Askofu wa Geita ni adui wa Tanganyika.

Nawashukuru mno wote waliochangia uzi wangu mpaka hapa, nadhani pana wawili ama watatu hivi wamenielewa. Mie ni RC na si mwandishi wa habari lakini nilichokusudia ni kutokubali upotoshaji wa historia kwa hoja dhaifu.
Labda niseme hivi:-
1. Tareha 9 December, 1961 ni Tanganyika ndio iliyopata UHURU na si Tanzania wala Tanzania bara.
2. Tanzania ni jina lililobuniwa la muungano wa nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar, hivo bila mojawapo ya nchi hizo huwezi kuwa na Tanzania.
3. Tanganyika ni jina la Kiafrika kama Uganda na Kenya tokea ukoloni, nchi nyingine wakati wa ukoloni zilikuwa na majina ya kikoloni zaidi kama Belgian Congo sasa DRC, Northern Rodhesia sasa Zambia, Portuguese East africa sasa Mozambique nakadhalika lakini pindi zilipokuwa zikipata uhuru zilibadilishwa kupata majina ya Kiafrika.
Mie simpingi baba Askofu kwa kuichukia Tanganyika ila nilisema hoja hizo alizotoa ni dhaifu mno (kipuuzi) hata hiyo ya majina ya watu nayo haina mashiko. Mtoto azaliwapo hupewa jina la asili (ukoo au uji) na wakatoliki wanapobatiza watoto jina la asili (uji) huliweka katika cheti cha ubatizo na ndio maana wengine wakiishapata elimu ya kutosha huamua kutanguliza majina yao ya asili kama Tundu Lisu, Mwesiga Baregu, Jenerali Ulimwengu, Zito Kabwe, Jakaya Mrisho na kadhalika.
Nawaomba radhi kwa wale waliokwazika na jambo hilo ila nawapongeza mno walionielewa.
Heri ya mwaka mpya.
 
Umekosea sana kumtukana mtumishi wa Mungu,hata kama una mawazo tofauti yatoe bila kutukana -------- sana wewe.

You are right ila ulitaka asemeje? Hawa vijana wetu product ya shule za kata hawawezi kabisa kujenga hoja independent of fallacies. Ukishaondoa parts zenye personal attack kitaalam-ad hominem, hawana kingine cha kusema, assuming unafanya tathmini ya argument zao.
 
huhitaji kua na akili au shule ili uwe askofu.
Angalia Kakobe. Gwanyuma. Upako. Yule mzinzi Mwingira. Rwakatare wote hawa hakuna anaejua mlango wa chuo cha biblia lakini ni maaskofu. hata wewe ukitaka unaupata

Ni kweli kwa baadhi ya madhehebu
Lakini kwa RC huwezi hata kuwa katekista bila kupitia mafunzo ya ukatekista
 
Kumbuka huu ni uwanja mpana sana ambapo safari moja uanzisha nyingine,usije ukadhani kinachojadiliwa hapa ni moja tu kama unavyotaka wewe!!

Na pengine njia moja wapo ya kuachana na upotoshaji wa mleta mada ni hii ya kujadili jambo ambalo ni real ama nyeti kama people wataona inafaa!

Sio lazima alicholeta mtoa mada ndio lijadiliwe na kama unaona ni upotoshaji achana nayo njoo sasa kwenye ukweli huu

Ninaposema ni 'Dikteta'

Namaanisha kwamba,kwanza tangu awe askofu kwenye jimbo hilo mara nyingi sana amekuwa akitoa matamshi ya kupingana na maelekezo ya serikali!

Kwa mfano anazungumzi suala a elimu,tangu awe askofu hakuna mchango wowote ambao kanisa umetoa katika kusaidia elimu hiyo ama afya kama anavyosema!

Amefisha hata kituo chs kulelea watoto wasiojiweza chs moyo wa huruma ambacho kikiachwa kikiwa katika hali nzuri na marehemu Balina!

Ni mtu ambaye kila siku kazi yake ni kuiponda serikali lakini hakuna alichokifsnya!

Ni mtu ambae anawakumbatia mapadri wake,hata pale waumini wanapompelekea malalamiko juu ya ndoa zao kuvunjwa na Mapadri wake!

Yeye na huyo aliyekuwa katibu wake ni watuhumiwa wakubwa juu ya uzinzi!,nenda pale anapoishi angalia mazingira ya pale halafu jaribu kuzungumza na wale masista wanaomfulia,wanaompikia,na kumtandikia mahali pa kulala usikie!!

Kuna wakati walifikia hatua ya kichapana makonde mpaka ikabidi afanye uhamisho!

Mkuu hebu acha utafanya tuzungumze mengi sana!

Kuna padri huyo aliyekuww katibu wake ni mchezaji wa mpira amewahi kuvu ja ndoa ya mchezaji mwenzake ambaye alikataa kuendelea kucheza nae kwenye timu moja!

Masista ndo ufanya kazi ya kumpikia? Kimfulia? Kumtandikia kitanda? Naona hujui unachoandika unaendeshwa kwa hisia.
Kazi ya sista ni kuhudumia kanisa na kimuhudumia padre sehemu ya misa na mahitaji ya kiibada ikiwemo mavazi ya ibada sio kwenye maisha binafsi.
 
Kwanza naomba kudeclare conflicts of Interest:
Mimi ni mkatoliki mlei...Mwaka 2000 wakati Damian Dallu anachaguliwa na Pope John Paul II mimi nilihudhuria misa ya kumpongeza pale parokiani Ifunda Kigango cha Kiponzero paroko akiwa Marehemu Pd.Mwamwilawa.
Nimeisikiliza misa yooote,iliyorushwa na TBC na TUMAINI toka Parokia ya Bikira Maria-Jimbo la Geita.
Baba Askofu Dallu ameongea mengi sana mazuri,amesisitiza juu ya umoja,amani na upendo,amesisitiza kuwa mali na tamaa ya utajili ni chanzo cha kupotea kwa amani ya nchi,uroho wa madaraka na ubinafsi ni chanzo cha migogoro,wakati wengine wanazungumzia kuungana kuna watanzania wengine wanataka tutengane,ilipopatikana gas kuna waliotumia rasilimali hiyo ili kujenga utengano ili sisi kama Taifa tutengane,walipogundua sehemu moja ya Muungano ina mafuta,wapo wanaopandikiza chuki tutengane.
Akasema sisi sote ni Watanzania,hata kama kabla ya hapo palikuwa na Tanganyika na Zanzibar,hakuna ajabu ya sisi kuhisahau Tanganyika na kujivunia Utanzania...akasema hata sisi Wakristo kabla ya ubatizo huwa tuna majina ya asili,lkn baada ya kuzaliwa upya kwa njia ya ubatizo basi hata majina huwa mapya,nchi nyingi kabla ya uhuru hazikuwa na majina ya sasa, mfano Z'bwe,Malawi,Zambia,Ghana na Benin...akasema ukitazama kwa undani wanaotaka kututenganisha ni sbb ya mali na madaraka,hata kama watu watataka kututenga lkn sisi ni wamoja,si umoja uliowekwa kikatiba bali kimwili na kiroho,tuna undugu ambao ni zaidi ya ule wa kikatiba.
Akakemea wanaopandikiza chuki za kidini na ukabila,wanaochoma nyumba za ibada,akasema hawa wote ni sbb ya maisha magumu na kukosa kazi,kukiwa na mfumo wa kumuweka kila mtu busy na kazi,hakuna atakayewaza kuchoma nyumba ya ibada ya mwenzake.Kazi ni kipimo cha utu.
Amewasisitiza wananchi wa Geita kujijengea uwezo wa kujitegemea,wajenge shule na huduma za afya ktk mkoa wao mpya mana huduma za mwanzo kama Shule na hospital kubwa hazipo tena ndani ya mkoa wa Sengerema,wasiishie kulalamika,bali wapeleke watoto wao shule na kuwatoa maporini kuchunga.
Askofu Dallu pia amesisitiza juu viongozi kuepuka na ufisadi,amewaasa waumini kuchukuliana kwa upendo,wayaishi maisha ya upendo miongoni mwao bila kujali tofauti zao za kiimani wala kiitikadi.Mwisho akasisitiza kazi na sala...kwa kusema ”Ora et Labora“....!!!!
Sijaona mahali alipoongea ”upuuzi“ kama mleta mada alivyosema,hajaonyesha ”udictator“,zaidi ya kuongea kwa Commanding spiritual Tone,ambayo ndiyo lugha ya kibaba na kiungozi...zaidi ni majungu tuuuuu ya mleta mada.
Mkuu, hapo (bolded) panatosha kuelewa upo upande gani, kumbuka mauaji ya Rwanda yalivokuwa kwa kanisa kutochukua maamuzi. Yawezekana baba Askofu huyu ni bosi wako na yawezekana katika kutafuta ujiko (cheo) utamuonesha huu uzi na jinsi ulivomtetea ili upate kitu hapo, kwangu mimi huyu ni kiongozi tu wa kiroho sitegemei kitu chochote toka kwake ila neno la Mungu tu tena kama hivi TBC ilivowatembelea wana wa Geita.
 
Heri ya Krismas, naangalia misa kupitia TBC na katika mahubiri yake Askofu huyu wa Geita kajipambanua kabisa kuhusu kuichukia Tanganyika na sababu anazozitoa ni za kipuuzi kabisa. Kumbe kuwa kiongozi wa kidini sio kujua yote na anavoonekani ni 'dictator' huyu kwa kuwalazimisha watu waikatae historia ya nchi yetu. Majanga mno.

1. Askofu wa Geita ndio nini?
2. Ameongea nini cha kipuuzi?
3. Je, mojawapo ya masharti ya kuwa kiongozi wa dini ni kuung mkono Tanganyika?
4. Je, kuunga mkono hoja ya Tanganyika ni usomi?
5. Je, kina prof. Issa Shivji wanaopinga Tanganyika tuwatambuaje?
6. Kati ya wewe na "askofu wa Geita" nani anayelazimisha mawazo yake?
 
Pamoja na maoni yote yaliyotolewa lkn kwa nn tunaingiza siasa kwenye nyumba za dini? hv vitu haviendani kabisa,watumishi wa mungu wache kuchanganya dini na siasa.
 
Kama ndio msimamo wa Maaskofu na Wachungaji kuwa Tanganyika izimwe basi serikali ya Tanganyika haitafufuka.

Plan B:
Ni kuwa provocate Wa-Pwani wadai kuwe na Tanzania Pwani, pia yaani tuwe na Tanzania Bara na Tanzania Pwani.

Kwa namna hii tutawaweka kwenye kona ya aidha wawashikilie Maaskofu na Taifa liendelee kugawanyika au wairudishe Tanganyika.

Wazee wa "mfumo kristo"
 
Quran 40: 60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike.

Mungu wa Waislam ajulikanaye kwa Jina la Allah amesema kiuwazi kabisa kuwa "wale wote ambao wanajivunia Uislam na kumuabudu Allah wataingia Motoni"
 
Sasa wewe kwa akili yako kila mtu kaangalia hiyo TBC???!!! Si ungesema basi hicho alichosema ili na sisi ambao hatukuangalia tujue nini kinaendelea. Unakuja hapa jazba kibao na maneno yasiyofaa halafu ndio unataka tukuone wewe wa maana sana??!!

Unaposti kitu tumia akili.
 
Quran 40: 60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike.

Mungu wa Waislam ajulikanaye kwa Jina la Allah amesema kiuwazi kabisa kuwa “wale wote ambao wanajivunia Uislam na kumuabudu Allah wataingia Motoni”
Kweli wewe ni kichwa! maana yake tafsiri haingii akilini kabisa katika mizani ya Uislamu.

Na mtu kama wewe hastahiki kuwa pengine popote zaidi ya kwenye Uislamu -May Allah guide you to Islam.

Baada ya kuyasema hayo:

Kiarabu aya ya yenyewe iko hivi:
إن الذين يستكبرون عن عبادتي

Hakika wale ambao wanafanya kibri katika kuniabudu mimi.
Mfasiri kibri ametafsiri kujivuna halafu aidha kosa la mwandishi au mchapishaji ametumia NA badala ya KWA, kitu ambacho wenye uelewa finyu wataelewa vingine kabisa.

Tofauti ya NA na KWA inabadilisha maana yote ya Aya!

Kivyovyote vile kama ningekuwa na uwezo nigewasiliana na wanafunzi wa Mfasiri waishereheshe Aya ili isieleweke vibaya.

Angalia Dr.Muhammad Muhsin Khan anavyoitafsiri kwa sherh katika lugha ya Kiingereza:
40:60. And your Lord said: "Invoke Me, [i.e. believe in My Oneness (Islamic Monotheism)] (and ask Me for anything) I will respond to your (invocation). Verily! Those who scorn My worship [i.e. do not invoke Me, and do not believe in My Oneness, (Islamic Monotheism)] they will surely enter Hell in humiliation!"
 
Ni kweli unachokisema mkuu umemsikiliza kwa makininsana,lakini unajua yanayoendelea kwenye jimbo la Geita chini ya Askofu Damian Dallu?!

Umesoma maelezo yangu hapo juu?!

Tafadhali naomba zungumzia na comment yangu hapo juu nitafurahi.

Halafu sengerema sio mkoa ni wilaya iliyoko ndani ya mkoa wa mwanza ambayo inapakana na Mkoa wa Geita!
Mkuu, huyu jamaa kweli alimsikiliza na kurekodi hotuba yake lakini ana upungufu wa kufikiri kwa maana kila aambiwacho huchukulia hivo hivo. Mfano baba Askofu kasema kuwa mtoto azaliwapo hupewa jina (la asili) lakini akibatizwa (kikristu) basi linakufa sasa mbona tuna akina Mwigulu, Zito, Jakaya, Jenerali, Senkondo na wengine wengi tu ambao wanaona kuwa ni utumwa kuacha asili yako. Angalia Wahindi wamebadilisha hata jina la mji wao maarufu wa Bombay na kuuita Mumbai ila hawa jamaa zetu wanaona fahari kubaki na Dar es Salaam na kupinga jina asili la nchi yetu. Kwanza bila Tanganyika hiyo Tanzania wangeipata wapi?
 
Sasa wewe kwa akili yako kila mtu kaangalia hiyo TBC???!!! Si ungesema basi hicho alichosema ili na sisi ambao hatukuangalia tujue nini kinaendelea. Unakuja hapa jazba kibao na maneno yasiyofaa halafu ndio unataka tukuone wewe wa maana sana??!!

Unaposti kitu tumia akili.
Sawa mkuu, lakini kwa matukio makubwa kama haya ni vizuri kufuatilia, pia pana msamalia mwema humu alirekodi hiyo hotuba yake hebu jaribu kuipitia hapo juu kuhusiana na katiba na si mambo mengine kwani huko niliishasema yupo sahihi kabisa.
Kwa kuwa mie si mwandishi wa habari hivo inaniwia vigumu kunakiri matukio mkuu.
 
Tanzania haijawahi kutawaliwa zilizotawaliwa ni Tanganyika na Zanzibar.
Kweli kabisa mkuu, lazima tuupinge kwa nguvu zote upotoshaji wa historia ya nchi yetu. Nafurahi kwa Zanzibar sasa vijana wanaelewa hili na katika sherehe hii ya miaka 50 kweli wameamka.
 
1. Askofu wa Geita ndio nini?
2. Ameongea nini cha kipuuzi?
3. Je, mojawapo ya masharti ya kuwa kiongozi wa dini ni kuung mkono Tanganyika?
4. Je, kuunga mkono hoja ya Tanganyika ni usomi?
5. Je, kina prof. Issa Shivji wanaopinga Tanganyika tuwatambuaje?
6. Kati ya wewe na "askofu wa Geita" nani anayelazimisha mawazo yake?
Mheshimiwa, kifupi kabisa mie simpingi yeye kuikataa Tanganyika ila sababu alizotoa ni nyepesi na potofu mno ndio maana nimetumia za kipuuzi. Kama ungebahatika kumsikiliza sio kusoma kilichowekwa humu tayari nadhani ungekereka kwa msomi kama yeye kuwa vile. Samahani kama nimekukera ila pana watu ambao hutukubali kuburuzwa hivi hivi na wanasiasa au dini.
 
Pamoja na maoni yote yaliyotolewa lkn kwa nn tunaingiza siasa kwenye nyumba za dini? hv vitu haviendani kabisa,watumishi wa mungu wache kuchanganya dini na siasa.
Kweli kabisa mkuu, tena kushawishi maoni yake kwa waamini ni hatari sana. Pana baadhi ya viongozi wengine wa dini katika jambo hili la katiba wamesema vizuri mno. Tume imetayarisha katiba kutokana na maoni ya wananchi wengi ya kutaka serikali tatu na sasa inapelekwa kwenye bunge maalum la katiba, iweje huyu baba Askofu aturejeshe nyuma tena kwa ushawishi kuikataa Tanganyika?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom