ATC Taabani! yaomba serikali Bilioni 7!

Siwezi kuamini kwamba mwaandishi makini kama Mzee Mwanakijiji ameshindwa kukaa na habari yake mpaka asikilize upande wa pili alafu ndio atuletee habari kamili...? Sio habari nusu ijaziliwe na wananchi...

Hahaha... sijui uandishi lakini kwa speed hii!!! Taifa linazama...

Kwi kwi kwi Kasheshe,

Ndio maana imeandikwa kuwa inaendela,..... moja ya news inayoendelea huwa ni kuwa yaweza kubadilika ..... siamini hukuona hilo mzee......lol
 
wasipewe kitu.....hawa kwanza wazembe wawajibishwe kisha ndio pafikiriwe kama wapewe au la.
hivi kila siku tutaendelea kujaza kifuu tundu kwa nini!!
 
Ndiyo ndege imeanza kuruka kwenda Afrika Kusini.. lakini inaruka kwa hasara! miye yangu macho siku everything is said and done tutajua huyo aliyependekeza tukodishe jidege hilo na kununua mpya toka Hamburg angetiwa pingu siku nyingi tu.

Hio Airbus inakwenda hata Mwanza...
 
Ndiyo ndege imeanza kuruka kwenda Afrika Kusini.. lakini inaruka kwa hasara! miye yangu macho siku everything is said and done tutajua huyo aliyependekeza tukodishe jidege hilo na kununua mpya toka Hamburg angetiwa pingu siku nyingi tu.

Kwa nini iruke kwa hasara wakati hii route siku zote iko almost full-booked? A320-200 series ni moja kati ya ndege nzuri sana kama iko Ok. Kwa hiyo kama kuna mapungufu itakuwa ni kwenye mkataba mzima wa kukodisha, kitu ambacho kisingetakiwa kitokee hasa baada ya Richmond.

Kukodisha pia wakati mwingine sio kubaya ili uweze kuwa na routes nyingi mwanzoni mwa kuanzisha shirika. Hii ni capital management, lakini haina maana kuingia mikataba ya kirichimondi. Kama huu mkataba ni mbovu, someone has to go, not home-----Jail.
 
Inaruka ikiwa na chini ya abiria 100 (nadhani ina uwezo wa kuchukua abiria 150). Sijui bei yake ni bora kuliko ndege nyingine zinazoenda Afrika ya Kusini... halafu imepewa kikomo cha umbali wa kuruka angani kutokana ma masuala ya kiufundi....
 
mie napinga atc kufa hivi hivi. kwa sababu hatujashindwa kwa kuwa hali imetushinda ya ushindani wa masoko ila kwa uzembe wa watu fulani.
mpaka watu hao watakapowajibishwa na zikapita juhudi za kuokoa zikashindwa ndio atc ife.
atc kama inakufa ife na hao walafi wake. wafe wapotee kabisa katika uso wa dunia.
 
Ndiyo ndege imeanza kuruka kwenda Afrika Kusini.. lakini inaruka kwa hasara! miye yangu macho siku everything is said and done tutajua huyo aliyependekeza tukodishe jidege hilo na kununua mpya toka Hamburg angetiwa pingu siku nyingi tu.

Nimetoka South Africa juzi (Jumapili), Inasemekana flight zote za ATC kutoka Joburg kuja Dar zimekua canceled until further notice.
 
Nimetoka South Africa juzi (Jumapili), Inasemekana flight zote za ATC kutoka Joburg kuja Dar zimekua canceled until further notice.

Kwa route ya SA wala tusiwalaumu sana ATC, nadhani kaburu kwa makusudi kapania kuchukua route hiyo. Nakumbuka a month a go nilienda SA ndege ya watu 150 abiria tulikuwa si zaidi ya 20, na hapo tuliondoka na ndege ya asubuhi lakini pia ilikuwepo nyingine ya mchana, kwa maana kwamba SA wamejiandaa kulipia hiyo hasara ili wamtoe ATC katika route hiyo!. Kibaya zaidi ni kwamba pia nauli ya SA iko cheap ukilinganisha na ATC japo ukienda kata tiketi wanakuvutia kwa bidii zote utumie ATC!

Hilo ndo tatizo lingine nililo liona la kichuguu kupambana na mlima!
 
Rwabugiri sasa watu wa Marketing wa ATC walipoamua kuiweka dege hilo kwenda Afrika ya Kusini walikuwa wanafikiria nini? Kwanini kuanza na route ngumu kama hiyo? Mwanzoni walikuwa wanafikiria kuipeleka njia ya Khartoum pia!
 
Back to stratergies.............. Sidhani kama kuna mpango wowote wa kukabiliana na ushindani kwenye shirika letu na ndio maana kila kukitokea tatizo kwenye funding wanakimbilia kwenye ruzuku!!

KJ amesema huko nyuma matatizo yetu pia tulishaliongelea hili huko nyuma, MANAGEMENT!! Hili sio kwa MD/CEO pekee bali hata wakurugenzi wengine pamoja na wakuu wa Idara mbalimbali!!
 
Rwabugiri sasa watu wa Marketing wa ATC walipoamua kuiweka dege hilo kwenda Afrika ya Kusini walikuwa wanafikiria nini? Kwanini kuanza na route ngumu kama hiyo? Mwanzoni walikuwa wanafikiria kuipeleka njia ya Khartoum pia!

Hapo ndo shida ilipo, siasa na propoganda zinapotangulia utaalamu! Naamini utaalamu wa biashara ungethaminiwa hakukuwa na haja ya kukodi dege kubwa lenye mkataba wa kirichmond wakati abiria wenyewe wa kulitumia hilo dege ili lilete tija hawapo!

Nadhani adui yetu mkubwa mwingine wa maendeleo ya Tanzania ni upungufu wa utaalamu katika 'decision makers team'! sorry to say it but ndo ukweli
 
mtu anapozowea spoon feeding hawezi kujihangaisha hata siku moja.
atc wamezowea kupewa ruzuku....na ndio maana unakuta hawawezi kuzituma akili zao.
management ya resources ovyo, strategies ovyo, shirika linaendeshwa kwa risks tu na wala watu hawajali wanajua wakikwama serikali inawajazia mapesa.
haya sasa, kama walivyolindwa mafisadi wengine, na hapa serikali na iwalinde. iendelee kuingia hasara kwa mambo ya kujitakia.
 
Katika strategic Marketing: Kaburu wanachofanya ni kutaka kuwatoa hao jamaa kwenye route ya South Africa. Kwa kuteremusha bei kwa makusudi ni kutaka kuwaondoa kwenye market, wakishaondoka wao wanapandisha bei mara mbili au tatu kufidia pesa zao zilizopotea.

Mfano ni Coca-cola (USA) walipoingia India, kwa kutengeneza coca za cane waliuza kwa bei ya hasara kwa mwaka mmoja, hivyo viwanda vingine ambavyo vilikuwa vinatengeneza Coca za chupa ikabidi vifunge biashara zao maana watu walishift toka soda za chupa na kununua za cane ambazo ni bei ya chini. Baada ya hivyo viwanda kufunga biashara, Coca (USA) waliongeza bei mara tatu.

Kwa hiyo strategy wanayotumia hao Makaburu ni sawa tu na hiyo ya Coca-Cola (USA).

Best strategies for ATC to win the market:
Use Travel search engine & Travel Finds Specials these will showcase ATCL best fares to millions of travelers each month through Web site.

Engage directly with consumers, enable consumer to buy the ticket on the Internet

Use email newsletter send to your customer every week/month etc.

Engage direct or tied up with the big hotel.

Strategic alliance with Tanzania tourism Industry

Promotion per milleage
 
Kokolo.. point nzuri hiyo. Sasa hawa ATC walipoenda kupata hizo Dash 8 mbili na Airbus moja... walikuwa wamefanya market analysis ya kujua soko wanalotaka kuziingiza ndege hizo likoje?
 
Kokolo.. point nzuri hiyo. Sasa hawa ATC walipoenda kupata hizo Dash 8 mbili na Airbus moja... walikuwa wamefanya market analysis ya kujua soko wanalotaka kuziingiza ndege hizo likoje?

MWKJJ,

usinifurahishe, hivi ni govt institution gani yenye kujua huo msamiati wa "Market Analysis" ama "Business Plan"? Kama institutions zetu zikiweza kufahamu hiyo misamiati na kuweza kuifanyia kazi basi serikali yetu haitakuwa na bajeti tegemezi tena!! Na wala haitakuwa na wababe wa kuitisha kila kukicha!!
 
Think naona sasa ndio wewe unanitisha.. hivyo Vyuo Vyetu vikuu havina kozi za Marketing? Au watu wanasoma ili wafaulu mitihani tu...?
 
MWKJJ,

usinifurahishe, hivi ni govt institution gani yenye kujua huo msamiati wa "Market Analysis" ama "Business Plan"? Kama institutions zetu zikiweza kufahamu hiyo misamiati na kuweza kuifanyia kazi basi serikali yetu haitakuwa na bajeti tegemezi tena!! Na wala haitakuwa na wababe wa kuitisha kila kukicha!!

..si kweli,

..kinachotufanya tuwe tegemezi si kufahamu hayo!,bali ni kutotaka kafanya kazi ya ziada,kuendekeza rushwa na kukubali kuongopewa na wazungu!
 
Katika strategic Marketing: Kaburu wanachofanya ni kutaka kuwatoa hao jamaa kwenye route ya South Africa. Kwa kuteremusha bei kwa makusudi ni kutaka kuwaondoa kwenye market, wakishaondoka wao wanapandisha bei mara mbili au tatu kufidia pesa zao zilizopotea.

Mfano ni Coca-cola (USA) walipoingia India, kwa kutengeneza coca za cane waliuza kwa bei ya hasara kwa mwaka mmoja, hivyo viwanda vingine ambavyo vilikuwa vinatengeneza Coca za chupa ikabidi vifunge biashara zao maana watu walishift toka soda za chupa na kununua za cane ambazo ni bei ya chini. Baada ya hivyo viwanda kufunga biashara, Coca (USA) waliongeza bei mara tatu.

Kwa hiyo strategy wanayotumia hao Makaburu ni sawa tu na hiyo ya Coca-Cola (USA).

Best strategies for ATC to win the market:

Use Travel search engine & Travel Finds Specials these will showcase ATCL best fares to millions of travelers each month through Web site.

Engage directly with consumers, enable consumer to buy the ticket on the Internet

Use email newsletter send to your customer every week/month etc.

Engage direct or tied up with the big hotel.

Strategic alliance with Tanzania tourism Industry

Promotion per milleage

..in short,aggressive marketing campaign.
 
Jamani, shida kubwa zilizopo ATC ni mbili tu kama nilivyosema hapo nyuma, uongozi mmbovu na liquidity. Liquidity walishahidiwa kusaidiwa na serikali ili kufufuka, alkini kuoperate effectivelly na efficiently itategemeana sana na uongozi.

  1. Binafsi yangu sidhani kama route ya J'burg ina hasara hata kidogo kama watendaji wakiwa makini. Abiria wake ni wengi as long as wanajitangaza vizuri hasa upande wa SA na kuwa na huduma nzuri na on time. Pia sio kweli kuwa SAA wanatoa bei za chini kuliko ATC, on contrary ATC wako cheaper mara kwa mara kwa btn $10-40. Search kwenye net utaona.
  2. Tatizo kubwa la ATC ni uongozi ambao pamoja na mengine mengi mabovu kwenye utawala, wanashindwa pia kuli-structure shirika ili lika-optimize wafanyakazi na resources zake. Wafanyakazi 300 kwa ndege sita ni wengi mnno. Nafikiri bado wanaoperate kama ilivyokuwa zamani lilipokuwa kama idara ya serikali.
  3. Huo mkataba wao wa hiyo A320 unatakiwa pia uangaliwe kama uko safi maana hata wakati wa ATCL (yaani + SAA), walikodisha mara kwa mara ndege za SAA kwa bei ya juu sana ukilinganisha na bei za sokoni.
  4. Suala lingine ni la kodi ya mafuta ya ndege na airport fees. Hii ni kodi ambayo ingefutiliwa mbali au kupunguzwa sana kwani mchango wake kwenye budget ni mdogo sana, lakini inavifanya viwanja vyetu bado viwe vya ghali sana kutumia hasa ukitilia maanani pia udogo wa soko lake. Tukipunguza gharama zake tutaweza kuvutia hata mashirika mengine kutua hapo, na hivyo kuongeza connection na hapo hapo kuyapata hayo mapato ya hizo kodi tutakazoondoa kwenye matumizi mengine ya wasafiri. Biashara ni ujanja tu na kujua jinsi ya kupunguza gharama lakini hapo hapo kuongeza mapato.
  5. Pia ATC haitaweza kuwa na abiria wengi unless waanzishe safari za mbali, ulaya (kwenye hubs kubwa kama Hethrow, Charl. De Gaule n.k.) na zinazoibukia kama Dubai, India n.k. Hii itasaidia kuunganisha na abiria wa nchi jirani waweze kufanyia connection zao Dar. Ndege zao za Dash 8 na Boeing 737 wanaweza kuzitumia vizuri zaidi kukusanya wasafiri wa nchi kama Rwanda, Burundi, Congo, Zambia, Malawi n.k. na kuwaleta kwenye hub yao ya Dar kama wanavyofanya SAA, Kenya Airways na Ethiopian Airlines.
Haya mawazo yetu mengi ni obvious kwa watu waelewa wa hii biashara na sidhani kama hawanayo, lakini utekelezaji wao nafikiri ndio mbovu, hasa ukitilia maanani hawajibiki kwa yeyote kama shirika likienda mrama.
 
Hapo ndo shida ilipo, siasa na propoganda zinapotangulia utaalamu! Naamini utaalamu wa biashara ungethaminiwa hakukuwa na haja ya kukodi dege kubwa lenye mkataba wa kirichmond wakati abiria wenyewe wa kulitumia hilo dege ili lilete tija hawapo!

Nadhani adui yetu mkubwa mwingine wa maendeleo ya Tanzania ni upungufu wa utaalamu katika 'decision makers team'! sorry to say it but ndo ukweli

..utaalamu upo,tatizo ni waamuzi hawasikilizi vya kutosha ushauri wa wataalamu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom