Ninahitaji Mwekezaji kwenye biashara yangu ya uzalishaji wa vipodozi

Jane Msowoya

JF-Expert Member
Aug 20, 2017
4,046
7,118
Heshima kwenu wakuu,

Ninahitaji mwekezaji kwenye biashara yangu ya uzalishaji wa vipodozi ni kiwanda kidogo kinachojihusisha na uzalishaji wa bidhaa za urembo Mafuta, sabuni, lotions, scrubs, serums nk

Biashara imesajiliwa na mamlaka zote na inajiendesha kihalali

Thamani ya biashara kwa sasa ni 20m
Ambayo inajumuisha machines na working capital

Uhai wa biashara ni miaka miwili na kuna feedback nzuri sana za wateja

Wateja
Tunatumia social media (duka mtandao)
Beauty botiques
Machinga (kkoo hawa tunawasambazia sabuni)
mawakala wa mikoani na nchi jirani (Congo,Malawi na Zambia)

Nahitaji mwekezaji awekeze 10m ambayo itaingia kwenye working capital na mwekezaji atapata 10% equity share huku mtaji wake ukiwa upo pale pale na endapo akaamua kusitisha mkataba atarudishiwa pesa yake kulingana na muda tutakao kubaliana

NB: 10% ni ownership, profit split ni annualy ambapo mwenye ownership ya 10% atapata 10% of the profit generated annualy.

Mwekezaji atakuwa mjumbe wa bodi pia kushiriki vikao vya bodi ya washauri tunavyofanya Kila baada ya miezi mitatu pia atapata access ya taarifa zote za biashara (sales,purchase,transactions and contracts) muda wowote atakaohitaji

Biashara ina team ya watu 6 na mawakala zaidi ya 20

Kwa ambae atakuwa interested

Karibu whatsapp 0769922210 nikutumie company profile,pitch deck,pitch video na financial reports za mwaka 2022-2023

Pia napokea appointment za meeting za ana kwa ana ofisini kwetu au zoom meeting kwa waliombali

Niwatakie mapumziko mema ya juma
 
I love how ypu presented your business.

Ningekua nayo hakyanan vile i would invest.

I wonder why BOngo hakuna shark tank for ideas kama hizi.

Nakuombea upate zaidi ya mwekezaji mmoja tena walio serious

Swali la kizushi, kama siko na hyo mtonyo, cam i still ask for company profile,pitch deck,pitch video na financial reports za mwaka 2022-2023 ili nijifunze zaidi kwa ajili ya kampuni yangu pia nnayo plan kufungua huko mbeleni?
 
Ikiwa bado hmn muwekezaji wa hyo capital moja kwa moja nashauri tenga fungu la hisa stahiki litakaloleta hyo total amount ya capital unayotaka kuraise ili tununue kama hisa na binafsi nitakua interested ili ku mitigate risk kwa upande wangu

Sent from my 21051182G using JamiiForums mobile app
Wazo zuri sana mkuu
Ngoja nilifikishe kwa team tuone inakuaje ntakurudia
 
10% ni ownership, profit split ni annualy ambapo mwenye ownership ya 10% atapata 10% of the profit generated annualy,

For istance if we make the total profit of 10M annualy, you get 10% of 10M
Asante kwa ufafanuzi kwahio unauza 10% ya ownership.

Suali jengine huyu 10% partner anahitajika nae kwenye mauzo(supplier)au yeye ni investor tu na kupata gawio lake end of the year tu.

Kwenye mauzo unatumia accountant wako tu au investors anaweza leta wake?.
 
Naomba kuuliza. Thamani ya biashara ni 20m, mwekezaji anaweka 10m, kwa nini awe na 10% share badala ya 50% share?
Valuation ya biashara haipimwi kwa thamani ya mtaji wa biashara pekee.

Kuna trust ya brand kwa wateja ambayo tumeijenga for years now, biashara bado ina long run siwezi uza 50% kwa 10m mkuu

NB: Y combinator wanatoa $500k kwa startups in exchange of 10% equity share tena zingine zikiwa in ideation stage
 
Asante kwa ufafanuzi kwahio unauza 10% ya ownership.

Suali jengine huyu 10% partner anahitajika nae kwenye mauzo(supplier)au yeye ni investor tu na kupata gawio lake end of the year tu.
Kwenye mauzo unatumia accountant wako tu au investors anaweza leta wake?.
Hapana yeye anawekeza tu nakusubiri mgao wake mwisho wa mwaka lakin atakuwa anahudhuria vikao na kupata reports za kila mwezi namna biashara inavyokwenda.

Swala la accountant kwa sasa tuna outsource anakuja kwa wiki mara moja lakin ukileta wako its fine na ukiwa wewe mwenyewe na taaluma hiyo pia itakuwa vzr zaidi maana kuna kiasi fulani utapata kwa ajili ya kazi hiyo
 
Karibu whatsapp 0769922210 nikutumie company profile,pitch deck,pitch video na financial reports za mwaka 2022-20
Umewezaje kutengeneza financial reports za mwaka 2022-2023 ikiwa ndo kwanza upo katika mwezi wa kwanza kwa robo ya mwisho wa mwaka 2023?
Uhai wa biashara ni miaka miwili na kuna feedback nzuri sana za wateja
Kama uhai wa biashara ni miaka miwili, kwa nini usimpatie nakala ya financial reports "prospect investor" za mwaka 2020/2021 na 2021/2022?
 
Back
Top Bottom