Azimio La Arusha: Why We Were Dead Wrong!

Namshukuru sana JK Nyerere kwa kuhakikisha John Jumanne Malecela kamwe hawi Rais wa nchi hii, kumbe Nyerere aliona mbali, Guess kilaza kama huyu William ndio angekuwa mtoto wa Raia pangetosha hapa?

Asante sana JK Nyerere na sisi wazalendo tutakuenzi kwa kuhakikisha huyu mchumia tumbo William bunge atakuwa analiangalia kupitia tv tu na siyo kuwa ndani ya nyumba kama Mbunge.
 
Marekani ni nchi ya kibepari lakini ina miiko ya uongozi. Bila miiko ya uongozi taifa linakuwa kama meli inayoyumba baharini bila kepteni kujua inakoelekea. Kwa mfano, Obama hawezi kumuajiri mkewe, mwanae, au ndugu yake katika serikali. Huo ni mwiko. Obama hawezi kuendesha kampuni ya biashara akiwa White House. Huo ni mwiko. Obama hawezi kumpigia mkuu wa polisi na kumtaka amwachie mhalifu fulani kwa sababu ni rafiki au ndugu yake Obama. Huo ni mwiko. Azimio la Arusha liliweka miiko ya uongozi ambayo ilifutwa na Mwinyi na Mzee Malecela pale Zanzibar na matokeo yake ndiyo haya tunayoyaona. Kulaumu Azimio kwa matatizo tuliyo nayo Tanzania ni kuwa myopic. Kenya wamekuwa mabepari tangu walipopata uhuru. Tena wao viongozi wao walijinyakulia ardhi na mali za serikali bila aibu tangu enzi za Kenyatta, lakini ukienda mashambani Wakenya wanaishi maisha ya dhiki kuliko hata sisi Watanzania. Azimio la Arusha lilitoa matumaini ya maisha bora kwa Watanzania waliokuwa wanaishi vijijini ambao ni zaidi ya 80% ya population yetu. Mnaoshangilia kufa kwa azimio hamna lolote la kuonyesha ila tu kukithiri kwa wizi wa viongozi na ndiyo sababu kila mtu anakimbilia sasa kuwa mbunge ili ama achaguliwe kuwa waziri, atajirike kwa muda mfupi, au awe na maisha mazuri ya haraka kuliko Mtanzania wa kawaida.

Jasusi,

Miiko ya uongozi iliyopo Marekani inafuata misingi ya katiba na sio document ya vyama vya kisiasa. Tanzania ina katiba yake na Azimio la Arusha aliwezi kuwa juu ya sheria na katiba ya nchi.
 
- Mkuu Jasusi, heshima yako sana America kuna sheria, hakuna miiko ya uongozi you know better huko taifa huongozwa kwa sheria, matatizo ya Clinton na Monica yalitatuliwa na sheria sio miiiko ya uongozi, hapana!

- Kenya wamekwua mabepari kwa muda mrefu kuliko sisi, ndio maana wana viwanda vingi kuliko sisi na pesa yao ni kubwa kuliko yetu, na pia Watalii wanawajali wao kuliko sisi, yaaani haya hata bila shule yanaeleweka sana kuwa ni matunda ya ubepari!

William.
Tofauti ni zipi kati ya sheria zinazowabana viongozi na miiko? Code of conduct? To me it is one and the same. Kiongozi anajua mipaka ya madaraka yake. Hili lilikuwepo Tanzania kabla ya hawa vilaza kutupeleka Zanzibar. Kiongozi ulikuwa hutakiwi kuwa share holder kwenye private companies. Unaweza kusema huo ni mwiko au sheria. The difference is the same. Leo sisi hatuna. Tanzania imegeuzwa kuwa shamba la bibi na watafunaji ni hao hao vilaza tunaowaita viongozi. That is all I am saying. Kenya walikuwa na viwanda tangia enzi za ukoloni. Kenya was a colony, Tanganyika was a trust territory. Waingereza kwa makusudi hawakujenga viwanda Tanganyika kwa sababu walijua wataondoka siku moja. Kenya ilibidi mau mau waingie msituni kuwaondoa kwa sababu kule Waingereza waliigeuza kuwa Rhodesia ya pili. Tumepata uhuru mwaka 1961 tulikuwa na kiwanda kimoja tu kikubwa, Tanganyika Packers. Nakumbuka nilipokuwa mdogo tulikuwa tunaletewa maziwa ya packet kutoka Nairobi, twice a week pale Musoma. Hatukuwa na hata kiwanda kimoja cha kusindika maziwa. Mafuta ya Kimbo, sabuni ya Omo, na dawa za Aspro, zote zilitoka Kenya. Hata tungeamua kuwa mabepari kuanzia 1961 sidhani tungeweza ku catch up na Kenya katika viwanda. Hiyo ni ndoto ya mchana.
 
Jasusi,

Miiko ya uongozi iliyopo Marekani inafuata misingi ya katiba na sio document ya vyama vya kisiasa. Tanzania ina katiba yake na Azimio la Arusha aliwezi kuwa juu ya sheria na katiba ya nchi.
Zakumi,
Kwanza pongezi kwa Avatar mpya. At least najua sasa unazo buti za kutembelea mjini/mashambani badala ya zile ndala. Ni kweli miiko ya uongozi Marekani inafuata katiba. Lakini si wakati wote. Mwaka 1960 Kennedy aliposhinda urais, alimteua mdogo wake Robert kuwa Attorney General. Mpaka sasa Wamarekani watakwambia Robert Kennedy was the best attorney general ever, lakini baada ya hapo walipitisha sheria kwamba rais asimchague ndugu yake, mke wake au mtoto wake katika nafasi za kazi serikalini. Hili halikuwemo katika katiba, lakini walihofia kujengwa kwa himaya ya kifamilia na sheria ikatungwa kuzuia hili. Naliangalia azimio la Arusha, na hasa miiko ya uongozi katika mizani hii. Kanuni za uongozi si lazima ziwe kwenye katiba.
 
It disturbs me to see we dont want to confront the fundamental and thorny issues that affects us today, without referring to Nyerere and his term in the office. The nature of the problems that we face today have got nothing to do with Nyerere. Kwa mfano, ningeona tatizo kama Nyerere angesaini mkataba wa miaka mia mbili na nchi au kampuni fulani ya nje ili kuiendesha bandari yetu au mbuga zetu za wanyama au hata migodi yetu.
Nyerere hakufanya hivyo ila sisi tunafanya. Tukiulizwa tunasema tatizo ni kwasababu ya Nyerere na siasa zake. Tuache kuzidanganya nafsi zetu wenyewe. Tupambane na vizingiti vinavyoikabili Tanzania ya leo kwa ubunifu zaidi na matumizi sahihi ya vichwa vyetu.
Naona tulio wengi nia ni kuwa viongozi wa wananchi bila hata kujua hao wananchi tutawafanyia nini. Anyway, labda like father like son. Who knows???!!!

Ndahani,

You quote my post, but you don't take time to read it. If you had read it, you would have found that I didn't mention Nyerere or his descendants or disciples.

Brain is a terrible thing to waste. Miaka ya utekelezaji ya hizo siasa za Azimio la Arusha, watanzania mmepoteza muda mwingi kujifunza vitu vya kishambashamba na kushindwa kujenga capabilities za kuendesha nchi. Na haichangazi kwa viongozi wa sasa kushindwa kuendesha nchi. Kwani wakati nchi zingine zinafanya juhudi za kujenga capabilities zao, kazi zenu zilikuwa kuandamana na kukimbiza mwenge.
 
Zakumi,
Kwanza pongezi kwa Avatar mpya. At least najua sasa unazo buti za kutembelea mjini/mashambani badala ya zile ndala. Ni kweli miiko ya uongozi Marekani inafuata katiba. Lakini si wakati wote. Mwaka 1960 Kennedy aliposhinda urais, alimteua mdogo wake Robert kuwa Attorney General. Mpaka sasa Wamarekani watakwambia Robert Kennedy was the best attorney general ever, lakini baada ya hapo walipitisha sheria kwamba rais asimchague ndugu yake, mke wake au mtoto wake katika nafasi za kazi serikalini. Hili halikuwemo katika katiba, lakini walihofia kujengwa kwa himaya ya kifamilia na sheria ikatungwa kuzuia hili. Naliangalia azimio la Arusha, na hasa miiko ya uongozi katika mizani hii. Kanuni za uongozi si lazima ziwe kwenye katiba.

Jasusi

Kwikwikwi, nimepata viatu. Kwanza Marekani katiba is the supreme law of the land. Na sheria za nchi ni extensions za katiba. Kama walipitisha sheria ya kuzuia kuajiri ndugu, walichofanya ni ku-extend katiba.

Sina Tatizo lolote na miiko ya uongozi ambayo inafuata katiba ya jamuhuri wa muungano na sheria za nchi. Katiba JMT inasema kuwa mtanzania na haki ya kumiliki mali na kushiriki kwenye maamuzi ya kisiasa. Hivyo Mzee Mengi anazo haki zote za kikatiba na sheria kuwa rais wa nchi. Lakini kama anamiliki hotel ambayo ni nyumba ya kupangisha basi Azimio la Arusha linazuia haki hizo.

Mbele yangu hapa nimefungua katiba ya nchi na azimio la Arusha.
 
Jasusi,

Miiko ya uongozi iliyopo Marekani inafuata misingi ya katiba na sio document ya vyama vya kisiasa. Tanzania ina katiba yake na Azimio la Arusha aliwezi kuwa juu ya sheria na katiba ya nchi.
Zakumi. Sawa. Unaonaje sasa katika suala la kuandaa katiba mpya, tusianze kujadili namna ya kuchukua yale mazuri ya azimio ili yaweze kuwekwa kwenye katiba?
 
Last edited by a moderator:
Namshukuru sana JK Nyerere kwa kuhakikisha John Jumanne Malecela kamwe hawi Rais wa nchi hii, kumbe Nyerere aliona mbali, Guess kilaza kama huyu William ndio angekuwa mtoto wa Raia pangetosha hapa?

Asante sana JK Nyerere na sisi wazalendo tutakuenzi kwa kuhakikisha huyu mchumia tumbo William bunge atakuwa analiangalia kupitia tv tu na siyo kuwa ndani ya nyumba kama Mbunge.

Una mapungufu ya kifikra. Willie na Mzee John ni watu wawili tofauti. Mzee Malecela hana shughuli zozote katika mjadala huu.
 
Una mapungufu ya kifikra. Willie na Mzee John ni watu wawili tofauti. Mzee Malecela hana shughuli zozote katika mjadala huu.
Ni heri yangu mwenye mapungufu ya kifikra kuliko wewe mwenye Fikra mgando, hata kama Mzee Malecela hana shughuli yoyote kwenye mjadala huu mwambie shoga yako William asahau kuwa Mbunge ndani ya nchi hii, Bunge letu siyo kijiwe cha ku accommodate Failures & losers.
 
Zakumi. Sawa. Unaonaje sasa katika suala la kuandaa katiba mpya, tusianze kujadili namna ya kuchukua yale mazuri ya azimio ili yaweze kuwekwa kwenye katiba?

Wengi mnaolitetea Azimio la Arusha, mnapenda kanuni za uongozi. Kanuni za uongozi ni code of ethics. Code of ethics zinaweza kuwepo katika sheria za nchi, kanuni za uendeshaji wa vyombo mbalimbali.

Mwanafunzi anapokuwa shuleni anatakiwa asi-copy kazi ya mtu. Daktari anatakiwa atoe huduma kwa kila mgonjwa. Mwanasheria anatakiwa asiwe biased, n.k

Code of ethics zinabadilika kutokana na mabadiliko ya jamii. Hivyo hazina nafasi katika katiba.
 
Ni heri yangu mwenye mapungufu ya kifikra kuliko wewe mwenye Fikra mgando, hata kama Mzee Malecela hana shughuli yoyote kwenye mjadala huu mwambie shoga yako William asahau kuwa Mbunge ndani ya nchi hii, Bunge letu siyo kijiwe cha ku accommodate Failures & losers.

Posti yako inazungumza mengi yanayokuhusu. William hawezi kuwa mbunge bila ya ruhusa ya watu wajimbo lake na sio JF.
 
Zakumi. That is too low mzee. Read between the lines in my post.

Nimesema ukitoa sura ya kwanza,azimio bado lina mambo mengi ya msingi kwa taifa letu. Sasa unapokuja na hoja ya nisome sura ya kwanza,nakushangaa.

Hakika nakwambia,licha ya mapungufu ya azimio hilo,lina mambo mazuri. Jambo la msingi kwetu ni kujadili namna gani tuliboreshe. Tuchukue mazuri yake tuchanganye na mazuri ya ubepari,then tunakua na mfumo mchanganyiko ambao unakuwa na manufaa kwa taifa nzima.

Nzi,

Watanzania ni wavivu wa kujisomea na kujiendeleza. Mambo mazuri ya Azimio la Arusha yanapatikana katika documents nyingi duniani. Kwanini tusifunue upeo na kuangalia mambo mengine.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Ndahani,

You quote my post, but you don't take time to read it. If you had read it, you would have found that I didn't mention Nyerere or his descendants or disciples.

Brain is a terrible thing to waste. Miaka ya utekelezaji ya hizo siasa za Azimio la Arusha, watanzania mmepoteza muda mwingi kujifunza vitu vya kishambashamba na kushindwa kujenga capabilities za kuendesha nchi. Na haichangazi kwa viongozi wa sasa kushindwa kuendesha nchi. Kwani wakati nchi zingine zinafanya juhudi za kujenga capabilities zao, kazi zenu zilikuwa kuandamana na kukimbiza mwenge.

I think tatizo halikua Azimio la arusha, tatizo kama kawaida ilikua ni ile process management

Mimi mara nyingi huwa najiangalia kama mtanzania na tabia yetu ya "easy way out" or "easy does it"

Ukichunguza hata ubepari ulipokuja, asilimia kubwa yetu ilikomalia yaliyo rahisi, this could a mindset, vizazi vilivyotangulia au hata genetic... haiwezekani wachagga wajue pesa halafu directly tuwaone wana tamaa na mmakua awe bize kwenye ngoma, ngono na majungu, then tusingizie ujamaa... KAMWE

As always, we tend to put blames on someoen else, and in many cases anakua either mtoto mdogo, marehemu au siyekuwepo

HII MADA NI NZURI, ILA IMEANZA NA BLAME GAME, DEAD END ETC!!! WE COULD USE IT POSITIVELY KAMA MCHAMBUZI NA WENGINE WANAVYOJARIBU KUTUSAIDIA

HATA UNGEKUA UBEPARI NDIYO SERA YA 1967, BADO WATANZANIA TUNGEISHIA KUULAANI, KUUTUKANA NA KUUKASHIFU, WE HAVE THAT CURSE SOMEHOW
 
Wengi mnaolitetea Azimio la Arusha, mnapenda kanuni za uongozi. Kanuni za uongozi ni code of ethics. Code of ethics zinaweza kuwepo katika sheria za nchi, kanuni za uendeshaji wa vyombo mbalimbali.

Mwanafunzi anapokuwa shuleni anatakiwa asi-copy kazi ya mtu. Daktari anatakiwa atoe huduma kwa kila mgonjwa. Mwanasheria anatakiwa asiwe biased, n.k

Code of ethics zinabadilika kutokana na mabadiliko ya jamii. Hivyo hazina nafasi katika katiba.

Mkuu Zakumi, yaani unaweza ukatoa conclusive statement kama hiyo kweli? Umesoma bandiko langu la awali la kumjibu @W.J.Malecela?
Mimi sitetei azimio katika msingi wa hizo code of ethics pekee; ninasema kuna mambo mazuri ambayo yapo katika azimio, mambo ambayo bado yana maana kwa mustakabali wa taifa letu. Masuala la kujitegemea na maendeleo yenye kuzingatia walio wengi (hapa nazungumzia kutilia mkazo kilimo na wakulima wadogo wadogo, kwani ndiyo walio wengi). Haya yapo zaidi ya code of ethics.

Licha ya hayo, mbona hatuoni hizo code of ethics zikatiliwa mkazo? Au unataka kumaanisha kwamba, Tanzania sasa haina code of ethics kwa vile zinabadilika kutokana na mabadiliko ya jamii? Seriously??!? Hata code of ethics zilizobadilika na mabadiliko ya jamii sioni kama zipo au zinafanya kazi.

Halafu mkuu, ni kweli kuna haja ya code of ethics kwa viongozi na watumishi wa umma kubadilika kutokana na mabadiliko ya jamii? Unataka kumaanisha kutokana na mabadiliko fulani, itafika kipindi daktari pale Muhimbili atapaswa kutoa huduma kwa matajiri au masikini tu?! Au jaji/hakimu wa mahakama, itafika kipindi atapaswa atoe hukumu kwa kupendelea upande fulani, bila kuzingatia taratibu za kisheria?! Seriously??!

Last edited by a moderator:
Nzi,

Watanzania ni wavivu wa kujisomea na kujiendeleza. Mambo mazuri ya Azimio la Arusha yanapatikana katika documents nyingi duniani. Kwanini tusifunue upeo na kuangalia mambo mengine.
Kwakuwa wewe ni Mtanzania nina uhakika ulijitazama na ukajitathimini na ukafikia hitimisho kwamba hivi ndivyo ulivyo, umechelewa sana kudeclare hili otherwise usingetusumbuwa akili Watu tunaojisomea na ambao tumeendelea maana hatuna hitaji la kujiendeleza.
Nilikuwepo....
 
Mkuu Zakumi, yaani unaweza ukatoa conclusive statement kama hiyo kweli? Umesoma bandiko langu la awali la kumjibu @W.J.Malecela?
Mimi sitetei azimio katika msingi wa hizo code of ethics pekee; ninasema kuna mambo mazuri ambayo yapo katika azimio, mambo ambayo bado yana maana kwa mustakabali wa taifa letu. Masuala la kujitegemea na maendeleo yenye kuzingatia walio wengi (hapa nazungumzia kutilia mkazo kilimo na wakulima wadogo wadogo, kwani ndiyo walio wengi). Haya yapo zaidi ya code of ethics.

Licha ya hayo, mbona hatuoni hizo code of ethics zikatiliwa mkazo? Au unataka kumaanisha kwamba, Tanzania sasa haina code of ethics kwa vile zinabadilika kutokana na mabadiliko ya jamii? Seriously??!? Hata code of ethics zilizobadilika na mabadiliko ya jamii sioni kama zipo au zinafanya kazi.

Halafu mkuu, ni kweli kuna haja ya code of ethics kwa viongozi na watumishi wa umma kubadilika kutokana na mabadiliko ya jamii? Unataka kumaanisha kutokana na mabadiliko fulani, itafika kipindi daktari pale Muhimbili atapaswa kutoa huduma kwa matajiri au masikini tu?! Au jaji/hakimu wa mahakama, itafika kipindi atapaswa atoe hukumu kwa kupendelea upande fulani, bila kuzingatia taratibu za kisheria?! Seriously??!

Nzi,

Kuhusiana na masuala ya kujitegemea na maendeleo ya walio wengi Azimio isn't a sound guidance. Kumwambia masikini maneno matamu haina kuwa unamsaidia.
 
Jasusi,

Miiko ya uongozi iliyopo Marekani inafuata misingi ya katiba na sio document ya vyama vya kisiasa. Tanzania ina katiba yake na Azimio la Arusha aliwezi kuwa juu ya sheria na katiba ya nchi.

Upo sahihi kabisa lakini kwa bahati mbaya sana, nchi yetu ilikuwa inaongozwa na katiba ya CCM kama ndio katiba ya nchi kwa miaka mingi sana mpaka umma/upinzani ulipoanza kuamka. Katiba ya nchi ilikuwa inapuuzwa. isitoshe, Tanzania ilikuwa haina katiba kwa kipindi cha miaka 12 i.e 1964 - 1977, katika kipindi hiki, tulikuwa na katiba ya mpito. Na hata hiyo katiba ya 1977 mara nyingi sana ilikuwa haifuatwi na kuheshimiwa kama katiba katiba ya CCM.
 
Kwakuwa wewe ni Mtanzania nina uhakika ulijitazama na ukajitathimini na ukafikia hitimisho kwamba hivi ndivyo ulivyo, umechelewa sana kudeclare hili otherwise usingetusumbuwa akili Watu tunaojisomea na ambao tumeendelea maana hatuna hitaji la kujiendeleza.
Nilikuwepo....

Nenda kajisomee Azimio la Arusha.
 
Back
Top Bottom