Kwanini unapofanya miamala kwa benki gharama za miamala huwa haziwekwi wazi ujue kabla hujatuma?

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,308
6,884
Kama ni mtumiaji wa simu katika kufanya miamala kwa mitandao ya simu na bank kuna jambo moja la tofauti utaligundua.

Unapofanya miamala kwa kampuni hizi za mitandao ya simu gharama za muamala huwa zinawekwa wazi ujue kabla hujatuma.

Lakini kwa bank hali ni tofauti hawaonyeshi gharama ni mpaka utume na kurudi kuangalia tena salio. Kwanini wanaficha? Au ni kwasababu wanagharama kubwa za gharama miamala? Wana wasiwasi zikiwa wazi watu watasitisha kufanya miamala?

Mfano juzi nimetuma hela kutoka bank nyingine kwenda nyingine kiwango cha 100,000 nimekatwa 10,000. Je ningejua kabla hii gharama ningefanya muamala?

Kwanini gharama zao ni kubwa sana?
 
Ni changamoto kwa kweli sijui kwanini hawafanyi hivyo wakati inawezekana kabisa, japo kwa kila benki nafikiri kila mwaka hutoa tariff (nafikiri jina sahihi ni bank charges) za gharama zao zote kuanzia kutuma mpaka kutunza akaunti na huwa inapostiwa kwenye tovuti zao.

Inabidi ufanye kazi ya ziada kidogo kuingia mtandaoni na kudownload hiyo PDF kitu ambacho hakina ulazima walipaswa kufanya hivyo kwenye muamala unaofanya.
 
Lakini kwa bank hali ni tofauti hawaonyeshi gharama ni mpaka utume na kurudi kuangalia tena salio.
Kwanini wanaficha? Au ni kwasababu wanagharama kubwa za gharama miamala?
Mkuu kila benki kila mwaka wanatoa orodha yote ya charges kwa mwaka husika. Ikiwa mteja hajui inakuwa ni uzembe.
 
Kama ni mtumiaji wa simu katika kufanya miamala kwa mitandao ya simu na bank kuna jambo moja la tofauti utaligundua.

Unapofanya miamala kwa kampuni hizi za mitandao ya simu gharama za muamala huwa zinawekwa wazi ujue kabla hujatuma.

Lakini kwa bank hali ni tofauti hawaonyeshi gharama ni mpaka utume na kurudi kuangalia tena salio.
Kwanini wanaficha? Au ni kwasababu wanagharama kubwa za gharama miamala? Wana wasiwasi zikiwa wazi watu watasitisha kufanya miamala?

Mfano juzi nimetuma hela kutoka bank nyingine kwenda nyingine kiwango cha 100,000 nimekatwa 10,000. Je ningejua kabla hii gharama ningefanya muamala?

Kwanini gharama zao ni kubwa sana?
kwani ukienda benki kufanya TISS kwenda benki nyingine makato ni kiasi gani?
 
Ni changamoto kwa kweli sijui kwanini hawafanyi hivyo wakati inawezekana kabisa, japo kwa kila benki nafikiri kila mwaka hutoa tariff (nafikiri jina sahihi ni bank charges) za gharama zao zote kuanzia kutuma mpaka kutunza akaunti na huwa inapostiwa kwenye tovuti zao.

Inabidi ufanye kazi ya ziada kidogo kuingia mtandaoni na kudownload hiyo PDF kitu ambacho hakina ulazima walipaswa kufanya hivyo kwenye muamala unaofanya.
Mitandao ya simu inazo pia mpaka kwa mawakala wamebandika lakini bado kwenye kufanya transaction wanakuonyesha
 
Week hii nmefanya miamala 4 benki ya NBC jumla sh 40000 wamenifyeka elfu 13 kama makato, nmekuja kugundua baada ya kuangalia salio... Aisee makato ya benki ni makubwa hasa hizi Sim banking yani ni bora uende ATM
 
Back
Top Bottom