ATCL kuanza na kosa la kwanza

ATCL kuanza na kosa la kwanza

Kukatisha ticketi sio lazima mtu awe na ofisi siku hizi..Watu wanalipia kwa mobile money na wanatumiwa ticket kwenye email au wanalipia online. Inategemea tu njia watakayoitumis na kuipa airtime ili wananchi wengi wajue jinsi ya kupata ticket.
 
Watu wanapotosha sana. Hao fastjet pamoja na kukupa fursa ya kukata ticket online, bado wanawatumia mawakala. Kuhakikisha hili, nenda website ya fastjet chagua destination utaona ratiba ya ndege na upande wa chini kushoto utaona link ya 'Travel Agents Login'.

Dhana ya mawakala sio mbaya, kuna watu wanadeal na wageni (or tourists) kila cku mfano hotel na tour companies. Hawa ni rahisi kurecommend usafiri maana wanakuwa na mgeni kwa muda mrefu na mgeni anajenga trust kwao. Hivyo hata akisuggest wapande ndege flani hawawez kataa. Wakala hatumii hakupunguzii mapato bali anaweza kuongeza maana yeye anakula cha juu, ndo maana kukata tiketi kwa wakala ni gharama zaid kuliko kukata moja kwa moja kwenye kampuni ya ndege.

Mwisho, hata mashirika makubwa ya ndege kama etihad yana mawakala, ndivyo industry ya ndege ilivyo. Haina maana kujaribu kitu ambacho watu wengine walifanya wakaona hakina faida. Shida pekee ya mawakala ni kwamba wanatoza zaid ambayo si tatizo kama mtu anakubali kulipia.
 
Ticket tunauza kwa M-pesa, airtel money, tigo pesa na booking online ukifika airport unaonyesha ticket kwenye simu yako huhitaji kubeba karatasi wala kukutana na mtu atakayekudanganya kuwa ndege imejaa. Chagua kiti online ofisi za nini acha basi Mkuu
Hoja ni je ATCL itahitaji mawakala au la? hata kama unachagua kiti online tayari umelipa kwa M- Pesa n.k hao tayari ni mawakala, kile unacholipa hao MPESA tayari wanachukua chao, sema kitakachokupunguzia ghasia wewe mlipaji ni kutolipa nauli kwenda kununua hiyo huduma physically, ila kwa biashara za sasa huwezi kuzifanya bial wakala. Wengi mmezoea kuona mawakala kwenye majengo siku hizi kuna wakala yuko nyumbani kwake fedha na mfumo huo anapiga kazi.
Hivyo, mkubwa naamini atashauriwa kwamba lazima ATCL itafanya kazi kupitia mawakala vinginevyo itashindwa hata kabla haijaanza
 
Mkuu Msambichaka, kwenye digital world, inawezekana kabisa kuuza tiketi online bila kuwatumia mawakala. Mawakala wanaozungumzwa hapa sio mawakala traveling agents, bali mawakala commissioned agents wana operate kama ofisi za
ATCL, badala ya kutumia mawakala, wanauza tickets on line. Fast Jet wana ofisi zao kule tuu mdege yao inakotua, na hawana wakala popote na mauzo yote ni online!, ila kwa mujibu wa sheria ya kimataifa ya shirika la kimataifa la wakala wa usafiri wa Anga, IATA, wakala yoyote aliyesajiliwa IATA kupitia mtandao wa Galileo, anaweza jyfanya booking yoyote ya ndege yoyote, hivyo abiria wa Tanzania yote watapata tiketi za ATCL popote kupitia traveling agents wengine, ila kule ATCL inatua, lazima wawe na agents for clearing.

Pasco

Nimekuelewa Pasco.
Sasa kama mtu anataka kufanya connection ya ndege kama mbili na kuendelea itakuwa je? Chukua mfano mtu anatoka Ifakara na anataka kwenda Namibia, akinunua tiketi kwa simu nani atakaye msaidia kutafuta connection ya ndege nyingine mpaka afike mwisho wa safari yake?
 
Pasco,
Usidanganye watu, hata ukiuza online bado unatumia agents. Hata mpesa au Tigo pesa au credit cards ni agents.

Ina maana atcl itengeneze utaratibu wake yenyewe wa kupokea malipo kitu ambacho haina uwezo.
Nyie watu mnaishi dunia gani na huyo rais wenu?
Mkuu Mrembo Jenifa, heshima ni kitu cha bure tena kwa mtoto wa kike, mrembo kama wewe, thamani yako heshima yako jinsi unavyojiheshimu na kuheshimu wengine!. Kumuita rais wa nchi "huyo rais wenu" sio kosa kuonyesha jinsi usivyompenda, ila sio heshima!. Wewe ukiwa ni Mtanzania popote pale ulipo, Rais Mhe. Dr.John Pombe Joseph Magufuli ndio rais wako ndio rais wangu, ndio rais wetu ndie rais wa Mbowe, ndie rais wa Lowassa, ndie rais wa Seif, ndie wa wote, waliomchagua na wasio mchagua hata wale ambao hawakupiga kura kabisa bado Magufuli ndio rais wao ndie rais wa nchi.

flights connections hufanywa na travel agents only hata fast jet hawaku connect na ndege nyingine yoyote na ndio maana travel agents wapo.
Pasco
 
ATCL kama yalivyo mashirika mengine ya umma, kila mara imekuwa ikizaliwa na kufa kutokana na muundo wake usiokuwa wa kibiashara. TANESCO isiyo na mshindani yeyote, TTCL ambayo awali haikuwa na mshindani, na mengine mengi yaliyokwishakufa na yaliyouzwa, mashirika yote hayo yalikufa kwa sababu yalianzishwa, kuendeshwa na kusimamiwa kiserikali/kisiasa.

Serikali haijawahi kuendesha biashara ikafanikiwa. Tatizo linaanzia kwenye muundo wa haya mashirika/makampuni. Wanasiasa/viongozi wa serikali ambao kimsingi si wafanyabiashara ndiyo waliotengeneza muundo wa uendeshaji na ndiyo wenye kauli ya mwisho. Vigezo vya wajumbe wa bodi na watendaji wakuu wanavyo wao. Na siku hizi PhD imekuwa ni kigezo kikubwa sana ingawa kiuhalisia, kwa Dunia nzima, ni nadra sana kuwaona wenye PhD wakiwa wafanyabiashara wazuri na waliofanikiwa.

Juzi wakati Mh. Rais akizindua ujio wa ndege mpya alisema ATCL imezaliwa upya, ina ndege mpya, bodi mpya na uongozi mpya, sikusikia kama ina muundo mpya wa uendeshaji na usimamizi. Bado inaonekana ATCL itandeshwa kwa mkono wa serikali.

RAIS - 'ATCL ISITUMIE MAWAKALA WA KUKATISHA TIKETI'

Hili tayari ni agizo ambalo naamini ni agizo lisilo sahihi. Tayari serikali imeanza toka hatua za mwanzo kuingilia uendeshaji wa ATCL. Rais anapoagiza ATCL isitumie mawakala wa kukatisha tiketi inamaanisha ATCL iwe na wafanyakazi waajiriwa kila mahali nchini. Gharama za maelekezo hayo itakuwa kama ifuatavyo:
  • ATCL italazimika kuwalipa wakatisha tiketi mishahara, matibabu, posho, michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, usafiri, n.k. ATCL italazimika kulipia gharama hizo zote bila ya kujali mkatisha tiketi anakatisha tiketi ngapi au kama amepata wateja au hakupata kabisa
  • ATCL italazimika kulipia ofisi na kuweka miundombinu ya ukatishaji ticket nchi nzima. Ifahamike kuwa ukitaka kuwa na ufanisi unalazimika kuwa na ofisi za ukatishaji tiketi hata mahali ambapo ndege haitui, kwaajili ya kuhudumia abiria wanaotoka maeneo hayo wanaotarajia kutumia usafiri wa ATCL kutokea uwanja ulio karibu
  • ATCL italazimika kuwapa mafunzo wakatisha ticket watakaotapakaa nchi nzima
Wakati ATCL watakapokuwa wanahangaika na kuwa na wakatisha ticket wao na ofisi zao, washindani wao wataendelea kuwa na wafanyakazi wachache, wakiwa na mawakala wengi wanaolipwa kutokana na idadi ya ticket na thamani ya ticket walizokatisha. Hawalipii ofisi, hawalipii matibabu, hawalipii michango ya hifadhi ya jamii, hawalipii likizo ya mfanyakazi. Mawakala wao wanalipwa kutokana na wanachozalisha, wasipozalisha hawalipwi chochote.

ATCL wanaanza na quandary ya kwanza, wafuate maagizo ya mwenye mali au kanuni za biashara? Je, hii ni ya mwanzo na ya mwisho au zitaendelea kuja na nyingine? Kwa kuwa tatizo la msingi la uendeshaji biashara zilizo chini ya serikali halijatatuliwa, haitakuwa jambo la ajabu ATCL kufuata projectile ya mashirika/makampuni ya umma.
nadhani kama cericarly yetu ingekuwa inazingatia ushauri kama huu kwa kipindi cha 2-3 years tungekuwa na Tanzania ambayo kila investor angetaka opportunity.. well said brother
 
wenyewe wenye nini? tuliwaachia ndege kibao tu zote wameua, nazo hizi unataka waziue?

Kama hamuwaamini mmewapa wa nini?

Si bora MD wa ATCL awe Magufuli basi kuliko kuwaamulia kila kitu halafu mkishindwa mnawasingizia.
 
Pasco,
Usidanganye watu, hata ukiuza online bado unatumia agents. Hata mpesa au Tigo pesa au credit cards ni agents.

Ina maana atcl itengeneze utaratibu wake yenyewe wa kupokea malipo kitu ambacho haina uwezo.
Nyie watu mnaishi dunia gani na huyo rais wenu?
Msambichaka ameeleza vizuri aina ya agents kwamba kuna ma agents Fulani hawatokwepeka katika biashara hii lakini wengine si wa lazima kama travelling agents. Lakini unapokata tickets online lazima ulipe kupitia agents mfano maxmalipo, m-pesa, tigo pesa, airtel money, halotel money na n.k./
 
Nilivyokwambia unasumbuliwa na stomach gases ulidhani nakutania? By profession mimi ni daktari wa akili. Soma hapo chini kwenye RED
Inabidi ukasomee tena huo Udaktari wako...Kusema kwamba Emirates et al wanakata ticket online haimaanishi kwamba nimelinganisha ATCL na Emirates au hayo mashirika (kioperesheni na kiuwezo)...

Btw ni kweli naumwa stomach gases...Ila sio kwa kuniwekea maneno mdomoni ama kunifikirisha unachotaka
 
Yes, lakini bado Fasjet ina agents! Tanzania haijafikia level ya Ulaya mzee. Hata ukiwa na online systems, lazima pia uwe na agents.......
Tuko pamoja...

Concern yangu ilikuwa ni kwenye 'uwakala'..Sio operations..

Kwamba sasa hivi kwenda kukata ticket kwa mawakala sio ishu sana..Watu wanakata online...Ingawa bado kuna mtu katikati i.e Tigopesa..Airtel Money..M-Pesa , 3G Direct pay n.k...Sasa hivi hauna haja ya kwenda Waljis ama Gazelle kukata ticket...Bei ya ticket utakayoinunua online ni ndogo ikilinganishwa na ile utakayoinunua kwa Wakala (Mfano hao Waljis au Gazelle)....
 
Mkuu Mrembo Jenifa, heshima ni kitu cha bure tena kwa mtoto wa kike, mrembo kama wewe, thamani yako heshima yako jinsi unavyojiheshimu na kuheshimu wengine!. Kumuita rais wa nchi "huyo rais wenu" sio kosa kuonyesha jinsi usivyompenda, ila sio heshima!. Wewe ukiwa ni Mtanzania popote pale ulipo, Rais Mhe. Dr.John Pombe Joseph Magufuli ndio rais wako ndio rais wangu, ndio rais wetu ndie rais wa Mbowe, ndie rais wa Lowassa, ndie rais wa Seif, ndie wa wote, waliomchagua na wasio mchagua hata wale ambao hawakupiga kura kabisa bado Magufuli ndio rais wao ndie rais wa nchi.
Pasco
Mbona imekuuma sana! kunani? Sioni kosa alilolifanya binti! "huyo rais wenu" ni tusi? Mahaba yasizidi uhalisia wa jambo, hajatukana hata kidogo.
 
Nashukuru kuwa wapo watanzania wanaotafakari kabla ya kusema. Inajitokeza sana sasa kuwa kila ushauri mtu ukitoa ambao ni tofauti na msimamo wa utawala basi wewe ni mpinzani wa CCM. Inakera sana hivi hili kuwa Mhe. Rais kakosea kukataa mawakala wa kukatisha tickets nalo iwe shiiida !!!? Shirika gani la ndege dunia ambao hawana mawakala. Kwa nini Tz tusiwe na mawakala. Hata baada ya akina Msambichaka n.k. kudadavua kwa nini mawakala bado wa Lumumba mnabisha!!!? Hivi Rais no Mungu hakosei!!!? Rais anapokuwa "uchi" basi tupige makofi tu na kusema "umependezaaa" Jamani nchi lazima iongozwe kwa misingi ya kitaasisi.
 
ATCL kama yalivyo mashirika mengine ya umma, kila mara imekuwa ikizaliwa na kufa kutokana na muundo wake usiokuwa wa kibiashara. TANESCO isiyo na mshindani yeyote, TTCL ambayo awali haikuwa na mshindani, na mengine mengi yaliyokwishakufa na yaliyouzwa, mashirika yote hayo yalikufa kwa sababu yalianzishwa, kuendeshwa na kusimamiwa kiserikali/kisiasa.

Serikali haijawahi kuendesha biashara ikafanikiwa. Tatizo linaanzia kwenye muundo wa haya mashirika/makampuni. Wanasiasa/viongozi wa serikali ambao kimsingi si wafanyabiashara ndiyo waliotengeneza muundo wa uendeshaji na ndiyo wenye kauli ya mwisho. Vigezo vya wajumbe wa bodi na watendaji wakuu wanavyo wao. Na siku hizi PhD imekuwa ni kigezo kikubwa sana ingawa kiuhalisia, kwa Dunia nzima, ni nadra sana kuwaona wenye PhD wakiwa wafanyabiashara wazuri na waliofanikiwa.

Juzi wakati Mh. Rais akizindua ujio wa ndege mpya alisema ATCL imezaliwa upya, ina ndege mpya, bodi mpya na uongozi mpya, sikusikia kama ina muundo mpya wa uendeshaji na usimamizi. Bado inaonekana ATCL itandeshwa kwa mkono wa serikali.

RAIS - 'ATCL ISITUMIE MAWAKALA WA KUKATISHA TIKETI'

Hili tayari ni agizo ambalo naamini ni agizo lisilo sahihi. Tayari serikali imeanza toka hatua za mwanzo kuingilia uendeshaji wa ATCL. Rais anapoagiza ATCL isitumie mawakala wa kukatisha tiketi inamaanisha ATCL iwe na wafanyakazi waajiriwa kila mahali nchini. Gharama za maelekezo hayo itakuwa kama ifuatavyo:
  • ATCL italazimika kuwalipa wakatisha tiketi mishahara, matibabu, posho, michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, usafiri, n.k. ATCL italazimika kulipia gharama hizo zote bila ya kujali mkatisha tiketi anakatisha tiketi ngapi au kama amepata wateja au hakupata kabisa
  • ATCL italazimika kulipia ofisi na kuweka miundombinu ya ukatishaji ticket nchi nzima. Ifahamike kuwa ukitaka kuwa na ufanisi unalazimika kuwa na ofisi za ukatishaji tiketi hata mahali ambapo ndege haitui, kwaajili ya kuhudumia abiria wanaotoka maeneo hayo wanaotarajia kutumia usafiri wa ATCL kutokea uwanja ulio karibu
  • ATCL italazimika kuwapa mafunzo wakatisha ticket watakaotapakaa nchi nzima
Wakati ATCL watakapokuwa wanahangaika na kuwa na wakatisha ticket wao na ofisi zao, washindani wao wataendelea kuwa na wafanyakazi wachache, wakiwa na mawakala wengi wanaolipwa kutokana na idadi ya ticket na thamani ya ticket walizokatisha. Hawalipii ofisi, hawalipii matibabu, hawalipii michango ya hifadhi ya jamii, hawalipii likizo ya mfanyakazi. Mawakala wao wanalipwa kutokana na wanachozalisha, wasipozalisha hawalipwi chochote.

ATCL wanaanza na quandary ya kwanza, wafuate maagizo ya mwenye mali au kanuni za biashara? Je, hii ni ya mwanzo na ya mwisho au zitaendelea kuja na nyingine? Kwa kuwa tatizo la msingi la uendeshaji biashara zilizo chini ya serikali halijatatuliwa, haitakuwa jambo la ajabu ATCL kufuata projectile ya mashirika/makampuni ya umma.

Mkuu, nadhani raisi yuko sahihi kwa wazo lake hilo, kwani amepata ufafanuzi wote na anazo taarifa zote kuhusu hilo la mawakala na ndiyo ameweka mkakati na amemteua CE mpya atekeleze mwelekeo mpya wa ATCL.

Kama unafuatilia habari za mashirika ya ndege, karibu yote kuanzia mwaka 2013 wamewekeza sana kwenye mifumo ya IT ili kufanya mauzo ya tiketi ya moja kwa moja kupitia mtandao.

Hivyo, kuuza moja kwa moja kwa mteja na kadi yake ya benki unaondoa mawakala wengi na unabakia na benki ambae kwenye mfumo wa CGI au common gateway interface (wale watu wa IT watanielewa) anaitwa merchant na anatoza sehemu ndogo sana ya transaction.

Ukiweka mauzo yote ya tiketi kwenye online services una uwezo wa kuongeza mapato ya moja kwa moja na mambo mengine kama offers mbalimbali kwa wateja na promotions.

Hivyo kama una lengo la kuuza asilimia hadi 55 ya tiketi zako online basi unakuwa una uhakika hata viosks kwenye viwanja vya ndege zinakuwa na tiketi .

Sasa hiyo ndiyo "vision" na CEO atakuwa na hakikisha IT department inajikita kwenye kutoa huduma zenye ubora na kiwango cha juu.

Kuhusu kiosks, simu za mikononi ATCL inaweza kabisa kuondokana na commission agents kwa kuendeleza applications ambazo ni interactive na ambazo zitaweza kuunganishwa na tovuti ya ATCL wateja wataweza kufanya manunuzi moja kwa moja kutoka kwenye tovuti ya ATCL bila kushirikisha MPESA au Tigo Pesa.

Lakini mwanzoni wanaweza kufanya makubaliano na wenye makampuni ya simu lakini huku kimyakimya wakiwatumia wataalam wa IT kutengeneza hizo applications.

Ni wakati sasa wa mashirika na taasisi za serikali kuajiri watalaam khasa wa mambo kama haya ya kutengeneza tovuti imara na thabiti ili kuwa na uhakika wa mauzo na kujikinga na wadukuzi na majasusi wa kiuchumi.

Wapo wataalam wengi tu na hata ikiwezekana CEO anaweza kutafuta hata wa kutoka nje ya nchi kwa kuzungumza na ofisi za mabalozi wa nchi kama India nchi ambayo inaongoza kwa kuwa na wataalam wa IT katika fani mbalimbali.

Wataalam hawa wanakuja TZ na wanafanya kazi na wataalam wa kitanzania ili kubadilishana ujuzi na uzoefu wa masuala mbalimbali ya kitaalam kwenye neo hili la IT na khasa usalama wa mitandao.

Ila mawakala wengine yaani travel agents wanaweza kuwa na tiketi lakini siyo kama yule wa visiwa vya Comoro ni namba ndogo tu inatolewa.

Kwa kuwa ATCL sasa hivi ipo kwenye muundo mpya na wanafanya uhakiki kimuundo ni bora CEO mpya angeachwa halafu tuje tuone amefanya nini ndani ya miezi sita ijayo.

Tusipende kukimbilia kukosoa kila kitu ambapo vingine kama ATCL ni kama mgonjwa alie mahututi hospitali na alikuwa kadhoofu kwa kutokula hata chakula na sasa imepatikana "breakthrough" na anapata dawa sahihi na kaja daktari mwingine ambae amebadili namna ya kumshughulikia mgonjwa.

Huyu daktari anapitia mstakabali mzima wa mgonjwa tangu kaingia hosplitalini, nini kinamsumbua, dawa gani amekuwa akipewa, nani alikuwa akimshughulikia na nani alikosea akampa dawa tofauti kiasi cha mgonjwa kudhoofu kiasi hiki bila kuonyesha dalili za unafuu.
 
Tatizo wengi wanadhani wakala ni lazima akae ofisini wamwone. Unapokata ticket online ya fastjet au Precision au kampuni nyingine yoyote, pale kuna wakala, na kuna wakati kunakuwa na mawakala wawili. Kwa fastjet kuna mtandao unaokuwezesha ufanye hayo malipo (Mpesa, Airtel Money, MaxMalipo, etc) na pia kuna PayPal ambaye ndiye wakala wa Fastjet.

Kwa hiyo kwa ujumla unazidi kuniunga mkono kuwa ni ngumu sana kwa ulimwengu wa leo kufanya biashara 100% bila ya kutumia wakala.
Nadhani ni kutofautiana lugha tu Chifu....

Kimsingi tuko pamoja....

Concern yangu ilikuwa ni kwenye 'uwakala'..Sio operations..

Kwamba sasa hivi kwenda kukata ticket kwa mawakala sio ishu sana..Watu wanakata online...Ingawa bado kuna mtu katikati i.e Tigopesa..Airtel Money..M-Pesa , 3G Direct pay n.k...Sasa hivi hauna haja ya kwenda Waljis ama Gazelle kukata ticket...Bei ya ticket utakayoinunua online ni ndogo ikilinganishwa na ile utakayoinunua kwa Wakala (Mfano hao Waljis au Gazelle)....

Btw Fastjet unaweza kulipa kwa kutumia M-Pesa, Tigopesa, Airtel Money, VISA, Master Card, NMB Mobile au 3G Direct Pay...Kama nilivosema hapo juu, gharama za kununua moja kwa moja kwa kulipia online ni ndogo ukilinganisha na zile za kwa Travel agent....
 
Nilivyokwambia unasumbuliwa na stomach gases ulidhani nakutania? By profession mimi ni daktari wa akili. Soma hapo chini kwenye RED
Daktari wa kupasua goti vs kichwa and vice versa. Unaweza ukawa daktari lakini ukawa na mapungufu tena kama ulisoma hivi vyuo vya "leo", mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh AU wale wa Urusi enzi hizo waliokuwa hawakubaliki Muhimbili!
Anyway nataka kukupa notion kuwa issue siyo una profession gani, issue je unaimudu? Si umesikia utafiti unasema kuwa around 46% ??? walimu na madaktari hawajui kazi zao!???????
 
ATCL kama yalivyo mashirika mengine ya umma, kila mara imekuwa ikizaliwa na kufa kutokana na muundo wake usiokuwa wa kibiashara. TANESCO isiyo na mshindani yeyote, TTCL ambayo awali haikuwa na mshindani, na mengine mengi yaliyokwishakufa na yaliyouzwa, mashirika yote hayo yalikufa kwa sababu yalianzishwa, kuendeshwa na kusimamiwa kiserikali/kisiasa.

Serikali haijawahi kuendesha biashara ikafanikiwa. Tatizo linaanzia kwenye muundo wa haya mashirika/makampuni. Wanasiasa/viongozi wa serikali ambao kimsingi si wafanyabiashara ndiyo waliotengeneza muundo wa uendeshaji na ndiyo wenye kauli ya mwisho. Vigezo vya wajumbe wa bodi na watendaji wakuu wanavyo wao. Na siku hizi PhD imekuwa ni kigezo kikubwa sana ingawa kiuhalisia, kwa Dunia nzima, ni nadra sana kuwaona wenye PhD wakiwa wafanyabiashara wazuri na waliofanikiwa.

Juzi wakati Mh. Rais akizindua ujio wa ndege mpya alisema ATCL imezaliwa upya, ina ndege mpya, bodi mpya na uongozi mpya, sikusikia kama ina muundo mpya wa uendeshaji na usimamizi. Bado inaonekana ATCL itandeshwa kwa mkono wa serikali.

RAIS - 'ATCL ISITUMIE MAWAKALA WA KUKATISHA TIKETI'

Hili tayari ni agizo ambalo naamini ni agizo lisilo sahihi. Tayari serikali imeanza toka hatua za mwanzo kuingilia uendeshaji wa ATCL. Rais anapoagiza ATCL isitumie mawakala wa kukatisha tiketi inamaanisha ATCL iwe na wafanyakazi waajiriwa kila mahali nchini. Gharama za maelekezo hayo itakuwa kama ifuatavyo:
  • ATCL italazimika kuwalipa wakatisha tiketi mishahara, matibabu, posho, michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, usafiri, n.k. ATCL italazimika kulipia gharama hizo zote bila ya kujali mkatisha tiketi anakatisha tiketi ngapi au kama amepata wateja au hakupata kabisa
  • ATCL italazimika kulipia ofisi na kuweka miundombinu ya ukatishaji ticket nchi nzima. Ifahamike kuwa ukitaka kuwa na ufanisi unalazimika kuwa na ofisi za ukatishaji tiketi hata mahali ambapo ndege haitui, kwaajili ya kuhudumia abiria wanaotoka maeneo hayo wanaotarajia kutumia usafiri wa ATCL kutokea uwanja ulio karibu
  • ATCL italazimika kuwapa mafunzo wakatisha ticket watakaotapakaa nchi nzima
Wakati ATCL watakapokuwa wanahangaika na kuwa na wakatisha ticket wao na ofisi zao, washindani wao wataendelea kuwa na wafanyakazi wachache, wakiwa na mawakala wengi wanaolipwa kutokana na idadi ya ticket na thamani ya ticket walizokatisha. Hawalipii ofisi, hawalipii matibabu, hawalipii michango ya hifadhi ya jamii, hawalipii likizo ya mfanyakazi. Mawakala wao wanalipwa kutokana na wanachozalisha, wasipozalisha hawalipwi chochote.

ATCL wanaanza na quandary ya kwanza, wafuate maagizo ya mwenye mali au kanuni za biashara? Je, hii ni ya mwanzo na ya mwisho au zitaendelea kuja na nyingine? Kwa kuwa tatizo la msingi la uendeshaji biashara zilizo chini ya serikali halijatatuliwa, haitakuwa jambo la ajabu ATCL kufuata projectile ya mashirika/makampuni ya umma.

Kwa kifupi hili litakluwa shirika la ndege la kwanza duniani kuacha kutumia agents kuuza tickets zake. Hivyo uamuzi huu hauko practical. Kuhusu board composition nayo haija nyooka moja kwa moja kama ilivyonyooka kwenye position ya CEO. Nadhani kuna mameneja wawili wa miko wa Tanroads. Na maprofessor watatu. Hapo sioni kama kuna mtu kwenye board mwenye uzoefu na mambo ya usafiri wa anga.
 
RAIS - 'ATCL ISITUMIE MAWAKALA WA KUKATISHA TIKETI'

Hili tayari ni agizo ambalo naamini ni agizo lisilo sahihi. Tayari serikali imeanza toka hatua za mwanzo kuingilia uendeshaji wa ATCL. Rais anapoagiza ATCL isitumie mawakala wa kukatisha tiketi inamaanisha ATCL iwe na wafanyakazi waajiriwa kila mahali nchini. Gharama za maelekezo hayo itakuwa kama ifuatavyo:
  • ATCL italazimika kuwalipa wakatisha tiketi mishahara, matibabu, posho, michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, usafiri, n.k. ATCL italazimika kulipia gharama hizo zote bila ya kujali mkatisha tiketi anakatisha tiketi ngapi au kama amepata wateja au hakupata kabisa
  • ATCL italazimika kulipia ofisi na kuweka miundombinu ya ukatishaji ticket nchi nzima. Ifahamike kuwa ukitaka kuwa na ufanisi unalazimika kuwa na ofisi za ukatishaji tiketi hata mahali ambapo ndege haitui, kwaajili ya kuhudumia abiria wanaotoka maeneo hayo wanaotarajia kutumia usafiri wa ATCL kutokea uwanja ulio karibu
  • ATCL italazimika kuwapa mafunzo wakatisha ticket watakaotapakaa nchi nzima
Wakati ATCL watakapokuwa wanahangaika na kuwa na wakatisha ticket wao na ofisi zao, washindani wao wataendelea kuwa na wafanyakazi wachache, wakiwa na mawakala wengi wanaolipwa kutokana na idadi ya ticket na thamani ya ticket walizokatisha. Hawalipii ofisi, hawalipii matibabu, hawalipii michango ya hifadhi ya jamii, hawalipii likizo ya mfanyakazi. Mawakala wao wanalipwa kutokana na wanachozalisha, wasipozalisha hawalipwi chochote.
Mkuu hili jambo muhimu umeliweka hapa wahusika wasome wampe ushauri Mh. Rais. Sina cha kuongeza ktk hoja yako umemaliza yote tuliyotaka kuyasema. Wengi wameliona tatizo katika tamko/agizo lile la mheshimiwa Rais na tuna amini anashaurika na msikivu atautendea kazi ushauri huu. Tunahitaji constructive criticism kama hizi sio zile za kukatisha tamaa na kubomoa nchi.
 
Back
Top Bottom