ATCL: Another Richmond!

toleola18.jpg


HABARI ZA KINA NA UTHUBUTU WA HOJA!

Kwa wale ambao wanakipokea kijarida chetu kwenye email zao haitakuwa hivyo leo kutokana na matatizo yetu ya kuhamisha mafaili yetu yote toka klhnews.com kuja mwanakijiji.com* Tunasikitika kuwa kwa leo haitawezekana na tunajitahidi kuweza kufanya hivyo wakati wowote siku chache zijazo.

Tunawaomba radhi kwa usumbufu wowote, lakini bado tunawaomba wale mnaokichukua toka hapa kukituma kwenye email zenu kwa watu wengine na kuendeleza "cheche" na tunaanza kutengeneza back up mailing list ili wakati wote tuweze kuwasiliana nanyi. Tafadhali tumia email ya mwanakijiji.com kuwasiliana nasi siku hizi chache hadi tukitengemaa kwenye email ya back up.

NB* - Tafadhali angalia mabadiliko ya email kwenye kijarida (ukurasa wa mwisho)
 

Attachments

  • TOLEOJIPYA18.pdf
    374 KB · Views: 404
hakikisha umeupdate Adobe Reader yako (kama ni 7 inaweza kuwa ngumu) jaribu kudownload new version kutoka adobe.com halafu jaribu kufungua tena.
 
Mimi naomba sasa maandishi yaonngezeke ili tusitafute lens kubwa zaidi tafadhali .
 
Wafanyakazi wengi wa ATCL wanawatetea sana wakurugenzi wa bodi na sio Mwenyekiti; sababu wanazotoa ni kwamba Mattaka alikuwa anawaficha taarifa muhimu kwahiyo wakurugenzi walikuwa hawajui mambo mengi.Inasemekana wakati mwingine wakurugenzi walikuwa wanaitisha vikao na kujadili mambo bila mwenyekiti wao mara walipogundua mshikamano kati ya mwenyekiti na CEO. Mimi nakubaliana na wafanyakazi kwa hilo kwani hata ukikumbuka sakata la mahujaji walohusika kikamilifu bila kuwahusisha wajumbe wengine wa bodi walikwa Nyan'ganyi na Mattaka;wajumbe hao wengine walitoa taarifa kusisitiza kuwa wahusika wa sakata lile alikuwa mwenyekiti na watendaji . Inaelekea mambo mengi Nyan'ganyi alikuwa anafanya na watendaji bila wakurugenzi wengine kujua. Inasemekana mpaka wizara ikaamuru asiruhusiwe kutumia ofisi pale ATC house aliyopewa na Mattaka kwani alikuwa anaingilia daily operations za shirika. Kutokana na kutoridhishwa na jinsi ATCL ilivyokuwa inaendeshwa wakurugenzi wengine wa bodi walijiuzuru to safe guard their intergrity!!.
 
Wafanyakazi wengi wa ATCL wanawatetea sana wakurugenzi wa bodi

mkuu bulesi hakuna kitu kama hicho kwenye bodi,,kuna mwenyekiti na wajumbe tu.sasa basi kama mwenyekiti kaaribu laxzima wajumbe wote wafwatane nae hakuna kubkiza uozo nafikiri ulikuwa na maana hii....
 
Poleni watanzania, maana kila kukicha tuna pata kustaajabu. Mambo ya mashirika yetu kila siku yako hivyo sijui wapi tunakwenda, na je tutafika???
lakini labda tujiulize sisi JF tunafanya nini, labda tuanze na kujitayarisha kwa mbinde kuwa na uwezo wa kuendesha makampuni vizuri halafu tutafute hizo nafasi

food for thought
 
Jamani tafadhali naomba tuache "arch chair " jounalism. Ebu tuwaombe "investigative" jounalists wetu wafanye uchunguzi wa kina kuhusu nini kinatokea ATCL ili umma upate balanced view. sasa hivi kila article is full of hysteria with very liitle substance regarding ATCL fiasco. Kwa mfano Umma haujui kama ATCL imezuiwa kuruka kwa sababu ya "airworthness" au "AOC". Hivi ni vitu viwili tofauti kabisa na hata Waziri wa Miundombinu anavichanganya! Ukitaka kujua undani wa tatizo ili ebu anzia Tanzania Civil Aviation (TCCA) ili ujue nini kilijiri. Usikubali kupewa taarifa ya maadishi maana nao hawataki kusema ukweli. Kisha nenda ATCL na uchunguze huko. Usikubali kuongea na kila mfanyakazi wa ATCL ila tafuta mtu wa operations (sio rubani). Kisha nenda Miundombinu ukamalizie huko. Amini usiamini story itakayotoka ni tofauti na mambo yanayoandikwa sasa hivi. ATCL ni kama Tanzania Railways (TRL). Waandishi wanaulumu muwekezaji wa kihindi lakini ukichunguza nani ana makosa na ameshindwa kutimiza masharti utashangaa. Ni SERIKALI! Kama mnabisha chunguza. Suala la ATCL ni gumu kuliko watu wanavyofikiria na ili kujua inabidi waandishi wasiishie kwenye Press conference ambazo mara nyingi ni "Gabbage in, gabbage out".
 
nDUGU WANANCHI,KUMEKUWA NA MAWAZO YA WATU MBALIMBALI AMBAO KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE WANAPEWA MADARAKA YA KUONGOZA NCHI MAKAMPUNI AMA MASHIRIA MBALIMBALI KWA KUPEANA AMA KUJUANA KINDUGU,,SASA BASI IMEFIKA SASA WANANCHI WAMEONA BASI INATOSHA NA YOYOTE ALIETUMIA MADARAKA YAKE VIBAYA LAZIMA AFIKISHWE KWENYE MKONDO WA SHERIA,,JF KAMA SEHEMU YA KUFUNDISHANA NA KUMSHAURI RAISI NINI AFANYE NANAI AMTEUE...TUMEONA MAWAZIRI MBALI MBALI MRH MRAMBA NA MH YONA WAKIKWAA GARI LA KIJANI KUELEKEA KEKO KUJIBU TUHUMA ZA UBADHIRFU WA MALI YA UMMA KWA KUTOA MISAADA YA AJABU AJABU..SASA BASI HIVI SASA TUSIKIMBILIE TU SIMBA WAKUBWA WAKUBWA TWENDE KUWAONYESHA ADABU WALE WANAOPEWA HAKI YA KUONGOZA MASHIRIKA YA UMMA KAMA ,,BOT.TANESCO.TRLA,TTCL.ATCL NA MENGINEYO....MAJUZI NIMESOMA KIJARIDA KIMOJA KUTOKA HAPA JF KINAONYESHA JINSI BAADHI YA VIONGOZI WA ATCL WALIVYOLITAFUNA SHIRIKA LA AIRTANZANIA BILA AIBU...NA KILICHONIUMA ZAIDI NILIPOONA KUNA BAADHI YA WANABODI WAMEGAWANA DOLLER 11,000 NDANI YA WIKI MBILI HUKU KUKIWA NA WAFANYAKAZI AMBAO HAWAJALIPWA MISHAHARA YAO MPAKA LEO HII....NADHANI KUNA TATIZO KUBWA SANA KAMA KIONEKANAVYO HAPO CHINI...MH RAISI HIVI SASA TUANZE KUWAFUNDISHA ADABU HAWA VIONGOZI WA MASHIRIKA YA UMMA WANAOIBA WAKIJUA UMEWACHAGUA NA HIVYO HAKUNA MKONDO WA SHERIA UTAKAOWAFWATA
NA KATIKA KUANZA NA HILI TUNAOMBA

MH MUSTAFA NYANGANYI NA MKURUGENZI WAKE BWANA DAVID MATTAKA WAWE FUNDISHO KWA WALE WOTE WALIOPEWA DHAMANA YA KUONGOZA MASHIRIK YA UMMA KUANZA KUYAHESHIMU KWA KUWAFIKISHA KWENYE MKONDO WA SHERIA(MAHAKAMANI),HARAKA IWEZEKANAVYO
NINA UHAKIKA KAMA MH UJUAVYO BWA DAVID ALIONDOLEWA KWA UBADHIRIFU PALE PPF NA KWA USWAHIBA WAKO UKAAMUA KUWASAKAZIA MASIKINI WAFANYAKAZI WA ATCL..NAAMINI KAMA ALIPOONDONDOLEWA
ANGEFIKISHWA KWENYE MKONDO WA SHERIA LEO HII ASINGE FANYA UBADHIRIFU WA HALI YA JUU KAMA UNAVYOSOMA HAPO CHINI.....

LENGO LETU SI TU WAJIUZULU MANAGEMENET NA BODI YAKE ,LA HASHA KUNA USHAHIDI WA KUTOSHA KATIKA YALIOANDIKWA HAPO CHINI KUHUSU WIZI WA MALIZ A KAMPUNI HIVYO NI LAZIMA WARUDOSHE MALI ZA WATANZANIA.....HAIWEZEKANI GARI USED INANUNULIWA DUBAI KWA MILLION 25,000 MTU KWA MOYO WAKE WOTE NA KWA ROHO YAKE YOTE NA NAFSI YAKE ANAANDIKA GARI IMENUNULIWA KWA DOLLER 72,000.....
MFANO MDOGO NI HIZO NDEGENDOGO SOKO LA DUNIA KILA SEHEMU NI USD MILL4.5 LAKINI UNAAMBIWA WAMENUNUA KWA USD MILLION7.5....MFANO MWINGINE NI UNUNUZI WA AIRBUS...SOKO LA DUNIA NI 260,000USD LAKINI WAKANUNUA 360,000USD LEO HII WANGEKUWA WAPI KWA DIFF YA 100,000USD AMA 3MILLION USD KWA KILA NDEGE NDOGO WALIONUNUA...JE SWALI LANGU UKIACHA PESA WANAZOPATA KUTOKA KWA MARUBANI KAMA KAMISHENI DOLLER 3000USD INAINGIA MIFUKONI MWAO MOJA KWA MOJA NA USHAHIDI UPO....KUNA HAJA GANI YA WAO WAJIUZULU TU..

TUNAOMBA RAISI WOTE WALIOSHIRIKI KUIUA ATCL WAFIKISHWE MAHAKAMANI MARA MOJA
WAKO SWEETBABY
UKIPENDA MALOVE
 
Bodi ya ATCL inapaswa kujiuzulu kwa kuwajibika.

______________________________
[SIZE="3[COLOR="Red"]"]Mimi sikushiriki wala kushauri, sikuagiza wala kuelekeza kwa kuwa haya yamefanyika katika Wizara yangu.......... kwa dhamana yangu kama Waziri naomba kujiuzulu [/SIZE][/COLOR]-------- Ali Hasan Mwinyi Waziri, Mambo ya Ndani
 
Date::12/23/2008
ATCL yawatupia mzigo Mramba, Chenge, Lowassa

Leon Bahati
Mwananchi

SAKATA la kusimamishwa kwa Shirika la Ndege Tanzania Tanzania (ATCL) katika kuto huduma limechukua sura mpya baada ya Ikulu pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Basil Mramba na Andrew Chenge kuhusishwa hivyo kutakiwa kutoa maelezo.

Wengine ambao nao watatakiwa kutoa maelezo kuhusiana na suala hilo ni Ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi pamoja na maofisa watendaji wa Wizara ya Miundombinu wakati ikiwa chini ya mawaziri wawili wa kwanza wa serikali ya awamu ya nne, Basil Mramba na Andrew Chenge.

Habari za kuaminika zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana zilieleza kuwa maelezo yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa ATCL, Balozi Mustapha Nyang'anyi kwa Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa wiki iliyopita, zimehusisha vigogo hao katika kiini cha matatizo ndani ya shirika hilo.

Wiki iliyopita, Dk. Kawambwa alimpa siku saba Nyang'anyi kutoa maelezo yanayohusu sababu zilizosababisha Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Anga (TCAA) kunyang'anywa ATCL leseni ya kurusha ndege.

Nyang'anyi aliwasilisha maelezo hayo wiki iliyopita na kutaja baadhi ya mamlaka hizo za serikali kuwa zilipatiwa maelezo ya kina kuhusu hali ilivyo ndani ya ATCL pamoja na mapendekezo yanayotakiwa kufanywa, lakini hakuna kilichofanyika katika kuliokoa shirika hilo.

Waziri Kawambwa pamoja na timu ya wataalamu wake waliyapitia maelezo hayo mwishoni mwa wiki walibaini kuwa katika kufikia maamuzi ya utetezi huo, inabidi wapate maelezo ya kina kwa mamlaka hizo ambazo kwa nyakati tofauti siku za nyuma, walitakiwa tarifa ili wanusuru shirika hilo.

Dk. Kawambwa jana aliliambia gazeti hili kuwa bado wanaendelea kushughulikia maelezo hayo ya bodi na kuahidi kutoa tamko rasmi baada ya kukamilisha mchakato.

Chanzo chetu ndani ya wizara hiyo, zilisema kuwa mkakati huo umefikia mahali pagumu kwa kuwa mbali na kupata maelezo ya vigogo kadhaa, itabidi wachunguze msimamo wa serikali tangu ilipoazimia kuvunja mkataba na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA).

"Utetezi wa bodi umetupa wakati mgumu na wala sifikiri kama maamuzi yanaweza kutoka mapema," kilieleza chanzo hicho kikifafanua:

"Ofisi nyeti sasa zimehusishwa... Maamuzi hayawezi kufikiwa mpaka tupate kauli zao, kama ni kujikwaa itajulikana ni wapi."

Ingawa chanzo hicho hakikuweza kuweka bayana namna watakavyoweza kupata maelezo ya mamlaka hizo, lakini kimeweka wazi kuwa chunguzi huo, utafanywa pia kwa kuzingatia mikakati na mipango ya serikali kwa ATCL kuanzia utawala wa serikali ya awamu ya tatu.

Kulingana na maelezo ya bodi, serikali ya awamu ya nne ilipoamua kuvunja mkataba na SAA, iliweka maazimio ya kutoa fedha za kuifufua ATCL jambo ambalo halikutekelezwa.

Miongoni mwa mambo ambayo yamo kwenye maelezo hayo na ambayo pia Balozi Nyang'anyi aliwahi kulieleza gazeti hili ni serikali kutotekeleza ahadi yake ya kulipa deni la ATCL linalofikia Sh19 bilioni pamoja na mtaji wa dola za Marekani 67 milioni.

Wakati huo huo, serikali imetoa zaidi ya dola 100,000 kwa ajili ya kusafirisha maofisa wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Anga (TCAA) kwenda kukagua karakana zinazotumika kufanyia matengenezo ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) nchini Kenya na Afrika Kusini.

Sehemu ya fedha hizo pia itatumika kwa ajili ya kununua vipuri vya ndege ambavyo ni kwa ajili ya matengenezo madogomadogo ya dharura kwenye karakana ya ATCL.

Habari zilizopatikana jijini Dar es salaam jana na kuthibitishwa na Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa zilisema kuwa mkakati huo ni sehemu ya kuhakikisha kuwa ATCL inarejeshewa haki yake ya kurusha ndege waliyonyang'anywa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Anga (TCAA).

Katika kufanikisha hilo, alisema serikali imekusudia kutumia dola za Marekani 273,000 kwa ajili ya kufanikisha kusudio hilo.

Hata hivyo, Dk. Kawambwa hakuwa tayari kuelezea kwa undani taarifa ya serikali kutoa zaidi ya dola 100,000 kwa ajili ya kusafirisha maofisa wa TCAA na ununuzi wa vipuri, kwa maelezo kwamba ni suala la kiutendaji zaidi.

Wakati huo huo, Ofisa Uhusiano wa TCAA, Abel Ngapemba alithibitisha kuwa wataalamu wake wanaendelea kupitia nyaraka mbalimbali za ATCL zilizopelekwa mahususi kusahihisha kasoro zilizoonekana ndani ya shirika hilo.

Hata hivyo, alisema ni vigumu kueleza iwapo kuna uwezekano wa ATCL kurejeshewa leseni yake katika siku za karibuni kwa maelezo kuwa wataalamu wa TCAA, kwa sasa wametingwa kiasi kwamba imekuwa vigumu kupata upenyo wa kueleza hatua waliyofikia.

"Wataalamu wetu wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana. Hata walipo siyo rahisi kuwasiliana nao maana 'wako-buzzy' (wametingwa) sana," alisema Ngapemba.

ATCL ilikuwa imeahidi kukamilisha mpango wa masahihisho wa nyaraka zake ndani ya siku 10 ambazo ziliisha jana.

Ngapemba alisema kuwa ATCL tayari imewasilisha vielelezo hivyo na sasa inasubiri maamuamuzi ya TCAA.

TCAA waliinyang'anya ATCL baada ya kubainika kuwa na kasoro kadhaa kwenye nyaraka zake za kuendeshea shirika ambazo ni kinyume na kanuni za Umoja wa Mashirika ya Ndege Duniani (IATA).

Serikali iliamua kuingilia kati na kusaidia fedha za kufanikisha mpango wa ATCL kurejeshewa leseni yake baada ya kubaini kuwa shirika hilo linakabiliwa na hali mbaya ya fedha.
 
Date::12/23/2008
Serikali iliamua kuingilia kati na kusaidia fedha za kufanikisha mpango wa ATCL kurejeshewa leseni yake baada ya kubaini kuwa shirika hilo linakabiliwa na hali mbaya ya fedha.

Hivi mbona wanapenda sana kuweka kwamba tatizo ni fedha? na naona washaanza kutupiana lawama. Weka jela kwanza hiyo menejimenti na waende kwa akili na sio pupa, kwa sababu hela sio kila kitu, kama uongozi ni ovyoo hakuna kitakachofanyika baada ya muda tutaambiwa tatizo ni hela tena. Shirika gani halipati faida? Na inabidi kukagua mikataba na ununuzi wowote walioufanya kama unalingana na gharama walizotumia ama sivyo tutarudi palepale.
 
Nadhani serikali ilifanya vizuri kuchukua ATCL kutoka mikononi mwa SAA. Ila uamuzi wao haukuwa na maandalizi ya kutosha. Hasa kuzingatia kwamba SAA walikuwa wakisimamia utendaji na mapato ya shirika. Walitakiwa kufanya tathmini ya nini kinachowezekana kufufua shirika baada ya kuchukua miliki upya.

Sidhani kuwa serikali ilikuwa na budget ya kuendesha ATCL. Kama ingekuwepo, nadhani kasoro nyingi zisingekuwepo.
 
miradi yote tanzania hua-haipati fedha za kutosha na mingine inaendelea ni kutokana na kutuia vizuri hicho kidogo kilichopo, tukifuata ya nyangani na mataka, basi miradi mingi itakufa kabla hata haija anza. hivyo basi wao walianza kula zile zilizo kuwepo wakitarajia hilo fungu kubwa lije waendeleza ulaji wao, maana viongozi wengi ndio zao hizo kutafuta njia ya kula, kwa suala hili kama Mramba, lowasa, chenge wanayo yakwao, na pia na mustafa na david wanayo ya kwao.
 
Date::12/23/2008
ATCL yawatupia mzigo Mramba, Chenge, Lowassa

- Saafi sana, unaona sasa effect ya kuepeleka viongozi wabovu Kisutu? Hao ATCL tayari wanajua kuwa soon mmoja wao ata-roll Kisutu sasa wanaanza kutajana wenyewe,

- saaafi sana waachwe wajiseme halafu ni kupeleka wote tu Kisutu hakuna huruma, tutachambua mbele ya safari, I mean how good can this fight get hasa wanapoanza kutajana wenyewe kwa wenyewe, let them sing hakuna huruma!
 
Date::12/23/2008
Wakati huo huo, serikali imetoa zaidi ya dola 100,000 kwa ajili ya kusafirisha maofisa wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Anga (TCAA) kwenda kukagua karakana zinazotumika kufanyia matengenezo ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) nchini Kenya na Afrika Kusini.

Sehemu ya fedha hizo pia itatumika kwa ajili ya kununua vipuri vya ndege ambavyo ni kwa ajili ya matengenezo madogomadogo ya dharura kwenye karakana ya ATCL.

Habari zilizopatikana jijini Dar es salaam jana na kuthibitishwa na Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa zilisema kuwa mkakati huo ni sehemu ya kuhakikisha kuwa ATCL inarejeshewa haki yake ya kurusha ndege waliyonyang'anywa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Anga (TCAA).

Katika kufanikisha hilo, alisema serikali imekusudia kutumia dola za Marekani 273,000 kwa ajili ya kufanikisha kusudio hilo.

Hata hivyo, Dk. Kawambwa hakuwa tayari kuelezea kwa undani taarifa ya serikali kutoa zaidi ya dola 100,000 kwa ajili ya kusafirisha maofisa wa TCAA na ununuzi wa vipuri, kwa maelezo kwamba ni suala la kiutendaji zaidi.

Sasa serikali ilikuwa wapi kutoa fedha hizo ambazo ziliombwa kupitia Bodi ya ATCL? Yaani sasa wamefungiwa ndo wanaona umuhimu wa kutoa hizo pesa. Ukiangalia hizo pesa zitakazotumika ni zaidi ya pesa ambazo Bodi iliziomba. Tanzania tutajifunza lini juu ya responsibilities?
 
Kwani wewe unadhani kazi ya jalala la taka ni nini?

Mkuu hapo tupo ukurasa mmoja yaani wanaleta siasa
Hivi kama mtu anachagukiwa kuwa mkurugenzi lazima abobee kwenye hiyo fani kama tatizo pesa hamna si wangefanya wenyewe ?
Na kuokoa pesa za walipa kodi
Hii inaonyesha hao viongozi ATC hawajiamini au vihiyo bora watolewe tuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom