Askofu wa Geita ni adui wa Tanganyika.

Kama ndio msimamo wa Maaskofu na Wachungaji kuwa Tanganyika izimwe basi serikali ya Tanganyika haitafufuka.

Plan B:
Ni kuwa provocate Wa-Pwani wadai kuwe na Tanzania Pwani, pia yaani tuwe na Tanzania Bara na Tanzania Pwani.

Kwa namna hii tutawaweka kwenye kona ya aidha wawashikilie Maaskofu na Taifa liendelee kugawanyika au wairudishe Tanganyika.
Ndio hapo tunapoona kakosea kutumia madhahabuni kutoa hoja ya kuizima Tanganyika maana wengi tunaamini mtoa hoja huwa ama anamwakilisha Mungu au msimamo wa kanisa/msikiti. Mengi yanayohusu jamii kazungumza vizuri ila hili la katiba ndipo alipovurunda labda katumwa!
 
mtoa mada ni mfinyu wa mawazo halafu hajui hata kutoa hoja ya kujadili, hajafafanua kiundani issue akifikiri kila mtu yupo home anaangalia tbc. sisi wengine hatupo home, hatujaona hiyo tbc, tulikuwa tunatarajia wewe ulete story yote from A to Z alichokisema, ili katika kujadili tuone kama tutamsapoti yeye au tutakusapoti wewe. sasa unakuja tu kutaja Tanganyia, sijui askofu, hata hatujui kilichotokea, tatizo umekuja kwa kukurupuka kama umefumaniwa.
 
Heri ya Krismas, naangalia misa kupitia TBC na katika mahubiri yake Askofu huyu wa Geita kajipambanua kabisa kuhusu kuichukia Tanganyika na sababu anazozitoa ni za kipuuzi kabisa. Kumbe kuwa kiongozi wa kidini sio kujua yote na anavoonekani ni 'dictator' huyu kwa kuwalazimisha watu waikatae historia ya nchi yetu. Majanga mno.

sio kila anachoongea mtumishi wa nyumba ya ibada kina mkono wa mungu, lazima ujue kutofautisha nenola MUNGU na maoni binafsi ya mtumishi wa nyumba ya MUNGU.

HAY0M NI MAONI YAKE NA YATABAKI KUWA MAONI YAKE SIO MAAGIZO YA KANISA WALA MUNGU.

HAUNA SABABU YA KUTUMIA LUGHA ISIYO NA STAHA KUKABILIANA NA MAONI HURU YA MTU, YAPINGE KWA HOJA BILA JAZBA UTAELEWEKA
 
Sawa mkuu nadhani maoni yako hata yeye yamemlenga. Aksante kwa hilo.
 
mtoa mada ni mfinyu wa mawazo halafu hajui hata kutoa hoja ya kujadili, hajafafanua kiundani issue akifikiri kila mtu yupo home anaangalia tbc. sisi wengine hatupo home, hatujaona hiyo tbc, tulikuwa tunatarajia wewe ulete story yote from A to Z alichokisema, ili katika kujadili tuone kama tutamsapoti yeye au tutakusapoti wewe. sasa unakuja tu kutaja Tanganyia, sijui askofu, hata hatujui kilichotokea, tatizo umekuja kwa kukurupuka kama umefumaniwa.
Nilichogundua mpaka sasa takriban wote waliochangia thread hii hawajaangalia/kufuatilia ibada hiyo ya misa (hilo ndilo kosa langu,ila kama ningemzungumzia mwanasiasa ningeeleweka) lakini mwenye upeo wa kuelewa atakuwa keshaelewa nilichokuwa namaanisha. Tena ni bahati mbaya mno kwa wengine kusema eti nimemtusi Askofu. Pana mmoja kaelewa nilichokuwa namaanisha humu.
 
Wewe chokora toa upuuzi wako humu, Askofu awe mpuuzi au wewe ndiyo Ovyooo. Kundadadeki.
Punguza jazba mzee, sijasema Askofu ni mpuuzi ila mifano aliyoitoa ni ya kipuuzi. Yeye ni binabamu tu kama wewe hivo hawezi kuwa sahihi kwa kila jambo. Huo uaskofu kasomea tu kama Askofu wengine na hakuteuliwa na Mungu ndugu.
 
askofu kasisitiza watu kuwa wamoja wasikubali kutenganishwa na mali tulizonazo , wanasiasa wala dini akasema hata zanzibar na tanganyika zikiachana bado sisi tutaitwa watanzania tu ..... amesisitiza umoja we unasema mambo ya kipuuzi ... huyo ndio ASKOF Damiani Dallu mtaalam wa sheria za kanisa CANON LAWS
 
Punguza jazba mzee, sijasema Askofu ni mpuuzi ila mifano aliyoitoa ni ya kipuuzi. Yeye ni binabamu tu kama wewe hivo hawezi kuwa sahihi kwa kila jambo. Huo uaskofu kasomea tu kama Askofu wengine na hakuteuliwa na Mungu ndugu.

Huyu ni miongoni mwa maaskofu ambao ni Madikteta sana katika kanisa la RC hapa nchini,na uaskofu wake kaanzia hapo hapo Geita alisimikwa wakati wa uongozi wa Mkapa,alilala chini hapo hapo kwenye hilo kanisa wakati ambapo lilikuwa halijakamilika.

Pia ni Askofu ambaye amekuwa akiwatetea sana mapadri wake ambao wanatuhumiwa kwa tuhuma mbalimbali hapo Geita!

Maaskofu wengi walioko hapo Geita wanatuhumiwa kuvunja ndoa za watu,kuoa na kuwajengea vimada nyumba pamoja na kuzaa nao,mmoja ambaye alikuwa ni katibu wake anadaiwa kuvunja ndoa ya mtu,na kutokana na kashfa kumzidi amempelekea nchini Italy kwa ajili ya kusoma na sasa kaacha mwanamke ana mimba na kamjengea nyumba hapo hapo Geita.

Kifupi huyo Askofu sijui sana lakini mhhhhhhhhhhhhhhh!!
 
Kwanza naomba kudeclare conflicts of Interest:
Mimi ni mkatoliki mlei...Mwaka 2000 wakati Damian Dallu anachaguliwa na Pope John Paul II mimi nilihudhuria misa ya kumpongeza pale parokiani Ifunda Kigango cha Kiponzero paroko akiwa Marehemu Pd.Mwamwilawa.
Nimeisikiliza misa yooote,iliyorushwa na TBC na TUMAINI toka Parokia ya Bikira Maria-Jimbo la Geita.
Baba Askofu Dallu ameongea mengi sana mazuri,amesisitiza juu ya umoja,amani na upendo,amesisitiza kuwa mali na tamaa ya utajili ni chanzo cha kupotea kwa amani ya nchi,uroho wa madaraka na ubinafsi ni chanzo cha migogoro,wakati wengine wanazungumzia kuungana kuna watanzania wengine wanataka tutengane,ilipopatikana gas kuna waliotumia rasilimali hiyo ili kujenga utengano ili sisi kama Taifa tutengane,walipogundua sehemu moja ya Muungano ina mafuta,wapo wanaopandikiza chuki tutengane.
Akasema sisi sote ni Watanzania,hata kama kabla ya hapo palikuwa na Tanganyika na Zanzibar,hakuna ajabu ya sisi kuhisahau Tanganyika na kujivunia Utanzania...akasema hata sisi Wakristo kabla ya ubatizo huwa tuna majina ya asili,lkn baada ya kuzaliwa upya kwa njia ya ubatizo basi hata majina huwa mapya,nchi nyingi kabla ya uhuru hazikuwa na majina ya sasa, mfano Z'bwe,Malawi,Zambia,Ghana na Benin...akasema ukitazama kwa undani wanaotaka kututenganisha ni sbb ya mali na madaraka,hata kama watu watataka kututenga lkn sisi ni wamoja,si umoja uliowekwa kikatiba bali kimwili na kiroho,tuna undugu ambao ni zaidi ya ule wa kikatiba.
Akakemea wanaopandikiza chuki za kidini na ukabila,wanaochoma nyumba za ibada,akasema hawa wote ni sbb ya maisha magumu na kukosa kazi,kukiwa na mfumo wa kumuweka kila mtu busy na kazi,hakuna atakayewaza kuchoma nyumba ya ibada ya mwenzake.Kazi ni kipimo cha utu.
Amewasisitiza wananchi wa Geita kujijengea uwezo wa kujitegemea,wajenge shule na huduma za afya ktk mkoa wao mpya mana huduma za mwanzo kama Shule na hospital kubwa hazipo tena ndani ya mkoa wa Sengerema,wasiishie kulalamika,bali wapeleke watoto wao shule na kuwatoa maporini kuchunga.
Askofu Dallu pia amesisitiza juu viongozi kuepuka na ufisadi,amewaasa waumini kuchukuliana kwa upendo,wayaishi maisha ya upendo miongoni mwao bila kujali tofauti zao za kiimani wala kiitikadi.Mwisho akasisitiza kazi na sala...kwa kusema ”Ora et Labora“....!!!!
Sijaona mahali alipoongea ”upuuzi“ kama mleta mada alivyosema,hajaonyesha ”udictator“,zaidi ya kuongea kwa Commanding spiritual Tone,ambayo ndiyo lugha ya kibaba na kiungozi...zaidi ni majungu tuuuuu ya mleta mada.
 
Ndio hapo tunapoona kakosea kutumia madhahabuni kutoa hoja ya kuizima Tanganyika maana wengi tunaamini mtoa hoja huwa ama anamwakilisha Mungu au msimamo wa kanisa/msikiti. Mengi yanayohusu jamii kazungumza vizuri ila hili la katiba ndipo alipovurunda labda katumwa!

Bahati mbaya unaandika kitu usichokijua,ndani ya kanisa katoliki ni mtu mmoja tu ndio hutoa msimamo wa kanisa..Baba Mtakatifu,Askofu wa Roma na Khalifa wa Mtume Petro,sio Pengo wala Balozi wa Baba Mtakatifu ktk ubinafsi wao.
Homilia aliyoitoa Mhashamu Askofu Dallu wala si msimamo wa kanisa,ni mahubiri yake..na si lazima uyachukue.
Kila kitu mnaweweseka na kuingiza Siasa.
This is a kind of a fallacy,its like Argumentum ad hominem,you attack yr opponent instead of discussing the content of the msg given..
 
Kwanza naomba kudeclare conflicts of Interest:
Mimi ni mkatoliki mlei...Mwaka 2000 wakati Damian Dallu anachaguliwa na Pope John Paul II mimi nilihudhuria misa ya kumpongeza pale parokiani Ifunda Kigango cha Kiponzero paroko akiwa Marehemu Pd.Mwamwilawa.
Nimeisikiliza misa yooote,iliyorushwa na TBC na TUMAINI toka Parokia ya Bikira Maria-Jimbo la Geita.
Baba Askofu Dallu ameongea mengi sana mazuri,amesisitiza juu ya umoja,amani na upendo,amesisitiza kuwa mali na tamaa ya utajili ni chanzo cha kupotea kwa amani ya nchi,uroho wa madaraka na ubinafsi ni chanzo cha migogoro,wakati wengine wanazungumzia kuungana kuna watanzania wengine wanataka tutengane,ilipopatikana gas kuna waliotumia rasilimali hiyo ili kujenga utengano ili sisi kama Taifa tutengane,walipogundua sehemu moja ya Muungano ina mafuta,wapo wanaopandikiza chuki tutengane.
Akasema sisi sote ni Watanzania,hata kama kabla ya hapo palikuwa na Tanganyika na Zanzibar,hakuna ajabu ya sisi kuhisahau Tanganyika na kujivunia Utanzania...akasema hata sisi Wakristo kabla ya ubatizo huwa tuna majina ya asili,lkn baada ya kuzaliwa upya kwa njia ya ubatizo basi hata majina huwa mapya,nchi nyingi kabla ya uhuru hazikuwa na majina ya sasa, mfano Z'bwe,Malawi,Zambia,Ghana na Benin...akasema ukitazama kwa undani wanaotaka kututenganisha ni sbb ya mali na madaraka,hata kama watu watataka kututenga lkn sisi ni wamoja,si umoja uliowekwa kikatiba bali kimwili na kiroho,tuna undugu ambao ni zaidi ya ule wa kikatiba.
Akakemea wanaopandikiza chuki za kidini na ukabila,wanaochoma nyumba za ibada,akasema hawa wote ni sbb ya maisha magumu na kukosa kazi,kukiwa na mfumo wa kumuweka kila mtu busy na kazi,hakuna atakayewaza kuchoma nyumba ya ibada ya mwenzake.Kazi ni kipimo cha utu.
Amewasisitiza wananchi wa Geita kujijengea uwezo wa kujitegemea,wajenge shule na huduma za afya ktk mkoa wao mpya mana huduma za mwanzo kama Shule na hospital kubwa hazipo tena ndani ya mkoa wa Sengerema,wasiishie kulalamika,bali wapeleke watoto wao shule na kuwatoa maporini kuchunga.
Askofu Dallu pia amesisitiza juu viongozi kuepuka na ufisadi,amewaasa waumini kuchukuliana kwa upendo,wayaishi maisha ya upendo miongoni mwao bila kujali tofauti zao za kiimani wala kiitikadi.Mwisho akasisitiza kazi na sala...kwa kusema ”Ora et Labora“....!!!!
Sijaona mahali alipoongea ”upuuzi“ kama mleta mada alivyosema,hajaonyesha ”udictator“,zaidi ya kuongea kwa Commanding spiritual Tone,ambayo ndiyo lugha ya kibaba na kiungozi...zaidi ni majungu tuuuuu ya mleta mada.

Ni kweli unachokisema mkuu umemsikiliza kwa makininsana,lakini unajua yanayoendelea kwenye jimbo la Geita chini ya Askofu Damian Dallu?!

Umesoma maelezo yangu hapo juu?!

Tafadhali naomba zungumzia na comment yangu hapo juu nitafurahi.

Halafu sengerema sio mkoa ni wilaya iliyoko ndani ya mkoa wa mwanza ambayo inapakana na Mkoa wa Geita!
 
Hapa tunajadili juu ya upotoshaji wa mtoa mada na homilia ya Mhashamu Askofu Dallu,wewe umeleta tuhuma mpya za ”udictator" wake na ”kashfa“ za Mapadre wake...Unafikiri hapa ktk uzi huu ni mahala pake??
Unaposema "dictator“ una maana gani??...kumuelezea kama ni askofu aliyepata uaskofu wakati wa Mkapa ni kumuweka “kiulimwengu“ zaidi badala ya kiroho,hakuwa responsible kwa Mkapa,bali kwa waumini wake na Papa,hivyo nikusahihishe kuwa alipata uaskofu wakati wa Papa Yohane Paulo wa Pili na si “wakati“ wa Mkapa.
Hapo kwenye mkoa nilikosea,nilitaka kumaanisha kuwa shule na huduma zimebaki Sengerema ambao ni mkoa wa Mwanza na Geita inabidi wajipange upya!!
 
Tudai serikali moja tu. Muungano uonekane kuwe na Tanzania (achana na Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar). Huu sasa ndio uwe msimamo wetu Watanganyika
 
Hapa tunajadili juu ya upotoshaji wa mtoa mada na homilia ya Mhashamu Askofu Dallu,wewe umeleta tuhuma mpya za ”udictator" wake na ”kashfa“ za Mapadre wake...Unafikiri hapa ktk uzi huu ni mahala pake??
Unaposema "dictator“ una maana gani??...kumuelezea kama ni askofu aliyepata uaskofu wakati wa Mkapa ni kumuweka “kiulimwengu“ zaidi badala ya kirohohakuwa responsible kwa Mkapa,bali kwa waumini wake na Papa,hivyo nikusahihishe kuwa alipata uaskofu wakati wa Papa Yohane Paulo wa Pili na si “wakati“ wa Mkapa.
Hapo kwenye mkoa nilikosea,nilitaka kumaanisha kuwa shule na huduma zimebaki Sengerema ambao ni mkoa wa Mwanza na Geita inabidi wajipange upya!!

Kumbuka huu ni uwanja mpana sana ambapo safari moja uanzisha nyingine,usije ukadhani kinachojadiliwa hapa ni moja tu kama unavyotaka wewe!!

Na pengine njia moja wapo ya kuachana na upotoshaji wa mleta mada ni hii ya kujadili jambo ambalo ni real ama nyeti kama people wataona inafaa!

Sio lazima alicholeta mtoa mada ndio lijadiliwe na kama unaona ni upotoshaji achana nayo njoo sasa kwenye ukweli huu

Ninaposema ni 'Dikteta'

Namaanisha kwamba,kwanza tangu awe askofu kwenye jimbo hilo mara nyingi sana amekuwa akitoa matamshi ya kupingana na maelekezo ya serikali!

Kwa mfano anazungumzi suala a elimu,tangu awe askofu hakuna mchango wowote ambao kanisa umetoa katika kusaidia elimu hiyo ama afya kama anavyosema!

Amefisha hata kituo chs kulelea watoto wasiojiweza chs moyo wa huruma ambacho kikiachwa kikiwa katika hali nzuri na marehemu Balina!

Ni mtu ambaye kila siku kazi yake ni kuiponda serikali lakini hakuna alichokifsnya!

Ni mtu ambae anawakumbatia mapadri wake,hata pale waumini wanapompelekea malalamiko juu ya ndoa zao kuvunjwa na Mapadri wake!

Yeye na huyo aliyekuwa katibu wake ni watuhumiwa wakubwa juu ya uzinzi!,nenda pale anapoishi angalia mazingira ya pale halafu jaribu kuzungumza na wale masista wanaomfulia,wanaompikia,na kumtandikia mahali pa kulala usikie!!

Kuna wakati walifikia hatua ya kichapana makonde mpaka ikabidi afanye uhamisho!

Mkuu hebu acha utafanya tuzungumze mengi sana!

Kuna padri huyo aliyekuww katibu wake ni mchezaji wa mpira amewahi kuvu ja ndoa ya mchezaji mwenzake ambaye alikataa kuendelea kucheza nae kwenye timu moja!
 
Mkuu, katika mifano yake ya kutetea Tanganyika isahaulike alitoa mifano finyu kama nchi za Malawi, Msumbiji, Zambia, Ghana na alituacha hoi kwa Ivory Coast. Inauma kwa msomi kama yeye kupotosha HISTORIA kwa kutumia cheo alichokuwa nacho. Mkuu ungesikiliza/angalia TBC ungetuelewa.

We ni kilaza unaandika vitu hata havieleweki
 
Dah wewe jamaa acha kupotosha watu hapa, mimi mwenyewe nimeangalia hiyo ibada Live TBC, mantiki kubwa aliyokuwa ana maanisha ni umoja wetu kama watanzania, watu wasianze kudai Zanzibar au Taganyika yao sababu ya rasilimali mpya zilizogundulika nchini(mafuta, gas etc), matukio/michakato kama ya katiba mpya isiwafanye watu wakaiua Tanzania yao ambayo majority ya vijana wa leo waliukuta.
Hivyo alimaliza kwa kusema kamwe Tanzania haitatoka kwenye akili za watu kutokana na chokochoko zinazoletwa na wachache kwa maslahi yao fulani!!
 
Heri ya Krismas, naangalia misa kupitia TBC na katika mahubiri yake Askofu huyu wa Geita kajipambanua kabisa kuhusu kuichukia Tanganyika na sababu anazozitoa ni za kipuuzi kabisa. Kumbe kuwa kiongozi wa kidini sio kujua yote na anavoonekani ni 'dictator' huyu kwa kuwalazimisha watu waikatae historia ya nchi yetu. Majanga mno.

huhitaji kua na akili au shule ili uwe askofu.
Angalia Kakobe. Gwanyuma. Upako. Yule mzinzi Mwingira. Rwakatare wote hawa hakuna anaejua mlango wa chuo cha biblia lakini ni maaskofu. hata wewe ukitaka unaupata
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom