Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,086
- 6,568
Watanzania wanahitaji katiba mpya maana wanajua fika mwarobaini wa matatizo yao.
Katiba mpya ndio itayokata mzizi wa fitina wa kila shida inayowakabili Watanzania.
Mfano tunataka Katiba ambayo itaruhusu kila mtanzania kuwa na mamlaka ya kusimamia haki za binadamu wenzake,mathalani mtu akiuliwa na vyombo vya dola katiri visivyojali haki za binadamu, ndugu au jamaa za marehemu wawe na uwezo kufungua kesi na kushitaki sio mpaka Jamhuri ifungue kesi.
Tunataka Katiba itayolinda uhuru wa raia wa Tanzania. Raia wawe huru, sio kuwa wanakamatwa hovyo na vyombo vya dola bila sababu. Sio kuwa wanateswa na kuumizwa kisa tu ni watuhumiwa. Tunataka katiba ambayo itamfanya kila mtanzania aache uharifu. Kama ni mharifu apewe adhabu kwa mujibu wa sheria za nchi.
Kwa muktadha huu sioni sababu ya kufanya unafiki na kumuita Askofu Mwamakula muhuni wakati anapambana watanzania kupata katiba itayowasaidia.
Ni wapi aliwahamasisha watanzania kuleta vurugu wakati wanaandamana? Alihamasisha watu wabebe siraha?