuondoa kipengele cha ukomo wa madaraka ktk katiba yao.

..Lissu hajasema kwamba kusiwe na ukomo wa madaraka kwa nafasi ya RAISI wa Jamhuri na wa SMZ.

..Na kwa taarifa yako, ukomo wa madaraka uko kwa nafasi ya Raisi pekee, nafasi nyingine zote kama Ubunge, Udiwani, etc hazina ukomo.
 
Ni lazima tutambue maisha na hesabu zake, kwa umri wa tundu lisu na mbowe sasa ni muda wa kutafuta pensheni baada ya mikikimikiki ya siku nyingi.

Mbowe na lissu watawashangaza wengi, nadhani wameanza wanatafuta namna ya ku survive kwa uhakika kwa miaka mingi ijayo. Sitoshangaa kabisa huko mbele wakipewa vyeo au kuunga mkono juhudi, kamwe usiwaanini wanasiasa.
 
Ukomo Wa Madaraka ni 'Anasa'...

Kasema Lissu..

Ndo Maana 'Mbowe Kaking'ang'ania Kiti...! ni Mwenyekiti Wa Kudumu.
Mbowe hana kiasi...
Ni mtumbuizaji mzuri ila hajui ni wakati gani wa kuachia stage....sasa ameishiwa staili na stepu watazamaji tumechoshwa nae...

Fisiem tumechoshwa nayo sema hamna namna.
 
Ndugu usipotoshe kwa makusudi, hivi nyie ma CCM mbona mnajikuta saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaanaa, kama nyie ni vilaza si wote ni vilaza, jifunzeni kufanya tafakari na kutafuta maana halisi "muktadha" juu ya mambo yanayoongelewa na watu wote makini, si Tundu Lissu tu hata viongozi wenu ndani ya CCM, msiwe matutusa
 
Siku Daktari wa Sheria na Spika wa bunge Mhe.Tulia aliposema CCM haitoacha dola kamwe , kwa mara ya kwanza nilishtuka lakini baada ya kujiridhisha na hotuba nzima, nakiri kusema nukuu ya kipande hicho kinatumika kupotosha.

Siku zote natumia kanuni ya Thomaso, kujiridhisha kwa kuona na baada ya hapo nafanya uamuzi na ninachagua upande ulio sahihi. Kwa kauli ya Mhe.Dkt. Tulia huo ndio upande ninaochagua kwamba CCM haitaacha dola kamwe.

Ukimsiliza Spika Tulia katikati ya mistari unaona msingi wa hoja ya Spika umesimamia kwenye utendaji, usimamizi na utekelezaji wa miradi unaofanywa na Serikali ya CCM na matokeo yake. Kimsingi dola ni Wananchi, kama Wananchi wanaona utendaji mzuri, usimamizi wa hali ya juu na utekelezaji wa miradi sidhani kama hawataichagua CCM. Spika Tulia ni mkuu wa muhimili unaousimamia serikali na lolote analoongea ni kweli tupu .

Haya ni kwa utangulizi wa mada yangu kulingana na kichwa Cha mada. Baada ya kuruhusiwa mikutano ya hadhara, nimekuwa ni msikilizaji mzuri wa hoja za upinzani kwa kuwa sasa ni muda wa siasa za hoja. Kuna baadhi ya hoja nakubaliana na wapinzani lakini kwa nyingine hususani anazotoa Tundu Lissu zinaniachia maswali zaidi.

Siku za nyuma nilikuwa na imani kuwa miaka 50-100 ijayo upinzani ukipambana na kuamiwa na watanzania wanaweza kushika dola lakini kauli ya Tundu Lissu ya ukomo wa madaraka ni anasa imenifnaya nipoteze Imani.

Ukomo wa madaraka unawekwa kwa lengo la kuimarisha demokrasia na siasa safi. CCM Cha Mapinduzi toka uongozi wa Mwalimu mpaka sasa viongozi wote wanakuzwa na kulelewa katika Imani ya ukomo wa Madaraka. Uongozi wa Mwalimu ulikuwa na ukomo na ninaamini uongozi wa Rais Samia utakuwa na ukomo pia.

Kitendo cha kiongozi mwandamizi wa chama kuona ukomo wa madaraka sio mzuri ni jambo la kushangaza sana na kitendo hicho kina lengo baya. Kwamba kesho wakipewa dola ,kwa sababu waliondoa kipengele hicho kwenye Chama bila kelele kupigwa si wataamua kukiondoa kwenye katiba ya nchi na tukatawaliwa kifalme?

Yaani Tanzania iwe na utawala na mtawala asiye na ukomo wa madaraka hapa nasimama na wote wenye mtazamo wa CCM kuongoza milele.

Tusimhukumu Dkt.Tulia kwa kauli yake kabla ya kuukunjua upinzani tujue lengo lao la kutengeneza katiba za kifalme kwenye utawala wa kidemokrasia.
Andishi refu lakini pumba tupu
 
Back
Top Bottom