ATCL kuanza na kosa la kwanza

ATCL kuanza na kosa la kwanza

Sasa hivi inawezekana mtu akalipia tiketi yake hata kwa m-pesa, akapata SMS yenye namba ya ticket na akifika airport atapata ticket halisi na kusafiri kwa hiyo wafanyakazi 'redundant' hawana nafasi tena!

Nikweli hio inawezekana.

Lakini pia ATCL wakiwekeza kwenye IT wanaweza kukuzia tiketi au e-ticket na ukaitumia kufanya check-in na ukasafiri nayo bila shida.

Unaweza kuiona kwenye simu yako au kui-print kabisa.

Ila kwa wakti huu kuuziwa tiketi kwa M-pesa sio tatizo ila huko mbele mauzo ya tiketi kwa mtindo huu kutaondolewa.
 
Hadi Raha!
KQ wanajiharishia safari 49 kwa wiki!42 zilitakiwa ziwe za ATC,wamemualika Magufuli,moja ya ajenda itakuwa hiyo tu
Airbus ikifika,Ethiopean,Qatari na Emirates watakosa abiria wa China
Kwa hizi Dash 8,Harare,Moroni,J'burg,Lusaka na LBB itakula vichwa vyote
Hii akili iliotumika kufufua hili shirika ibarikiwe milele
 
Sawasawa mkuu, maslahi ya taifa ni lazima yapewe kimaumbele.

Tena kama ATCL wanasoma hapa JF, nyie vijana wa IT muanze kazi sasa imarisheni website yenu na muachane kwanza na Facebook na Twitter imarisheni website mama kwanza.

Kuna mambo bado hayajakaa sawa.
 
Kaka dunia imebadilika unaweza kata ticket ya ndege popote ulipo bila msaada wa mtu yeyote kilichopo nikuchukua nafasi zetu katika jamii kutoa elimu au kuwasaidia kupata elimu waendane na dunia ya sasa kuleta ukinzani katika kila jambo linalokuwa initiated na serikali haliwezi kukufanya ukawa na busara za kuongoza bali kutatua changamoto zilizoko katika jamii yako ndio ngazi itakayokupandisha daraja na kuwa kiongozi. Je unamkumbuka Marehemu Deo Filikunjombe vaa viatu vyake vikikutosha basi hayo mambo mengine hayatakusumbua. Hongera Magufuli kwa kuonyesha tofauti hata sisi tusio wanachama wa ccm tunaona mwanga kupitia wewe.
hapo kwenye RED ndio tatizo, mtoa mada hkutaja issue za chama hapa, come on!!!!!!!!!!!!
 
ATCL kama yalivyo mashirika mengine ya umma, kila mara imekuwa ikizaliwa na kufa kutokana na muundo wake usiokuwa wa kibiashara. TANESCO isiyo na mshindani yeyote, TTCL ambayo awali haikuwa na mshindani, na mengine mengi yaliyokwishakufa na yaliyouzwa, mashirika yote hayo yalikufa kwa sababu yalianzishwa, kuendeshwa na kusimamiwa kiserikali/kisiasa.

Serikali haijawahi kuendesha biashara ikafanikiwa. Tatizo linaanzia kwenye muundo wa haya mashirika/makampuni. Wanasiasa/viongozi wa serikali ambao kimsingi si wafanyabiashara ndiyo waliotengeneza muundo wa uendeshaji na ndiyo wenye kauli ya mwisho. Vigezo vya wajumbe wa bodi na watendaji wakuu wanavyo wao. Na siku hizi PhD imekuwa ni kigezo kikubwa sana ingawa kiuhalisia, kwa Dunia nzima, ni nadra sana kuwaona wenye PhD wakiwa wafanyabiashara wazuri na waliofanikiwa.

Juzi wakati Mh. Rais akizindua ujio wa ndege mpya alisema ATCL imezaliwa upya, ina ndege mpya, bodi mpya na uongozi mpya, sikusikia kama ina muundo mpya wa uendeshaji na usimamizi. Bado inaonekana ATCL itandeshwa kwa mkono wa serikali.

RAIS - 'ATCL ISITUMIE MAWAKALA WA KUKATISHA TIKETI'

Hili tayari ni agizo ambalo naamini ni agizo lisilo sahihi. Tayari serikali imeanza toka hatua za mwanzo kuingilia uendeshaji wa ATCL. Rais anapoagiza ATCL isitumie mawakala wa kukatisha tiketi inamaanisha ATCL iwe na wafanyakazi waajiriwa kila mahali nchini. Gharama za maelekezo hayo itakuwa kama ifuatavyo:
  • ATCL italazimika kuwalipa wakatisha tiketi mishahara, matibabu, posho, michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, usafiri, n.k. ATCL italazimika kulipia gharama hizo zote bila ya kujali mkatisha tiketi anakatisha tiketi ngapi au kama amepata wateja au hakupata kabisa
  • ATCL italazimika kulipia ofisi na kuweka miundombinu ya ukatishaji ticket nchi nzima. Ifahamike kuwa ukitaka kuwa na ufanisi unalazimika kuwa na ofisi za ukatishaji tiketi hata mahali ambapo ndege haitui, kwaajili ya kuhudumia abiria wanaotoka maeneo hayo wanaotarajia kutumia usafiri wa ATCL kutokea uwanja ulio karibu
  • ATCL italazimika kuwapa mafunzo wakatisha ticket watakaotapakaa nchi nzima
Wakati ATCL watakapokuwa wanahangaika na kuwa na wakatisha ticket wao na ofisi zao, washindani wao wataendelea kuwa na wafanyakazi wachache, wakiwa na mawakala wengi wanaolipwa kutokana na idadi ya ticket na thamani ya ticket walizokatisha. Hawalipii ofisi, hawalipii matibabu, hawalipii michango ya hifadhi ya jamii, hawalipii likizo ya mfanyakazi. Mawakala wao wanalipwa kutokana na wanachozalisha, wasipozalisha hawalipwi chochote.

ATCL wanaanza na quandary ya kwanza, wafuate maagizo ya mwenye mali au kanuni za biashara? Je, hii ni ya mwanzo na ya mwisho au zitaendelea kuja na nyingine? Kwa kuwa tatizo la msingi la uendeshaji biashara zilizo chini ya serikali halijatatuliwa, haitakuwa jambo la ajabu ATCL kufuata projectile ya mashirika/makampuni ya umma.

Sio lazima kuwa na travel agencies istoshe mashirika ya ndege yanadiscourage ufanyaji wa booking through,
Ukitembelea website zao Kuna mahala utakutana na jumbe km hizi

'Booking online through our website is the easiest way to book your flights. You can get the latest special offers, find out about our amazing low fares and avoid booking agent fees'

Sasa ndo ujue logic yako ni finyu ndugu
 
hizo ndege mradi wake utafeli tu.wala sina haka ya kuelezea mpaka malaika mtoa roho aje aitoe roho JF

Zikishindwa na wewe utakua umeshindwa hakika taifa zima la tanzania litakuwa limeshindwa ila kama wewe sio mtanzania hutakuwa ndani ya kundi la kushindwa....
 
Hoja hapa ni serikali/wanasiasa kuingilia uendeshaji wa haya makampuni ya umma. Haya maelekezo sio mara zote yanaweza kusaidia kampuni, mengine yana hatari zake. Ni vema bodi na menejimenti zikaachwa huru kwenye uendeshaji. Serikali kama mmiliki iipe bodi ya ATCL, Targets and kuweka KPIs tu ambazo kwazo itakuwa inapima performance ya hiyo bodi/menejimenti.

Kama zikiachwa huru na uhuru huo ndio mwanya wautumiao kufilisi au kuiba mali za shirika husika...,Je huoni kuna haja ya serikali kutoa miongozo yake..!?
 
Tatizo wengi wanadhani wakala ni lazima akae ofisini wamwone. Unapokata ticket online ya fastjet au Precision au kampuni nyingine yoyote, pale kuna wakala, na kuna wakati kunakuwa na mawakala wawili. Kwa fastjet kuna mtandao unaokuwezesha ufanye hayo malipo (Mpesa, Airtel Money, MaxMalipo, etc) na pia kuna PayPal ambaye ndiye wakala wa Fastjet.

Kwa hiyo kwa ujumla unazidi kuniunga mkono kuwa ni ngumu sana kwa ulimwengu wa leo kufanya biashara 100% bila ya kutumia wakala.

Na lazima ufahamu vizuri na uwe mweledi, Rais aliposema wastumie agencies hakumaanisha shirika lisiruhusu kuuza ticket kwa njia ya maxmalipo au mpesa etc, alimaanisha mawakala wenye ofisi zao mitaani ambao wanahudumia mashirika tofautitofauti, kitu ambacho kilipelekea shirika kuhujumiwa, kinachoongelewa hapa ni HUJUMA sasa km mtu ananunua online huyo wakala wa online atamhujumu vipi?

Ingia website ya fastjet usome maelezo ya namna ya kufanya booking utaona maelezo yanayodiscourage matumizi ya agencies lakini ukifikia hatua ya kufanya malipo utachagua either through m-mpesa, mastercard au vyovyote, hao pia ni mawakala, unataka kuniambia fastjet walimanisha mawakala wapi ingawa hao pia ni mawakala?
 
Si bora MD wa ATCL awe Magufuli basi kuliko kuwaamulia kila kitu halafu mkishindwa mnawasingizia.
Mkuu mi naona huo wadhifa tayari anao indirectly maana kasema anampango wa kuagiza zingine mbili ya watu 160 na ya watu 240 ambayo anasema itakuwa inatoka na watalii marekani moja kwa moja bila kutua popote hadi dar.maajabu haya nadhani itakuwa na air refuelling.
 
Mkuu, ni wakala yupi unaemtetea, anaechukua kamisheni (tigo Pesa, Airtel Money) au yule wakala wa safari anaetambulika yaani travel agent?

Anaechukua kamisheni (makampuni ya simu) hawahusiki na tiketi kwasababu hawajawa travel agents, wao wanangoja kukata tu kamisheni.
kamisheni ndo mgao wao mkuu.
 
Hii moja ya post zenye hoja zenye mantiki sana. Big up mleta mada.
Hili la kuwatumia mawakala halikwepeki. Napenda kuamini Prof. Mbarawa anao uwezo wa kumpa taarifa sahihi Rais na akabadili mawazo yake.

Sibonike,
Wewe inaonekana humtakii mema Prof. Mbarawa. Kwa sasa tuna Rais asiyeshaulika hasikii la mwazini wala mpiga swala! Kumshauri au kutaka kumpa JPM ushauri tofauti na mawazo yake ni uchochezi na upinzani na mwisho wako ni kutumbuliwa au kushtakiwa kwa uchochezi!!
Chezea JPM!
 
Kama zikiachwa huru na uhuru huo ndio mwanya wautumiao kufilisi au kuiba mali za shirika husika...,Je huoni kuna haja ya serikali kutoa miongozo yake..!?
Mkuu yaani serikali ikiamua kufanya hivyo basi bodi itakuwa haina kazi yoyote pale itakuwa wanapokea maagizo kila uchao na biashara isipoenda vizuri bodi na huyo CEO watalaumiwa na kufukuzwa-serikali iwaache huru waendeshe shirika kwa weledi wao,wao na kamati za bunge wakague mahesabu tu.
 
ATCL kama yalivyo mashirika mengine ya umma, kila mara imekuwa ikizaliwa na kufa kutokana na muundo wake usiokuwa wa kibiashara. TANESCO isiyo na mshindani yeyote, TTCL ambayo awali haikuwa na mshindani, na mengine mengi yaliyokwishakufa na yaliyouzwa, mashirika yote hayo yalikufa kwa sababu yalianzishwa, kuendeshwa na kusimamiwa kiserikali/kisiasa.

Serikali haijawahi kuendesha biashara ikafanikiwa. Tatizo linaanzia kwenye muundo wa haya mashirika/makampuni. Wanasiasa/viongozi wa serikali ambao kimsingi si wafanyabiashara ndiyo waliotengeneza muundo wa uendeshaji na ndiyo wenye kauli ya mwisho. Vigezo vya wajumbe wa bodi na watendaji wakuu wanavyo wao. Na siku hizi PhD imekuwa ni kigezo kikubwa sana ingawa kiuhalisia, kwa Dunia nzima, ni nadra sana kuwaona wenye PhD wakiwa wafanyabiashara wazuri na waliofanikiwa.

Juzi wakati Mh. Rais akizindua ujio wa ndege mpya alisema ATCL imezaliwa upya, ina ndege mpya, bodi mpya na uongozi mpya, sikusikia kama ina muundo mpya wa uendeshaji na usimamizi. Bado inaonekana ATCL itandeshwa kwa mkono wa serikali.

RAIS - 'ATCL ISITUMIE MAWAKALA WA KUKATISHA TIKETI'

Hili tayari ni agizo ambalo naamini ni agizo lisilo sahihi. Tayari serikali imeanza toka hatua za mwanzo kuingilia uendeshaji wa ATCL. Rais anapoagiza ATCL isitumie mawakala wa kukatisha tiketi inamaanisha ATCL iwe na wafanyakazi waajiriwa kila mahali nchini. Gharama za maelekezo hayo itakuwa kama ifuatavyo:
  • ATCL italazimika kuwalipa wakatisha tiketi mishahara, matibabu, posho, michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, usafiri, n.k. ATCL italazimika kulipia gharama hizo zote bila ya kujali mkatisha tiketi anakatisha tiketi ngapi au kama amepata wateja au hakupata kabisa
  • ATCL italazimika kulipia ofisi na kuweka miundombinu ya ukatishaji ticket nchi nzima. Ifahamike kuwa ukitaka kuwa na ufanisi unalazimika kuwa na ofisi za ukatishaji tiketi hata mahali ambapo ndege haitui, kwaajili ya kuhudumia abiria wanaotoka maeneo hayo wanaotarajia kutumia usafiri wa ATCL kutokea uwanja ulio karibu
  • ATCL italazimika kuwapa mafunzo wakatisha ticket watakaotapakaa nchi nzima
Wakati ATCL watakapokuwa wanahangaika na kuwa na wakatisha ticket wao na ofisi zao, washindani wao wataendelea kuwa na wafanyakazi wachache, wakiwa na mawakala wengi wanaolipwa kutokana na idadi ya ticket na thamani ya ticket walizokatisha. Hawalipii ofisi, hawalipii matibabu, hawalipii michango ya hifadhi ya jamii, hawalipii likizo ya mfanyakazi. Mawakala wao wanalipwa kutokana na wanachozalisha, wasipozalisha hawalipwi chochote.

ATCL wanaanza na quandary ya kwanza, wafuate maagizo ya mwenye mali au kanuni za biashara? Je, hii ni ya mwanzo na ya mwisho au zitaendelea kuja na nyingine? Kwa kuwa tatizo la msingi la uendeshaji biashara zilizo chini ya serikali halijatatuliwa, haitakuwa jambo la ajabu ATCL kufuata projectile ya mashirika/makampuni ya umma.
acha kukariri. siku hizi njia ziko nyingi za kukatisha tiketi. kuna m/airtel/tigo pesa, through bank payment na kadhalika.
 
mkuu sikuhizi systems zimebadirika! ulisafiri lini mala ya mwisho? I mean international freight? huwakilakitu kiko online na mawakala huwa makampuni mengi wanadiscourage! Ila ni hoja ukizingatia systems ya zamani hapo agents role yao ilikua kubwa
ATCL nayo inaanza na international freight? Hiki unachotaka kushauri ni kulizamisha asubuhi shirika hili ambalo brand yake haina mizizi ya kutohitaji mawakala!
 
Mkuu yaani serikali ikiamua kufanya hivyo basi bodi itakuwa haina kazi yoyote pale itakuwa wanapokea maagizo kila uchao na biashara isipoenda vizuri bodi na huyo CEO watalaumiwa na kufukuzwa-serikali iwaache huru waendeshe shirika kwa weledi wao,wao na kamati za bunge wakague mahesabu tu.
Katika mawaziri lazima wawepo wa kusimama na kuhesabiwa. Vinginevyo kama nchi tumekwisha. Mwl alikuwa anashaurika kwa hoja za nguvu.
 
ATCL kama yalivyo mashirika mengine ya umma, kila mara imekuwa ikizaliwa na kufa kutokana na muundo wake usiokuwa wa kibiashara. TANESCO isiyo na mshindani yeyote, TTCL ambayo awali haikuwa na mshindani, na mengine mengi yaliyokwishakufa na yaliyouzwa, mashirika yote hayo yalikufa kwa sababu yalianzishwa, kuendeshwa na kusimamiwa kiserikali/kisiasa.

Serikali haijawahi kuendesha biashara ikafanikiwa. Tatizo linaanzia kwenye muundo wa haya mashirika/makampuni. Wanasiasa/viongozi wa serikali ambao kimsingi si wafanyabiashara ndiyo waliotengeneza muundo wa uendeshaji na ndiyo wenye kauli ya mwisho. Vigezo vya wajumbe wa bodi na watendaji wakuu wanavyo wao. Na siku hizi PhD imekuwa ni kigezo kikubwa sana ingawa kiuhalisia, kwa Dunia nzima, ni nadra sana kuwaona wenye PhD wakiwa wafanyabiashara wazuri na waliofanikiwa.

Juzi wakati Mh. Rais akizindua ujio wa ndege mpya alisema ATCL imezaliwa upya, ina ndege mpya, bodi mpya na uongozi mpya, sikusikia kama ina muundo mpya wa uendeshaji na usimamizi. Bado inaonekana ATCL itandeshwa kwa mkono wa serikali.

RAIS - 'ATCL ISITUMIE MAWAKALA WA KUKATISHA TIKETI'

Hili tayari ni agizo ambalo naamini ni agizo lisilo sahihi. Tayari serikali imeanza toka hatua za mwanzo kuingilia uendeshaji wa ATCL. Rais anapoagiza ATCL isitumie mawakala wa kukatisha tiketi inamaanisha ATCL iwe na wafanyakazi waajiriwa kila mahali nchini. Gharama za maelekezo hayo itakuwa kama ifuatavyo:
  • ATCL italazimika kuwalipa wakatisha tiketi mishahara, matibabu, posho, michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, usafiri, n.k. ATCL italazimika kulipia gharama hizo zote bila ya kujali mkatisha tiketi anakatisha tiketi ngapi au kama amepata wateja au hakupata kabisa
  • ATCL italazimika kulipia ofisi na kuweka miundombinu ya ukatishaji ticket nchi nzima. Ifahamike kuwa ukitaka kuwa na ufanisi unalazimika kuwa na ofisi za ukatishaji tiketi hata mahali ambapo ndege haitui, kwaajili ya kuhudumia abiria wanaotoka maeneo hayo wanaotarajia kutumia usafiri wa ATCL kutokea uwanja ulio karibu
  • ATCL italazimika kuwapa mafunzo wakatisha ticket watakaotapakaa nchi nzima
Wakati ATCL watakapokuwa wanahangaika na kuwa na wakatisha ticket wao na ofisi zao, washindani wao wataendelea kuwa na wafanyakazi wachache, wakiwa na mawakala wengi wanaolipwa kutokana na idadi ya ticket na thamani ya ticket walizokatisha. Hawalipii ofisi, hawalipii matibabu, hawalipii michango ya hifadhi ya jamii, hawalipii likizo ya mfanyakazi. Mawakala wao wanalipwa kutokana na wanachozalisha, wasipozalisha hawalipwi chochote.

ATCL wanaanza na quandary ya kwanza, wafuate maagizo ya mwenye mali au kanuni za biashara? Je, hii ni ya mwanzo na ya mwisho au zitaendelea kuja na nyingine? Kwa kuwa tatizo la msingi la uendeshaji biashara zilizo chini ya serikali halijatatuliwa, haitakuwa jambo la ajabu ATCL kufuata projectile ya mashirika/makampuni ya umma.
Mkuu natumaini hili wazo lako litawafikia walengwa na haya maagizo yatatenguliwa hata kama ni kwa siri
 
Wapiga ramli wa Chadema kazini.

Kama mna ujuzi kiasi hiki mnashindwa nini kumshauri mbowe ajenge ofisi ya chama nzuri?
 
acha kukariri. siku hizi njia ziko nyingi za kukatisha tiketi. kuna m/airtel/tigo pesa, through bank payment na kadhalika.
Ni kweli boss ila ukiwa na akili za biashara lazima uhakikishe una capture possibility zote za wateja kufanya biashara na wewe. Kuna watu hasa wa umri mkubwa wapo comfortable zaidi hard copy ticket kuna watu wanafurahia e-tickets. Kuna watu wengine ni slow learners wanataka waulize maswali kama 10 hivi ndo wakubali kutoa hela kukata ticket
 
Back
Top Bottom