Baada ya DSTV kujichanganya kwa bei kubwa ya World Cup, AzamTv ni nafasi yenu hii kututangazia World Cup bei chee

Gharama za kuonyesha world cup ni kiasi gani mpaka ufikie conclusion hiyo?
Nimeona bid ya qatar kuonyesha kombe la dunia ilikuwa
QAT (2022)US$220 billion

Sasa kwa uelewa wangu kama hizi figure ni sahihi, itakuwa ni very very expensive kupata haki za matangazo, kuonyesha, na kadhalika. Sababu lazima Qatar watataka returns on investment.
 
TBC wanawezaje kuonyesha world cup?
Unafahamu hakuna TV company hata moja yenye thamani hiyo hapa Africa?
 
Dstv jana wamezindua ofa yao ya kombe la dunia ambapo ili uone mechi zote 64 mubashara utahitaji ulipe kifurushi cha Compact ambacho ni shilingi 56,000.

Ndugu zetu, wazalendo wenzetu AzamTv huu ndio muda wenu wa kuibuka na kututangazia Watanzania kuwa mtaonesha kombe la dunia kwa bei nafuu.

AzamTv amkeni kutoka kwenye usingizi mzito njooni mjichukulie point 3 muhimu
Ni basi tuu umasikini unatusumbua, hapo ni sawa na mechi moja unalipia Tsh 875.

Sasa tuje kwenye vibanda umiza tutalipia buku kila mechi au tutanunua vinywaji vya zaidi ya buku kwa kila mechi?

Si watetei DSTV ila najaribu kuwaza kwa uhalisia wa bei iliyopo.
 
Back
Top Bottom