Atlas Primary School - Madale, Dar

Atlas Primary School - Madale, Dar

Bahari shule nzuri sana, pia wanangu wanasoma bahari, sikutaka kabisa kuwapeleka atlas

Tatizo letu wazazi hatufanyi maandalizi mapema ya kuwatafutia watoto wetu shule, huwa tunafuata mkumbo na maandalizi ya zima moto, wakati tunataka watoto wasome shule nzuri

Lazima tuwatendee haki, kuanzia mazingira mpaka elimu
Hili dongo linanihusu maana mie nimeshawishiwa tu Na jamaa Angu kuwa Atlas wapo vizuri,lakini nadhani jamaa Angu aliangalia upande wa Taaluma tu.Sasa nami sikufanya upembuzi yakinifu naona hapa napata Challenge hiyo Bora nifanye Sasa upembuzi yakinifu
 
Aiseee Kiongozi hiyo peace and love wapo vizuri kitaaluma? Aiseee ngoja Jumatatu nikaulizie Aiseee
Kwa maoni yangu wapo vizuri, wanajali watoto na malezi ya watoto ni mazuri sana. Wamesajiliwa si muda mrefu mwakani ndo wanafunzi wao wa kwanza wanafanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nne. Kaulize ulete mrejesho kwa faida ya wengine pia.
 
Jamani kwa wale wote tulio na watoto katika shule hii ya Atlas, naomba kwa wale tuliopiga kelele sana kwa ishu ya usafiri tusaidiane tena kupiga humu jamvini ili mamlaka husika zisaidie...

Mimi nina watoto wawili katika shule hii, darasa la tatu na mwingine darasa la kwanza... Shule hii kitaaluma iko poa sana. Tatizo wanafeli sana ktk ishu ya usafirishaji wanafunzi.

Madereva wa shule hii hawana weledi ktk kazi zao, wenyewe kumuacha mtoto ubungo wakati alipaswa kushuka tcra cyo tatizo kwao.

Tumejaribu sana kuuelekeza uongozi wa shule hii kuhusu hili lakini naona wanatia pamba masikioni, baadhi ya magari yao ni mabovu, pia yako machache kiasi kwamba watoto wanapakatana.

Nimekwisha andika barua juu ya hili kwenda wizarani na nasubiria action yao dhidi ya shule hii. Watoto siwahamishi kwakua napenda mfumo wao wa ufundishaji ndiyo maana napambana wawe smart.
Ni vema uwahamishe tu
Maana sisi wa kwetu huku elimubure wanagombea daladala na hakuna noma yoyote.!
 
Kwa maoni yangu wapo vizuri, wanajali watoto na malezi ya watoto ni mazuri sana. Wamesajiliwa si muda mrefu mwakani ndo wanafunzi wao wa kwanza wanafanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nne. Kaulize ulete mrejesho kwa faida ya wengine pia.
Poa mkuu naenda Jumatatu Na nitaleta mrejesho humu
 
Hiyo shule si kuwa ni nzuri sana, basi tu wanakaririsha wanafunzi ili mwakani wapate wengi zaidi.
Mzazi unatakiwa utambue kuwa elimu pekee bila malezi Bora hamsaidii mtoto, mtoto atafaulu ila atafeli maisha
 
Aliniacha hoi siku ya kikao cha wazazi,wazazi wakatoa kero zao na dukuduku likiwepo hilo suala la usafiri.Jibu alilolitoa ni kwamba sisi tumeona ile shule ni nzuri ndiyo maana tunapeleka watoto wetu pale vinginevyo kama tunaona huduma siyo nzuri tusingewapeleka pale.Lilivyotoka hilo jibu niliondoka pale pale
Ni kweli lakini, jamani hiyo shule ina watoto wengi sijapata kuona, hilo naona ndilo linalompa jeuri. Halafu kama ile ya Ubungo mazingira ni hivyo tu hata viwanja vya kucheza watoto hakuna. Watoto wanavushwa barabara kwenda kwenye viwanja vya hosteli za Udsm pale Mabibo. Ukiwaona utawaonea huruma. Mazingira mabovu, ila wanafanya vizuri kwenye mitihani na ada ni nafuu sana ukilinganisha na shule nyingi. Mmiliki analitambua hilo ndio maana anawajibu atakavyo anaamini hamuwezi kuhama na vyuma hivi vilivyokaza.
 
Nilikuwa na mahusiano na dada mmoja mboga saba. Yeye kasoma international schools kuanzia kindergarten mpaka form six. Mwenzie mimi nimesoma public mpaka form six.

Sasa mtazamo wake na wangu juu ya shule ni tofauti. Anaamini mtoto ili afanikiwe lazima apelekwe international schools. Dah ilikuwa mbinde kufikia makubaliano.

Ila personally, siafikiani suala la kumuamsha mtoto saa kumi usiku kisa shule aisee.


NB: shule za serikali zinahitaji wazazi committed lakini. Msije mkaninukuu vibaya. Namshukuru sana baba yangu kwa tuition za nyumbani. Leo hii ninaweza kusimama na mwanafunzi wa background yoyote tukashindana hoja. So, kama unaweza kujitoa muda kumfundisha mwanao...mpeleke hata serikali. Kuamshana usiku si poa.
Unakuta mtoto anakaa mbagala..eti anaenda tusiime...unakutana na watoto saa kumi na moja kasoro wako barabaran kusubiri skul bus....aisee huu ni utesaji kwakweli...
Ofcz primary skul sio ya kutumia nguvu hivyoo km sekondary
 
Watu wanachoipendea hii shule ni Ufaulu na ada,
Kimkoa hua zinashindanaga kati ya Atlas ya Ubungo v/s Atlas ya Madale, zingine zinasubiri pemneni.
Pili ni ada kwani shule wakati shule hii ada ya Mwanafunzi wa chekechea haifikii Tshs 1.4mil, kwa shule ya Sunrise iliyoko pale Morocco eneo loa makochi chekechea hiyo hiyo ni zaidi ya Tshs 4mil na zinalipwa in term of UD
Sio kweli, kimkoa Hazina iko juu, na hiyo ya Madale ndio kabisaa inapitwa na shule kibao kama Lieberman, Rightway etc
 
Watu wanachoipendea hii shule ni Ufaulu na ada,
Kimkoa hua zinashindanaga kati ya Atlas ya Ubungo v/s Atlas ya Madale, zingine zinasubiri pemneni.
Pili ni ada kwani shule wakati shule hii ada ya Mwanafunzi wa chekechea haifikii Tshs 1.4mil, kwa shule ya Sunrise iliyoko pale Morocco eneo loa makochi chekechea hiyo hiyo ni zaidi ya Tshs 4mil na zinalipwa in term of UD
Vipi kuhusu King's ?
 
ATLAS MADALE KUNGUNI KUNGUNI NI KERO KWA WANAFUNZI WA BWENI.. Hili tatizo hata mwenye shule halijali kwani ktk mkutano na wazazi liliulizwa swali kuhusu kunguni na halikujibiwa kabisa. Kuhamiaha mtoto sio suluhisho. hao wanaobaki kunguni watahama na wao kuwa salama mkuu wa ahule aombe msaada wa kitaalamu kutatua tatizo hili vinginevyo aweke vitanda vya chuma na magodoro ya waliopo yapigwe dawa isiyo dhuru maji ya moto wanayo mwagia vitanda ni suluhisho la siku chache sana.

Sent from my HUAWEI Y330-U11 using JamiiForums mobile app
 
Siyo lazima ila kuna madhara anayopata mtoto kuhama shule moja kwenda nyingine. Loosing friends na kwenda ku adapt mazingira Maya. Nadhani unalitambua hilo
Kwaio ni heri uhatarishe maisha yake kisa atapoteza marafiki? hivi unae mtoto kweli wewe?
 
Tupeane uzoefu wa shule tofauti ili tusifanye makosa ya kupeleka mtoto shule kwa kuambiwa na rafiki/ndugu kumbe kimeo ....
 
Back
Top Bottom