ATCL: Another Richmond!

[QUOTE=DAR si LAMU;268641]..china ana historia yeyote katika aviation industry ya afrika?[/QUOTE]

Usijali. Hii ni TZ. Atapata uzoefu akiwa kazini!

Si umeona ya Tanzania Railways, TICTS, Kiwira, Kapunga Rice Farms........
 
Nashukuru sana wale wote ambao kwa mapenzi mema kabisa wamechangia thread hii. Nina imani watendelea kuchangia na hatimaye kupata muafaka wa nini kifanyike kabla ya mkataba haujasaini ili kuepuka matatizo yale yaliyojitokeza wakati wa SAA yasijirudie tena.

Kabla hatujafika kwenye tamati ya nini kifanyike, labda tujaribu kuchambua ni yapi huenda ni matarajio ya huyo 'mwekezaji wa kichina'? Uchambuzi wa kujua matarajio ya mwekezaji utaweza kutupatia wigo mkubwa wa kutafakari juu ya nini cha kufanya.

Labda tujikumbushe kidogo yaliyokuwa malengo makuu ya SAA kununua hisa za ATCL.
1) SAA ilianzisha mpango wa muda mrefu wa kutawala soko la biashara ya usafiri wa anga kwenye eneo la kusini mwa jangwa la Sahara. Katika Utekelezaji wa mpango huo ni kwamba ilijiwekea malengo ya muda mrefu na muda mfupi pamoja na mbinu za utekelezaji huo mojawapo ikiwa ni kuyafuta mashirika yote ya ndege kwa kuanzia na yale yaliyopo katika nchi za SADC na jirani na hizo.
Walianza kwa kuifungisha virago Zambia Airways, wakainunua Royal Swazi na kuifunga. Wakasimamisha shughuli za Uganda Airline kwa ku-replace na Alliance Air ambayo pia walikuwa wameomba serikali ya Tanzania isitishe shughuli za ATC wakati ule ili zichukuliwe na Alliance Air (Rejeeni hotuba ya Mh. Malecela wakati anaipokea ndege ya Aliiance Air ilipotua Dar es Salaam Int. Airport kwa mara ya kwanza, Ninamnukuu alivyosema ..."enzi ya vijishirika vya ndege vidogo-vidogo imekwisha sasa, tunataka shirika kubwa kama hili la Alliance Air"). Bahati mbaya kwa SAA ilikutana na pingamizi kubwa juu ya mbinu yake hiyo, lakini ilifanikiwa 'kuiteka' ATCL kwa kununua hisa hapo baadae. Baada ya kuinunua ATCL, SAA iliitelekeza Alliance Air na hatimaye ikajifia kifo cha ghafla.

Punde baada ya kuingia ATCL, SAA ilihakikisha kuwa miundombinu yote ambayo ndiyo ilikuwa ni mihimili ya ATCL inavunjwa ili kuifanya ATCL iwe dhaifu na hatimaye na yenyewe ife. Kwahiyo basi, ATCL iliyopo sasa hivi ni ATCL ambayo iko hoi taabani kimiundombinu hali ambayo ni hatari zaidi kama itaachwa kwa mwekezaji mwingine ambaye atakuwa na kazi rahisi ya ku-justify maslahi kwa kigezo cha hali halisi iliyopo sasa.

2) Lengo jingine la kununua hisa za ATCL ilikuwa ni kuhakikisha kuwa inakuwa karibu na kuimarisha himaya ya SAA dhidi ya Kenya Airways. Ukuaji wa Kenya Airways ni agenda muhimu katika biashara na shughuli za baadae za SAA. Ilichokifanya SAA ni kuhakikisha kuwa wanapambana na Kenya Airways kwa kuchukua soko la Tanzania, Uganda na Rwanda. Hali hiyo ndiyo iliyofanya Kenya Airways 'kuingiza majeshi yake ndani ya ardhi yetu kupamba na hasimu wake SAA' kwa kununua Precision Air. Ununuzi wa Precision Air ulikuwa ni wa kimkakati wa kujilinda kwa Kenya Air dhidi ya SAA. Na kwa upande mwingine uuzaji wa hisa za Precision kwa Kenya Airways ilikuwa ni muhimu kwao la sivyo SAA wangehakikisha kuwa Precision inafutika haraka sana. (Rejeeni kesi ya SAA dhidi ya Sun Air ya Afrika kusini ambapo SAA iliinunua kampuni hiyo ya ndege na kuifunga papo hapo bila ya kufanya kazi.

3) Lengo jingine ilikuwa ni kuongeza mapato na ajira kwa raia wa South Africa. Ni wazi kuwa shughuli za SAA zilitarajiwa kupanuka sana endapo mpango mzima wa kutawala soko la kusini mwa jangwa la Sahara kama ungefanikiwa, sina idadi kamili lakini ilikadiriwa kuwa shughuli zitokanazo na biashara ya anga zingekuwa kwa kiasi kikubwa sana na kukuza uchumi wa SA. Hapa hawakulenga juu ya abiria na mizigo pekee bali na kazi nyingine zitokanazo na sekta hiyo kama vile Mafunzo, Bima nk.

Baada ya kujikumbusha yale machache tuangalie je Mchina anahitaji nini?
Ni wazi pamoja na mambo mengine, anahitaji kutatua matatizo yaliyomo ndani ya nchi yake pia hasa kuhakikisha kuwa masoko ya bidhaa zinazozalishwa China zinapata soko la uhakika. Hili ndilo muhimu kuliko yote. (Rejeeni Makampuni ya ujenzi yaliyozagaa sasa hivi barani Afrika, yote kwa sehemu kubwa yanatumia bidhaa za kutoka nchini mwao).

Kujitanua kwa China kutasaidia kuongeza nafasi za ajira kwa wananchi wake kule China na wengine wataletwa Afrika (Rejeeni vibarua wa uwanja wa Taifa).

China inahitaji kuendeleza na kusambaza teknolojia yake. Kwa nchi yeyote ili katika kutekeleza hili huwa inaagalia maslahi yake kwanza, kwa maana hiyo basi tusitegemee kuwa kutakuwa na enough transfer ya teknolojia kutoka China. Ni wazi kuwa tutatumia equipment 'Made in China' basi hata mafunzo na mambo mengine itabidi yapatikane China. Tutaona msururu wa manunuzi ya vifaa na huduma kutoka China, tutachukua pesa zetu tulizouzia pamba, korosho, chai, kahawa nk na kuzipeleka China ama kama siyo kulipia ukodishaji wa ndege basi kulipia matengenezo ya ndege au mafunzo ya wafanyakazi nk.

tuendelee kuchangia lili hatimaye tuwezekupata mwelekeo wa pamoja.[/COLOR]
 
Punda thanks kwa analysis zako kaka....inafikiwa wakati unakata tamaa, kwani wapiganaji halisi wa maisha ya watanzania hawapo...Yule mwekezaji Halisi hapewi hizo tender, wanaopewa tender ni wezi watupu..

Tujiulize ni lini walitangaza Hii Tender? na Bidders kina Nani waliingiza ktk hio tender...

Hio $350,000 hata vijisent vya Chenge havijafikia...? Hivi Gazeti limekosea au wazir kakosea...
 
so ile project ya kupanua Uwanja wa Ndege imekwisha au pesa zimetafunwa?....naona ni zaid ya miaka 10 sasa...hakuna chochote kilichofanywa!!!!
 
Pundamilia07,
Mkuu maelezo yako mazito sana.. yaani kama kuna kiongozi anayasoma haya nadhani umetoa somo zito sana...Ni mahala pazuri pa kuanzia bila shaka.
Binafsi sina mapendekezo ktk mfumo wa serikali ambayo UFISADI bado umesimama. It's a waste of time...
Kifupi nimechoka kuandika maanake tulikuwa tunalaumiwa kila siku kwa kulalamika, yet nothing has changed na kila siku tunaliwa...
Wanachotaka wao ni sisi wananchi tuzungumie mafanikio, mafanikio ya hatua za mashua inayoingiza maji katika bahati kuu....Kila step deep into the Ocean ndivyo itakuwa vigumu kwa mashua na abiria wake kuokolewa!..Sasa sijui tusifie kitu gani!
Kama kujifunza tumejifunza mengi toka Ujamaa na mengi tumeyaona kwa ubaya wake zaidi ya uzuri lakini kila siku tunazidi kutokomea deep ndani ya umaskini.
 
Chuma,
All we need right now ni Changes ktk Utawala tu.. hakuna dawa zaidi!.. inachosha mkuu ktk kujaribu kuibadilisha CCM ambayo tayari wameisha weka pamba masikioni..
Hili ni sikio la kufa mkuu..
 
PundaMilia,

Ulichofanya hapa ni upembuzi yakinifu wa kiuchumi!

Hivi tujiulize, zile fikra za Nyerere tunazozipiga vita ambazo alitumia umahiri kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa salama kwa kusaidia Frontline na kuleta uhuru Msumbiji si sawa na walichofanya KAA kununua Precision ana kupiga mweleka SAA?

Sasa sisi Watanzania tunashindwa nini kuwa na mikakati mikubwa ya kibiashara na kiuchumi ya kujipatia masoko kama KAA na SAA wanavyofanya na kudhaminiwa na nchi zao?

Au sisi mtaji wetu ni kuuza na kuingia ubia na kukaribisha wawekezaji?

We do not have any competetive strategies, always dwelling on quick buck over here and over there!

Ikiwa tutaendelea kulijenga Taifa letu kwa mtindo huu, kamwe hatutaachana na umasikini!

Brilliant presentation and Analysis Zebra!
 
mkuu [pundamilia

kwanza hongera kwa kukimbia atcl na kuikimbia nchi nadhani kwa maneno haya
ungekuwa umeshawalaza wakina mattaka pale kinondoni CEMENTRY)NAKUSHUKURU KWA UAMUZI WA KUONDOKA MAPEMA MAANA HATA WENGINE 2MEFUKUZWA KWA KUSEMA UKWELI NA KUAPIWA KAMWE ATCL ITASIKIKA NA KIZAZI CHETU.ANY WAY
BADO KAMA NILIVYOKUWA NA UWEZO WA KUFIKISHA UKWELI PALE IKULU NA WAZEE WAKAPAA TA SHIDA NA KUAMUA KUNIONDOA NI MUDA TU NAJIANDAA KURUDI NA SITOACHA KUELEZA UKWELI WA YOYOTE PALE ATC KWA WAH;;HATA NIKIWA NJE YA KAMPUNI;;;;;;;


KAMA UNALETEWA KONTENA KUBWA 50 ZIMEJAA VITU FEKI TOKA CHINA

UNATARAJIA NINI KAMA HUTOLETEWA SPARE MBOVU ZA NDEGE MAINTANANCE UKIMBILIE KWAKE KILA SIKU....


YETU MACHO
 
Inaonekana China Sonangol International Holding Limited ndiyo itachukua ATCL.

Waht to know:

Established in 2004, China Sonangol International Holding Limited mainly engages in oil, gas and minerals investment and exploration, crude oil trading and large-scale national reconstruction projects. With the headquarter office in Hong Kong, the company also has branch offices in China, Africa and Latin America.

In Tanzania, already it has entered into an agreement with Tanzania government to carry out Improvement and expansion of Dar es Salaam International Airport through Tanzania Airports Authority by developing Julius Nyerere International Airport including development of Terminal III.

In Angola, China Sonangol's oil trade has experienced solid development. Currently, over several hundreds thousands barrels of oil are exported and traded from Angola to China every day. In that country, it has undertaken several projects, which include Railway Rehabilitation Projects of Luanda Railway, Benguela Railway and Mocamedes Railway.

The Chinese are also carrying out Improvement Projects in Luanda New International Airport at Luanda, which is the largest airport in Africa.
 
Inaonekana China Sonangol International Holding Limited ndiyo itachukua ATCL.

What to know:

Established in 2004, China Sonangol International Holding Limited mainly engages in oil, gas and minerals investment and exploration, crude oil trading and large-scale national reconstruction projects. With the headquarter office in Hong Kong, the company also has branch offices in China, Africa and Latin America.

In Tanzania, already it has entered into an agreement with Tanzania government to carry out Improvement and expansion of Dar es Salaam International Airport through Tanzania Airports Authority by developing Julius Nyerere International Airport including development of Terminal III.

In Angola, China Sonangol’s oil trade has experienced solid development. Currently, over several hundreds thousands barrels of oil are exported and traded from Angola to China every day. In that country, it has undertaken several projects, which include Railway Rehabilitation Projects of Luanda Railway, Benguela Railway and Mocamedes Railway.

The Chinese are also carrying out Improvement Projects in Luanda New International Airport at Luanda, which is the largest airport in Africa.
 
Mimi sitoshangaa hata kidogo nikija kusikia uendeshwaji wa serikali umebinafsishwa kwa muwekezaji wa nje. Hizo sehemu walizopewa hakuna hata mmoja anayejua tumefikia wapi. Leo mtu aniambie muwekezaji wa zile mbuga za wanyama ameishilia wapi? Muwekezaji wa sekta ya reli naye anaendeleaje? Ile migodi nayo vipi? Kuna madini yoyote yanatoka kule? Ili angalau wananchi wa maeneo ya jirani na migodi hiyo wapate angalau mwanga wa umeme? Oooh, nimesahau ya kuwa suala la umeme alipewa Richmond! Dah, tutafika kweli hivi?
 
- Wahandisi wao watimuliwa usiku kutoka New Afrika kwa ATC kushindwa kulipa pango
- Marubani wao waliokuwa Movenpick wameendelea kukaa kwa wasiwasi baada ya wao kutishiwa kutimuliwa pia (wote hawa ni kwa Airbus)
- Wahandisi wa Dash8 pia wako matatani.

ATCL ina ukata mkubwa wa fedha kiasi cha kutishia usalama wa usafiri wa ndege hizo hasa kama wahandisi na marubani wanaishi maisha ya kuwa na wasiwasi. Wahandisi ilibidi walale kwenye makochi hadi usiku wa manane walipokimbiza cheki New Afrika.

Kuelewa nini kinaendelea pata kijarida usome makala ya kwanza kuhusu ATCL na ukwasi na sakata lake na marubani.
 
Tuendako ni wapi?kama tunasamehe mafisadi wa EPA huku shirika letu tukishindwa kuwalipia hata gharama za kulala hotelini, jamani taifa lipo njia panda.
 
Hivi kweli tuna haja ya kuwa na shirika la ndenge kwa nchi kama yetu, maskini taabani. Kwa mfano Zambia walishajiuzia shirika lao zamani na leo hawana shida za kuli-bail everyday. Nafikiri kwa nchi maskini kama TZ ni bora tusiwenayo tu. Shirika limekuwa politcs tupu na mahali pa wajanja kujitajirisha. Usha ona wapi shirika liko tabaani lakini mabosi kwanza ndiyo wnapeta tu? Anyway, ni maoni yangu tu, msije mkanicharukia!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hizi ndege za ATC imekuwaje tena? Tatu zimeharibika mfululizo! Zimebaki mbili tu ambazo nazo ni 'supana mkononi.' Moja (Boeing 737) imepata matatizo ya injini na iko grounded Mwanza, inasubiri injini ya kukodi. Nyingine (Dash 8) imepata matatizo kwenye nozzles ambazo zimeagizwa nje. Ipo Zanzibar imelala! Nyingine (Dash 8 nayo) ipo DIA hoi bin taaban!
Boeing 737 na Air Bus zinazoweza kuruka nazo zineelezwa kuwa zinahitaji major overhaul.
Hizi ndege zilikuwa katika hali gani zilipoagizwa na ATC? Kulikuwa na technical assessment yoyote kuhakikisha durability yake?
Wasije wakatuua bure na midege mibovu
 
soma kijarida toleo la kwanza na la pili... "tumewaita hawakuja, tumeimba hawakucheza"... tunachosubiri ni ajali ya anga kuwaamsha!
 
Date::10/23/2008
Sh600bilioni zatakiwa kwa mtaji wa kuinusuru ATC
Na Hussein Kauli
Mwananchi

BAADA ya kuvunjwa kwa mkataba kati ya Shirika la Ndege Tanzania(ATC) na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA), shirika hilo sasa linahitaji mtaji wa takribani Sh600 bilioni kwa ajili ya kuimarisha mtaji wake.

Ili kuluipatia ufumbuzi tatizo hili serikali iko kwenye mchakato wa kuingia ubia na mwekezaji kutoka China kampuni ya China Sonangol International Ltd (CSIL).

Mahitaji hayo ya mtaji wa mabilioni yatokana shirika hilo kuendesha shughuli zake kwa kiwango kisichoridhisha.

Akizungumza baada ya mkutano kati ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu na menejimenti ya ATC, Mwenyeketi wa kamati hiyo Alhaji Mohammed Misanga, alismea baada ya kupokea ripoti ya uendeshaji wa shirika hilo, ilibainika linahitaji msaada wa kimtaji.

"Shirika linahitaji dola 507 (karibu Sh600 bilioni) kama mtaji wa kuliwezesha kumudu vema majukumu yake na kujiimarisha katika soko, " alifafanua Misanga na kuongeza:

"Tumekutana na uongozi wa ATC na kupokea ripoti ya uendeshaji wa shirika hilo, lakini liko katika hali mbaya. Hawana mtaji wa kujiendesha na wanalazimika kununua mafuta kwa fedha taslimu. Sasa huwezi kuendesha shirika kwa mtindo huo."

Wakati hali ikiendelea hivyo, Misanga alisema serikali imeshindwa kutekeleza ahadi ilizotoa kwamba itaisaidia ATC kuchukua madeni ambayo inayodaiwa pamoja na mtaji wa uendelezaji.

"Serikali kupitia Wizara ya Miondombinu iliahidi kuisaidia ATC, kwa kuwalipia madeni wanayodaiwa pamoja na kuwapa mtaji wa kujiendesha, lakini yote mawili hayajafanyika," alisema Misanga.

Akieleza mikakati iliyopo hadi sasa kuisadia ATC, alisema serikali iko kwenye mchakato wa kumpata mwekezaji ili kuboresha huduma za shirika hilo na kwamba sasa inaendelea na mazungumzo na kampuni ya CSIL kutoka China.

Misanga ambaye ni Mbunge wa Singida Kusini, alisema katika mchakato wa kumpata mwekezaji huyo serikali iko makini ili kuepusha kuiingiza nchi kwenye mikataba mibovu isiyo na maslahi kwa wananchi na kuongeza kwamba, watahakikisha kuwa kampuni hiyo inafanya kazi zake ipasavyo.

"Serikai itahakikisha kampuni hiyo inafanya kazi zake kwa ufanisi na hivyo ndivyo tutakavyokubaliana, ili tusirudie makosa yaliyojitokeza huko nyuma na kufanya mkataba wetu unakuwa na maslahi kwa wanandhi," aliongeza Misanga.

Alisema ATC kwa sasa ina ndege tatu tu zinazofanya kazi, huku nyingine moja hiaifanya kazi kutoka na kupitwa na wakati na kutumia mafuta mengi na kwamba wako kwenye mchakato wa kuiza ndege hiyo.
 
Wachina wainyemelea ATC
Maulid Ahmed
Daily News; Thursday,October 23, 2008 @20:25

Serikali inatarajia kuingia ubia na Shirika la Ndege la China Sonangol (CSIL) kwa ajili ya kuliendesha Shirika la Ndege Tanzania (ATC). Hadi sasa mazungumzo kati ya serikali na shirika hilo yanaendelea na yamefikia kiwango cha juu cha kuridhisha. Kuungana huko kutakuwa kwa mara ya pili kwa ATC iliyoungana na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) na kuitwa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), iliyovunjika miaka miwili iliyopita.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mohamed Missanga aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa shirika hilo linalazimika kuingia ubia kutokana na sasa kuwa katika hali mbaya kiuendeshaji.

Alisema wakati ndoa kati ya SAA na ATC inavunjika, serikali iliahidi kuchukua madeni ya ATC na kuipatia mtaji ili ijiendeshe vizuri, ahadi ambayo haijaitekelezwa hadi leo.

"Kutokana na yote hayo kutofanyika, hivi sasa ATC haifanyi vizuri, haikopesheki kwa sababu vitabu vyake vya hesabu vinaonyesha ina madeni. Sasa ATC inalazimika hata kununua mafuta kwa fedha taslimu wakati mwingine inakuwa haina fedha kwa wakati husika," alisema.

Hata hivyo, Missanga ambaye ni Mbunge wa Singida Kusini (CCM), alisema serikali imeshaanza kuhangaika kutafuta kulipa deni hilo na kutolea mfano, imechukua hatua ya kuiandikia barua SAA kutowasumbua ATC juu ya deni hilo na badala yake waidai serikali.

Missanga alikuwa akizungumza baada ya kumaliza mkutano na viongozi wa ATC akiwamo Mwenyekiti wa Bodi, Mustapha Nyang'anyi na Mkurugenzi wake, David Mattaka, pamoja na viongozi wengine wa Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu.

Kamati hiyo iliishauri serikali kuwa makini na mwekezaji huyo kwa kuhakikisha mkataba inayoingia nayo hauna kasoro, unaozingatia maslahi ya Watanzania ili makosa yaliyotokea kwa SAA yasijirudie na kuitaka kuharakisha mazungumzo hayo.

Kuhusu wabunge kuuona mkataba huo, Missanga alisema, "serikali imeshatuambia tunaweza kuiona mikataba mbalimbali ila kwa utaratibu wa Spika kuiomba serikalini."

Wakati inajiandaa kuingia ubia, ATC imeanza mchakato wa kuuza ndege yake aina ya Boeing 737-200 ambayo inadaiwa inatumia mafuta mengi. Ndege hiyo ilirithiwa kutoka Shirika la Ndege la Afrika Mashariki. Mbali na ndege hiyo, shirika hilo lina ndege tatu zinazofanya kazi ambapo mbili ni zake na moja imekodi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom