Nafsi yenyewe ni chanzo cha uovu kwa sababu ya ule uelekeo wake mbaya. Katika Malaka yake, Effects of Sins on the Human Personality: In the Light of Islam and Modern Psychology, Dkt. Gohar Mushtaq wa Chuo Kikuu cha Rutgers, Marekani, kaandika,
“There are two enemies who persuade human beings to commit evil acts. One is internal-human self (nafs), and the other is external-Satan.”
Kwamba kuna maadui wawili wanaowachochea watu kutenda maovu-wa kwanza ni wa ndani- yaani nafsi, na wa pili ni wa nje-yaani Shetani.”
Qur’an imeainisha nafsi tatu; Nafs al-Ammara yenye uelekeo mbaya (12:53), Nafs al-Lawwama (75:2) ambayo hujisikia vibaya kutenda maovu, hujuta na kutubu, Nafs al-mut’mainna (89:27) ambayo ni tulivu na ambayo hufikiwa baada ya mtu kufaulu mitihani mingi.
Tuone jinsi Yusuf alivyoushinda mtihani wa zinaa licha ya shinikizo la upande wa pili. “Nami siiendekezi nafsi yangu; kwa hakika nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu.” (12:53).
Yusuf hakusema, nami simuendekezi Shetani bali kaitaja nafsi mbaya, na kweli alipoidhibiti, akashinda mtihani bila kujali uwepo wa Shetani.Hapo tunapata ufafanuzi wa moja kwa moja kuwa binadamu ana mtihani na nafsi yake hata kabla ya kushawishiwa na Shetani.
Hata ukimuondoa Shetani, nafsi inaweza kujitumbukiza katika uovu yenyewe ndiyo maana Yusuf kasema yeye asingeiendekeza nafsi yake.