DOKEZO Gharama za Lipa namba ziwekwe wazi kama miamala mingine

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Mtandao ya simu imerahisisha huduma ya kulipa vitu mbalimbali ikiwemo malipo ya serikali na biashara binafsi. Ni kawaida kwa sasa kukuta biashara ina LIPA NAMBA ambapo mtu anaweza kulipa kwa namba hiyo.

Hata hivyo katika kutumia lipa namba, kuna gharama ambayo mteja anakatwa, lakini gharama hizi haziko wazi kama gharama za kutuma, kupokea na kutoa fedha, ambazo makato yake utaona yameandikwa.

Naona ni muhimu mitandao yote inayosapoti lipa namba iweke gharama za kila muamala wazi ili mteja achague kutumia lipa namba au kulipa kwa fedha taslimu.

Nawasilisha, nikiwa nimekasirika kwa kukatwa 800Tsh kwa kufanya malipo ya Tsh 15,000

Kwa wenzetu wa Kenya gharama za Lipa Namba ziko wazi, angalia hapa https://www.safaricom.co.ke/images/Downloads/paybill-standard-tariff.pdf

Screenshot 2024-01-30 at 10-03-17 paybill-standard-tariff.pdf.png
 
Sasa umekatwa 800 tu kwenye 15000 vipi aliyekatwa 7000?
Aliyekatwa 7,000 akiwa anatoa bei gani?umeelewa kwanza hoja ya mleta mada?

Iko hivi, ukiingia kwenye uwanja wa kulipa ukifika hatua ya kukamilisha muamala ilibidi uonyeshwe kwa muamala huo utakatwa kiasi gani cha pesa?

Unakuta mteja anataka kufanya manunuzi store zaidi ya moja, hapa alipe 15K, pale 12K kule 25k ni kusema ada atalipa zaidi ya 3K sasa kama anaonyeswa mapema kwa kila muamala kwamba atakatwa kiasi gani ni bora aende kwa wakala kutoa 52K ambayo makato hayazidi 2K.
 
Hivi hii kabla ya kulipa haioneshi gharama? Natumia Tigo App kulipa na LipaNamba huwa inanionesha makato kabla sijalipa.
 
Mimi pia nakazia. Kama mtoa mada alivyosema, huduma ya LIPA NAMBA ni wizi tu, kwani wakala anakukadiria gharama atakayokutoza huyu ni tofauti na wakala mwingine. Sasa mteja, unatafuta wapi wakala mzuri ambaye hana makato makubwa? Nyakati nyingine mnakubaliana kwenye pesa yako.

Na patwa na gazabu pindi wakala unapofika ofisini kwake anakwambia utumie LIPA NAMBA. Unamwambia, "Mimi LIPA, sitaki kutumia." Unajibiwa, "Huduma hiyo haipo."

Issue ya LIPA NAMBA ipo shida sehemu, ila mtu ukiwa na haraka zako huwezi kuelewa. Mimi LIPA NAMBA nimeikataa kutumia. Bora pesa yangu nigawane na wenye mtandao wao na nchi yangu.
 
Mtandao ya simu imerahisisha huduma ya kulipa vitu mbalimbali ikiwemo malipo ya serikali na biashara binafsi. Ni kawaida kwa sasa kukuta biashara ina LIPA NAMBA ambapo mtu anaweza kulipa kwa namba hiyo.

Hata hivyo katika kutumia lipa namba, kuna gharama ambayo mteja anakatwa, lakini gharama hizi haziko wazi kama gharama za kutuma, kupokea na kutoa fedha, ambazo makato yake utaona yameandikwa.

Naona ni muhimu mitandao yote inayosapoti lipa namba iweke gharama za kila muamala wazi ili mteja achague kutumia lipa namba au kulipa kwa fedha taslimu.

Nawasilisha, nikiwa nimekasirika kwa kukatwa 800Tsh kwa kufanya malipo ya Tsh 15,000

Kwa wenzetu wa Kenya gharama za Lipa Namba ziko wazi, angalia hapa https://www.safaricom.co.ke/images/Downloads/paybill-standard-tariff.pdf

View attachment 2888087
Kwenye chati ya hizo tozo za Kenya wana makato madogo sana ukilinganisha na TZ.

Ukitoa/lipa 70,000 hadi 250,000 ya kenya mteja anatozwa KSh 24 tu sawa na Tsh 384 tu.
 
Back
Top Bottom