KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,601
Kwanza, ninampongeza sana Spika Dkt.Tulia kwa ushindi wa kishindo kama Rais wa IPU, kama Taifa linajivunia juhudi na jitihada zake za kuitangaza nchi kimataifa.
Spika Tulia au tumuite Rais wa IPU ni jasiri na mpambanaji na historia yake inajieleza vema. Kwa ufupi ni mwanamke wa shoka na yuko "very determined" maana sio rahisi kufika alipofika kama ni mtu wa kukata tamaa na kukubali kushindwa kabla hujaanza shindano.
Safari yake ya ujasiri inaanza pale jimboni Mbeya kwenye kiti Cha Ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa 2020. Jimbo la Mbeya ni Moja ya majimbo yaliyokuwa na ushindani mkubwa sana lakini alijitoa na akafanikiwa kushinda na mpaka sasa hakuna mwanaume wala mwanamke wa kumtia Tulia kwenye Ubunge wa Mbeya. Amefanya mengi makubwa Kwa kipindi kifupi.
Na hili la kugombea Urais wa IPU Kwa Imani na matumaini ya kushinda na kufanikiwa kushinda ni kielelezo Cha kuthibitisha uwepo wake ni baraka kubwa Kwa nchi yetu Kwa siku za mbeleni.
Hapa ndipo ishara kuu zinaonekana mbeleni kwamba huyu si mtu wa kawaida hata kama sisi watanzania tuna tabia ya kuwachukulia watu kawaida. Spika Tulia ana roho ya kufanikiwa na kushinda kwa kila anachofanya. Roho hii itaendelea kufanya kazi kwa mengine mengi juu yake.
Wakati Mhe.Rais akifungua tovuti ya historia ya Dkt.Salim alisema tumerudi nyuma kwenye diplomasia uwe unguli tuliokuwa nao miaka ya 2000 kurudi nyuma haupo tena,tunahitaji kulibadili hili.
Unguli unaosemwa na Rais Samia ni kupitia Kwa Dkt.Salim, mtanzania aliyekuwa na historia ya kusisimua ambaye kama sio fitna basi angeukwaa ukatibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Namtazama Spika Tulia kama Dkt.Salim wa leo ambaye atabeba jukumu la kuipaisha diplomasia ya nchi yetu kimataifa. Namtazama Spika Tulia mtu sahihi Kwa kizazi Cha Sasa kuturejeshea unguli wetu kwenye diplomasia ya kimataifa.
Zaidi, namtazama kwenye nafasi kubwa zaidi za kimataifa. Alishindwa Dkt.Salim kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa naamini njia ipo wazi Kwa Dkt.Tulia kuja kuwa Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu. Tunakuombea na Taifa linajivunia wewe.
Sasa, Taifa linakutazama kama nguli wa diplomasia za kimataifa wa kizazi cha leo na lina matarajio makubwa kutoka kwako.