ATCL kuanza na kosa la kwanza

ATCL kuanza na kosa la kwanza

Mbona imekuuma sana! kunani? Sioni kosa alilolifanya binti! "huyo rais wenu" ni tusi? Mahaba yasizidi uhalisia wa jambo, hajatukana hata kidogo.
Mkuu Chuakacha, hakuna aliyesema katukana, nimesema amekosa heshima, makabila mengine, kazi ya mwanamke mrembo ni moja tuu, inapotokea akakosa heshima kwa wengine, kwenye yale mengine inaweza kuwa hatari! . Imeniuma kwa sababu huyo binti nampenda.
Pasco
 
Kaka,
Inasemekana ukitoa ushauri murua ka huu weye ni chocheziii kwa sababu umepinga maagizo au unasababisha watu wapinge maagizo. Lakini, umeeleza kiufasaha japo tofauti ni heading yako ila wenye akili wamesikia ujumbe.
Swali ni Je, kuna CEO atakayethubutu hata kujifanya kasahau maelekezo afuate ushauri wako murua?? Hapo sasa kwa sababu atakuwa ameokoa nyingi tu. Lakini huwezi kujua, pengine kuna mtu wangu au nyumba yangu nataka viufaidi mchezo huu kwa maagizo kufuatwa. Mkija ng'amua nimeshapata angalao nusu.

Kuhusu uthubutu wa CEO muulize Tido Mhando kama kuna mtu ana namba yake akutumie
 
Mkuu Chuakacha, hakuna aliyesema katukana, nimesema amekosa heshima, makabila mengine, kazi ya mwanamke mrembo ni moja tuu, inapotokea akakosa heshima kwa wengine, kwenye yale mengine inaweza kuwa hatari! . Imeniuma kwa sababu huyo binti nampenda.
Pasco
Pasco unamfahamu au ni ya humu JF? Pasco una kitu sijakipenda: Kazi ya mwanamke makabila mengine!!!!? It signifies mfumo dume on the move! Mwanamke kwa sasa we are on the equal footing. Akikusikia Kisimba mtagombana. Kazi ya mwanamke mrembo ni moja!!! Omba radhi!
 
Hii moja ya post zenye hoja zenye mantiki sana. Big up mleta mada.
Hili la kuwatumia mawakala halikwepeki. Napenda kuamini Prof. Mbarawa anao uwezo wa kumpa taarifa sahihi Rais na akabadili mawazo yake.
Subutu yaani aonekane kamzidi uelewa ambapo yeye kaelekeza vile kwanza atakuwa hajipendi kwa mfumo huu kwa sasa kila mmoja anaogopa kutumbuliwa hivyo hata kama unauelewa wa kutosha juu ya jambo flani inakulazimu uwe kimya kwa muda
 
Hoja ya msingi ya mtoa mada ni kuwa ATCL itakufa kwa sababu wakilala wakiamka, siku baada ya siku, watafanya kazi kwa kuzingatia matakwa ya Juma badala ya matakwa ya shirika na ya biashara!
 
Hoja ya msingi ya mtoa mada ni kuwa ATCL itakufa kwa sababu wakilala wakiamka, siku baada ya siku, watafanya kazi kwa kuzingatia matakwa ya Juma badala ya matakwa ya shirika na ya biashara!

Hayo matakwa ya Juma ni yepi hayo?
 
mkuu sikuhizi systems zimebadirika! ulisafiri lini mala ya mwisho? I mean international freight? huwakilakitu kiko online na mawakala huwa makampuni mengi wanadiscourage! Ila ni hoja ukizingatia systems ya zamani hapo agents role yao ilikua kubwa
Hivi mkulu mwenyewe anamaanisha hivi unavyosema wewe? Je, wa-TZ wataweza kulipa online? Hizo kadi wote wanazo? Au fedha inapolipwa kwa mpesa, tigopesa, Halomoney, zainpesa huo siyo uwakala? Naye anaongea sana huyu hebu aachie wataalam wa Biashara wafanye kazi yao!
 
ATCL kama yalivyo mashirika mengine ya umma, kila mara imekuwa ikizaliwa na kufa kutokana na muundo wake usiokuwa wa kibiashara. TANESCO isiyo na mshindani yeyote, TTCL ambayo awali haikuwa na mshindani, na mengine mengi yaliyokwishakufa na yaliyouzwa, mashirika yote hayo yalikufa kwa sababu yalianzishwa, kuendeshwa na kusimamiwa kiserikali/kisiasa.

Serikali haijawahi kuendesha biashara ikafanikiwa. Tatizo linaanzia kwenye muundo wa haya mashirika/makampuni. Wanasiasa/viongozi wa serikali ambao kimsingi si wafanyabiashara ndiyo waliotengeneza muundo wa uendeshaji na ndiyo wenye kauli ya mwisho. Vigezo vya wajumbe wa bodi na watendaji wakuu wanavyo wao. Na siku hizi PhD imekuwa ni kigezo kikubwa sana ingawa kiuhalisia, kwa Dunia nzima, ni nadra sana kuwaona wenye PhD wakiwa wafanyabiashara wazuri na waliofanikiwa.

Juzi wakati Mh. Rais akizindua ujio wa ndege mpya alisema ATCL imezaliwa upya, ina ndege mpya, bodi mpya na uongozi mpya, sikusikia kama ina muundo mpya wa uendeshaji na usimamizi. Bado inaonekana ATCL itandeshwa kwa mkono wa serikali.

RAIS - 'ATCL ISITUMIE MAWAKALA WA KUKATISHA TIKETI'

Hili tayari ni agizo ambalo naamini ni agizo lisilo sahihi. Tayari serikali imeanza toka hatua za mwanzo kuingilia uendeshaji wa ATCL. Rais anapoagiza ATCL isitumie mawakala wa kukatisha tiketi inamaanisha ATCL iwe na wafanyakazi waajiriwa kila mahali nchini. Gharama za maelekezo hayo itakuwa kama ifuatavyo:
  • ATCL italazimika kuwalipa wakatisha tiketi mishahara, matibabu, posho, michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, usafiri, n.k. ATCL italazimika kulipia gharama hizo zote bila ya kujali mkatisha tiketi anakatisha tiketi ngapi au kama amepata wateja au hakupata kabisa
  • ATCL italazimika kulipia ofisi na kuweka miundombinu ya ukatishaji ticket nchi nzima. Ifahamike kuwa ukitaka kuwa na ufanisi unalazimika kuwa na ofisi za ukatishaji tiketi hata mahali ambapo ndege haitui, kwaajili ya kuhudumia abiria wanaotoka maeneo hayo wanaotarajia kutumia usafiri wa ATCL kutokea uwanja ulio karibu
  • ATCL italazimika kuwapa mafunzo wakatisha ticket watakaotapakaa nchi nzima
Wakati ATCL watakapokuwa wanahangaika na kuwa na wakatisha ticket wao na ofisi zao, washindani wao wataendelea kuwa na wafanyakazi wachache, wakiwa na mawakala wengi wanaolipwa kutokana na idadi ya ticket na thamani ya ticket walizokatisha. Hawalipii ofisi, hawalipii matibabu, hawalipii michango ya hifadhi ya jamii, hawalipii likizo ya mfanyakazi. Mawakala wao wanalipwa kutokana na wanachozalisha, wasipozalisha hawalipwi chochote.

ATCL wanaanza na quandary ya kwanza, wafuate maagizo ya mwenye mali au kanuni za biashara? Je, hii ni ya mwanzo na ya mwisho au zitaendelea kuja na nyingine? Kwa kuwa tatizo la msingi la uendeshaji biashara zilizo chini ya serikali halijatatuliwa, haitakuwa jambo la ajabu ATCL kufuata projectile ya mashirika/makampuni ya umma.
Tiketi utanunua kwa internet,M-Pesa na Tigo pesa,wakala wa nini?wizi mtupu
 
Mleta mada anaonekana anawatetea mawakala au "middlemen".
Kuna wakala kapiga milioni 700 Comoro,siku hizi kila kitu mtandaoni,ikifika jioni hela yote inaonekana kwenye akaunti ya shirika
 
Pasco nakubaliana nawe kuwa siku hizi mashirika ya ndege karibia yote Duniani yanatumia online services. Lakini hata huko kuna agents. Unaposema ATCL wasitumie mawakala, ina maanisha itakuwa na miundombinu yao? Lakini pia tusiukatae ukweli kuwa bado watanzania wengi hawatumii online services. Ndiyo maana ukienda ofisi za fastjet, pamoja na kuwepo online service bado unawakuta wateja wamejazana. Sina uhakika kati ya wateja wanaotumia online service na wale wanaokata ticket zao kwenye ofisi, ni ipi idadi ambayo ni kubwa.

Unayefanya biashara, unatafuta faida na wateja wengi, hata kama una online service bado utalzimika uwatafute kwa njia nyingine yoyote ambayo itakupa wateja wengi zaidi.
Ungesoma vizuri majibu ya Pasco usingeendelea tena na ubishi usio na mbele wala nyuma.
 
Hii moja ya post zenye hoja zenye mantiki sana. Big up mleta mada.
Hili la kuwatumia mawakala halikwepeki. Napenda kuamini Prof. Mbarawa anao uwezo wa kumpa taarifa sahihi Rais na akabadili mawazo yake.
Waache wataalam kutoka Rwanda wafanye kazi yao kaeni KIMYAAAA
 
Sio kila anayepinga ni bavicha or whatever you think. Kwa dunia ya sasa huwezi kufanya kazi bila agents, agents wa kielectroniki sio wale wa kizamani, na ndio maana hata UDART aliamua kutumia agent ie, MAXMALIPO kuongeza ufanisi wa kukusanya mapato.

ATCL waweke online ticket and booking(that's an agent), watumie networks kama mpesa nk(hao ni maagenti) na wawe na clearing office kwenye destination zote.

Kwa karne hii huwezi kukwepa mawakala, hata KLM nk wanatumia online agents kuuza tickets.

Angalau sasa unaanza kuja na hoja zinazojadilika
 
Mbona nasikia anapeta tu huko,kanunua majumba,kwa nini isiambiwe serikali rafiki sana ya Comoro itupe hizo nyumba tuzipige mnada tu

Labda kama si mtanzania lakini kesi za namna hii huwa haziishi na ataendelea kuwa "fugitive"
 
Back
Top Bottom