Atlas Primary School - Madale, Dar

Atlas Primary School - Madale, Dar

Jamani kwa wale wote tulio na watoto katika shule hii ya Atlas, naomba kwa wale tuliopiga kelele sana kwa ishu ya usafiri tusaidiane tena kupiga humu jamvini ili mamlaka husika zisaidie...

Mimi nina watoto wawili katika shule hii, darasa la tatu na mwingine darasa la kwanza... Shule hii kitaaluma iko poa sana. Tatizo wanafeli sana ktk ishu ya usafirishaji wanafunzi.

Madereva wa shule hii hawana weledi ktk kazi zao, wenyewe kumuacha mtoto ubungo wakati alipaswa kushuka tcra cyo tatizo kwao.

Tumejaribu sana kuuelekeza uongozi wa shule hii kuhusu hili lakini naona wanatia pamba masikioni, baadhi ya magari yao ni mabovu, pia yako machache kiasi kwamba watoto wanapakatana.

Nimekwisha andika barua juu ya hili kwenda wizarani na nasubiria action yao dhidi ya shule hii. Watoto siwahamishi kwakua napenda mfumo wao wa ufundishaji ndiyo maana napambana wawe smart.
Kwani umeshikiwa bastola kwa watoto wako kusoma huko?
 
Ipo wapi? Mimi namuonea huruma mwanangu kumpeleka shule za mbali, afadhali ya hii anapitiwa saa 1.
Ipo karibu na bahari beach hotel,, ukipita chuo cha Jeshi (DEFENCE COLLEGE )
pale kunduchi
 
Nyie wazazi mabashite kweli. Hilo linawashindaje wakati shule ni private na mnatoa hela zenu.
Watu wanachoipendea hii shule ni Ufaulu na ada,
Kimkoa hua zinashindanaga kati ya Atlas ya Ubungo v/s Atlas ya Madale, zingine zinasubiri pemneni.
Pili ni ada kwani shule wakati shule hii ada ya Mwanafunzi wa chekechea haifikii Tshs 1.4mil, kwa shule ya Sunrise iliyoko pale Morocco eneo la makochi chekechea hiyo hiyo ni zaidi ya Tshs 4mil na zinalipwa in term of USD
 
Namtoa kabisa Atlas sitaki wanipe presha, Dereva unampigia anakupa majibu mepesi kabisa kama vile kaacha boga
Na chakushangaza dereva ndiyo anapanga kituo cha kumpitia mtoto,na darasa lina wanafunzi wengi mno.
 
Me mwanangu nishamtoaga nimempeleka bahari primary kitambo
Bahari shule nzuri sana, pia wanangu wanasoma bahari, sikutaka kabisa kuwapeleka atlas

Tatizo letu wazazi hatufanyi maandalizi mapema ya kuwatafutia watoto wetu shule, huwa tunafuata mkumbo na maandalizi ya zima moto, wakati tunataka watoto wasome shule nzuri

Lazima tuwatendee haki, kuanzia mazingira mpaka elimu
 
Hili tatizo lipo mno..sio Atlas ya madale tu hata ya Ubungo watoto wanapakatana wengine wanasimama.Ilitulazimu kuwaamisha watoto Hazina tu maana walikua wanasimama kutokea Kinondoni hadi Ubungo.Ila kwa taaluma wanajidahidi usafir ndo wanakosea mno.Wajirekebishe kwa hili.
 
Jamani kwa wale wote tulio na watoto katika shule hii ya Atlas, naomba kwa wale tuliopiga kelele sana kwa ishu ya usafiri tusaidiane tena kupiga humu jamvini ili mamlaka husika zisaidie...

Mimi nina watoto wawili katika shule hii, darasa la tatu na mwingine darasa la kwanza... Shule hii kitaaluma iko poa sana. Tatizo wanafeli sana ktk ishu ya usafirishaji wanafunzi.

Madereva wa shule hii hawana weledi ktk kazi zao, wenyewe kumuacha mtoto ubungo wakati alipaswa kushuka tcra cyo tatizo kwao.

Tumejaribu sana kuuelekeza uongozi wa shule hii kuhusu hili lakini naona wanatia pamba masikioni, baadhi ya magari yao ni mabovu, pia yako machache kiasi kwamba watoto wanapakatana.

Nimekwisha andika barua juu ya hili kwenda wizarani na nasubiria action yao dhidi ya shule hii. Watoto siwahamishi kwakua napenda mfumo wao wa ufundishaji ndiyo maana napambana wawe smart.
Sasa mkuu haya maoni yako si ungeyatoa moja kwa moja kwa management ya shule?
 
Back
Top Bottom