Kwasababu inakuja kabla ya CS300 then baadaye CS300 itaweza kwenda. Lakini pia wataangalia kama abiria wengi wataendelea kutumia 787.
Ningewajua waliotumwa kununua ndege ningewauliza maswali yafuatayo:
Nyie ni marubani wazoefu na mnafaham hali ya shirika letu kifedha na nia ya serikali ya kulifufua.Ni nini kilipelekea mkachagua Bombardier CS 300 badala ya Boeing 737 MAx au A320 neo (Kama tungekuwa tumeopt kuleta A330 au A350)?
Kwa mashirika machanga inashauriwa kumaintain aircraft kutoka kampuni moja kwa sababu ya upunguzaji wa gharama (ufundi na mafunzo).sisi tunataka kugrow kwa maana ya kuwa na ndege za classes tofauti mfano B737-B787-B777 au A320-A330-A350.Ilikuwa kuwaje tukaagiza CS 300 ? kwa sasa Bomardier wameuza program ya Bombardier CS series kwa Airbus hivyo tutarajie CS series zitachukua sura ya Ki airbus airbus. Inachukua ciku chache sana za mafunzo kwa rubani kutoka mfano B737 kwenda b787.Ukitokea CS 300 kwenda B787 ni miezi sita darasani.nani analipa fee na per diem ? kumbukeni hatuna mpango wa kuajiri marubani wazungu hivyo kuna suala la training hapa kwa wazawa.
Mumbai ni ruti nzuri lakini kwa maoni yangu shirika lina grow vibaya.Ingekuwa mimi ni sehemu ya timu iliyotumwa na mheshimiwa kununua ndege pamoja na wataala wengine wa wizara na ATCL ningeshauri tugrow hatua kwa hatua.tungenunua Bombardier Q400 na bombardier CRJ 900 kwa ajili ya soko la ndani na Africa mashariki na kati.tuna bandari pamoja na mpango ule wa Bagamoyo ecoomic zone tungejaza hizi ndege kila siku.Then tunaorder boeing 737 MAX 9/10 kwa ajili ya ruti za Africa magharibi,kusini mwa Africa,Middle East na India.Tukimaliza hapo tunaleta B787-800 kwa ajili ya ruti za ulaya na B787-900 kwa ajili ya Marekani na Uchina.
I hope kuna mipango mizuri once terminal three itakapokwisha basi tutengeze Hub yetu kwa ajili ya nchi za mashariki na kusini mwa Africa.Location ya Dar ina favor burning cost wakati wa kutake off hivyo faida itakuwa nzuri.
Nimalize kwa kusema:
Kila siku ukiwa Zanzibar zinakuja Charttered airlines kama Aero lingus,Thomas cook n.k Zikileta wataalii na ni ndege kubwa sana.Investment ya Airliners tukiiweka vizuri inalipa.Na hapa namaanisha ununuzi wa ndege ,Menejiment ya shirika la ndege,Mafunzo ,Maslahi ya Marubani na Waandisi na muunganiko wa mkakati na Taasis nyingine kama wizara ya Utalii na Maliasili.
Ikiwezekana tuanzishe Sub sidiary airline kwa jina la Air Tanzania Express itakakyokua na ndege ndogo za abiria kati ya 50 mpaka 30.Tuanze na ile 5H-MWF na tutafute ndege kama Beechcraft superking,Dornier 328 au Saab 340.Mtalii akitua KIA Zanzibar au DAR anaweza tumia Shirika letu lingine kwenda Mbugani na kwingine kwa utaratibu uliopangwa vizuri