AZAM MILK, artificial au maziwa halisi?

AZAM MILK, artificial au maziwa halisi?

Haya ni maziwa ya unga .
Anaagiza kwa wingi na kuya badilisha kuwa ya maji.
Kama unahitaji virutubisho vitokanavo na maziwa basi Azam milki sio yenyewe hayana kitu cha faida .
Ni artificial milk yakiwa na ladha ya maziwa.
Nunua Tanga fresh
Asas
Serengeti milk
Au maziwa kutoka kenya .
Azam ni kujaza tumbo tu
Hii ni kweli,kuna jamaa mmoja anafanya kazi TFDA ameniambia bidhaa nyingi za Azam ni magumashi ..
Pia bidhaa za Mo ndio bomu kabisaaaaaa!
 
ASAS kule nduli iringa anao ng'ombe kibao anafuga, na anakamua maziwa na kutengeneza products nyingi. azam maziwa yake ni kweli anayatengeneza artificial kama wanavyosema watu mtaani? ng'ombe wake anafugia wapi, anakamua wapi hayo maziwa jamani?

NB: lengo sio kumharibia biashara, nafikiri kama yuko humu ni nafasi yake kujisafisha ili kuondoa doubt kwasababu kusema kweli binafsi huwa napenda products zake, sasa nilipoambiwa na wenzangu kuwa maziwa ya azam ni artificial nilisita kuendelea kuyanunua.

najua kwamfano juisi za maembe, anatumia maembe halisi, nanasi halisi na matunda mengine halisi (pamoja na kwamba mapera sijajua anachuma kwenye shamba gani?), ila maembe ni halisi. kwa wale wenye ufahamu, tuambieni azam maziwa yake anakamua wapi, au anaagiza uarabuni ya ngamia kama wanavyosema huku mitaani?

ASAS anachukua maziwa mengi Kitulo Makete. Hana uwezo wa kuzalisha maziwa binafsi.
 
Azam milk ni sawa na Nido ikikorogwa...
 
......hiyo juice ya maembe ni chemicals tupu, hayo maziwa nayo chemicals. Maziwa ya ukweli ni asas na tanga fresh. Au nunua moja kwa moja kutoka kwa mfugaji wa cows.
 
Ukimchunguza bata haumli. Mchicha tunaokula unamwagiliwa kwa maji ya kinyesi, kuku wanachomwa masindano na kupewa madawa kila kukicha, Samaki siku hizi wanafugwa na kupewa madawa wanakuwa kwa siku tano. Ngombe nao wanachomwa masindano. kwa ufupi hayo maziwa ya Azam, ASAS, Tanga fresh na mengi ni ugonjwa tu.
 
Na Dar milk je? hilo shamba liko pande zipi Kg la co. milk.

Dar milk ipo Kigamboni mbele ya Dar es salaam zoo.Idadi ya ng'ombe alionao haitoshelezi ukubwa wa hii factory aliyoijenga labda awe anakusanya maziwa toka kwa wafugaji wengine.
 
Oil Com nao wana shamba kubwa la ng'ombe Kigamboni nao wanatengeneza maziwa yanaitwa Com Milk.

Bora oilcom ni wafugaji wa miaka mingi sana tangu 80's kabla hata biashara ya mafuta.
 
Na Dar milk je? hilo shamba liko pande zipi Kg la co. milk.

kiwanda cha oilcom kinaitwa milkcom na maziwa yenyewe yanaitwa dar fresh pia ranchi ya kufuga ng'ombe ipo maeneo ya kisawarawe 2 ni kama km 10 kutoka kibada stendi ni barabara inayoelekea kijiji cha mwasonga wilayan temeke kipo karibu na dar zoo.
 
ASAS kule nduli iringa anao ng'ombe kibao anafuga, na anakamua maziwa na kutengeneza products nyingi. azam maziwa yake ni kweli anayatengeneza artificial kama wanavyosema watu mtaani? ng'ombe wake anafugia wapi, anakamua wapi hayo maziwa jamani?

NB: lengo sio kumharibia biashara, nafikiri kama yuko humu ni nafasi yake kujisafisha ili kuondoa doubt kwasababu kusema kweli binafsi huwa napenda products zake, sasa nilipoambiwa na wenzangu kuwa maziwa ya azam ni artificial nilisita kuendelea kuyanunua.

najua kwamfano juisi za maembe, anatumia maembe halisi, nanasi halisi na matunda mengine halisi (pamoja na kwamba mapera sijajua anachuma kwenye shamba gani?), ila maembe ni halisi. kwa wale wenye ufahamu, tuambieni azam maziwa yake anakamua wapi, au anaagiza uarabuni ya ngamia kama wanavyosema huku mitaani?

kiwanda kipo znz anapeleka pumba ya ngano ranchi boswana yeye anachukua maziwa
 
Juice za azam ndio nilishaziachaga kabisa unakuta juice ina sukari sana alafu nzito kama mlenda hayo maziwa ni unga ule artificial hakuna natural pale.
 
Dar milk ipo Kigamboni mbele ya Dar es salaam zoo.Idadi ya ng'ombe alionao haitoshelezi ukubwa wa hii factory aliyoijenga labda awe anakusanya maziwa toka kwa wafugaji wengine.

Oil com anao ng'ombe wengi sanaa.ila hawatoshelezi kiwango kinachohitajika. Kiwanda cha dar fresh kipo karibu sana na dar zoo. Kwahiyo maziwa yote ya dar zoo wanauza kwa dar milk ukizingatia dar zoo wanao ng'ombe wengi sanaa. Pia haijatosha, mtuu ýyt mwenye maziwa kiwango chochote anakaribishwa dar fresh wananunua kwa 1500 per liter. Hawa dar fresh wamepandisha sanaa soko la maziwa kigamboni. Ila mm nadhani hawa jamaa wote wenye viwanda vya maziwa wanachakachua sanaaa. Ukiangalia dar fresh wananunua maziwa fresh 1500 per lit. Wakati wao wanauza bei ya kiwandani 800 per 0.5lit. Ina maana wanauza 1600per lit na wao wamenunua 1500per lit. Lazima tuu watakuwa wanachakachua sanaaaa. nawaomba poteza tym yako tafuta maziwa bora katika eneo lako. Ni bora ununue 5lit uweke kwenye frige kuliko kununua maziwa ya packet. Mungu atujaalie afya.
 
Maziwa siyo original. Wakati fulani nikiwa naumwa nilitumia sana maziwa fresh. Ukinywa ni kama kuna ladha ya vitu kama miti ffulani. Wanatuibia tu.
 
Kiingilishi sii kila mtu anajua wee binti, na pia kuna mi term ya chemistry pale sio wote wanayajua

Heshima kitu cha muhimu, na hukuwa na sababu ya kujibu. Kama hujui kusoma kamlalamikie Mama Yako.
Hapa JF hatujuani hivyo usiniite binti. Kama Baba yako ni binti niite hivyo
 
Hivi hakuna teknolojia ambayo inawezesha maziwa ya maji kuwa ya unga?kama ipo kwanini mnasema si maziwa halisi?hilo ni badiliko la kiumbo !
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom