Mzuvendi
JF-Expert Member
- Apr 28, 2009
- 561
- 544
Ndugu yangu umegonga kwenyewe, nilipoangalia hiyo website ya hao jamaa wa Learn IT nikakuta kuna elimu inaitwa International Diploma, kweli nilichoka kweli kweli, kwa sababu katika Marekani diploma ni cheti unachopata baada ya kuhitimu elimu fulani. Kuna high school diploma, Associate degree Diploma, College Degree Diploma, Graduate degree diploma, n.k.
Hakuna hakuna kitu kama international degree, international diploma au international certificate. Ukitambulisha digrii yako, lazima vile vile uonyeshe uliitoa chuo gani. Angalia, watu wanatambulisha elimu ya Obama kuwa "a graduate of Columbia University and Harvard Law School"
Kichuguu,
Mambo mengine yanatokana na mifumo yetu ambayo imekazania sana kutoa vyeti.
Mtu anafanya juhudi zote hili afaulu kwenda A level. Na akipata nafasi ya A level anafanya juhudi zote ili aende mbele.
Hivyo vyeti vinakuwa motivation na sio process yenyewe ya kupata elimu.
Kama process ya kupata elimu ingekuwa ni juhudi yetu, elimu ya A level ni sawa na elimu mwaka wa kwanza au wa pili katika vyuo vikuu vya nchi nyingi.