Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,731
- 40,838
Shirika la ndege la ATC ambalo liko katika hali mbaya ya kifedha linakabiliwa na ukata mkubwa kiasi cha kukimbilia serikalini na kuomba wabebwe tena kwa kupewa ruzuku ya Shilingi bilioni 7! Hii inafuatia deni kubwa walilonalo kwa kampuni ya Wallis Trading ya Liberia ambayo kutoka huko walikodisha lile dege bovu ambalo linaruka kwa masharti magumu la Airbus 320.
Hadi hivi sasa haijajulikana ni lini na kama serikali iko tayari kutoa kiasi hicho cha fedha kuinusuru tena kampuni hiyo ambayo mwishoni mwa mwaka jana chini ya uongozi wa kizembe wa David Mattaka na bodi ya kina Mustaffa Nyang'anyi ilijikuta inalazimia kuingiliwa kati na serikali ili kuwasafarisha mahujaji kwenda na kurudi toka hija takatifu.
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu ndani ya shirika hilo, hali ni mbaya sana kiasi kwamba "tunasubiri bajeti ipite kwa haraka vinginevyo siri za huku zikigundulika tumekwisha". Afisa huyo ambaye amepata nafasi ya kuona barua za kuomba ruzuku hiyo ameiambia KLHN kuwa bila kuletwa kwa wakaguzu huru wa mahesabu ya shirika hilo basi Watanzania kamwe hawatajua kilele cha uzembe na ubadhirifu ndani ya shirika hilo.
Hadi hivi sasa kwa mujibu wa chanzo hicho "ni Rais tu ndiye mwenye uwezo wa kubadilisha kwani alimuweka mshikaji wake hapo na sasa kumuondoa imekuwa mbinde, ndiyo matatizo ya ushkaji hayo".
Chanzo muhimu toka shirika la Wallis Trading lililosajiliwa huko Liberia kimesema kuwa "tumeanza kuchoka kweli na hii ATC tungejua tusingewakodisha Airbus wamekuwa wakituzungumza mno" Jitihada za kumpata kiongozi wa ATC kuzungumzia suala hili zinaendelea.
Kwa habari zaidi tembelea KLH News...