Athari za Ongezeko la Tozo mpya za Miamala ya Simu kwa Watanzania

Jul 14, 2021
5
45
Siku chache baada ya tozo za miamala ya simu kuongezeka kutoka makato ya awali wakati wa kutuma pesa au kutoa pesa mpaka Makato ya sasa amambayo yapo na yanatumika Nini athari zake kwa watanzania

1. KUDORORA KWA BIASHARA ZA MTANDAONI

Biashara za mtandaoni zitapoteza wateja na kudorola hususani kwa vijana wanaofanya biashara za nguo na kadharika kwa njia ya mtandao na makampuni ambayo huuza bidhaa zao kwa njia ya mtandao hii ni kwasababu ya gharama kuwa kubwa ya kutuma pesa lakini pia kwa waujazi kuhofia kupoteza faida wakati wa kutoa pesa hivyo kunauwezekano mkubwa wa kushindwa kufanya biashara ya mtandao hivyo biashara hii kukosa wadau na kudorola

2. WATU KUPOTEZA AJIRA

Watu wengi waliojiajiri kwa njia ya mtandao watapoteza ajira kwa kukosa wateja ambao ndio wanunuzi wakubwa wa bidhaa zao kwa kuhofia kupoteza fedha nuingi wakati wa uagizaji bidhaa mtandaoni au kuhofia kulipia kiwango kikubwa Cha fedha wakati wa uagizaji bidhaa hivyo watu itawalazimu kwenda madukani kununua bidhaa hizo na Wala sio kuagiza online hivyo Basi waliojiali kwa kuuza bidhaa online watapoteza ajira zao kwa kukosa wateja.

Lakini pia mawakala watafunguka kazi zao kwa kukosa ajira hii nikutokana na KUPUNGUA kwa watumiaji wa huduma za kifedha kwa njia ya simu hili litafanya mawakala kupoteza kazi zao

3. MZUNGUKO WA FEDHA KUPUNGUA

Kutokana na ongezeko la tozo mzunguko wa fedha utapungua hii ni kwasababu watu hataweka fedha katika simu zao kwaajili ya kufanya manunuzi ya bidhaa kwa kuogopa kukatwa kiasi kikubwa Cha fedha wakati wa kutoa au kutuma hivyo watu watabaki na fedha zao majumbani na sio kuzizungusha katika biashara

4. KUONGEZEKA KWA VITENDO VIOVU

Mfano ukabaji na ujambazi: Vitendo hii vitaongeza kwasababu watu watajua wakitembea na fedha tasilimu badala ya kuweka kwenye simu kwa kuhofia Makato makubwa wakati wa kutoa pesa hizo hivyo watu wenye Nia mbaya watatumia hili suala Kama fursa ya kufanya matendo mauvo ya kivamia watu na kuwanyang'anya fedha zao ongezeko la tozo litachochea majambazi kuwa wengi wakiamini kuwa watu wanaishi na fedha tasilimu ndani

Hivyo ili kunusuru hayo yote, serikali inapaswa kufanya mapitio ya Sheria ya Kodi ya mshikamano ili kuwasaidia watanzania na sio kuwaumiza watanzania
 

Come27

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
6,046
2,000
Bibi samahani sikuwa na ziada ya hela ndio maana imekuja pungufu kwakua Serikali imeichukua kwa nguvu. Samahani sana Bibi nakuombea upone haraka nikipata nitatuma tena na serikali itachukua tena.
Ukiwaambia watu wa mitandao kwamba ni ya matibabu, hawakati
Ugali na maharagwe, umearibu akili zetu waafrica
 

Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
11,835
2,000
Bibi samahani sikuwa na ziada ya hela ndio maana imekuja pungufu kwakua Serikali imeichukua kwa nguvu. Samahani sana Bibi nakuombea upone haraka nikipata nitatuma tena na serikali itachukua tena.
Huko ni kuichonganisha ccm na wazee
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom