ATCL kuanza na kosa la kwanza

ATCL kuanza na kosa la kwanza

Jamani bila wakala ni ngumu. Ticket kwa m pesa haiwezekani kwani hautajua kama ndege ina nafasi au imejaa.
 
ATCL kama yalivyo mashirika mengine ya umma, kila mara imekuwa ikizaliwa na kufa kutokana na muundo wake usiokuwa wa kibiashara. TANESCO isiyo na mshindani yeyote, TTCL ambayo awali haikuwa na mshindani, na mengine mengi yaliyokwishakufa na yaliyouzwa, mashirika yote hayo yalikufa kwa sababu yalianzishwa, kuendeshwa na kusimamiwa kiserikali/kisiasa.

Serikali haijawahi kuendesha biashara ikafanikiwa. Tatizo linaanzia kwenye muundo wa haya mashirika/makampuni. Wanasiasa/viongozi wa serikali ambao kimsingi si wafanyabiashara ndiyo waliotengeneza muundo wa uendeshaji na ndiyo wenye kauli ya mwisho. Vigezo vya wajumbe wa bodi na watendaji wakuu wanavyo wao. Na siku hizi PhD imekuwa ni kigezo kikubwa sana ingawa kiuhalisia, kwa Dunia nzima, ni nadra sana kuwaona wenye PhD wakiwa wafanyabiashara wazuri na waliofanikiwa.

Juzi wakati Mh. Rais akizindua ujio wa ndege mpya alisema ATCL imezaliwa upya, ina ndege mpya, bodi mpya na uongozi mpya, sikusikia kama ina muundo mpya wa uendeshaji na usimamizi. Bado inaonekana ATCL itandeshwa kwa mkono wa serikali.

RAIS - 'ATCL ISITUMIE MAWAKALA WA KUKATISHA TIKETI'

Hili tayari ni agizo ambalo naamini ni agizo lisilo sahihi. Tayari serikali imeanza toka hatua za mwanzo kuingilia uendeshaji wa ATCL. Rais anapoagiza ATCL isitumie mawakala wa kukatisha tiketi inamaanisha ATCL iwe na wafanyakazi waajiriwa kila mahali nchini. Gharama za maelekezo hayo itakuwa kama ifuatavyo:
  • ATCL italazimika kuwalipa wakatisha tiketi mishahara, matibabu, posho, michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, usafiri, n.k. ATCL italazimika kulipia gharama hizo zote bila ya kujali mkatisha tiketi anakatisha tiketi ngapi au kama amepata wateja au hakupata kabisa
  • ATCL italazimika kulipia ofisi na kuweka miundombinu ya ukatishaji ticket nchi nzima. Ifahamike kuwa ukitaka kuwa na ufanisi unalazimika kuwa na ofisi za ukatishaji tiketi hata mahali ambapo ndege haitui, kwaajili ya kuhudumia abiria wanaotoka maeneo hayo wanaotarajia kutumia usafiri wa ATCL kutokea uwanja ulio karibu
  • ATCL italazimika kuwapa mafunzo wakatisha ticket watakaotapakaa nchi nzima
Wakati ATCL watakapokuwa wanahangaika na kuwa na wakatisha ticket wao na ofisi zao, washindani wao wataendelea kuwa na wafanyakazi wachache, wakiwa na mawakala wengi wanaolipwa kutokana na idadi ya ticket na thamani ya ticket walizokatisha. Hawalipii ofisi, hawalipii matibabu, hawalipii michango ya hifadhi ya jamii, hawalipii likizo ya mfanyakazi. Mawakala wao wanalipwa kutokana na wanachozalisha, wasipozalisha hawalipwi chochote.

ATCL wanaanza na quandary ya kwanza, wafuate maagizo ya mwenye mali au kanuni za biashara? Je, hii ni ya mwanzo na ya mwisho au zitaendelea kuja na nyingine? Kwa kuwa tatizo la msingi la uendeshaji biashara zilizo chini ya serikali halijatatuliwa, haitakuwa jambo la ajabu ATCL kufuata projectile ya mashirika/makampuni ya umma.
katika kusafiri kwa siku za karibuni nimekata tiketi kwa wakala mara chache sana,. Mara zote nimetumia mfumo wa online ambao ni nafuu na unakua na uhuru zaidi..Ukiwa na mfumo huu wa online huitaji hata kuajiri hao wafanyakazi unaosema Na watu wengi wajanja wanakimbia kukata kwa wakala maana gharama zinakuwaga juu kwa uzoefu wangu labda huyo wakala awe nmshikaji wako ndo ata bother kukutafutia cheaper tickets
 
Jamani bila wakala ni ngumu. Ticket kwa m pesa haiwezekani kwani hautajua kama ndege ina nafasi au imejaa.
Visa, Mobile money zote nimeshawahi kuzitumia na unapata kile unataka. Wakala hana tofauti na intermediary. Na panapokuwa na intermediary gharama inaongezeka. Kama kuna mfumo mzuri wa kompyuta hiyo ni most effective way sababu database wanayo access wao ndo the same database unaweza kuiaccess directly kupitia web interface. Wakala unaweza kuwatumia pale ambapo kutakuwa na demand kubwa sana kwa hiyo kuongeza ufanisi wa huduma unajumulisha wao kama an alternative way of geting a service. Ila mwanzo lazima wajaribu kuminimize cost....
 
Ni kweli boss ila ukiwa na akili za biashara lazima uhakikishe una capture possibility zote za wateja kufanya biashara na wewe. Kuna watu hasa wa umri mkubwa wapo comfortable zaidi hard copy ticket kuna watu wanafurahia e-tickets. Kuna watu wengine ni slow learners wanataka waulize maswali kama 10 hivi ndo wakubali kutoa hela kukata ticket
unaweza capture possibility zote ila pia unaweza kuanza kwa kujaribu kuminimize cost wakati unasoma upepo wa biashara...
 
Well said bro. Hizi ni fact. Maana ama aamue kufuata misingi ya kobiashara au angojee maagizo ya wanasiasa. Hapo hata aje nani atashindwa tu. Lazima amteue mtu na amwamini kwamba atafanya kazi nzuri amwache aendeshe shirika
Hama fact zozote mkuu inawezekana wewe pamoja na mleta mada hamkumuelewa rais alichokuwa anasema.

Commissioned agents, hawa ndiyo walikuwa wanalengwa.

Sasa hivi watu wanakata tickets online, British Airlines wamefunga ofisi zao hapo Dar es Salaam lakini ticket unakata online kisha una print tu, airport unaenda na reference no:

Tatizo kubwa la watanzania kila mmoja mjuaji.
 
Umeeleza vyema.

Hata suala la lini na aina gani ya ndege zinunuliwe hapo baadae wangeachiwa ATCL wenyewe sababu ndiyo watakuwa field.

Wanasiasa watanunua ndege ili kuwaziba midomo wakosoaji wao tu.
Mkuu unaweza kufafanua kaeleza vyema kwenye lipi?

Alichoeleza wala siyo vyema anakuambia hivi hili uweze kukata ticket mahali popote ulipo ni lazima utumie mawakala.

Hii siyo kweli.
 
Nimeeeleza hapo juu kuhusu hilo la website, ikiwa imara haiwezi kusumbuliwa kiasi hicho yaani abiria 76 wanagombea tiketi za ndege moja tu ya Q400NG?

Ndiyo maana nikasema, wanahitaji kuwekeza kwenye IT.

Yaani kila ikifika usiku saa sita wataalam wanaingia kazini wanafanya updates na mengine.

Website ya atcl nayoo I boreshwe
 
Sasa hivi inawezekana mtu akalipia tiketi yake hata kwa m-pesa, akapata SMS yenye namba ya ticket na akifika airport atapata ticket halisi na kusafiri. Kwa hiyo wafanyakazi 'redundant' hawana nafasi tena!
Uwezikuwa NA kampuni kubwa ukakosa wakataji tkt sio kila MTU anauwezo wa kutumia condom hatakama anayo chumbani..so usifikiri tigopesampesa nk zinaweza kutumika kila Mara badosana..waimprove website yao eatuwamalizane online wenyeuwezo
 
Wabongo bwana,yani ATA mbongo mwenzake akiwa anatengenezewa ajira ya kukata japo tiketi wanasema yani kweli mbongo Hana jema ATA umfanyie nn.
 
Mkuu unaweza kufafanua kaeleza vyema kwenye lipi?

Alichoeleza wala siyo vyema anakuambia hivi hili uweze kukata ticket mahali popote ulipo ni lazima utumie mawakala.

Hii siyo kweli.
Asichojua huyo nmtau ni kwamba ndege si za ATCl bali ni za serikali kwa hiyo ATCL wanakodishwa tuuu
 
KAMA NDEGE IMEJAA UTAPATA MESSAGE YA KUKUFAHAMISHA NA KUKUELEKEZA KUHUSU SAFARI ZINAZOFUATA BAADA YA HIYO ULIYOKOSA!

Mdau huyo jamaa hajawahi kutumia mobile money kulipia ticketi ya ndege kwa hiyo hajui. MPESA ni njia malipo tu lakini booking inafanyika online. Sasa yeye nafikiri anadhani unafanya booking kwa mpesa teh teh
 
Nasafiri mara nyingi. Na sifahamu kama kuna shirika la ndege ambalo halitumia mawakala ila mawakala wamebadilika kutoka kwenye mazoea ya zamani ambapo ilikuwa mpaka uende kwenye ofisi zao, leo ni online agents.
OK sasa nadhani ATC wanaweza establishment ya online agency! management yake is not that complicated!
 
Ili uweze kukata ticket mahali popote ulipo ni lazima utumie mawakala. Haijalishi unakata ticket kwenye ofisi, simu au kwenye laptop yako, utatumia wakala. Kutaka kila kitu ufanye wewe mwenyewe ndiyo mbinu ya kizamani ya kuendesha biashara.

Hivi unajua hata unapokata ticket yako na kulipia kupitia mitandao kama Airtel, Vodacom na wengineo unatumia wakala? Hii niliyoitoa hapa ni sehemu ya elimu maana usiamini kuwa wanaohitaji elimu ni wale watu wa chini kabisa, kila mtu anahitaji elimu kwenye jambo fulani. Watawala na viongozi wa serikali wanahitaji elimu pia kwenye masuala ya biashara kama ilivyo kwa mfanyabiashara akiingizwa serikalini atahitaji elimu juu ya jinsi serikali inavyofanya kazi. Hakuna anayejua kila kitu, ndiyo maana ukifanya biashara kwa kutaka ufanye kila kitu wewe mwenyewe lazima uangukie pua.

Anayekuonesha mahali penye hitilifu ndiye anayekujenga kuliko anayekushangilia kila mahali. Ndiyo maana hata kwenye management performance assessment wewe uliye boss unatakiwa uwaombe direct reports wako wakueleze your weaknesses na siyo your strengths. Hayo ya Deo RIP ni out of context.
well said mkuu!!

huyu mooduke kusema siku hizi ticket waweza kuipata popote niwazi kuwa haelewi kuwa hata Mpesa ni uwakala.

licha ya kuwa ametoa mchango kwa lugha nzuri, pongezi kwa mkulu na pasi na uchochezi lakin hajui nini maana ya wakala.
 
Ndugu, niliposikia Mtukufu anasema ATCL wasitumie mawakala, nilimweleza jamaa yangu kuwa Wameshindwa kabla hawajaanza
 
Msambichaka nakubaliana na wewe! Elimu haina mwisho. Nilikuwa sijui kuwa mitandao tunakokatia tiketi ni agents vile vile. Ila najua kwa kutumia mitandao unalipa kama tunavyolipa kutuma msg, kutoa hela, kutuma hela etc. Sasa inanijia kuwa kwa vile unakata tiketi kupitia say Tigo and the like, unafanya biashara watakutoza zaidi. Hivyo ni agent! Am I right ?
Wewe CHUAKACHARA ndo ulisema unanizidi elimu Jana kwenye post ya @Gesi, mafuta vya patikana huko morogoro.
wakati hata mpesa kuwa agent hujui !!

am kidding !!
 
Wewe CHUAKACHARA ndo ulisema unanizidi elimu Jana kwenye post ya @Gesi, mafuta vya patikana huko morogoro.
wakati hata mpesa kuwa agent hujui !!

am kidding !!
Najua kuwa M pesa unalipia tiketi, vingamuzi, umeme, maji etc, lakini wanapata kamisheni kutokwa kwa hayo mashirika kutumia service /mitandao yao. Ile dhana kuwa ni agent was yet to come out clearly to me!
 
well said mkuu!!

huyu mooduke kusema siku hizi ticket waweza kuipata popote niwazi kuwa haelewi kuwa hata Mpesa ni uwakala.

licha ya kuwa ametoa mchango kwa lugha nzuri, pongezi kwa mkulu na pasi na uchochezi lakin hajui nini maana ya wakala.
Gharama za kutumia conventional travel agent wa kawaida na automated agent haziwezi kuwa sawa. By wakala they meant travel agents tunaowafahamu kwa hiyo acheni kupindua maneno bakini kwenye hoja mliyoanza nayo
 
Back
Top Bottom