Baada ya bandari kubinafisishwa kwa miaka 100, ninamuomba radhi chifu Mangungo

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,757
NATAMANI KUWAOMBA MSAMAHA KINA CHIEF MANGUNGO
____________________
Kuna nyakati huwa Natamani Sisi Watanzania Kuwaomba Msamaha mababu zetu akiwemo Chief Mangungo kwa KUWACHEKA na Kuwa na HASIRA nao kwa kuingia Mkataba wa Ulaghai na Dr. Carl Peters wa Ujerumani ambao ndio uliidhinisha mwanzo wa utawala wa Kikoloni Karne ya 19.

Ni wazi kabisa kizazi chetu cha sasa kila kinaporejea kusoma namna mababu zetu walivyoingizwa Kingi kwenye mikataba ya ulaghai hasa kwa kumrejea Chief Mangungo wa Msowero hucheka na kuona walikuwa wajinga kiasi gani mpaka wakubali?

Lakini mababu hawa kina Chief Mangungo hawakuwa na elimu yoyote, hawakuwa wametembea sehemu mbalimbali yaani hawakuwa na exposure, mababu hawa walidanganywa kwasababu hawakuwa na elimu yoyote ya darasani na hata kutia saini walitumia dole gumba huku wakiwa hawaelewi kilichoandikwa.

Kizazi hikihiki cha baada ya Ukoloni, kizazi chenye elimu, kizazi kinachojua lugha zote rasmi duniani, kizazi cha kidigitali, kinashindwa kujiuliza na kuhoji na kuwacheka viongozi wake ambao wamekuwa wakisaini mikataba ya miaka ya zaidi ya 100 ambayo ndani yake kuna athari za kizazi na kizazi. Mikataba inayokuwa inamnufaisha mwekezaji zaidi na kuwanyonya wazawa.

Mikataba inasainiwa na viongozi waliosoma na kusomeshwa kwa fedha za umma na wana Degree, Masters na PhD, mikataba wanayosaini ni ya kinyonyaji na ya hovyo lakini mikataba inatetewa kwamba wawekezaji hawa wataongeza ajira na kizazi cha Kisomi kinafurahia na kushangilia, hakuna kuhoji, hakuna kuuliza. Ajira zinazoongezwa ni za Malipo ya bora mkono uende kinywani. Ajira zisizo za ukombozi wa kiuchumi.

Nimebahatika kuona mahali kwa macho yangu, Kiwanda ambacho kipo Tanzania eneo kilipo kuna makubaliano ya kimkataba miaka 100 kinazalisha nguo ambazo zinakwenda kuuzwa nje. Nguo zimeandikwa Made in China ila zinatengenezwa hapa kwetu. Kina wafanyakazi zaidi ya 400 (Mia nne) Mishahara wanayolipwa take home Yaani baada ya makato yote ni Sh. 90,000TZS na masaa ya kufanya kazi ni saa mbili asubuhi hadi saa moja usiku, Jumatatu hadi Ijumaa na Jumamosi ni mwisho saa nane mchana. Makontena na makontena huingia na kutoka kila wiki. Je, huyu mwekezaji ana Faida gani kwa nchi yetu kama sio unyonyaji ni nini?
Hivi mbele ya kizazi chenye wasomi lukuki viongozi wanathubutu kusaini mkataba wa kuuza bandari ya Dares salaam kwa miaka mia moja?
Je, mkataba kama huu, ulisainiwa na Mangungo? Kwanini tuwacheke wazee wetu ambao hawakuwa na elimu yoyote?

Natamani Kuwaomba msamaha kina Chief Mangungo.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
20230606_201049.jpg
 
Rais anako ipeleka nchi anajua yeye. Yaani karne 21 ubinafshishe Bandari Kuu ya Nchi? Kitega uchumi kikuu ya Taifa! Hawa Waswazi shule ili wapita kushuto!!
Leo pia nimeona Mwigulu yupo na ma CEO wa Bank ya mikopo ya Ufaransa. Akope kwa jina la Tz. Pesa ziende kujenga Pemba!! Huu ujinga CCM kuna siku mta jibu!!
 
NATAMANI KUWAOMBA MSAMAHA KINA CHIEF MANGUNGO
Swali dogo tu" je ninyi ndiyo mliowachagua wawe pale "? Si kuna mtu aliweka falisafa kuwa wakiwa peke yao mjengoni, ndipo mtaishi kama muko peponi? Na nchi itakua kama Newyork kuanzia chatu mpaka zenzi,na kuanzia kiaka mpaka mbaba bay?? Siku zijazo mjifunze kuweka wenu ili wakiwa palee juu walinde maslahi yenu.Ni hayo tu kwa leo !!
 
Aise kwa kweli Tanzania sasa inaliwa. Kweli Bunge letu mmeridhia??? Kipi tumeshindwa kusimamia wenyewe.? Ndege tumeshindwa, bandari tumeshindwa,mbuga zetu tumeshindwa,migodi tumeshindwa,VIWANDA tumeshindwa, n.k. je sisi tunaweza kusimamia Nini???nchi hii tunaipiga mnada tu, kuna Nini Dubai?? Masikini TANZANIA 🤔🤔
 
Swali dogo tu" je ninyi ndiyo mliowachagua wawe pale "? Si kuna mtu aliweka falisafa kuwa wakiwa peke yao mjengoni, ndipo mtaishi kama muko peponi? Na nchi itakua kama Newyork kuanzia chatu mpaka zenzi,na kuanzia kiaka mpaka mbaba bay?? Siku zijazo mjifunze kuweka wenu ili wakiwa palee juu walinde maslahi yenu.Ni hayo tu kwa leo !!
Huyo mtu hakubinafisisha chochote
 
Aise kwa kweli Tanzania sasa inaliwa. Kweli Bunge letu mmeridhia??? Kipi tumeshindwa kusimamia wenyewe.? Ndege tumeshindwa, bandari tumeshindwa,mbuga zetu tumeshindwa,migodi tumeshindwa,VIWANDA tumeshindwa, n.k. je sisi tunaweza kusimamia Nini???nchi hii tunaipiga mnada tu, kuna Nini Dubai?? Masikini TANZANIA
Uafrika hasa utanzania ni LAANA
 
Nimebahatika kuona mahali kwa macho yangu, Kiwanda ambacho kipo Tanzania eneo kilipo kuna makubaliano ya kimkataba miaka 100 kinazalisha nguo ambazo zinakwenda kuuzwa nje. Nguo zimeandikwa Made in China ila zinatengenezwa hapa kwetu. Kina wafanyakazi zaidi ya 400 (Mia nne) Mishahara wanayolipwa take home Yaani baada ya makato yote ni Sh. 90,000TZS na masaa ya kufanya kazi ni saa mbili asubuhi hadi saa moja usiku, Jumatatu hadi Ijumaa na Jumamosi ni mwisho saa nane mchana. Makontena na makontena huingia na kutoka kila wiki. Je, huyu mwekezaji ana Faida gani kwa nchi yetu kama sio unyonyaji ni nini?
Kiwango cha mishahara kinacholipwa na WACHINA ni chini ya kima cha chini.
Sijui wanatumia sheria gani. Ni kama hakuna serikali hapa🙄
Inasikitisha sana!
 
Back
Top Bottom