Azimio la Arusha: Kuzaliwa upya?

Mwanagenzi

JF-Expert Member
Sep 11, 2006
706
222
...Angalau kuna watu wanathamini Azimio la Arusha...

Kuna umuhimu kwa Watanzania (si serikali), wakiongozwa na jumuiya za kiraia, kutafakari upya umuhimu wa Azimio la Arusha.

==========

London group re-launches Arusha Declaration

MBONEKO MUNYAGA | Sunday News; Sunday,June 17, 2007

A LONDON group of publishers yesterday re-launched the Arusha Declaration as one of the key documents for the emancipation of man in the 20th century.

Mwalimu’s son, Madaraka is in London for the event and has been invited by the publisher, Mrs Selma James, who, with her husband, CLR James, was active in the movement for independence and federation in the Caribbean, which drew many lessons from the struggle in Africa.

Madaraka was expected to deliver a keynote speech about growing up as Mwalimu’s son and about the practical benefits of living in an Ujamaa village. Since the death of Mwalimu on October 14, 1999, Madaraka has stayed at Butiama, Mwalimu’s birth village largely taking care of the family estate.

The Arusha Declaration focuses on Ujamaa or ‘African brotherhood’, self-reliance and co-operation. It also strongly fights corruption by government or ruling party officials. The London event will also mark 50 years of the independence of Ghana and 60 years of Indian independence, landmarks in human liberation, the organisers said.
“Though it was written 40 years ago, it has not been surpassed as a perspective for development in the whole Third World,” said a dispatch from the organisers.

June 16 is African Child Day as well as Soweto Day when children in South Africa expressed their collective opposition to apartheid and the Boer regime responded by shooting tens of them down.

The Arusha Declaration guided Tanzania’s political thought and philosophy for nearly 20 years before the ruling CCM set it aside at a meeting in Zanzibar in early 1986 in favour of market policies.

However, many economic transformation programmes have gone back to massive social spending on education, health and water supply as Mwalimu had argued under his “The Purpose is Man” philosophy for the development of societies.

Mwalimu said he had read and re-read the document several times after it was set aside and still saw nothing to change, although, he said, if given a second chance, he would have done certain things differently.


 
Mwanangezi, Hoja ya nguvu hiyo!

Mwalimu aliwahi kusema (ilikuwa Mei 1 1995) kwamba; "unaweza kuwa na almasi, akaja tapeli akaichukua na kukuambia kuwa hilo ni jiwe, badala yake akakupa kipande cha chupa eti ndiyo almasi halisi na akachukua jiwe lako!"

Watanzania wengi; wakiwemo wanasiasa, inabidi wakumbuke kuwa hapo walipo, na hali waliyo nayo, ni matunda ya Azimio la Arusha.

Lakini kwa sababu ya ubinafsi, tamaa ya kujilimbikizia mali pamoja na ulafi uliokithiri; viongozi wetu walilitupilia mbali Azimio hili huko Zanzibar mwaka 1991.

Sasa miaka 17 baadaye, Tanzania bado ni masikini na hali za wananchi zinaendelea kuwa mbaya; na kwa wengi, ni mbaya zaidi ya ilivyokuwa wakati wa siasa za Azimio la Arusha.

Je, ni wanabodi wangapi bado wanaamini kuwa umasikini wetu ulitokana na azimio la Arusha? Sisa hiyo ilituongoza kwa miaka 23; sasa hivi ni miaka 17 tangu litupiliwe mbali, je, kuna anayefikiri kuwa ndani ya miaka 5 ijayo yutakuwa tumeondokana na umasikini?

Watanzania tuamke!
 
Sidhani kama CCM watakubali au hata kukiri kuwepo kwa Azimio hilo. Jinsi walivyolizika kula Zanzibar, jaribu lolot la kulifufua ni kama kwenda kumfukua mtu makaburini!

Tatizo ni kuwa Azimio la Arusha halikufanyiwa msiba unaotakiwa na matanga yake hayakuanuliwa.

Hivyo limebakika kama ndondocha, na kama msukule ambao sasa unataka kuja tena kuishi katika ulimwengu wa walio hai. CCM haina budi kulikana Azimio hili na kila kitu kilichotokana nacho kama Miiko ya Viongozi.

Sidhani kama CCM kwa akili yake timamu wanaweza kujadili merits za Azimio na mambo machache ambaye Azimio hilo la kifalsafa ya usawa wa watu wote na haki ya watu wote kupata vitu vya lazima kabla ya wachache kuishi katika anasa. Kufufuka kwa Azimio la Arusha, Mzimu wa watu wa kale?
 
Mwanangezi, Hoja ya nguvu hiyo!

Mwalimu aliwahi kusema (ilikuwa Mei 1 1995) kwamba; "unaweza kuwa na almasi, akaja tapeli akaichukua na kukuambia kuwa hilo ni jiwe, badala yake akakupa kipande cha chupa eti ndiyo almasi halisi na akachukua jiwe lako!"

Watanzania wengi; wakiwemo wanasiasa, inabidi wakumbuke kuwa hapo walipo, na hali waliyo nayo, ni matunda ya Azimio la Arusha.

Lakini kwa sababu ya ubinafsi, tamaa ya kujilimbikizia mali pamoja na ulafi uliokithiri; viongozi wetu walilitupilia mbali Azimio hili huko Zanzibar mwaka 1991.

Sasa miaka 17 baadaye, Tanzania bado ni masikini na hali za wananchi zinaendelea kuwa mbaya; na kwa wengi, ni mbaya zaidi ya ilivyokuwa wakati wa siasa za Azimio la Arusha.

Je, ni wanabodi wangapi bado wanaamini kuwa umasikini wetu ulitokana na azimio la Arusha? Sisa hiyo ilituongoza kwa miaka 23; sasa hivi ni miaka 17 tangu litupiliwe mbali, je, kuna anayefikiri kuwa ndani ya miaka 5 ijayo yutakuwa tumeondokana na umasikini?

Watanzania tuamke!

....siwezi kushawishika kuhusu kurudisha azimio la arusha,lakini najua wazi kuwa silo lililotuletea umasikini....kwani umasikini ni nini?....utendaji wetu mbovu na ambao umekuwa ukiendelea kila mwaka ndio unaotutia umasikini.

kwani,ilitushinda nini kujenga central road network[corridor ukitaka]mpaka katika miaka hii?....uzembe huu umechangia kutubakiza kwenye umasikini. hiyo barabara ni muhimu sana kwa maendeleo ya taifa hili....nadiriki kusema kuliko hata hii ya kaskazini ambayo ni nzuri miaka yote.

utaleta azimio hata la milele,lakini kama watu hawafanyi majukumu yao...bali kudokoa vijifedha ili wacheuwe bia,wazini,wajenge vitambi,na vijinyumba....hatutafika tunakokuota!

hatuhitaji azimio lolote kwa sasa,tunachohitaji ni kupunguza rushwa,kutenda majukumu yetu....na muhimu kuwa watu wepesi kujifunza na kufanya kazi bora zenye viwango!

asaalam aleykhum!
 
.....sidhani kama utakubali! kwa lengo lipi hasa? kuleta maendeleo au mkanganyiko?....kwasababu azimio la arusha ni pana....sasa tutaling'oa baadhi ya meno au?
 
Azimio la Arusha kurudi hapa Bongo?... Noooo way!

OVER THEIR DEAD BODIES!...
 
ANINA Stapelberg is the Marketing Manager of Shimansky Collection -- the firm that markets Tanzanite in South Africa for Tanzanite International. Ms Stapelberg answered Staff Writer BONIFACE BYARUGABA when he met her at their showroom in Cape Town last week...

Q. How do you describe Tanzanite to prospective customers?

A. It's the Rarest of the rare -- and a true celebration of Africa.

Q. Is that all?

A. We impress on the enquiring public and especially prospective customers that at one thousand times more rare than diamonds, tanzanite is the rarest precious gem of all. We caution that, found only along a 4-kilometre strip at the foothills of Mount Kilimanjaro, Tanzania, its allure is heightened by the fact that in 10 to 12 years, the gem will be completely depleted.

Tanzanite is found in shades of either deep royal blue or vibrant violets. The colour dominance depends on whether the gem is cut and polished from the long axis or the short axis of the crystal shaped rough tanzanite; and the more intense the colour the better the quality.

We believe at Shimansky and Tanzanite International that customers will find an extensive range of only the finest quality loose tanzanite and tanzanite jewellery, all certified for our esteemed customers' peace of mind.

We are also proud stockists of the exclusive brand, AYANDA, the Queen of Tanzanite.

Q. How strategically placed is your store?

A. Our Tanzanite International store is based in the Clock Tower, Victoria & Alfred Waterfront, which is the most famous -- and most visited -- tourist destination in South Africa. It offers a safe environment where tourists can walk freely and admire the many things this working harbour has to offer, including the departure point to Robben Island (ferry tours), our famous Aquarium, the Nelson Mandela Museum, and many famous restaurants and activities. The Clock Tower itself is in the Waterfront, and has become a historic landmark.

Q. Is this the only shop you have? Which other gemstones are you selling together with Tanzanite?

A. We have eleven stores in total under the Shimansky Group, with two specialized Tanzanite International stores. We also sell diamonds (in our Shimansky stores), which is our speciality, and a little bit of sapphire and other semi-precious gemstones, but tanzanite and diamonds are definitely our focus.

Q. How old is your establishment?

A. Our company is about 15 years old and our Tanzanite International store is about four years old now.

Q. How popular is the product in South Africa?

A. Tanzanite is very popular because of its rarity, and the fact that it is so unique. It has recently been classified as a Precious Gemstone and the Birthstone for December. It was first made popular by Tiffany's in the 70s and its popularity has grown rapidly since.

I think Tanzanians should be very proud of their gemstone as it's completely unique to Tanzania . It's a pity that Tanzania does not have the infrastructure to market it properly, but as South Africans we are helping our African neighbours to make the stone more popular, and to ultimately make more of its unique riches, and through this, support the people of Tanzania.
Q. Infrastructure? You cut the gems here?

A. We don't cut the tanzanite in Cape Town but we source it direct from the mines in Arusha, and have a specialist cutter who cut it for us. We cut only our diamonds ourselves -- in our two Diamond Cutting Factories. All the cut tanzanite gets carefully selected and graded at our factory in the Waterfront, and certified accordingly. All the jewellery pieces in which the tanzanite is set, is also hand made in our own factory.
Q. And your experience in this field? - don't understand this question???

A. Experience brilliance is the making at our flagship Shimansky showroom and workshops, situated at the Clock Tower. Here a customer can enjoy a personalized workshop tour where the customer will be able to view the art of diamond cutting and polishing and the process of jewellery manufacturing. But the highlight of the customer's tour is definitely our extensive range of exquisite hand made jewellery and the array of loose diamonds and tanzanite on display. A customer's selection of the perfect stone can also be manufactured in the design of the customer's choice and in as little as 24 hours if time is of the essence.

Q. How competitive are your prices?

A. Our prices offer extremely good value, as we cut out the middleman; we don't buy from gem dealers -- and because of our sheer buying power. And as I have indicated earlier, we have 11 stores in total under the Shimansky Group.

Q. You are confident, aren't you?

A. We have The Shimansky Promise. We feel that in this fast-moving age, we seldom have time to appreciate the real important things in life. Precious moments slip through our fingers. At Shimansky we recognise that the experience of buying fine jewellery should be as uniquely personal as the milestone it celebrates. For this reason we pride ourselves not only in our exquisite design, creation and materials, but also in being able to provide our customers with unrivalled individual attention, service and attention to detail.

For us, it is important that you treasure the memory of the moment as much as you treasure the jewellery piece itself. This is our promise to our customers.

Unaona jinsi tunavyoibiwa na kukejeliwa aisee. Eti tujivunie madini yetu huku faida yote ikienda Afrika ya Kusini. Mbaya zaidi ni kuwa huyu dada ana uhakika kuwa katika miaka kumi na mbili watatuachia mashimo matupu yasiyokuwa na kitu; halafu watu hapa wanadiriki kutuzuia tusihoji mambo haya. Kwa kuwa ni sisi tu wenye madini hayo tulitakiwa kuyatumia sawasawa ikiwa ni pamoja na kupanga bei kulingana na demand ya soko, kama ambavyo OPEC wanavyofanya. Lakini, watu wachache walipewa vijihela vya kujengea majumba ya kifahari wakasahau kuwa wako pale kwa maslahi ya Tanzania siyo yao. Watanzania wakanyanyaswa kufukuzwa pale mgodini kama mbwa. Liliofanyika leo miaka yote hii hamna. Ni kama kaburu Vorster alivyowahi kusema kuwa viongozi wa watu weusi ni vipunga sana; ukiwapa hela kidogo au mwanamke mweupe tu, wako tayari kabisa kukupa kila kitu chao hata kuwauza wenzao.

Hebu angalia kuwa jamaa hawa wameunda kampuni miaka minne tu iliyopita baada ya kupewa ulaji huo na serikali yetu, na leo hii wanatamba duniani kote, siyo Tanzania inayotamba. Siku moja nilifika duka la Kay's hapa mtaani kwetu na kukuta pete ya Tanzanite, (tena kipande kimoja tu kidogo sana) iko kweye sale inauzwa $4999, wakati ile ya diamond size hiyo hiyo ilikuwa inauzwa $1999. Pete ile ilikuwa kwenye kiboksi kimeandikwa Found only in Tanzania, Imported from South Afrika.

Kama kweli Azimio la Arusha lingekuwapo, viongozi wetu wasingekuwa na tamaa ya kujipatia mali kwa hiyo rushwa iliyotumika kuuza eneo la mererani isingefanyika na matokea yake Tanzanite ingekuwa ni kwa faida ya nchi yetu.

Ninaamini kuwa Azimio la Arusha bado ni relevant kabisa. Kuna mambo machache ya kubadilisha; kwa mfano, badala ya kusema tunajenga "nchi ya kijamaa na kujitegemea" tuseme tunajenga "taifa lenye kuthamini uhuru na maendeleo ya raia wake wote kwa msingi wa kujitegemea."

Vifungu vyote vya utaifishaji wa njia kuu za uchumi vibadilishwe vihusu serikali kuhakikisha kuwa misingi yote ya uchumi inandeshwa na makampuni ya umma ambayo hisa zake nyingi ziko mikononi mwa wanachi wenyewe. Kuwe na sheria nzito zinazosimamia distribution ya shares kusudi kuhakikisha kuwa njia hizi za uchumi haziko mikononi mwa watu wachache tu.

Mtu akitaka kuanzisha kampuni yenye mtaji wa kiwango fulani Tanzania aambiwe ruksa, lakini ahahikishe anatoa hisa kadhaa kuwa traded publicly na kwenye bodi ya kampuni kuna mwakilishi wa wanachi wenye hisa anayechaguliwa na wananchi wenyewe. Sina uhakika kama hii itafanya kazi sawasa lakini nadhani itasaidia sana kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya faida inabaki hapa hapa nchini. Tatizo liliofanywa na serikali ya Mkapa ni kule kuleta kampuni ya kigeni na kuwaambia wachukue shemeji yake kuwa partner. Serikali ijenge utaratibu mzuri wa kukusanya kodi kutoka kwenye makampuni haya bila kuruhusu loophole yoyote.

Kuhusu huduma za jamii, kama elimu, na afya, mambo yabaki vile vile kama ilivyo katika Azimio la Arusha, ila katika afya raia waweza kuchangia kwa namna ya kujinunulia dawa za bei nafuu kama vile Aspirini, multivitamins bendeji na vijidawa vidovidogo kama hivyo. Vile vile kwenye elimu, wanachi wawe wanachangia kwa kununua mahitaji ya shule kama madafali vitabu kalamu na kadhalika. Wakati wetu sisi tulipata kila kitu bure: vitabu, kalamu zile za kuchovya na wino wake, na kule mahospitalini kulikuwa na mtumizi mabaya ya madawa. Kuna watu walikuwa wakienda hospitali huku hawaumwi, hivyo wakipewa zile dawa Asprini wailikuwa wazitupa tu.

Hata hivyo, shule na hospitali za binafsi ziendelee kuwapo kama zamani ikiwa ni alternative kwa wale wasiotaka kutumia public services. Kwa mfano Marekani kuna shule za umma na shule za binafsi, ingawa swala la hosptiali za umma zimewashinda pamoja na kwamba zipo. Mtu anawaza kujichagulia atakavyo mwenywe.

Miiko ya uongozi inadikwe upya kuhakikisha kuwa mtu anayepata uongozi akiwa tajiri, basi utajiri wake uendelee kuheshimiwa lakini asitumie nafasi ya uongozi kurudufisha utajiri wake. Vile vile mtu akisha kuwa kiongozi tu basi transactions zote zinazofanywa na bishara zake ziwe subject to public scrutiny wakati wowote hata kama hamna sababu yoyote. Hii itasaidia sana kuhakikisha kuwa hakuna mfanya biashara anyeingia kwenye siasa kwa nia ya kunufaisha biashara zake. Kwa jumla wafanya biashara wengi wasiokuwa serious hawatapenda kazi za siasa katika mazingira hayo.
 
Hivi kati ya Azimio la Arusha na zile imani kumi za TANU kipi ni muhimu kurudishwa katika falsafa ya uongozi katika nchi yetu? Kwangu mimi nafikiri kufikiria kuwa Tanzania ya sasa inaweza kurudisha azimio la Arusha ni kushindwa kutambua nafasi ya nyakati na mazingira tuliyopo sasa.

Hata hivyo imani kumi za TANU ambazo ukweli ndizo zinapaswa kuwa Nguzo kuu za utaifa wetu bado zinatosheleza kurudisha some sense katika Tanzania yetu.

Tanzanianjema
 
Azimio la Arusha ndilo lililotudumaza watanzania kiasi kwamba hatuwezi kufanya biashara ya maana. vilevile Azimio hilo ndilo limesababisha viongozi wawe wezi wakubwa.

Wakati wa mkoloni Mabenki ama mtu yeyote yule alikuwa hana ruhusa ya kumkopesha mwafrika["native".] kulikuwa na sheria inaelekeza kwamba ukimkopesha mwafrika na akashindwa kulipa basi huna haki mbele ya sheria. hali hiyo iliwafanya waafrika wawe watazamaji tu katika suala zima la biashara/commerce.

Miaka sita baada ya Uhuru Nyerere akapitisha azimio la arusha. Hatua hiyo iliwakatisha tamaa Waafrika waliokuwa na elimu kujiunga na biashara.

Serikali ya TANU ilianzisha mpango wa Africanisation of Civil Service, sijui kwanini hakukuwa na Africanisation of Commerce and Industrial sectors. Sijui hata kwanini CCM iliyotokana na TANU inapinga sera ya Uzawa.

Azimio la Arusha ndiyo limetukwaza mpaka leo hii tunaogopa kumezwa na Wakenya. Azimio la Arusha ndiyo limesimika tabia ya wizi na rushwa miongoni mwa viongozi wetu.
 
Wanakijiwe wenzangu; samahani nimeishia kizani siku hizi kwa kutokana na kasi ya utafutaji wa ugali. Hata hivyo huwa napitia hapa mara moja moja sana. Hufurahi sana kukuta mada kemkem zikendelea, najua kijiwe bado kiko moto moto. Kilichonifanya leo nikae kitako usiku huu wa manane kuandika hapa ni jinsi makamu mwenyekiti wa CCM Mzee Msekwa alivyopotosha ukweli. Mzee huyu huwa namheshimu sana kwa vile ni kati ya wanasiasa wachache sana ambao ni intelectual katika mfumo wetu. Baada ya Mwalimu Nyerere, na Dr. Salim, nadhani aliyebaki mbele yangu ni huyu Mzee Msekwa. Katika hotuba yake pale Ubungo Plaza amedai kuwa Azimio la Zanzibar halikufuta Azimio la Arusha, na hiyo ndiyo iliyonikera na kusema niweke neno kidogo..


Azimio la Arusha lililopititishwa na kikao cha mkutano mkuu wa TANU uliokaa pale Arusha kuanzia mwishoni mwa Januari hadi Februari 5, 1967 liliazimia mambo kadhaa, mimi nakumbuka msingi wake mkuu ulikuwa ni maendeleo ya nchi. Azimio hile lilisema hivi: "Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne: watu, ardhi, siasa safi, na uongozi bora."
 1. Katika kuhakikisha kuwa tuna watu walio tayari kwa kuendeleza nchi, Azimio liliweka bayana kuwa ni lazima tupambane na ujinga, umasikini, magonjwa na dhuluma miongoni mwa raia wetu.

  Kwa hiyo:
  • Ili kupambana na ujinga, elimu ilitolewa bure kwa watu wote katika ngazi zote hadi kukawa na kampeini kutoa elimu ya watu wazima ambao hawakupata nafasi ya kwenda shule utotoni.
  • Katika kupambana na umaskini, ambapo nadhani ndipo tulipokokosea kidogo tu: nchi ilitia mkazo umilikaji wa njia kuu za uchumi na kuweka usimamizi imara wa matumizi ya raslimali zetu.
  • Magonjnwa yalipigwa vita kutoka kona mbili: prevention and cure. Mabwana afya waliajiriwa kusimamia uzuiaji wa magonjwa yanayoweza kuzilika, wakati waganga waliajiriwa kusimamia tiba ya magonjwa mbali mbali kabla hayajawa sugu. Kukawa na mabwana afya na watu waliojulikana kama RMA
  • Vita dhidi ya dhuluma ilikuwa pana sana kwa vile iliunganishwa na misingi ya uongozi kama nitakavyoiweka hapo chini.
 2. Kwa vile nchi ina ardhi kubwa sana, serikali ilihakikisha kuwa ardhi hii pamoja na raslimali zake havimilikiwi na watu wachache, bali ni kwa ajili ya watanzania wote. Ndipo ardhi yote ilipotangazwa kuwa ni mali ya Taifa, na yale mashamba makubwa makubwa ya makapuni binafsi yakataifishwa.

 3. Siasa safi iliyotangazwa na Azimio lile ilikuwa ni ile ya ujamaa na kujitegemea. Mwalimu Nyerere alikuwa amejifunza kuwa hakuna "mjomba" wa kukusaidia kutimiza malengo yako hasa baada ya uzoefu aliokuwa ameupata kutokana na misukosuko iliyopelekea mauaji ya Patrice Rumbumba kule Congo 1961, Ubomoaji wa barabara zilizojengwa na wajerumani pale Dar kufuatia muungao wa Tanzania 1964, na msukosuko uliokuwa umetokana na Marekani kutaka tuutambue uhuru bandia wa Southern Rhodesia (Zimbambwe) wa 1966 chini ya Ian Smith. Hata hivyo siasa hii ya ujamaa ilitangazwa kama njia ya kumfanya mtanzania awe huru zaidi.

 4. Kingwamba cha azimio la Arusha kilikuwa kwenye uongozi bora. Azimio hili liliweka misingi imara ambayo mtu alitakiwa aikamilishe sawasawa ili akubalike kama kiongozi. Misingi hii yote ilikuwa na lengo la kuhakikisha kuwa kiongozi anasimamia ufanisi yale yote yaliyotajwa hapo juu. Zaidi ya yote, asitumie madaraka yake kama namna ya kujipatia au kujiongezea utajiri. Misingi hii iliunganisha na ule msingi unaopinga dhuluma kwenye jamii ikiwa inajumuisha aina zote za rushwa. Kulikuwa na Imani ilyosema, "Cheo ni dhamana, sitakitumia cheo chengu kwa manufaa binasfi." Nyingine ilikuwa inasema "rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa."

  Yote haya kwa pamoja yalijulikana kama miiko ya uongozi.

Azimio la Arusha lote lilichukuliwa kama nguzo ya ujenzi wa Taifa baada ya CCM kuzaliwa. Hata hivyo, mwishoni mwa miaka ya themanini, chini ya Rais Mwinyi, Chama cha Mapinduzi kilikaa kule Zanzibar na kuamua kufuta miiko yote ya uongozi iliyokuwa imewekwa na CCM, hivyo kufanya iwe ni halali kwa kiongozi kutumia madaraka yake kujipatia au kujiongezea mali. Ikawa ni halali kabisa kwa kiongozi wa serikali kuchukua "mkopo" pale NSSF kwa ajilia ya kujenga nyumba ambayo baadaye angeweza kuipangisha kwa meneja na NSSF kwa kodi yoyote ile. Uvunjaji huu wa miiko ya viongozi uliwaacha viongozi hawana la kuogopa na na ndipo hapo tulipoona msingi mmoja mmoja wa Azimio la Arusha ukifa. Leo hii tunasikia jinsi watoto wanavyofukuzwa shule kwa kukosa karo (Ukraine), tumesikia jinsi watu wasivyopata matibabu pale Muhimbili bila kulipia chochote au kwenda Tumaini, tumesikia jinsi watu wanavyohamishwa ardhi yao kwa nguvu ili kupisha makapuni ya madini. Yote hayo ni matokeo ya Azimo la Zanzibar na ni kinyume na matakwa ya Azimio la Arusha.


Kwa mtu yeyote anayejua maana ya uongozi wakati wa TANU na CCM first generation atajua wazi kuwa uongozi tuliojenga baada ya Azimio la zanzibar ni tofauti kabisa na ule uliokuwapoa chini ya Azimio la Arusha. Inawezekana kabisa kuwa uongozi wa zamani ulikuwa na dosari zake, lakini, nashindwa kukubaliana na Mzee Msekwa anaposema kuwa Azimio la Zanzibar liliimarisha misingi ya Azimio la Arusha kwa vile maazimio haya mawili hayakuwa yanalenga kitu kimoja. Lile la Arusha lilikuwa linalenga maendeleo ya nchi wakati lile la Zanzibar lilikuwa linalenga maendeleo ya viongozi.
 
Wanakijiwe wenzangu; samahani nimeishia kizani siku hizi kwa kutokana na kasi ya utafutaji wa ugali. Hata hivyo huwa napitia hapa mara moja moja sana. Hufurahi sana kukuta mada kemkem zikendelea, najua kijiwe bado kiko moto moto. Kilichonifanya leo nikae kitako usiku huu wa manane kuandika hapa ni jinsi makamu mwenyekiti wa CCM Mzee Msekwa alivyopotosha ukweli. Mzee huyu huwa namheshimu sana kwa vile ni kati ya wanasiasa wachache sana ambao ni intelectual katika mfumo wetu. Baada ya Mwalimu Nyerere, na Dr. Salim, nadhani aliyebaki mbele yangu ni huyu Mzee Msekwa. Katika hotuba yake pale Ubungo Plaza amedai kuwa Azimio la Zanzibar halikufuta Azimio la Arusha, na hiyo ndiyo iliyonikera na kusema niweke neno kidogo..


Azimio la Arusha lililopititishwa na kikao cha mkutano mkuu wa TANU uliokaa pale Arusha kuanzia mwishoni mwa Januari hadi Februari 5, 1967 liliazimia mambo kadhaa, mimi nakumbuka msingi wake mkuu ulikuwa ni maendeleo ya nchi. Azimio hile lilisema hivi: "Ili tuendelee tunahitaji vitu vinne: watu, ardhi, siasa safi, na uongozi bora."
 1. 1. Katika kuhakikisha kuwa tuna watu walio tayari kwa kuendeleza nchi, Azimio liliweka bayana kuwa ni lazima tupambane na ujinga, umasikini, magonjwa na dhuluma miongoni mwa raia wetu.

  Kwa hiyo:
  • Ili kupambana na ujinga, elimu ilitolewa bure kwa watu wote katika ngazi zote hadi kukawa na kampeini kutoa elimu ya watu wazima ambao hawakupata nafasi ya kwenda shule utotoni.
  • Katika kupambana na umaskini, ambapo nadhani ndipo tulipokokosea kidogo tu: nchi ilitia mkazo umilikaji wa njia kuu za uchumi na kuweka usimamizi imara wa matumizi ya raslimali zetu.
  • Magonjnwa yalipigwa vita kutoka kona mbili: prevention and cure. Mabwana afya waliajiliwa kusimamisa uzuiaji wa magonjwa yanayoweza kuzilika, wakati waganga waliajiliwa kusimamia tiba ya magonjwa mbali mabli kabla hayajawa sugu. Kukawa na mabwana afya na watu waliojulikana kama RMA
  • Vita dhidi ya dhuluma ilikuwa pana sana kwa vile iliunganishwa na msingi ya uongozi kama nitakavyoiweka hapo chini.
 2. Kwa vile nchi ina ardi kubwa sana, serikali ilihakikisha kuwa ardhi hii pamoja na raslimali zake havimilikiwa na watu wachache, bali ni kwa ajili ya watanzania wote.

 3. Siasa safi iliyotangazwa na Azimio lile ilikuwa ni ile ya ujamaa na kujitegemea. Mwalimu Nyerere alikuwa amejifunza kuwa hakuna "mjomba" wa kukusaidia kutimiza malengo yako hasa baada ya uzoefu aliokuwa ameupata kutokana na misukosuko iliyopelekea mauaji ya Patrice Rumbumba kule Congo 1961, Ubomoaji wa barabara zilizojengwa na wajerumani pale Dar kufuatia muungao wa Tanzania 1964, na msukosumoko uliokuwa umetokana na Marekani kutaka tuutambue uhuru bandia wa Sothern Rhodesia (Zimbambwe) wa 1966. Hata hivyo siasa hii ya ujamaa ilitangazwa kama njia ya kumfanya mtazania huru zaidi.

 4. Kingwamba cha azimio la Arusha kilikuwa kwenye uongozi bora. Azimio hili liliweka misingi imara ambayo mtu alitakiwa akikamilishe sawasawa ili akubalike kama kiongozi. Misingi hii yote ilikuwa na lengo la kuhakikisha kuwa kiongozi anasimamia ufanisi wa yale yote yaliyotajwa hapo juu. Zaidi ya yote, asitumie madaraka yake kama namna ya kujipatia au kuijiongeza utajiri. Misingi hii iliunganisha ni ule msingi unapinga dhuluma kwenye jamii ikiwa inajumuisha aina zote za rushwa. Yote kwa pamoja ilijulikana kama miiko ya uongozi.

Azimio la Arusha lote lilichukuliwa kama nguzo ya ujenzi wa Taifa baada ya CCM kuzaliwa. Hata hivyo, mwishoni mwa miaka ya themanini, chini ya Rais Mwinyi, Chama cha Mapinduzi kilikaa kule Zanzibar na kuamua kufuta miiko yote ya uongozi iliyokuwa imewekwa na CCM, hivyo kufanya iwe ni halali kwa kiongozi kutumia madaraka yake kujipatia au kujiongezea mali. Ikawa ni halali kabisa kwa kiongozi wa serikali kuchukua "mkopo" pale NSSF kwa ajilia ya kunjega nyumba ambayo baadaye angeweza kuipangisha kwa meneja na NSSF kwa kodi yoyote ile. Uvunjaji huu wa miiko ya viongozi uliwaacha viongozi hawana la kuogopa na na ndipo hapo tulipoona msingi mmoja mmoja wa Azimio la Arusha ukifa. Leo hii tunasikia jinsi watoto wanavyofukuzwa shule kwa kukosa karo (Ukraine), tumesikia jinsi watu wasivyopata matibabu pale Muhimbili bila kulipia chochote au kwenda Tumaini, tumesikia jinsi watu wanavyohamishwa ardhi yao kwa nguvu ili kupisha makapuni ya madini. Yote hayo ni matokeo ya Azimo la Zanzibar na ni kinyume na matakwa ya Azimio la Arusha.
Kwa mtu yeyote anayejua maana ya uongozi wakati wa TANU na CCM first generation atajua wazi kuwa uongozi tulijenga baada ya Azimio la zanzibar ni tofauti kabisa na ule uliokuwapoa chini ya Azimio la Arusha. Inawezekana kabisa kuwa uongozi wa zamani ulikuwa na dosari zake, lakini, nashindwa kukubaliana na Mzee Msekwa anaposema kuwa Azimio lka Zanzibar liliimarisha misingi ya Azimio la Arusha kwa vile maazimio haya mawili hayakuwa yanalenga kitu kimoja. Lile la Arusha lilikuwa linalenga maendeleo ya nchi wakati lile la Zanzibar lilikuwa linalenga maendeleo ya viongozi.

Mh Kichuguu!

Ukisoma hotuba ya Rais Mwinyi baada ya Azimio la Zanzibar, utaona kwamba kinachotendeka si kile walichoazimia kule. Zanzibar walilegeza kidogo masharti ya viongozi kumiliki mali.. kumbe ndo ikawa fungulia mbwa... jamaa wakaanza kukomba kwa kisingizio cha Azimio la Zanzibar.

Makamu Mwenyekiti Mh. Msekwa anaweza kuwa sahihi kwenye hili.. ila matendo ya viongozi yanawasuta. Sawa na Mafarisayo wa kipndi cha Yesu.." Fanyeni tunayosema.. msitende tunayotenda!"

CCM inahitaji reform kwenye policy zake!

Nilitarajia kwenye mabadiliko ya katiba ya CCm ya mwaka huu wangefanya reform ya hali ya juu, lakini bado wamekazania kufanya mabadiliko ya ku-recycle viongozi.. na kuwafanya wabaki madarakani kijanja hadi wakati wa kufa kwao!
 
Mh Kichuguu!
Ukisoma hotuba ya Rais Mwinyi baada ya Azimio la Zanzibar, utaona kwamba kinachotendeka si kile walichoazimia kule. Zanzibar walilegeza kidogo masharti ya viongozi kumiliki mali.. kumbe ndo ikawa fungulia mbwa... jamaa wakaanza kukomba kwa kisingizio cha Azimio la Zanzibar.

Makamu Mwenyekiti Mh. Msekwa anaweza kuwa sahihi kwenye hili.. ila matendo ya viongozi yanawasuta. Sawa na Mafarisayo wa kipndi cha Yesu.." Fanyeni tunayosema.. msitende tunayotenda!"
CCM inahitaji reform kwenye policy zake!
Nilitarajia kwenye mabadiliko ya katiba ya CCm ya mwaka huu wangefanya reform ya hali ya juu, lakini bado wamekazania kufanya mabadiliko ya ku-recycle viongozi.. na kuwafanya wabaki madarakani kijanja hadi wakati wa kufa kwao!

Kuna mtu yeyote mwenye Azimio la Zanzibar, ama hotuba hiyo ya Mwinyi Baada ya Azimio la Zanzibar? Mwenye uwezo wa kuvipata hivyo vitu atuwekee hapa tafadhali.

Natanguliza shukrani.
 
Kichuguu,

Karibu mkuu wangu karibu tena!

Unajua mwaka jana kulikuwa na maonyesho ya Utalii kule Montreal. Serikali yetu ilituma wajumbe wake kuja itangaza Serengeti na Ngorongoro. Maajabu ya Mussa ni kwamba hawa viongozi wetu walikuwa na kadi zao binafsi za kampuni zao za kitalii kwa hiyo kila mzungu aliyekuwa interested alipigwa na kadi hiyo na wakaambiwa ukitaka kuja Tanzania njoo nione mimi nina kambuni yangu pembeni itakupa deal nzuri sana (at the cost ya kodi yako).

Sasa wewe nambie hapa kweli hilo Azimio la Zanzibar linajenga nchi ama linajenga matumbo yao. NI vigumu kabisa kwa mzee Mzee Msekwa kuweza kuyaona haya ambayo huchezwa behind the scene na hata siku moja hawatakuelewa ikiwa huyo mtalii nia yake ni kuja Tanzania. Kwa mtazamo wao - Who gets the money isn't important maadam mtalii kaingia nchini. Huu ndio upeo wa viongozi wengi na hata wale wanaounga mkono hawaoni nje ya box hili.

Huwezi kuamini hata waziri aliyeambatana na kikosi hicho alikwenda zake huko Vancouver kutembelea ndugu na jamaa zake akawaacha jamaa ktk vibanda vyao vya maonyesho hadi siku ya kuondoka. Hotel waliyokuwa wakikaa hawa jamaa wali chargiwa 175 ka siku lakini invoice ya viongozi wetu ktk hotel hiyo hiyo ilikuwa ni zaidi ya dollar 1000 kwa siku.

Hii ndio tofauti kubwa kati ya Azimio la Arusha na Azimio la Zanzibar inapofikia ktk uwanja wa mapambano - that is "Reality"!
 
Mkuu Kichuguu,

Shukrani kwa darasa la nguvu. Azimio la Arusha lilishazimwa siku nyingi; Azimio la Zanzibar lilichofanya ni kuongoza mazishi, kisomo na hitma ya Azimio la Arusha.

Mkuu Mkandara,

Shukrani kwa mfano hai ambao ni kielelezo tosha.
 
Duuhh Prof Kichuguu

Karibu tena,

Bob Mkandara, Kumbe ndio maana.........utalii Tanzania haukuwi!!! duuhh...................hapa solution tunahitaji kiongozi JASIRI wa kulirudisha Azimio la Arusha period.
 
Duuhh Prof Kichuguu

Karibu tena,

Bob Mkandara
Kumbe ndio maana.........utalii Tanzania haukuwi!!! duuhh...................hapa solution tunahitaji kiongozi JASIRI wa kulirudisha Azimio la Arusha period.

Kubomoa ni rahisi sana, kujenga.
 
Kuna mtu yeyote mwenye Azimio la Zanzibar, ama hotuba hiyo ya Mwinyi Baada ya Azimio la Zanzibar? Mwenye uwezo wa kuvipata hivyo vitu atuwekee hapa tafadhali.

Natanguliza shukrani.

MAAMUZI YA ZANZIBAR, 1991


HOTUBA YA MWENYEKITI WA CCM, RAIS ALI HASSAN MWINYI WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAZEE WA CHAMA, VIONGOZI WA TAIFA, MASHIRIKA YA UMMA NA WATU BINAFSI JUU YA UFAFANUZI WA MAAMUZI YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA KATIKA KIKAO CHAKE CHA ZANZIBAR: DIAMOND JUBILEE DAR ES SALAAM, TAREHE 25/2/1991


Ndugu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Mkoa wa Dar es Salaam,
Ndugu Katibu Mkuu,
Ndugu Mwenyekiti wa Wazee wa Dar es Salaam,
Ndugu Viongozi wa Chama na Serikali na
Ndugu zetu waalikwa,

Kabla ya yote, labda niseme kwamba kwa kuwa tumo katika mwezi wa pili tokea kuanza kwa mwaka mpya, nami sijapata nafasi ya kukutana nanyi wazee, na vyema nitumie nafasi hii kwanza kukutakieni heri ya mwaka mpya, na baraka zote za mwaka 1991. (Makofi). Ninakuombeeni uzima, nguvu, baraka na mafanikio.

Pili, tuna kawaida katika nchi yetu, kwamba kila linapotokea jambo muhimu katika Taifa, tunatafuta nafasi ya kukutana nanyi na kukuelezeni. Hivyo, leo napenda kuzungumza nanyi wazee wa dar es Salaam na, kupitia kwenu, iwe ninazungumza na Wazee wenzenu wa tanzania nzima. Kwa hiyo, hayo nitakayokuambieni nyinyi, ninawaambia pia Wazee wa Taifa letu wote kwa jumla.

Hivi karibuni Halmashauri Kuu ya Taifa ilifanya kikao chake cha kawaida Zanzibar, ambacho kilijadili mambo mbalimbali. Kikao hicho kilimalizika kwa kutoa maamuzi maalum. Maamuzi hayo yana uzito mkubwa. Inaelekea baadhi yetu, pamoja na vyombo vyetu vya Habari, hatukuyaelewa vizuri maamuzi hayo. Kwanza, nataka nivivue na lawama Vyombo vyetu vya Habari. Maana hatukuwa nao huko. Kwa hivyo walitangaza vile walivyoelewa. Kwa sababu hiyo nimeona ni vyema kuzungumza nanyi ili kusahihisha matangazo ya vyombo vyetu. Nimeona ni vyema kutumia nafasi hii kutoa ufafanuzi.

LAZIMA TWENDE NA WAKATI

Inaelekea kuna hofu kwamba Azimio la Arusha linageuzwa. Kwa hiyo, tokea mwanzao, kabla ya kusema lolote, nataka tuelewane kwamba siasa yetu bado ni ile ile ya Ujamaa na Kujitegemea. (Makofi). Haikugeuka wala hatutazamii kuigeuza. Kwa hali yoyote sisi Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi hatutaigeuza Siasa hii. (Makofi) . Kule Zanzibar tulizungumza mambo mengi, miongoni mwao, ni kutoa tafsiri ya baadhi ya vipengele vya Azimio ili vifanane na wakati tulionao.

Azimio la Arusha, kama tunavyojua, limetangazwa mwaka 1967. Hii leo tuko katika mwaka 1991. Imepita miaka mingi, zaidi ya 20 tokea kutangazwa kwa Azimio la Arusha. Na katika kipindi cha miaka 20 yametokea mabadiliko mengi duniani na pia katika hali ya maisha yetu. Hali yetu ya sasa, hasa ya kiuchumi, siyo ile ile ya mwaka 1967. Ndio maana mishahara ya wafanyakazi ingawa imeongezeka sana lakini bado haikidhi mahitaji yao - haiwatoshi hata wale wanaopokea mishahara mikubwa miongoni mwetu. Isitoshe, wakati wa Azimio idadi ya Watanzania ilikuwa ndogo. Sasa hivi idadi yetu imeongezeka zaidi ya mara mbili. Kwa sababu ya wingi wetu mahitaji yetu nayo yemeongezeka sana, wakati mapato yetu yamekuwa yakipungua wakati wote.

Kwa hivyo ni dhahiri kwamba jamii ya Tanzania lazima itie maanani mabadiliko haya na ijiandae kwenda na wakati. Kama hatukwenda na wakati, kazi yetu itakuwa ni kufukuzia wakati - jambo ambalo hatulimudu.

Tabia ya wakati ni kama ile ya bahari. Bahari inakupwa na kujaa mapaka ukiongoni mwa maji. Baadaye maji hukupwa polepole, mpaka kufika wakati ikawa maji yote yamekwishaondoka ufukoni. Samaki werevu huondoka nayo hayo maji, yaani yakijaa huja nayo, yakitoka kutoka nayo, vinginevyo hupwelewa. Samaki watakaozembea kufuta maji watajikuta wamechelewa wanatapatapa juu ya mchango wakati maji hayo hayapo. Hiyo ndiyo maana ya kupwelewa (Makofi).

Hapa Afrika, kwa mfano, imeanzishwa mipango mbalimbali ya ushirikiano wa uchumi. Mipango hiyo ni pamoja na Ushirikiano wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADCC) na Eneo la Soko Nafuu (PTA). Afrika pia imeazimia kuunda Jumuiya ya Uchumi. Nchi zinazoendelea nazo zimedhamiria kuzidisha ushirikiano miongoni mwao. Nchi yetu lazima ifanye mabadiliko ili iweze kushiriki kwa ukamilifu katika shughuli zote hizo zinazosaidia maendeleo yetu.

KILA ZAMA NA MWONGOZO WAKE

Ndugu Wazee, Msahafu wa Waislam unasema ‘LIKULLI AJALIN KITABU” Mwingereza mmoja kaitafsiri aya hiyo hivi: ‘ TO EVERY AGE ITS BOOK” yaani “Kila zama ina Kitabu (Mwongo) chake”. Na sisi Wana-CCM tunakubali kuwa “kila Zama zinahitaji kuwa na Mwongozo wake”. Azimio la Arusha ni Mwongozo wetu wa msingi. Ni dira inayoongoza mwelekeo wa jamii yetu. Lakini tafsiri zake zinabidi zirekebishwe kila inapohitajika ili zisipitwe na wakati. Miongozo ina tabia moja: inakuja ili kufafanua, kuelekeza au kukemea hali mbaya inayojitokeza.

Mojawapo ya malengo ya maamuzi ya Zanzibar ni kutoa tafsiri sahihi ili kupunguza kebehi inayofanywa dhini ya siasa yetu ya Ujamaa na Kujitegemea na pia kwenda na wakati.

Mwaka 1967 lilitangazwa Azimio la Arusha. Mwaka 1971 ulifuatiwa na tamko la Iringa la “Siasa ni Kilimo”. Tamko hili lilikuwa ni mbinu na msisitizo wa Siasa yetu ya Kujitegemea. Zlilipanua tafsiri ya Azimio la Arusha. Katika mwaka 1981 ilionekana kuna haja ya kutolewa mwongozo mwingine kulingana na wakati ule ambao nao ni upanuzi wa tafsiri ya Azimio. Ulitangazwa ili kukidhi haja ya wakati ule.

Aidha, kabla ya hapo, katika mwaka 1974, Chama kilipitisha Agizo la Musoma kuhusu Elimu ya Kujitegemea ambalo madhumuni yake yalikuwa kutazama upya suala la uingizaji wanafunzi Chuo Kikuu na kupanua Elimu ya Msingi ili kutoa fursa kwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule kufanya hivyo.

Maandiko yote hayo hayakupingana na Azimio la Arusha ila yakiongeza mwangaza kwa mambo ambayo yalihitaji yafanane na wakati wake. Na lazima iwe hivyo, kwani bila ya kwenda na wakati tungechekesha.

Kwa mfano wakati wa Azimio la Arusha, mtakumbuka kuwa tafsiri ya neno Kiongozi ni pamoja na yule mwenye mshahra uliofikia shilingi 1,066/= kwa mwezi. Tungeng’ang’ania tafsiri hii tu, basi leo pasingekuwapo wafuasi. Wafanyakazi wote wangetafsirika kuwa ni viongozi wa CCM. Kwani ukiacha wakulima wafanyakazi wote sasa kwa tafasiri ya 1987 ni viongozi tena maradufu. Maana kima cha chini sasa ni Sh.2,500/=, ambazo ni zaidi ya mara mbili ya Sh.1,066/=. Ndiyo maana tukasema jamii yetu italazika Kufanya marekebisho kila inapokuwa lazima kufuatana na wakati. Tutafanya hivyo bila ya kuachana na misingi ya siasa yetu.

Kwa hivyo, tulichokifanya kule Zanzibar ni kupanua tafsiri za Azimio ili ilingane na wakati tulionao. Kufanya hivyo si kuua Azimio bali ni kuliimarisha.

CHIMBUKO LA AZIMIO LA ARUSHA

Historia ya Azimio la Arusha tunaijua sote. TANU ilipigania kwa maneno mpaka nchi ikapata UHURU wake. Tanganyika ilipopata Uhuru na tukaanza kujitawala ishara potofu zilianza kuchomoza. Baadhi ya Viongozi walianza kuutumia uongozi wao kama mradi wa kujineemesha. Kwa kutumia nyadhifa zao, wakikopa fedha benki na kuanza kujijengea mashamba - si ya miti - bali ya majumba; si nyumba za kuishi tu bali majumba mengi ya kupangisha.

Tabia hiyo ilizusha manung’uniko ya watu. Jamii ilianza kugawanyika makundi mawili; manaizi na makabwela. Kitendo hicho ndio chimbuko la kutangazwa kwa Azimio la Arusha. Azimio lilikuja kutoa mwongozo wa maadili ya wanachama na viongozi wa TANU. Kwa hivyo nia ya Azimio la Arusha, miongoni mwa mambo mengine, ilikuwa ni kuwazuia viongozi kutumia uongozi wao kujitajirisha. Hilo ndilo lililokuwa tatizo la hatari miongoni mwa matatizo wakati ule. Azimio lilikuja kuokoa jahazi - kukemea tabia potofu.

ATATIZO LA SASA NI UCHUMI TEGEMEZI

Mtu anaweza kuuliza je sasa kuna tatizo gani? Tatizo letu katika miaka ya tisini na kuendelea ni lile la uchumi tegemezi. Tatizo letu sasa ni kwamba uchumi wetu ni duni mno. Wakati idadi yetu inaongezeka, mapato ya Taifa, hasa ya fedha za kigeni, hayaongezeki. Wakati wa Uhuru idadi yetu ilikuwa ni watu milioni tisa. Lakini leo, tuko milioni tisa na tisa tena na nusu ya tisa. Lakini mapato yetu ya pesa za kigeni yapo pale pale, $ milioni 400. Wakati Azimio la Arusha lilitutaka tujitegemee, hali halisi ni kuwa tumekuwa wategemezi wakubwa. Maana Taifa letu hizi sasa, kwa pato lake lenyewe la fedha za ndani, linaweza kujitegemea kwa kipindi cha miezi saba tu katika mwaka. Tunategemea watu wengine, kwa njia ya ruzuku na mikopo, kumalizia miezi mitano inayosalia katika mwaka. Hii ni hatari. Lazima tunendelee kubuni mbinu za kuondokana na hali hiyo.

MBINU ZA KUJITEGEMEA

Ilani ya Uchaguzi inasema hivi:

“Makusudi ya Chama katika kipindi cha miaka mitano ijayo ni kwa Taifa kukusanya nguvu zote za wananchi kwa kusaidiana na Serikali zao (Mbili), na kuzitumia katika kila eneo la maendeleo ili kutoa msukumo mpya wa utekelezaji wa siasa ya Ujamaa na Kujitegmea”.

Hivyo, Chama na Serikali zake zinawajibika kuwarahisishia wananchi wao kujitegemea kwa chakula, kujitegemea kwa mavazi na kujitegemea kwa malazi. Ili kutimiza lengo hilo Taifa lazima liwawezeshe wananchi wake kuzalisha mazao ya biashara na chakula kwa wingi. Pia ni wajibu wa Chama na Serikali kuandaa mbinu za kuwasaidia wananchi kujijengea nyumba zao za kuishi ili ziwasitiri wanapostaafu au kuwa wazee.

Je wananchi wakituuliza: hivi ni mbinu gani mlizofanya kumshirikisha kila mmoja wetu kutumia nguvu zake zote katika kuzalisha kama Ilani inavyosema? Tungejibu nini? Lakini sasa kila mwananchi, pamoja na mwana CCM, hataweza kutoa kisingizio kwa kusema:-

“Mimi sikuweza kutumia nguvu zangu zote katika kufanya kazi ya kuzalisha kwa sababu nimezuiwa na Azimio la Arusha.”

MWANACHAMA KUCHANGIA UCHUMI KIKAMILIFU

Azimio la Arusha lipo. Narudia tena kusema kuwa wanaohusika na tafsiri hii ni wanachama. Sisemi Viongozi, bali wanachama wa CCM. Tunataka kumpa Mwanchama wa CCM, kama mwanachama mwingine yeyote, uhuru zaidi wa kuzalisha ili kuchangia kadiri ya uwezo wake katika pato lake yeye mwenyewe na pato la Taifa Kwa jumla.

Ili tujitoe, kitaifa, kwenye shimo la utegemezi tulimo hivi sasa, mbinu bora ni kutoa uhuru kwa kila mwananchi wa kila Kaya, wa kila Kata, wa kila Tarafa, wa kila Wilaya na wa kila Mkoa kutumia nguvu zake zote katika kuzalisha. Matokeo ya hatua hii ni kumwezesha kila mtu katika Kaya, Kata, Tarafa, Wilaya na Mkoa kujigemea. Tukifika hapo ndipo Taifa litapokuwa limeondokana na hali ya sasa ya uchumi tegemezi.

KUPANGISHA NYUMBA

Jambo la kupangisha nyumba nalitaja tu, kwani si lazima kwa sababu si jipya; hata hivyo ni vyema nalo litajwe. Mwenyekiti Mstaafu alilisemea jambo hili mahali pengi sana, tena alianza zamani kulisemea, sijui. Kwa mfano, hivi karibuni alilitaja tena katika hotuba yake ya kuadhimisha miaka ishirini ya Azimio aliposema hivi:

“Nasharti hayo yanamkataza kiongozi wetu kuishi kikabaila kwa mbinu za kupangisha majumba.

Lakini sharti hili halimkatazi mtu mwenye vyumba vya ziada katika nyumba yake anamoishi kuvipangisha kwa watu wengine kwa kodi nafuu, Hili ni jambo la kawaida kabisa katika nyumba zetu za “Waswahili”’ na upangishaji huu mimi nimekuwa nikiutetea tangu zamani. Utaratibu huu unawasaidia sana watu wenye mapato madogo, wanafunzi, au wafanyakazi ambao bado hawajaoa au kuolewa kupata vyumba vya kupanga kwa kodi nafuu.

Ni kweli kwamba huko nyuma tumekuwa wakali mno katika kutafsiri msharti haya.

Azimio la Arusha linachokataa ni unyonyaji. Hivyo maskini ya Mungu mwenye kijumba chake cha mbavu za mbwa akimwona maskini mwenziwe anapata taabu, hana pakukaa, asimpangishe? Je akimpangisha atakuwa anamnyonya? Au anamstiri? Kwa hiyo tangu zamani kustiriana ni ruhusa (Makofi).

Hatukuishia hapo kule Zanzibar, tulikwenda zaidi, tulisema pia kwamba wapo viongozi miongoni mwetu ambao baadhi yao wamefanya kazi za Chama au za Serikali kwa miaka 30 au zaidi. Lakini hawana nyumba; ukifika wakati wao wa kustaafu viongozi hao huwa wanababaika kwa kutojua wataishi wapi. Ndipo wanapoanza kutafuta mbinu - ndiyo maana siku hizi utakuta misururu mirefu katika Ofisi ya Vyeti vya kuzaliwa. Watu wanakwenda kubadilisha tarehe zao za kuzaliwa, kujifanya bado wangali vijana ili wachelewe kustaafu. (Makofi).

Sisi tunaamini kwamba baada ya kipindi kirefu cha utumishi, mtu aweze kuwa na nyumba ili, hata akiwa kipofu angalau aweze kupapasa kuta zake na kusema: Hii ni nyumba yangu niliyoipata kwa jasho langu la kazi ya miaka 30. Tunataka awe na kitu. Lakini, Ndugu Wazee, bahati nzuri wanachama wa CCM, kama wananchi wengine, wanaruhusiwa kukopa. Wanaweza kukopa kwenye benki zetu wakajenga nyumba za kukaa. Sasa jamani tukisema kwamba hata mtu aliyekopa asiipangishe nyumba hiyo atalipia nini huo mkopo?

Vinginevyo tutakuwa tunamfanyia mzaha mtu huyo. Maana atachukua mkopo, ajenge nyumba, kisha ashindwe kulipa huo mkopo. Waliomkopesha wataikama hiyo nyumba na kuiuza ili kurudisha fedha yao. Katika hali hiyo mwana-CCM gani atakayekuwa na nyumba iwapo mwisho wake ni kuchukuliwa na kile chombo kilichomkopesha? Kwa hivyo nasema mtu kama huyu ana dharura; ana dharura ya deni. Amejenga nyumba kwa nia ya kukaa mwenyewe lakini ana deni la mkopo. Kama anaweza kukaa nyumbani mwake, akae. Lakini pia awe na ruhusa ya kupangisha nyumba yake, akitaka, ili imsaidie kulipa mkopo. Anapostaafu awe anayo nyumba ya kumstiri uzeeni. Kitendo hicho kisimpotezee uanachama wake wa CCM.

Kwa hivyo Ndugu Wanachama, huko ndiko kwenda na wakati, vinginevyo tutapwelewa. Mtu kama huyu aruhusiwe kupangisha nyumba yake, iwe nusu ya nyumba, ama robo ya nyumba au yote: (makofi).

BIASHARA YA KUPANGISHA MAJUMBA BADO NI MWIKO

Lakini kikao cha Zanzibar hakikutengua miiko ya kiongozi wala ya mwanachama wa CCM. Bado ni mwiko kwao kuwa na biashara ya kupangisha majumba. Kwa mfano, kama kuna mwanachama anayeomba mkopo, akipata anajenga nyumba, halafu anaikodisha, akipata fedha za kodi anajenga nyingine mpya, ambayo nayo anaikodisha na kuendelea kujenga nyingine. Huyo ni mfanyabiashara. Kazi yake ni kujenga na kupangisha majumba. Kikao cha Zanzibar hakikusudii mwanachama wa aina hii. Huyu siye (Makofi).

Vile vile, Mwanachama wa CCM, hata akiwa kiongozi katika mazingira maalum, aruhusiwe kukodisha nyumba yake, ikiwa haihitaji kuikaa wakati ule. Inawezekana haihitaji kuishi katika nyumba yake kwa kuwa kapata uhamisho. Mfano, mtu kahamishiwa Iringa kwa kazi wakati nyumba yake iko Dar es Salaam. Je ikae bure watu waitumie bure tu kweli? (Makofi).

Ni mwanachama wa aina hii ndiyo tulisema huko Zanzibar kuwa aruhusiwe kupangisha nusu ya nyumba ama robo ya nyumba au yote, maadam mtu huyo anapo pengine pa kukaa. Lakini tunasisitiza kuwa bado si ruhusa kwa mwana CCM wala kiongozi wa CCM kuendesha biashara ya kupangisha majumba.

HISA KATIKA MAKAMPUNI YA UMMA, KUPUNGUZA UKWASI!

La pili lililoamuliwa huko Zanzibar ni kuwaruhusu wanachama wa CCM, kwa kufuatana na hali ya wakati ulivyo, sasa aruhusiwe kuwa na hisa katika kampuni ya Umma. Hii leo tunayo Mashirika ya Umma zaidi ya 400, lakini mengine yao hayana fedha za kuendeshea kazi zao.

Mfano kuna mwananchi mmoja alikwenda kwenye kiwanda cha Umma kutaka huduma ya kusafishiwa ngozi zake. Alipofika hapo alikuta “pamelala paka” Yaani palikuwa kimya, hapakuwa na kazi yoyote inayofanyika. Kumbe kile kiwanda kilikuwa kimefungwa kwa kukosekana fedha za kukiendeshea ........... umeme ulikatwa na wafanyakazi walipewa likizo.

Meneja alimfahamisha huyo mteja kuwa kiwanda kimefungwa kwa sababu ya deni la maji na umeme pamoja na pesa za mishahara ya wafanyakazi. Huyo mteja alikubali kulipa arubuni (advance ) ya milioni saba ili kukikwamua kiwanda. Wiki ya pili yake kiwanda kilianza kufanya kazi zake za kuzalisha kama kawaida.

Kisa cha kiwanda hicho kusimama kazi ni kukosa fedha za kuendeshea. Kiswahili cha siku hizi huitwa ukwasi. Kwa hiyo kazi ilisimama.

Katika hali kama hii, tumeona ni vyema kuwaruhusu wananchi wote pamoja na wakulima, na wafanyakazi wa shirika lenyewe wakiwemo wanachama wa CCM kununua hisa chache kwa kila atakaetaka

UBIA WA UMMA NA DOLA KATIKA SHIRIKA

Narudia, watakaoruhusiwa kununua hisa ni wananchi wowote watakaopenda pamoja na wakulima wa pamba, korosho, kahawa, tumbaku na wafanyakazi wa hilo shirika lenyewe. Kwa njia hiyo, Shirika hilo sasa litapata sura mpya, litakuwa ni la ubia kati ya Serikali, wafanyakazi na wananchi. Fedha tunazozizungumzia hivi sasa, za kulipia taa na mahitaji mengine zingetokana na ununuzi wa hisa ili uzalishaji uendelee. Katika hali kama hiyo kiwanda kitakuwa ni mali ya umma kweli. Maana kuna tofauti ya Shirika la Dola na Shirika la Umma kwa maana ya wananchi wenyewe.

Endapo shirika la umma litataka kuwashirikisha wananchi na wafanyakazi wake kwa kulichangia ili kuondoa tatizo la Ukwasi, jambo hilo liwe ni halali, na Mwana CCM naye aruhusiwe kuwa miongoni mwao. (Makofi)..Kilichofanywa na maamuzi ya Zanzibar ni kumruhusu mwanachama wa CCM naye kushiriki kikamilifu katika sera ya Taifa ya uwekezaji wa rasilimali nchini.

Katika sera ya uwekezaji rasilimali tunaruhusu ubia katika uchumi wetu. Ubia huo unaweza kuwa baina ya watu wa ndani ya nchi peke yao, au kati ya wawekezaji wa nje na wa ndani. Baada ya kuikubali misingi hiyo hatuoni kwa nini tusianzie kwa kuwaruhusu wananchi, wakulima na wafanyakazi kuwa na hisa katika Mashirika wanayofanyia kazi (Makofi).

WAFANYAKAZI KUSIMAIA UWAJIBIKAJI

Nia nyingine ya kufanya hivyo inatokana na kutambua kuwa wafanyakazi wenye hisa katika kiwanda watakuwa wasimamizi wakereketwa wa uwajibikaji katika viwanda hivyo. Watakereketwa zaidi pakiwa na ubadhirifu au kutowajibika.

Hivi leo baadhi ya mashirika ya Umma ni mashirika ya umma kwa jina tu. Watu wanayaibia wakidai wanachukua chao. Pengine wanashindana kufanya hivyo ili wasipunjwe. Baadhi ya mashirika ya Umma yanahujumiwa kana kwamba hayana wenyewe. Baada ya maamuzi ya Zanzibar kuanza kutekelezwa, Mashirika hayo yatakuwa na wenyewe.

MWONGOZO WA 1981 KUHUSU UWAJIBIKAJI

Maamuzi ya Zanzibar si mapya. Mwongozo wa chama wa 1981 umetoa ilani juu ya kupungua kwa uwajibikaji katika Mashirika ya Umma, jambo ambalo hivi sasa tunalitafutia ufumbuzi. Mwongozo wa 1981 unasema hivi:

“Imezuka tabia ya aibu nchini ambayo imekuwa ikiongezeka ya vitendo vya kuharibu na kuvitumia vibaya vyombo muhimu vya kazi na mali ya umma kwa jumla. Magari, matrekta, zana nyingine muhimu z chama, serikali, mashirika ya umma mara nyingi hayadumu muda mrefu kama ambavyo ingetazamiwa kutokana na matumzi mabaya.”

Lakini ikiwa watu pale pale wenyewe wana hisa katika kampuni au shirika - mfano - TANESCO kuwa Mkurugenzi katika kampuni ya Kibepari. Napenda suala hili lieleweke vizuri ili kujibu fikra zilizojengeka kuwa uamuzi huo umevunja Azimio la Arusha.

Kwanza inafaa tufafanue maana ya Mkurugenzi. Tafsiri ya Mkurugenzi inayojulikana sana ni ile ya mjumbe wa bodi ya wenye hisa katika Kampuni fulan. Kwa hiyo wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi katika Kampuni ya Kibepari huwa ni miongoni mwa wale wenye hisa zao katika kampuni inayohusika Watu hao huchanguliwa na wenzao wenye hisa kama wa kuongoza shughuli za Kampuni yao kwa faida ya pamoja. Mkurugenzi wa aina hii hawezi kuwa mwanachama wa CCM.

Lakini kuna Mkurugenzi wa aina nyingine ambaye ni tofauti kabisa na Mkurugenzi mwenye mali. Mkurugenzi huyu ni yule ambaye ameajiriwa tu na wenye mali yao, kutokana na sifa zake za utaalam, kuendesha kampeni. Mtu huyu huwa ni mwajiri tu, anayefanya kazi. Huyu ni mtumishi tu kama watumishi wengine, hana chake katika kampuni inayohusika. Anachotegemea ni mshahara wake na marupurupu mengine kama yapo. Huyu ndiye Mkurugenzi anayeruhusiwa kuwa mwanachama wa CCM.

Azimio la Arusha bado lilo pale pale kwa wale wakurugenzi wa aina ya kwanza. Wao Azimio linawabana, hawawezi kuwa wanachama wa CCM. Lakini huyu wa aina ya pili aliyeajiriwa tu, akija kuomba uwanachama tunamkubali. Azimio la Arusha kamwe halijamkataa mfanyakazi mwenziwao kwa “koa” la kutumikia Kampuni ya Kibepari, hivyo ndivyo tulivyoamua Zanzibar


MWANA - CCM KUWA NA HISA KATIKA KAMPUNI YA KIBEPARI

Jambo jingine ambalo halikueleweka vizuri na linahitaji ufafanuzi ni lile la kumruhusu mwanachama wa CCM kuwa na hisa katika kampuni ya Kibepari. Hili nalo tumeliruhusu huko Zanzibar, lakini sharti iwe katika mazingira maalum.

Ni vyema kukumbushana kuwa yapo makampuni ya kibepari ambayo tumekuwa nayo hata kabla ya Azimio la Arusha. Kampuni hizo zimekuwa zikidhi kiasi fulani cha ajira ya Watanzania, pamoja na Wanachama wa CCM.

Ni jambo hili lieleweke vizuri, nitatoa mfano tu wa Kampuni ya mtu binafsi. Mwenye Kampuni ya binafsi anaweza kabisa akaamua kwa hiari yake kuuza baadhi ya hisa kwa wafanyakazi wake ili kuwapa motisha ya kazi Tajiri yeyote akiamua kufanya hivyo, Chama na Serikali vitamwona kuwa amechukua hatua ya kimaendeleo. Kitendo chake hicho ni halali. Kwa sababu itakuwa ameuzimua ubepari kwa kuifanya kampuni yake ni ya ubia kati yake na wananchi aliowaajiri. Kwa kweli kampuni hiyo itakuwa kama chama cha ushirika.

Katika hali hiyo, hata Mwanachama wa CCM anaruhusiwa kupokea/kununua hisa alingane na wafanyakazi wenzie.

Ni mazingira maalum ya namna hii tu ndiyo yanayoruhusu Mwanachama wa CCM, kama mfanyakazi mwingine, kuchukua hisa katika Kampuni anayofanyia kazi. Atakapostaafu ataweza kuendelea kupokea faida ya hisa yake au kuiuza.

MISHAHARA MIWILI KWA MWANA-CCM

Kuhusu mishahara miwili, Azimio la Arusha linasema hivi:

“Kwamba kila mtu anayo haki ya kupata malipo ya haki kutokana na kazi yake”.

Kufuatana na ukweli huo, anayefanya kazi mbili za halali anastahiki kupata malipo ya kazi ya pili. Tuchukue mfano wa Profesa ambaye mchana kutwa anasomesha Chuo Kikuu. Baada ya saa za kazi anaweza kuamua kufanya azi ya akili, kwa mfano kutoa ushauri au kuandika mradi kwa aliyemwomba huduma hiyo.

Mwanachama huyo atastahiki kupata malipo ya kazi hiyo. Hili si geni, katika sherehe za kuadhimisha miaka 20 ya Azimio la Arusha, baba wa taifa alisema hivi:

“Lile sharti la kutopokea mishahara miwili kwa kweli ni sharti la tahadhari tu. Ni vigumu sana kufanya kazi mbili za kuajiriwa na zote mbili ukazifanya vizuri. Huwezi kuwatumikia mabwana wawili! Lakini sharti hili halimkatazi kiongozi wetu kujiongezea pato kwa kutumia muda wake wa kupumzika kwa kufanya shughuli nyingine: kama kulima au kufuga, ikiwa yeye si mkulima au mfugaji, kuandika, kufanya kazi ya useremala, au kufanya shughuli nyingine yoyote kwa mikono yake au kwa ajili zake”.

Jambo la msingi ni kwamba lazima twende na wakati. Mwaka 1987 lilipotungwa Azimio la Arusha ilikuwa hakuna haja ya kuwa na mishahra au malipo ya kazi zaidi ya moja kwa sababu wakati ule mshahara mmoja ulikuwa unatosha kukidhi mahitaji yote muhimu. Kwa mfano, mimi, mwenyewe, mshahara wangu wakati ule ulikuwa shilingi 2,200/= kwa mwezi. Mshahara huo, hasa kwa Zanzibar, ulikuwa ukinitosha kukidhi mahitaji yangu yote ya lazima.

Wazee wangu watakumbuka kwamba wakai ule kule kitunguu, pilipili na bizari -yote hivyo kwa senti tano tu. Ilikuwa inawezekana pia kununua samaki mkubwa kiasi kwa senti ishirini mpaka 50 tu; au kununua kuni za kuweza kupikia mlo mzima kwa senti kumi tu.
Siku hizo iliwezekana mnunuzi kujaziwa mafuta ya kupikia au samli kikombe kizima kwa senti ishirini hasitini tu. Halikadhalika kwa senti ishirini tu mtu aliweza kununua matunda, kama vile fungu la ndizi mbivu au machungwa au papai. Kwa ufupi, kwa mahitaji ya siku nzima, tangu asubuhi hadi jioni, iliwezekana mtu kutumia pesa kidogo sana.

Katika hali hiyo, kulikuwa hakuna ulazima wa kufanya kazi ya pili. Afanyae kazi zaidi ya moja huonekana ni mlafi au ana tamaa. Kwa mshahara huo huo niliweza kudunduliza pesa na mwishowe kununua gari mpya kabisa. Gari hilo lilinigharimu pesa nyingi kwa wakati huo - shilingi 13,000/=!! Wakati huo bei ya mafuta nayo ilikuwa shilingi tatu tu kwa galoni zima. Katika mazingira ya aina hii mshahara mmoja ulimudu kukidhi mahitaji ya wafanyakazi wengi ukiacha walevi.

HALI IMEBADILIKA

Lakini leo mambo yamebadilika. Gharama ya maisha imepanda san. Serikali yenyewe imeungama waziwazi kuwa haina uwezo wa kumlipa mfanyakazi wake mshahara unaomwezesha kumudu gharama za maisha. Kutokana na hali hiyo, wafanyakazi wengi, wanashindwa kukidhai mahitaji yao muhimu. Ndio maana Chama na Serikali yake vimekuwa vikiwahimiza wafanyakazi kufanya shughuli nyingine za halali, baada ya saa za kazi, ili kujiongezea mapato. Mfano wa kazi hizo ni kama vile: kutibu, kuandika vitabu, kuandikamradi, kutoa ushauri wa kitaalamu, kufundisha, overtime, useremala, ufundi bomba, ufundi umeme, ufundi cherahani, kilimo, ufugaji, kuziba mipira ya magari, kuteka maji ya kuuza, kupiga matofali, kutengeneza baiskeli na kadhalika.

KOFIA MBILI MSHAHARA MMOJA

Lakini lazima tuelewane kuwa hii mishahara miwili tunayozungumzia haimhusu kiongozi mwenye kofia mbili. Kwa mfano, Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya, ambao vile vile ni Katibu wa Chama wa Mkoa au Wilaya, hawaruhusiwi kupokea mishahara miwili. Hawa watalipwa mshahara mmoja tu, maana hii kazi ya pili ni sehemu tu ya ile ya kwanza. Lakini wanaruhudiwa kufanya kazi za ziada kama vile kilimo, ufugaji na kadhalika, baada ya saa za kazi, kama walivyoruhusiwa wafanyakazi wengine. Hapa nitapenda kusisitiza kuwa wale watu wanaoeneza maneno ya kejeli kuwa ati Maamuzi ya Zanzibar ni mbinu tu za “wakubwa” kujifufanisha wenyewe, ijulikane kuwa si kweli. Kazi zilizoorodheshwa hapa si za wakubwa bali ni kazi zinazoweza kufanywa na kila mtu kufuatana na ujuzi alionao na mazingira ya mahali anapofanyika kazi.MWANA-CCM MKULIMA NA MFUGAJI

Watanzania wengi ni wakulima, wakulima ndio wengi zaidi. Mkulima kwa maana pana ni pamoja na mfugaji. Katika siku za nyuma, baadhi ya wanachama waliwahi kutiwa msukosuko kwa kuwa na mashamba makubwa au kufuga kuku 500. Lakini baadaye Chama kilijisahihisha kama inavyosema Programu ya Chama:

“Chama Cha Mapinduzi ni Chama kinachokua (haikudumaa). Kinakaa katika nadharia na falsafa yake, (ili kwenda na wakati)”.

Hii ndio ilivyokifanya Chama kijisahihishe kila kinapokosea.

Kwa hiyo kama siku moja tulimtia mwenzetu msukosuko kwa kuwa na shamba kubwa, mbuzi 18 au kuku 500, sasa Chama kimekua katika falsafa yake. Falsafa ya sasa inatia maanani hali halisi ya wakati wa sasa. Ndio maana kule Zanzibar tukaruhusu kiongozi awe na shamba lisilozidi hekta 20, hasa kama shamba hilo limo katika eneo la kijiji.

class=Section2>
Kuhusu ufugaji, kuna baadhi ya wenzetu katika makabila ya Tanzania ambao kwao ni utamaduni wao kuwa na ng’ombe wengi. Mfano mzuri ni wenzetu wa makabila ya wamasai, Wasukuma na Wagogo. Je, mwenye utamaduni wa kumiliki ng’ombe wengi akataliwe katika Chama kwa sababu ya kumiliki ng’ombe wengi? Tunasema hapana. Akiomba uanachama wa CCM akubaliwe. Chama Cha Mapinduzi hakimkatai tajiri aliyepata utajiri wake kwa njia ya halali na kulipa kodi ya Serikali analipa. Anayekataliwa na CCM ni yule aliyepata utajiri kwa wizi, kwa rushwa, dhuluma na kwa kwa njia nyingine za haramu.

Huko Zanzibar tulifikria labda tuweke kiwango maalum cha mifugo, kama vile iwe mwisho ng’ombe 200 peke yake. Lakini tulijiuliza kama ng’ombe mmoja akizaa na jumla kufikai 201, je huyo ndama amnyonge shingo?

Hiyo ndio hali halisi iliyotufanya tukubaliane kuwa mfugaji yeyote anaetaka kuwa mwanachama bila ya kujali idadi ya mifugo yake. Mwenye mshahara mkubwa, vile cvile hata wa malaki, maadam ni mshahara wa kazi halali, naye pia aruhusiwe kuwa mwanachama wa CCM.

MAFUNZO YA MIEZI MITATU

Ili kukiimarisha zaidi Chama, tumewaruhusu wananchi kuwa wanachama wa CCM bila ya kuhdhuria yale mafunzo ya miezi mitatu.

BIASHARA NDOGO NDOGO

Huko Unguja hatukuishia hapo. Tuliamua kuwa Mwanachama wa CCM wa kawaida naye pia aruhusiwe kuwa na biashara ndogo ndogo ili kumwongezea kipato. Biashara hizo, ambazo sharti zifanywe baada ya saa za kazi, ni pamoja na uvuvi, kuwa na gari ndogo au pick-up ya kukodisha kwa kuchukulia abiria au mizigo, kushona, kusindika matunda, mafuta na mashine ya kukoboa au kusaga unga.

Mwanachama mwenye mashine ya kusaga unga hanyonyi bali anatoa huduma kwa jirani zake kijijini. Chama na Serikali vimo mbioni kuhimiza na kutafuta teknolojia ya kumrahisishia kazi Mtanzania, hasa wanawake. Ni vyema kukaribisha teknolojia ya kuwasaidia wanawake waondokane na kufanya kazi ngumu ngumu zinazoweza kuwapotezea wakati na kuathiri afya zao, kama vile kutwanga au kusaga nafaka, kubeba mizigo ya kuni, maji na mtoto mgongoni. Si vyema kwa jamii yetu kuingia katika karne ya ishirini na moja katika hali hiyo. Ndio maana kule Zanzibar tulamua kuruhusu biashara ndogo ndogo kuendeshwa na mwanachama wa CCM kwa manufaa yao na ya jamii.

Ndugu Wazee, haya kwa muhtasari ndio yaliyoamuliwa Zanzibar. Haya kamwe hayabomoi Azimio la Arusha, badala yake yanaliimarisha. Azimio la Arusha ni msingi wa siasa yatu ya ujamaa na Kujitegemea. Ili tuweze kujitegemea lazima tuandae mbinu na mikakati ya kuzalisha maji, huduma na chakula. Hili ndio lengo la maamuzi ya Zanzibar.

Mshairi mmoja amesema:-

“Kutaraji uongofu bila kupitia njia zake ni kama kulitaka
jahazi kutembea nchi kavu”

Ndugu Wazee Ahsanteni sana. (Makofi).

source humu humu JF
 
Mtu wa Pwani,

Shukuran kubwa sana kuweza kutupa hiyo hotuba na kusema kweli imezungumza mengi yenye manaa na yanaeleweka. Isipokuwa nadhani baada ya awamu ya Pili ya Mkapa kumekuwepo na tafsiri nyingine ya Azimio hilo hilo la Zanzibar kwani yote aliyosema Mheshimiwa ni tofauti kubwa sana na hali halisi iliyopo, tena viongozi hawa hawa wameijengea ngome kuwab wakitumia Azimio hilo la Arusha.

Kifupi nitasema kwamba Mh. Mwinyi mwenyewe alishindwa kuelewa kuwa siku zote samaki wanaokutwa na azima hizi ya maji kupwa na kujaa huwa ni samaki wadogo sio Papa na Nyangumi hao viongozi, aghalabu kujikuta ktk mazingara hayo labda hao watoto wao.

Pia alipozungumzia mishahara midogo alishindwa kuelewa kwamba tofauti ya mishahara ya mwaka 1987 na leo hii kifedha haiwezi kuepukwa kwa hiyo RUKSA ya viongozi wachache kuweza kujihusisha na biashara moja kwa moja hali thamani ya fedha kubadilika kulingana na soko na sio sio viongozi wala figure inayoandikwa.

Ukisoma mkwa makini taarifa nzima utakuja gundua kwamba ametumia sana lugha ya mabadiliko ya kwenda na wakati kwa wananchi wote lakini in real fact hotuba nzima ilikuwa inahusu RUKSA kwa viongozi wetu kujihusisha na biashara nje ya madaraka waliyokabidhiwa, otherwise sikuona kitu chochote tofauti na wakati wa Nyerere kwani viongozi wengi walikuwa na mashamba yao ya ukulima na Ufugaji. Na neo Kiongozi liliokuwa na tafsiri ya kipato badala ya wadhifa kilichotakiwa kubadilishwa ni ni tafsiri ya neo hili kutoka kipato na kuwa nafasi ya wadhifa anaoushika. Huwezi kuendelea kutumia kipato wakati fedha yetu tahamani yake hushuka kila mwaka.

Kama mwaka 1987 alikuwa na mshahara wa shilingi 2,200 hizo fedha haziwezi kuwa na thamani ile ile leo hii na ndio maana aliweza kununua gari kwa shilingi 13,000. Tunakwenda na wakati kwa kuthamini mabadilisho ya shilingi yetu ktk soko na sio kuvikana kofia za biashara kama ndio suluhisho la Utawala ktk ulimwengu wa Utawazi.

Yote tisa hawa jamaa wameisha tuvika mkenge na ndio maana Mkapa aliweza fungua ofisi yake Ikulu maanake ndio nyumbani kwake na mahala pekee anakoweza kuwa na kipato zaidi ya mshahara wake.

Kama mmegundua hapa It's all about them CCM members na viongozi na ndio maana niliwaambieni toka zamani kuwa CCM wanajiandaa na mkakati wa kujitajirisha wao. Wengi walinipinga hasa namkumbuka vizuri sana dogo Tito Mwiula ambaye alikuwa mdhamini mkubwa wa hoja za CCM.
 
Kichuguu

X-mass ndio iko njiani hivyo angalia mabox yasikuumize.


gamba la nyoka

Azimio la Arusha hilo hapo chini, sina hotuba ya mzee rukhsa.

Ni kweli mkuu wangu, maboksi haya yanazidi kuongezeka ukubwa.

Hata hivyo je hivi wewe ukienda porini kutafuta maembe ukakuta yapo maembe mengi utalalmika au utafurahi? Nilikuja huku kubeba maboksi, kwa hiyo kadri yanavyozidi ukubwa ndivyo na mimi ninavyofurahi. KWI!! KWI!! KWI!! KWI!! KWI!!.

Nashukuru kwa nakala ya Azimio la Arusha
 
Back
Top Bottom