Mawazo kwamba, Mungu hayupo ni upotofu wa baadhi ya watu walio au wanaoelewa kimakosa sayansi. Hawa si tu kwamba wanaelewa kimakosa sayansi, lakini pia hawaelewi sayansi inatokana na nini. Hawa humkataa Mungu kwa madai kwamba, ameshindwa kuwasaidia wanadamu katika matatizo yao kama vile magonjwa, vita, njaa, umasikini, n.k. Wakati huohuo, wao hawatazami; wala hawazingatii namna wao walivyo chanzo cha uharibifu huo-hili hawafikiri kama wanahusika, inasikitisha! Kama unaelewa vizuri mafundisho ya dini sahihi, utaelewa wazi kabisa kwamba, sayansi haiwezi kuwepo bila kwanza kuwepo dini sahihi-Mungu na hivyo sayansi inafafanua na kumdhihirisha waziwazi Mungu kwetu. Pia, watu ni lazima tutafute elimu nzuri, bila ya elimu sahihi hakuna tutakachoweza kujua na kuelewa kuhusu sayansi, saikolojia, falsafa na kisha teolojia. Bila elimu sahihi ya sayansi, saikolojia na falsafa huwezi kujua Mungu. Vinginevyo ufunuliwe.