AU's dilemna and the Libyan crisis

Wanafiki wakubwa hao. Walikuwa wapi siku zote? Bora wamezuiwa. Wakatatue mataizo yao ya kawaida kwanza kama njaa,ukimwi,tb,ujinga n.k

some people they sound strong and confident behind keyboard. tehetehe JF raha
 
Hivi wanaposema wanaenda ku-mediate huwa wanenda kufanya nini haswa? Maana wameenda Ivory Coast - tunajua walichovuna. Sasa ni mbinu hizo hizo wangezitumia kwa Quadaffi? Wangemshawishi ateuwe jamaa wa Benghazi kuwa mawaziri? AU is a bunch of incompetent 'leaders'! They better stay out.
 
Ni kweli. Lakini kila nchi ya watu wenye akili timamu inaangalia maslahi yake kwanza! Hebu tu tujiulize, kwa nini Arab League ilikomalia suala la no fly zone Libya na si Yemen?!
 

Hapo kwenye red. Walibya hawana katiba.
 
baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa Gaddafi amesema atafungua maghala kuwapa silaha wananchi kuilinda nchi yao. hivi hii ni kweli? wasiwasi wangu ni kuwa asije akawa anawapa silaha walewale ambao aliwashambulia na kuwaua ndugu zao wakati wa maandamano, nadhani mwisho wake utakuwa mbaya sana!
 
Good move,ukilingansha maisha ya tz na libya utashangaa kwwa nini wanaandamana huku wana kila kitu.Lakini watz tunatanguliza amani kuliko maisha bora. Ipo siku nasi tutasisimuka na kuijenga tanzania mpya.

Una maana gani wanaandamana huku wana kila kitu? Japokuwa wabongo maskini tuna kila kitu. Uzembe wetu ndio unatufanya kuwa maskini. Walibya hawana kila kila kitu. Kwa mfano hawana freedom unayoitumia hapa JF kuandika unachoandika. Thats want they want. Kwako itaonekana kitu kidogo sana kulinganisha na utajiri. Lakini utakuja tambua when you loose your freedom and liberty. The way unavyoshangaa kwa nini wanaandamana huku wana kila kitu, ndivyo pia watu wanavyotushanga kwa nini tuko maskini wakati tuna kila kitu.
 
Pole mkuu naona 'umeinamisha kichwa na unalia kwa aibu'... Hivi hujui kama Congo kuna askari wa UN huko?! Somalia na Bahrain wameachiwa watu wa 'mashariki' wamalize mgogoro huo...au na wao hawawezi?!
 
Kwa hiyo unashauri tuwa worship mashetani wa mashariki au???
 
TATIZO LA WAAFRIKA NI KUKOSA AKILI!
WAAFRIKA HAWANA MUDA WA KUJIULIZA KWANINI!? WAAFRIKA HAWAHITAJI KUJUA SABABU BALI KUAMBIWA TU...
MASKINI AFRIKA, MASKINI TANZANIA!!!

Wengi wetu hakuna anaejiuliza pindi tukiwafukuza WAZUNGU ama kudai MRAHABA UNAOSTAHILI NINI KITATOKEA!

WASWAHILI WANASEMA KILA MSHEREHEKEA MSIBA WA MAMA WA KAMBO, MSIBA HUMFIKA *****.
TAFAKARINI KWANZA NDIPO MUANDIKE UPUPU!
 

Iko hivi, mwanzoni raia walihamasika na yaliyotokea Tunisia na Misri na wao wakaanzisha movement ya kumuondoa Gadafi kama ilivyo kwa nchi nyingi za Kiarabu hivi sasa Yemen, Bahrain, Saudi, n.k. Gadafi akaanza kutumia polisi kuwazuia waandamanaji kwa njia ya amani kama ilivyokuwa Misri jitihada ambayo ilishindwa kama ilivyoshindwa Misri. Gadafi akaenda mbali zaidi kwa kuanza kuwashambulia waandamanaji wa amani kwa risasi za moto badala ya mabomu ya machozi na risasi za mpira. Akaua waandamanaji kadhaa lakini bado akaendelea kuelemewa na dalili za wazi za kutokea ya Mubarak ikajidhirisha. Akaongeza kasi ya kutumia risasi za moto na akaenda mbali zaidi kwa kuwashambulia kwa mabomu mazito ardhini na kutoka angani kitu ambacho kiliwaudhi baadhi ya wanajeshi ambao walimuasi Gadafi na kuamua kuungana na waandamanaji na ndio wakaitwa waasi. Hata yemen sasa hivi kuna majeshi yameigeuka serikali kuu. Nadhani kwa historia hiyo fupi sidhani kama utawaona waasi kivipi lakini ujue kuwa ni watu wasiokubaliana na uamuzi wa Gadafi wa kuwashambulia raia kwa risasi na mabomu mazito
 
Viongozi wa Afrika bwana akili fupi sanaaaaaaaaaaaaaa! Wameng'ang'ania kujilinda dhidi ya raia wao wenyewe. Quadaffi katengeza jeshi la kujilinda yeye na familia yake dhidi ya watu wa Libya. Sasa njemba zinapiga za masafa marefu anaishia kulialia tu-hamna kitu. Halafu watu wanathubutu kusema Quadaffi kaifanyia Libya mambo mengi. Yepi hayo ikiwa hata kujilinda dhidi ya mashambulizi madogo tu hawezi.
 
Namshukuru Mungu kwaajili ya ufaransa, uingereza na marekani kwaajili ya kufanya huduma hii kubwa ya kitumishi, kumsambaratisha mtumishi wa mpinga kristo aliyekuwa anajiita mfalme wa wafalme...hana maana yoyote, na watamponda kama panya...go to hell gadafi/gaidi...pesa zake za kishetani ndo alizowajengea waislam wa Uganda/kampala na dodoma misikiti aliyoiita kwa jina lake..ni jini yule hana lolote, muuaji mkubwa, toka lini mtu anayejifanya kujenga mahekalu ya mungu anatumia mabomu ya ndege kushambulia raia wanaoandamana? wapi na wapi, do you think the world would every remain silent to witness another genocide just like they did in Rwanda? never ever, no more holocost, no more genocide....mtu yeyote yule hata kikwete akiwa anaua watu hovyohovyo, nchi zingine kwa sasa zitaingilia tu hata kama kuna watu ambao watalalamika namna gani..watakuja kuelewa badaaye,.....kwenda zako huko gadafi....
 
bravo sakozy, obama and cameron..bravoo bravoo....hongereni kwakweli kutuondolea dictator tena mchawi na shetani...cha ajabu zaidi, utakuta kuna watz ambao wanamsaidia gadafi, kama vile wanavyomsaidia na kumwombea osma bin laden tu...kwasababu wao ni magaidi,wauaji na waliojaa ukatili kama gadafi na osama...bravo mataifa ya magaribi...
 
JK kupeleka majeshi Comoro ilikuwa ni uvamizi?
huko hao wanajeshi walienda kunywa maji ya madafu au kiherehere cha kuingila mambo ya ndani ya nchi ingineeeeeeee.

KAMA Tz tuliingilia mambo ya nchi ingine basi hata America haijafanya cha ajabu
 

Mi nadhani mkuu,umezungumza kiushabiki zaidi na chuki tu,jaribu kufikiri japo kidogo faida watakayoipata hao walibya ambao vita inapiganwa nchini mwao baada ya ghadhaf kushindwa...ni kweli kabisa kutoka moyoni unaona hizo siasa za nchi za nje za nchi za kimagharibi zinamanufaa yoyote katika nchi wazazodai wanasaidia kama si kulinda maslahi yao binafsi?Hili amesema Obama,Marekani ipo tayari kufanya lolote kulinda maslahi ya watu wake nchini Libya.....je hilo ndilo unaloshangilia kiongozi?
 
Mohammed Bacar aliingia madarakani kwa mapinduzi mwaka 2001 kama huyo Gaddafi tu.. 2007 kwenye uchaguzi ambao haukutambuliwa na AU akajitangaza kuwa mshindi wa urais.

Hili swala tumelidiscuss hapa
https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/11018-majeshi-yetu-comoro-who-is-responsible.html
 
Harakati za jamii ya kimataifa zinazoendela dhidi ya Libya zimekosolewa Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

Katika tahariri yake kuhusu mgogoro wa Libya, iliochapishwa kwenye magazeti nchini humo Rais Museveni amemkosoa na pia kumtetea Kanali Muamar Gaddafi.


Kiongozi huyo amepinga upinzani ambao unaungwa mkono na mataifa ya kigeni na ameyaita mataifa hayo kama yenye undumila kuwili unaothibitishwa na kuweka haraka marufuku ya ndege kupaa kwenye anga ya Libya.


Museveni ambaye ni mmoja walioteuliwa kwenye jopo la kutatua mzozo huo na Umoja wa Afrika amehoji kwa nini nchi hizo zina puuza hali mbaya kama vile ya Bahrain ama maeneo mengine yenye kuegemea upande wa magharibi.


Katika tahariri hiyo, anauliza ikiwa Benghazi pekee ndio kuna raia na Mogadishu hakuna au ni kwa sababu nchini Somalia ambapo wameomba Umoja wa Mataifa kuingilia kati mzozo unaoendelea hakuna mafuta.


Aidha, Rais Museveni amemsifu Kanali Gadafi kama mmoja wa viongozi wa Kiarabu ambae hashabikii uislamu wa itikadi kali.


Kiongozi huyo pia amemsifu Gaddafi kama kiongozi wa Afrika ambaye ana mawazo yake binafsi asie shawishika na sera za kigeni.


Kwenye tahariri hiyo pia, Rais Museveni amekosoa sera za Gaddafi, na kutoa mifano kama alivyounga mkono utawala wa Iddi Amin alieongoza Uganda tangu mwaka wa 1971 hadi 1979.


Museveni ameongeza kuwa Gadaafi alikosa kuingilia mambo ya ndani ya nchi za kiafrika, kwa mfano kwa kuwahusisha viongozi wa kijadi ama kitamaduni, kama vile wafalame na watemi katika masuala ya kisiasa.


Tahriri yake imekamilika kwa kuutaka umoja wa Mataifa kudurusu azimio lake la marufuku ya ndege kupaa kwenye anga ya Libya.


http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2011/03/110322_uganda_libya.shtml
 
Museveni mwenyewe anajua fika kuwa dunia inaendeshwa mithli ya samaki baharini; "samaki nkubwa anamla mdogo." Mambo ndivyo yalivyo hata nchini mwake.
 
Not sure if has been posted.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…