Mkandara:
Unaboronga na unazidi ku-expose jinsi ujamaa ulivyokuwa product ya intellectual fraud.
Ujima hata wazungu wamepitia. Ni primitive form ya society yoyote. Hivyo compeleteness yake haitokani na maendeleo ya jamii bali na ugumu wa maisha katika jamii.
Hivyo advance form ya Ujima utaikuta kwa hadza, watindiga. Lakini huwezi kuikuta kwa wachagga au Wahaya. Hivyo basi huwezi kufikia level ya juu ya maisha kwa ku-copy characteristics za inferior level.
Tena basi angeweza pata tender Ikulu ya nyama choma toka Marekani..IMPORTED...heee heee hee!Angeweza hata kuvumbua mashine ya kuzi-recycle au kuzi-preserve further!
Pengine hakuwa na njaa wala kuwaza kesho yake atakula nini. Msosi ulikuwepo bwelele. Alikuwa na makazi yaliyo comfortable...hakung'atwa ng'atwa na mbu...etc
Uwingi wa chakula ni ishara ya prosperity. Huwezi ukawa na prosperity wakati watu wanakula mlo mmoja kwa siku.
Mimi juzi nimechoma minyama kibao hadi mingine nimetupa. Hiyo ndo prosperity bana...
I don't care whether it nullifies or validates....I care about inventions and innovations that will tame our environment.
If you care enough what are doing to make it happen - overeating and throwing minyama (imported from Mexico) in the bin (bought in the US) over a glass (made in China) of Heinekken (brewed in Holland)?
Zakumi,
Primitive form ya Watanzania ilikuwa nini?..
Hivi mnadhani kuvumbua ni kazi rahisi kaa kucheza mdundiko?
Kuna tofauti kati ya ku-copy (iga) na ku-adapt (tohoa). Nyerere alichofanya ni ku-adapt hasa baada ya kuona kuwa watu bado ni wajima. Ndio maana Rural and Social Development ambayo ni companion policy booklet ya Azimio la Arusha inasema hivi:
We must take our traditional system, correct it shortcomings, and adapt to its service the things we can learn from the technologically developed of other continents (Nyerere 1967: 4).
Nakula Angus beef. Umewahi kuisikia hiyo wewe? Na kuna ubaya gani kunywa Heineken made in China brewed in Holland? It's still the same Heineken, ain't it?
Vumbua ya kwako - kuna prototypes hizi huku Tz: Mnazi, Ulanzi, Mbege, Chibuku, Kangara, and the list goes on and on, kweli walevi ni wavumbuzi!
Kuna maana gani ya kumpa mwanafunzi wa chuo kikuu maisha mazuri kwa kipindi cha muda wa miaka mitatu wakati maisha yake ya primary school, sekondary school na yale anayoishi baada ya chuo yapo ovyo ovyo.
Haya ndio makosa makubwa ya nchi za kiAfrika. Kuwa na elite Universities wakati mambo mengine ni longolongo tu.
Maharage na makande wewe unaona ni vyakula vya maana?
Heheheee...umenikumbusha Masalo....wewe lazima utakuwa mtoto wa chuo wewe.
Kwikwikwi hizo ndio prosperity. Mwaka jana kulikuwa na ukama mkubwa Georgia. Lakini ukame huo haukufanya kuongezeka kwa bei ya chakula. Nyama watu waliendelea kula bila matatizo na umeme uliendelea kuwepo.
Mara nyingi inatokea drought hapa viwanja, lakini hakuna mtu anayeelewa kuwa ukame umetokea zaidi ya wakulima wachache ambao nao wanakamatishwa mshiko kufidia hasara.
Oya na wewe umesahau kuwa enzi za Azimio la Arusha kulikuwa na nyama za kusaza kutoka Tanganyika Packers na Ranchi za NARCO? Hao majamaa walikuwa wanakula mpaka sardines kwenye makopo na zile bifu za makopo! Usijifanye ulikuwa hupitii pale Cafeteria ukitoka shuleni kwako Mlimani Primary!
Zakumi,
Mkuu wangu umekataa niliposema Ujima yaani form ya maisha ya mwafrika ilikuwa collective work and responsibility..sasa nakuuliza wewe hiyo form ya maisha ya mwafrika unayoijua wewe ni ipi?.. kutembea uchi na mkuki mkononi au?
..we need to move on.
..Azimio will not come back as an entire documents.
..sehemu ndogo-ndogo za Azimio kama maadili ya viongozi, serikali kumiliki vyanzo vya kiuchumi, etc etc zinaweza kurudishwa.
..pia kuleta kitu kama maadili makali zaidi ya viongozi haimaanishi kurudisha azimio la arusha, kwani maadili hayo hapa Tanzania na hata duniani yakuanza na azimio.
Vipi tena mbona unaikana waziwazi bin laivu nadharia yako ya prosperity is the mother of inventions?