Baada ya kuacha kumlea mwanangu kimayai, nimeona akiimarika

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
Bado sijutii uamuzi niliofanya,

Hapo awali mtoto nilikuwa namlea kimayai huku nikijipa moyo sitaki apitie shida nilizopitia kumbe nilikuwa navuka mipaka kabisa ambayo haikuwa vema kwa mtoto,

Nikabadili malezi na kweli dhana yangu ya kutotaka mtoto asipate shida nilizopitia nliendelea nayo ila iliishia tu kuhakikisha mtoto anapata chakula, anavaa, anapata elimu, n.k na sio kuvuka mipaka.

Schoolbus nliacha kulipia maana shule ipo karibu tu kutembea ni dakika 25, kuna wenzake wanaosoma shule za kata hutembea masaa sasa mimi nikaona kwani huyu ni kilema hadi asitembee??

Anajifulia,,, Zamani lilikuwa jukum la haus gel ila nikaona huu upuuzi tu, kwani mikono yake imevunjika?? mama yake alisema namtesa ila nikamkumbusha adha atayopata mtoto endapo asipokua na msaada.

Anapalilia bustani ndogo .

Anafyeka nyasi (sio ombi)...Saizi silipi mtubaje kufyeka,

Kutandika kitanda,...Ashazoea kabisa,

kufagia uwanja ... Hapa saus gel nae kapunguza mzigo

Zamani mchana mama yake alipendelea kumwekea ratiba apikiwe wali au chips, nikaona hayo ndio ni mapenzi ya mama hasa ukiangalia uwezo wa kumudu hivi vitu upo lakini kama baba niliingilia kati hii ishu, Saizi mchana ni ugali kwa kwenda mbele nimempiga marufuku house girl kumpikia wali au chips, Saizi ni ugali tu na hii ni kwa faida ya mtoto.

Kucheza nje na wenzake,..ni haki yake, tatizo wazazibwenye uwezo huwa tunawaona watotot wetu ni kama malaika wasicheze nje na wenzao, Nlikuwa namfungia ndani nikamnunulia Playstation kuchezea game na kuangalia katuni ila kiukweli maisha halisi sio katuni bali ni watu, japo kwa tahadhari.

Shule kwangu nataka mtoto awe na uwezo kawaida tu, kipimo changu huwa ni wastani, yeye hushika nafasi ya tano kati ya wanafunzi 30 na mimi wala sina shida kabisa, sina mambo ya kuhakikisha anashika nafasi gani, ilimradi ana wastani unaoridhisha wala sina shida, ila huo wastani asipoufikia hata awe wa kwanza hapo nina shida.

Huu ni mwaka wa pili nadhani tangu nibadili style ya malezi na sijaona anakosa chochote zaidi ya kupata vingi zaidi.

Ushauri wangu kwa wazazi wenzangu ni kwamba wazazi wenye uwezo msitumie visingizio vya sitaki mwanangu aishi shida nlizopitia huku mkivuka mpaka huo na kutengeneza mtoto ambae ni mayai mayai.

Hata maua ukiyamwagilia sana maji mizizi yake huwa mifupi maana maji yapo tele ila mvua kali au upepo mkali ukipita maua yanatoka kwasababu mizizi haijaenda chini kutafuta maji kama maua yanayomwagiwa wastani tu yenye mizizi mirefu inayotafuta maji yaliyo chini hata mvua kali au upepo mkali ukipita mizizi inashikilia ua halitoki.

1620637429280.png
 
Wazazi wengine baadhi hawajui kulea watoto katika njia zipasazo... Huu usasa/utandawazi pia unachangia

"Mtoto mayai" unakuta hata chai kuchemsha hawezi, kujipikia hawezi, kufua, kudeki, kuosha vyombo hawezi pia

Wazazi msijisahau sana, tekelezeni wajibu wenu wa malezi, mfundishe shida na raha azijue pia akiwa mkubwa asijutie (Ajifunze kupitia changamoto zimkomaze, sina maana ya kumtesa)

Majukumu na kazi ndogondogo zitamjenga vizuri kujitegemea mwenyewe
 
Wangu alikuwa anaelekea huko.

Vijisenti vyangu vilitaka kumuharibia malezi mtoto wangu, ila nlistuka mapema
 
Wazazi wengine baadhi hawajui kulea watoto katika njia zipasazo... Huu usasa/utandawazi pia unachangia

"Mtoto mayai" unakuta hata chai kuchemsha hawezi, kujipikia hawezi, kufua, kudeki, kuosha vyombo hawezi pia

Wazazi msijisahau sana, tekelezeni wajibu wenu wa malezi, mfundishe shida na raha azijue pia akiwa mkubwa asijutie (Ajifunze kupitia changamoto zimkomaze, sina maana ya kumtesa)

Majukumu na kazi ndogondogo zitamjenga vizuri kujitegemea mwenyewe

Unamaanisha ni hata chai akichemsha anaweza kuunguza.
 
Misingi ya taifa inaanzia ngazi ya familia.....malezi mazuri yanaleta taifa safi na lenye maadili......malezi mabaya yanapelekea kujenga taifa lenye watu wa ajabu....
Yes...na kibaya zaidi ni kwamba mzazi ndio anaamua malezi, sasa unakuta mzazi akiwa na uwezo tu basi anafanya kufuru, mtoto unakuta hata kupasha chai hawezi kisa anapashiwa na house gel
 
Wa kwangu huwa nampigisha mchakamchaka kila asubuhi ya saa12

Akitoka apo anapiga usafi ya chumba chake ,fagia wanja,anangalia viji kuku vya Apo nyumbani badae anapika msosi wa majibwa na kuwatizama

Anapumzia kisha anajisomea

NB HAYA HUYAFANYA AKIWA LIKIZO IKUMBUKWE YUKO BWENI YENYE SHAMBA DUNIA NA WASTANI WA MCHUJO WA JUUH 80%
 
Back
Top Bottom