Authenticated leaders (viongozi wenye utashi hakika sahihi na wakweli) ndio msingi wa kwanza wa uongozi

Pascal Ndege

JF-Expert Member
Nov 24, 2012
2,977
1,897
Msomi wa vitabu Hayati Benjamin Mkapa alikuja na kauli mbiu ya UKWELI NA UWAZI sikumielewa sana kipindi kile. Ilikuwa ni kauli mbiu ya kisomi sana kwa mtu wa kawaida kung'amua.

Katika harakati zangu za Maisha longolongo ndio ilikuwa janja yangu. Katika kikao kimoja nilifanya na viongozi wa wizara ya kilimo baada ya kikao Kuna Jamaa akaniangalia akaniambia nenda kasome vitabu hivi akanipa listi ndefu ya vitabu.

Mimi binafsi nilikuwa na hulka ya kusoma novo za vita na story nyingi za kutosha. Kukaa na kusoma vitabu ilikuwa kazi nyepesi Kwangu. Nikapita kwenye internet Moja nikadownload vitabu Vyote kwenye softcopy.

Kwakweli haikuwa Kwangu kazi rahisi kusoma vile vitabu kwasababu sikuwa na PC kwahiyo nilisoma vitabu kwanye simu. Nakumbuka nilisoma vitabu Vyote ndani ya miezi mine. Vitabu vingi vilenga kumtambua mtu mwongo mwongo.

Vilimwelezea Tabia za mtu mwongo anapokuwa kwenye jukwaa au hata maongezi ya kawaida tu.
Nilifanya practice kwa kumtambua mtu mwongo nikacheka sana baadae usiku Nikirudi nyumbani kuendelea kusoma vitabu vyangu.

Niligundua watu wengi waliyonizunguka si watu wa kuaminika kabisa. Mwongo hawezi kuficha uongo wake atajikuna pua, atainama chini,kuinamisha kichwa, atajikuna, lazima atafanya tendo Moja linaloashilia jambo ni la uongo.

Kitabu cha mwisho kilieza na uongo unavyoathiri uongozi wa kampuni au Taasisi. Kitabu kile kilieleza kinagaubaga uongo ni adui number Moja wa uongozi.

Kwasababu unavyosema uongo Kuna kitu kinaitwa "contradiction" yaani wasikilizaji wanapata messages mbili mbili. Mtu mwongo macho yake, pua, yake, mikono yake, mabega yake, muonekano wake, mkao wake. Hutoa messages tofauti na sauti yake.

Hivyo wabobezi wa kung'amua uongo wenye kipaji cha kuzaliwa yaani wanawake. Wanaanza kupoteza Imani na mtu yule Mara Moja hata kama ameongea maneno mtamu ya kuchekesha na kuridhisha.

Katika vitabu vingi vya uongozi hasa uongozi wenye ufanisi wa VIWANGO kitu cha kwanza ni kiongozi kuwa mkweli na sahihi katika nyanja zote ni jambo la msingi la kwanza kwa uongozi.

Kiongozi mkuu ni kama mchungaji mwenye fimbo kila eandapo nyuma anafuatwa na Ng'ombe wake. Sasa mchungaji atasema uongo wowote Ng'ombe wote watapotea njia.

Ukija katika hili swala la Bandari hakika viongozi wengi watapoteza mvuto na kupotea kwenye ramani ya siasa kwa muda mrefu kutokana na kutosema ukweli.

Natabiri anguko la viongozi wengi sana kipindi cha Miaka kumi ijayo. Nadhani nafasi bado ipo kwao kujirudi kuwa Authenticated people. Hebu waje na ukweli wa mambo ili wananchi wengi wa amini. Wanawake wengi wamecha kuzungumza kabisa kuhusu Bandari na mostly wanahasira sana.

Kwakuwa Hawana tu la kufanya wamenyamaza. Wanahisi viongozi wamewasaliti sana wanawake.
 
Siasa zaTanzania zimejengwa na uongo mwingi sana. Sababu za uwongo hasa kwa chama tawala ni ili waendelee kuwa madarakani. Uongo na fitna umelifanya kundi la watu wachache liendelee kukaa madarakani kuanzi babu hadi wajukuu si kwa sababu ya akili nyingi bali uhodhi wa mali na madaraka kama mtaji muhimu.

Ccm kama wanathamini ukweli wangeliandaa taifa kwenye misingi ya kubadilishana mamlaka baina ya vyama endapo wananchi wataamua.

Lakini hilo ccm hawaruhusu kamwe. Watu wanalilia katiba mpya lakini wanakuja na uongo mwingi kuwa watu hawali katiba huku wakijua ukweli umuhimu wa katiba nzuri kwenye kujitawala na maendeleo ya watu.

Ccm bebeni jukumu la msingi kuruhusu katiba bora kwa watu wote na wakati wote, acheni uongo kwani, ndio, utawajenga lakini unaibomoa nchi ambayo mnaishi, sasa huko kujijenga kwenu kutatokeaje mkiwa kwenye nchi inayobomoka!

Narudia, CCM itajijengaje katika nchi inayobomoka?
 
Siasa zaTanzania zimejengwa na uongo mwingi sana. Sababu za uwongo hasa kwa chama tawala ni ili waendelee kuwa madarakani. Uongo na fitna umelifanya kundi la watu wachache liendelee kukaa madarakani kuanzi babu hadi wajukuu si kwa sababu ya akili nyingi bali uhodhi wa mali na madaraka kama mtaji muhimu.
Ccm kama wanathamini ukweli wangeliandaa taifa kwenye misingi ya kubadilishana mamlaka baina ya vyama endapo wananchi wataamua.
Lakini hilo ccm hawaruhusu kamwe. Watu wanalilia katiba mpya lakini wanakuja na uongo mwingi kuwa watu hawali katiba huku wakijua ukweli umuhimu wa katiba nzuri kwenye kujitawala na maendeleo ya watu.
Ccm bebeni jukumu la msingi kuruhusu katiba bora kwa watu wote na wakati wote, acheni uongo kwani, ndio, utawajenga lakini unaibomoa nchi ambayo mnaishi, sasa huko kujijenga kwenu kutatokeaje mkiwa kwenye nchi inayobomoka!!!
Narudia, ccm itajijengaje katika nchi inayobomoka?
Sioni hofu ya katiba mpya
 
Ukweli kabisa
 
Back
Top Bottom