kayanda01
JF-Expert Member
- Feb 14, 2014
- 1,086
- 913
Toyota IST ncp61. Huo mlio wa kugonga gonga kwenye engine unasikika baada ya engine kupata joto (warm up). Yaani unapowasha gari hausikiki, ila baada ya muda fulani engine ikiwa imewaka au ukiendesha halafu ukapark at idle ndipo huo mlio unasikika. Gari ikiwa kwenye mwendo hausikiki. Nikisimama at idle ndipo unasikika.
Huo mlio ni zaidi ya miezi 6 sasa. Nilianza kuunotice mara baada ya kuanza kuweka 'petrol treatment', japo sina hakika sana na hili.
Inshu nyingine pia: coolant huwa inapungua kwa kiwango kidogo.
Gari ina nguvu vizuri kwenye mwendo. Odometer ni 126,000 KM. Service nazingatia kwa wakati natumia engene oil 5W-30 TOTAL quartz 9000 (full synthetic).
Taa ya check-engine haijawahi kuwaka. Je, naweza kwenda kufanya machine diagnosis? If yes, ni gereji gani kwa hapa Moshi mjini wanafanya diagnosis kwa uhakika? au niende Arusha?
Matengenezo ya nyuma:
Mwaka jana engine iliwahi kukosa nguvu kabisa kwenye kilima/mpando. Tuliondoa 'masega' kwenye eksozi. Tatizo likaisha na engine power ikarejea upya!