Askofu wa Geita ni adui wa Tanganyika.

Mkuu, katika mifano yake ya kutetea Tanganyika isahaulike alitoa mifano finyu kama nchi za Malawi, Msumbiji, Zambia, Ghana na alituacha hoi kwa Ivory Coast. Inauma kwa msomi kama yeye kupotosha HISTORIA kwa kutumia cheo alichokuwa nacho. Mkuu ungesikiliza/angalia TBC ungetuelewa.

Hamjaeleza kile ambacho mnakiona kibaya mmebaki kulaumu huku wenyewe hamwezi kujieleza, leta hoja yake nawe weka yako tuzipime si unaleta hisia badala ya hoja mkuu
 
Mimi si mpuuzi, lakini naipinga Tanganyika. Naipinga kwa sababu ujio wake utaiua Tanzania. Sote hatuwezi kuwa na mawazo 'uniform'. Kupingana ni jambo la maana alimradi tu huko kupinga kuwe na mantiki.
 
Sawa mkuu, lakini kwa matukio makubwa kama haya ni vizuri kufuatilia, pia pana msamalia mwema humu alirekodi hiyo hotuba yake hebu jaribu kuipitia hapo juu kuhusiana na katiba na si mambo mengine kwani huko niliishasema yupo sahihi kabisa.
Kwa kuwa mie si mwandishi wa habari hivo inaniwia vigumu kunakiri matukio mkuu.

Mkuu kumbuka sio kila aliyeko humu yuko bongo. Wengine kwa maeneo waliyopo hawana access na TBC.
 
Heri ya Krismas, naangalia misa kupitia TBC na katika mahubiri yake Askofu huyu wa Geita kajipambanua kabisa kuhusu kuichukia Tanganyika na sababu anazozitoa ni za kipuuzi kabisa. Kumbe kuwa kiongozi wa kidini sio kujua yote na anavoonekani ni 'dictator' huyu kwa kuwalazimisha watu waikatae historia ya nchi yetu. Majanga mno.

Cc mzito pande za nyuma Mzito Kabwela Nicholas 2013 Nyenyere H1N1
Teh teh teh teh!
Mi napita tu! Wacha waje wanakondoo wamtetee mtumishi wao!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kumbuka sio kila aliyeko humu yuko bongo. Wengine kwa maeneo waliyopo hawana access na TBC.
Nakubaliana nawe mkuu, lakini wengine hawana ustaarab. Kama jambo hulijui si lazima kuandika humu, wakati mwingine kukaa kimya ni busara zaidi.
 
Mimi si mpuuzi, lakini naipinga Tanganyika. Naipinga kwa sababu ujio wake utaiua Tanzania. Sote hatuwezi kuwa na mawazo 'uniform'. Kupingana ni jambo la maana alimradi tu huko kupinga kuwe na mantiki.
Mkuu, hivi kwa nini uwepo wa Tanganyika tu ndio inafikiriwa kuua Tanzania? Mbona uwepo wa Zanzaibar bado Tanzania inadunda? Sidhani hii ni hoja convincing, hebu fuatilia shamrashamra za miaka 50 ya Mapinduzi matukufu uone.
 
Hamjaeleza kile ambacho mnakiona kibaya mmebaki kulaumu huku wenyewe hamwezi kujieleza, leta hoja yake nawe weka yako tuzipime si unaleta hisia badala ya hoja mkuu
Mkuu, nimeishaeleza kuwa mifano aliyoitoa ya ubadilishaji majina ya nchi na binadamu kwa kuhalalisha ufaji wa Tanganyika ni mfu. Mie si msukuma labda ningesema kiswahili sikifahamu uzuri kwani baba Askofu alikuwa akiongea kwa kiswahili tena fasaha. Na elewa kuwa sikusema baba Askofu ni mpuuzi ila sababu za kuikana Tanganyika tu ndio nilisema za kipuuzi. Mambo mengine yanayohusu jamii alisema vizuri kabisa hasa katika kudumisha amani.
 
Cc mzito pande za nyuma Mzito Kabwela Nicholas 2013 Nyenyere H1N1
Teh teh teh teh!
Mi napita tu! Wacha waje wanakondoo wamtetee mtumishi wao!

angalia na wewe unavyomsifia jacobus, utadhani amenukuu kifungu cha kwenye bibilia...

jacobus hatambui uhuru wa mawazo, anaweza kuwa dikteta kuliko askofu wake. nahisi yeye jacobus anaitaka tanganyika huru ili kuachana na wamwaga tindikali, anatakiwa ajue pia kule kisiwani kuna makanisa ambayo bado hayajachomwa moto, pia na waumini ambao bado hawajamwagiwa tindikali. hivyo ni rahisi kutabiri kitakachotokea iwapo muungano utavunjika na raia wa bara wakiwa wanaishi kule wamejenga kule wana mahoteli kule.

akatetee hoja zake kwenye mchakato wa kuunda katiba mpya. amwachie kaisari yalioyake kaisari .....na ya mungu vilevile, huu ni muda wa kumcha mungu.
 
Mkuu, aksante kwa kunichekesha. Mie si dikteta ila nilikuwa au namkosoa baba Askofu kwa hoja zake finyu mno za kuikataa Tanganyika kama msomi mzuri tu na kuwalazimisha waamini wake pale kanisani na dunia nzima kupitia TBC kumfuata kwa kutumia cheo chake cha uaskofu. Kiujumla hoja za kuikataa Tanganyika mpaka sasa ni dhaifu mno kama si kutumia nguvu ambazo zitapelekea kuuvunja muungano na kumbuka Zanzibar yote kwa ujumla ni watu toka Tanganyika kwa asilimia kubwa tu.
 
Mkuu, hapo (bolded) panatosha kuelewa upo upande gani, kumbuka mauaji ya Rwanda yalivokuwa kwa kanisa kutochukua maamuzi. Yawezekana baba Askofu huyu ni bosi wako na yawezekana katika kutafuta ujiko (cheo) utamuonesha huu uzi na jinsi ulivomtetea ili upate kitu hapo, kwangu mimi huyu ni kiongozi tu wa kiroho sitegemei kitu chochote toka kwake ila neno la Mungu tu tena kama hivi TBC ilivowatembelea wana wa Geita.

Jacobus,,,nshaelewa tatizo lako...hutaki kurekebishwa na unataka kila mtu aamini mawazo yako....from what i see ni kwamba hukumuelewa uyo Askofu and ujue ni nadra askofu wa RC kuongea pumba coz wapo makini with what they say na wakikosea tu wana shughulikiwa directly au indirectly mfano koda,kilaini nk kubali tu hukumuelewa and ukakurupuka next time tek ur time
 
Mkuu, pamoja na kunihukumu kuwa si 'muelewa' lakini weye nimekuelewa mno ila 'kuburuzwa' ndio sikubaliani asilani. Sitaki kuwa mfalme aliyeshonewa vazi la ajabu na kuaminishwa kulivaa wakati kumbe yu uchi wa nyama.
 
Mimi si mpuuzi, lakini naipinga Tanganyika. Naipinga kwa sababu ujio wake utaiua Tanzania. Sote hatuwezi kuwa na mawazo 'uniform'. Kupingana ni jambo la maana alimradi tu huko kupinga kuwe na mantiki.

Kwa maandishi yako ni kwamba huna hoja ya msingi ya kupinga kurudishwa kwa Tanganyika bali wewe unayo mahaba na jina Tanzania!!
 
Hahahaa, naona umeanza vizuri na wewe ukamalizia kwa kutukana, kwa hiyo na wewe ni walewale!
Mkuu, ni sawa na kumwambia mtoto wako 'mbwa wee.................' wakati mzazi ni wewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom