Kama Mkuu wa Wilaya analia kwa kuona watu wakila maembe huyo hafai kuwa Mkuu wa Wilaya. Watanzania umefika wakati wa kuacha kukariri, nani kasema maembe hayafai kuwa chakula? Tena mimi naona tungekuwa na vionzozi wenye maono wangehamasisha watu wale maembe kipindi hiki cha msimu wa maembe kwa wingi huku wakihifadhi chakula cha aina nyingine kwa vile maembe hayahifadhiki kwa tekinolojia tuliyo nayo mpaka sasa. Tuna tatizo kubwa la kufikiri. Taarifa kwa wajinga wenzangu, maembe ni chakula ghali dar kuliko hata huo mchele.