Infropreneur
JF-Expert Member
- Aug 15, 2022
- 5,250
- 10,747
Habari ndugu wana jamii forums.
Kwa muda mrefu sana watu wasio amini uwepo wa Mungu "Atheist" wamekuwa wakipingwa, kukosolewa na kuonekana kama watu wa ajabu kutokana na mitazamo yao tofauti kuhusu swala la uwepo wa Mungu.
Jamii ya watu wanao amini Uwepo wa Mungu na waamini wa dini mbalimbali wamekuwa wakipinga Hoja za "Atheist" kwa nguvu kubwa na kukataa kabisa kukubali Hoja na mawazo ya Atheist na Huona na huchukulia Hoja za "Atheism" kama ni za kipuuzi na zisizo faa wala kuwa na mantiki, kutokana na Mitazamo yao ya Kidini na kiimani.
Dhana ya "Uwepo wa Mungu" ama "kutokuwepo kwa Mungu" vyote ni HISIA NA MAWAZO YA KIBINADAMU.Wapo wanadamu waliwaza na wanahisi Mungu yupo na hawana ushahidi wala uthibitisho kamili wa kuonekana kwa macho kuthibitisha uwepo wa Mungu, ila wana Hisia na Imani tu iliyo kwenye maandiko wanayodai ni maandiko ya huyo Mungu, Maandiko ambayo pia hayana ukweli wala uthibitisho wowote.Maandiko ya kiimani (vitabu vya kidini) vinatumika na "waamini Mungu yupo" kwamba ndio Kielelezo na Hoja tosha na thabiti za kudhihirisha na kuelezea uwepo wa Mungu na Maandiko haya haya ya kiimani (Kidini) hutumiwa na waamini Mungu yupo kukosoa na kupinga Hoja za "Atheist" wanapo jaribu na wao kutoa hoja zao kuhusu kutokuwepo Mungu.
Wanao amini "Mungu Yupo" hutumia Vitu na maswali yaliyo washinda kupata majibu kwa kufikiri, kuwaza ama kwa kuvifanya wao, kama kigezo cha kudai "uwepo wa Mungu"na Hubakia kusema kwamba chanzo na majibu ya vitu hivi ni MUNGU bila kuwa na uhakika, ushahidi wala uthibitisho wa wakisemacho.
Mfano, Baada ya watu kushindwa kupata majibu ya Nani aliumba Dunia na vilivyomo ndani yake kama:Jua, Nyota, Mwezi,Bahari,Mito,Maziwa, Wanyama, Mimea, Ardhi,Anga,n.k pia maswali kama kwa nini tulizaliwa na tunakufa? Kwa nini tusi ishi milele? Watu hawa sasa, Wakaja na kuunda dhana kwamba Mungu ndiye chanzo cha haya yote lakini hawana uthibitisho wala ushahidi wa dhana hii, Wanabaki wanahisi tu Mungu ndiye chanzo cha uumbaji..Pia kwa vile ni Hisia, imani na mawazo tu ya kibinadamu Hakuna ULAZIMA wa Dunia na Vilivyomo ndani yake kuwa viliumbwa na Mungu kwa sababu hamna aliye na uthibitisho kila mtu ana hisi tu jinsi aonavyo yeye.. pengine kuna kitu kingine tofauti na Mungu ndio kilifanya Dunia iwepo.
Akili ya kila mwanadamu huwaza chochote ikipendacho na ipo huru kufanya hivyo..Anayewaza "Mungu yupo" Asimkosoe anaye waza "Mungu hayupo" maana wote wanawaza tu, Na wote wapo huru kimawazo na hamna aliye na mamlaka ya kukosoa mawazo ya mwenzake, ....."Atheist" pia wana mawazo na hoja zao za kupinga "Kutokuwepo kwa Mungu" na wapo huru kufanya hivyo maana wao pia wana Hisia za "Kutokuwepo Mungu"
Hivyo basi kama Huna uthibitisho,na ushahidi wa Uwepo wa Mungu USIJE kuona na kudhani hisia zako ndio sahihi kuliko za mwingine asiye amini Uwepo wa Mungu.
Usihalalishe Imani, Dini,Hisia, mawazo na mtazamo wako wa "Uwepo wa Mungu" kuwa mawazo ya kila mtu na jamii nzima kwa kigezo cha mafundisho uliyofunzwa au Hofu zako tu,na kuona Imani, hisia, mawazo na mtazamo wa "Kutokuwepo Mungu" kwa upande wa Atheist kuwa sio sahihi maana utakuwa unajaribu kulazimisha Akili na ubongo wa mtu kufuata jinsi Akili yako inavyo waza.Lazima utambue kwamba kila mtu yupo huru kufikiri na mawazo ya binadamu yanatofautiana hivyo kupinga hoja za Atheist kwa kigezo cha Imani au Dini yako ilivyo kufunza ni upofu wa fikra na uelewa mdogo wa kiakili.
Hitimisho, Ukisema "Mungu yupo" kwa vile unahisi tu, Au una amini hivyo kulingana na ulivyo aminishwa, Hiyo inabaki imani na mtazamo wako visivyo na ushahidi wala uthibitisho wowote bali ni imani na Hisia zako tu,..Vivyo hivyo usije kukosoa mawazo, mitazamo na Hisia za Atheist za "kutokuwepo Mungu" kwa hofu zako tu bila kuwa na uthibitisho kamili maana wote "Wanao amini Mungu yupo" na "Wasio amini Mungu Yupo",Tunawaza tu na kukisia mawazo yetu, bila kuwa na uthibitisho nayo.
Hivyo hisia,imani na mawazo ya mtu mmoja au kikundi cha watu fulani hayawezi kuthibitishwa na kuhalalishwa kama mawazo ya jamii nzima.. Atheist wapo sahihi, Na wanao amini Mungu Yupo pia wapo sahihi kila mtu kulingana na jinsi aonavyo yeye.. KILA MTU YUPO HURU KUFIKIRI...!!
BE A FREE THINKER...