Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Wakuu Mimi nakwenda Mbali zaidi, katika kuyajadili maneno ya huyu anayejiita Askofu Gwajima aliyoyatoa jana tar 08.09 katika ukumbi wa Landmark Hotel, kama majibu kwa Dr. Slaa kufuatia Dr. Slaa kumwita yeye (Gwajima} mshenga wa kukaribishwa kwa Mh. Edward Lowasa ndani ya CHEDEMA.

Ndugu zangu maneno ya Askofu Gwajima si tu yanashusha tu credibility ya Ukawa Ila Gwajima hanashusha hata credibility ya Maaskofu wenzake.

Gwajima anavyosema mambo ambayo yalikuwa siri kati yake na mtumishi wake wa dini Dr. Slaa ama Bi Mashumbushi, anadharirisha uaskofu wake, kwasababu kama baba wa kiroho unaanza kuropoka mambo ya siri ya kondoo zako, hivi ni nani? Leo mwenye akili timamu ataweza kukufuata na kukuambia jambo lake la siri.

Gwajima amejisifu kuwa yeye anakakitu kakurecordia, hivyo maongezi yote anayoyafanya huya-record yaani ni mtaalamu wa kurecord, sasa embu, Jiulize, muumini wake yupi Leo, mwenye akili timamu, atakaye weza kumfuata Askofu Huyu na kumweleza mambo yake ya siri ya kiroho yanayoitaji msaada wa kiroho, kama mtumishi huyu amekuwa mropokaji kwa kiwango hichi.

Mimi ni mkatoliki sisi kwetu tunakitu tunaita sacrament ya kitubio, Ambapo Mlei umfuata Padri nakukiri dhambi zake\kuungama Dhambi/Maungamo, hapo kwenye Maungamo mnakuwa na padri tu, na unamueleza dhambi ulizozitenda, kisha padri utamka maneno Fulani kisha dhambi zile kwa imani yetu tunaamini huondoka, sasa kinachofanyika pale huwa ni siri yako wewe unayetubu Padri, na Mungu wenu pekee,

Katika mazingira hayo watu uungama na kutaja dhambi mabalimblali, wengine unakuta alishawahi kuua na kuiba, unamkuta mtu anataja kuwa alishawahi kuzini na Mke Wa katekista pengine, sasa japo huyu padri anamjua Mke Wa katekista na katekista mwenyewe kama msaidizi wake ila hawezi kumfuata na kumwambia lolote Yale yanabaki kuwa siri na kwavile ni maungamo tunaamini yanakuwa yamekwisha lakini haimaanishi Bw. Huyo Mlei ameacha ama kukoma kutenda dhambi.

Huo ni mfano tu wa padri wa kanisa katoliki, haya sasa mfananishe huyu Gwajima kama angelikuwa Padri, si angekuja Jana kutuambia yote Ambayo Mama Mashumbushi. Mke Wa Dr Slaa aliyatubu kwake? Hakika huu ni mfano wa Upuuzi wa kiwango cha PHD.

Lakini mbali na hapo Gwajima ni Muhuni, kwasababu yeye mwenyewe alishawahi kumtolea maneno ya kashfa sana Kiongozi wangu Wa kanisa, Aliyenipa Kipaimara, Askofu Polycop Kardinali Pengo alimwita majina ya hovyoovyo na ni wazi kabisa kuwa yalikuwa matusi. Embu sasa tazama mambo yake Alafu Leo mtu yule yule Muhuni aliyemtukana kiongozi Mkuu wa kanisa katoliki nchini, anarudi kwetu kuwakemea watu wengine tena walei wake mwenyewe wanapowatukana Maaskofu. Kwani si yeye aliyewafunza?

Pengine Dr. Slaa alikuwa sahihi aliposema Maaskofu wananunuliwa kwa kumchukulia mfano wa Askofu mmoja tu, Askofu Gwajima ambaye ameonekana wazi wazi kabisa kununuliwa na Mh. Edward Lowasa.

Gwajima amejiaibisha na kuwaaibisha Maaskofu wenzake wa Madhehebu mengine, wala asijibaraguze yeye hawezi hata siku moja kafanana na Askofu Pengo, kwasababu yeye mwenyewe hana maadili wala hana utakatifu ni Muhuni tu kama wahuni wengine walioko kule Tandale kwa mtogole ama Manzese.

[h=1]Mithali 26[/h]1 Kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati wa mavuno; Kadhalika heshima haimpasi mpumbavu.

2 Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.

3 Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, Na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu.

4 Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Usije ukafanana naye.

5 Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake.

6 Apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavu Hujikata miguu, na kunywa hasara.

7 Miguu yake achechemeaye huwa dhaifu; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu.

8 Kama mfuko wa vito katika chungu ya mawe; Kadhalika mtu amheshimuye mpumbavu.

9 Kama mwiba uingiao katika mkono wa mlevi; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu.

10 Fundi stadi hufanyiza vitu vyote; Bali amwajiriye mpumbavu ni kama awaajiriye watu wapitao.

11 Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake; Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena.

12 Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye

Gwajama arudie tena kusoma vizuri hiyo Methali.....!!!!!
 
You are a block Head!!




QUOTE=Gervas255;13932418]Mchungaji


Josephat Gwajima nakusalimu bwana Yesu asifiwe.....

Hii ni saa ya ufufuo na uzimaaaaaaaaa..........halafu mbioo
Mchungaji jana wakati unazungumza na waandishi wa habari pale Land Mark nilidhani utajibu hoja za Daktari wa theolojia, falsafa na sheria za kanisa Padre Wilbroad Peter Slaa lakini ukaenda kuzungumza maisha yake binafsi,
Ulisahau kwenye eneo hilo bora Dkt. Slaa kuliko wewe unayevunja ndoa za waumini wako hata kufikia hatua ya kutaka kuvunja ndoa ya muimbaji wa nyimbo za injili FLORA MBASHA. Tuhuma hizi ni doa kubwa kwako kama mchungaji.


Unadai Dkt. Slaa aliwatukana viongozi wa dini wakiwemo maaskofu na masheikh wa kiislamu mbona katika mazungumzo ya Slaa na wanahabari hayo hayakuwepo! Lakini Mch. GWAJIMA inaonekana unasahau sana kama viongozi wanaokutumia ambao ni LOWASSA na MBOWE. Umeshasahau kuwa ni wewe uliyemtukana Kadinali Polycarp Pengo hata kufikia hatua ya kumuambia Kadinali Pengo ni kama mtoto mdogo anavishwa pampers, umesahau? Kati ya wewe na SLAA nani mwenye kuwatukana maaskofu?


Maneno yako kwa Askofu PENGO yalileta taharuki kubwa miongoni mwa waumini wa Kikatoliki na watanzania waliowengi ambao utamaduni wa kutukana viongozi wa dini hawajauzoea lakini nampongeza sana Kadinali PENGO kwani alionyesha ni kiasi gani kiongozi wa kiroho anavyopaswa kuishi kwani Mungu alimpa hekima ya kukujibu kwa kusema anakusamehe kwa moyo mweupe na Mungu akupe rehema ubadilike na akawaomba wote waliokwazika kwa kauli yako ya kumtukana na kumdhalilisha waungane naye kukusamehe na kukuombea ubadilike. Nilitegemea wewe au waliokutuma mngeomba msamaha kwa kupotoka ila mlikaa kimya sababu ni hulka yako kutukana wengine!


NIRUDI KWENYE MADA KUU


Mchungaji GWAJIMA ulitakiwa kujibu hoja hizi za DKT. SLAA

1. Kuwa wewe ndiye uliyempigia simu ya kumpa taarifa ya kukatwa kwa LOWASSA na hivyo CHADEMA wakaribishe, jambo ambalo ulilikubali.

2. Ushiriki wako kwenye mazungumzo ya kamati kuu ya CHADEMA ulienda kama nani?

3. Wewe ulimueleza SLAA kuwa wamkubali LOWASSA sababu viongozi wote wa dini wanamuunga mkono wakiwemo kanisa analosali LOWASSA yaani KKKT, masheikh na maaskofu wa 30 kati ya 34 wa kikatoliki ambao kila mmoja LOWASSA alimpa katili ya Milioni 60-300. Tulitaka ukubali au ukatae au ufafanue. Hukufanya hivyo! Maadam hukujibu tujue wewe ni kiongozi wa kanisa unayeunga mkono matumizi makubwa ya fedha kuwanunua watu hasa viongozi wa kiimani ili kupata madaraka jambo ambalo anapaswa ukafanye TOBA Mchungaji!

4. Dkt. SLAA alimtuhumu LOWASSA kwa kuidanganya CHADEMA kuwa angehamia na wenyeviti wa CCM wa Mikoa 22, wa Wilaya 88, na wabunge wanaomaliza muda wao 50. Kitu ambacho hakikufanyika hivyo LOWASSA akawa LIABILITY badala ya ASSET! Wewe uliyekubali kuwa ulikuwa mshenga hukueleza hili?

5. Dkt. SLAA anasema alieleza kabla ya LOWASSA kupokelewa aitishe waandishi wa Habari ajisafishe na makandokando ya ufisadi halafu ndio ahamie CHADEMA, Kitu ambacho hakikufanyika na hivyo kuendelea kuwa mchafu yaani FISADI. Tulitaka mshenga ufafanue hili kama kweli au si kweli?


DKT. SLAA BADO NI SHUJAA NA MSHUMAA WA SIASA ZA UPINZANI HAPA TANZANIA MAANA ALIZUNGUMZIA MISINGI YA KIONGOZI WA UMMA NA USALITI UNAOFANYWA DHIDI YA WANAMAGEUZI WALIOJENGA UPINZANI KWA JASHO NA DAMU HALAFU HARAKATI HIZO ZINASALITIWA KWA TAMAA YA FEDHA AU MADARAKA HUKU MISINGI ILIYOWEKWA IKIKIUKWA HASA YA UADILIFU.[/QUOTE]
 
Ipo siku mtagundua kwamba Dr.Slaa yuko sahihi kukataa kula na mafisadi

Mbona anakula nao huko ccm na mwenyewe alikiri hivyo? Katika orodha yake ya aibu mafisadi zaidi ya 10 bado wako huko ccm na ndio anaitetea sasa, tena wengine ndio wanamletea makaratasi ya kuzungumzia ie Mwakyembe ni mmoja wao na Slaa amekiri.
 
wakuu mimi nakwenda mbali zaidi, katika kuyajadili maneno ya huyu anayejiita askofu gwajima aliyoyatoa jana tar 08.09 katika ukumbi wa landmark hotel, kama majibu kwa dr. Slaa kufuatia dr. Slaa kumwita yeye (gwajima} mshenga wa kukaribishwa kwa mh. Edward lowasa ndani ya chedema.

Ndugu zangu maneno ya askofu gwajima si tu yanashusha tu credibility ya ukawa ila gwajima hanashusha hata credibility ya maaskofu wenzake.

Gwajima anavyosema mambo ambayo yalikuwa siri kati yake na mtumishi wake wa dini dr. Slaa ama bi mashumbushi, anadharirisha uaskofu wake, kwasababu kama baba wa kiroho unaanza kuropoka mambo ya siri ya kondoo zako, hivi ni nani? Leo mwenye akili timamu ataweza kukufuata na kukuambia jambo lake la siri.

Gwajima amejisifu kuwa yeye anakakitu kakurecordia, hivyo maongezi yote anayoyafanya huya-record yaani ni mtaalamu wa kurecord, sasa embu, jiulize, muumini wake yupi leo, mwenye akili timamu, atakaye weza kumfuata askofu huyu na kumweleza mambo yake ya siri ya kiroho yanayoitaji msaada wa kiroho, kama mtumishi huyu amekuwa mropokaji kwa kiwango hichi.

Mimi ni mkatoliki sisi kwetu tunakitu tunaita sacrament ya kitubio, ambapo mlei umfuata padri nakukiri dhambi zake\kuungama dhambi/maungamo, hapo kwenye maungamo mnakuwa na padri tu, na unamueleza dhambi ulizozitenda, kisha padri utamka maneno fulani kisha dhambi zile kwa imani yetu tunaamini huondoka, sasa kinachofanyika pale huwa ni siri yako wewe unayetubu padri, na mungu wenu pekee,

katika mazingira hayo watu uungama na kutaja dhambi mabalimblali, wengine unakuta alishawahi kuua na kuiba, unamkuta mtu anataja kuwa alishawahi kuzini na mke wa katekista pengine, sasa japo huyu padri anamjua mke wa katekista na katekista mwenyewe kama msaidizi wake ila hawezi kumfuata na kumwambia lolote yale yanabaki kuwa siri na kwavile ni maungamo tunaamini yanakuwa yamekwisha lakini haimaanishi bw. Huyo mlei ameacha ama kukoma kutenda dhambi.

Huo ni mfano tu wa padri wa kanisa katoliki, haya sasa mfananishe huyu gwajima kama angelikuwa padri, si angekuja jana kutuambia yote ambayo mama mashumbushi. Mke wa dr slaa aliyatubu kwake? Hakika huu ni mfano wa upuuzi wa kiwango cha phd.

Lakini mbali na hapo gwajima ni muhuni, kwasababu yeye mwenyewe alishawahi kumtolea maneno ya kashfa sana kiongozi wangu wa kanisa, aliyenipa kipaimara, askofu polycop kardinali pengo alimwita majina ya hovyoovyo na ni wazi kabisa kuwa yalikuwa matusi. Embu sasa tazama mambo yake alafu leo mtu yule yule muhuni aliyemtukana kiongozi mkuu wa kanisa katoliki nchini, anarudi kwetu kuwakemea watu wengine tena walei wake mwenyewe wanapowatukana maaskofu. Kwani si yeye aliyewafunza?

Pengine dr. Slaa alikuwa sahihi aliposema maaskofu wananunuliwa kwa kumchukulia mfano wa askofu mmoja tu, askofu gwajima ambaye ameonekana wazi wazi kabisa kununuliwa na mh. Edward lowasa.

Gwajima amejiaibisha na kuwaaibisha maaskofu wenzake wa madhehebu mengine, wala asijibaraguze yeye hawezi hata siku moja kafanana na askofu pengo, kwasababu yeye mwenyewe hana maadili wala hana utakatifu ni muhuni tu kama wahuni wengine walioko kule tandale kwa mtogole ama manzese.

umeandika uchafu mwingi siwezi soma yote,ila nataka nikushauri kitu kimoja,ushabiki na umburura ni kitu kibaya,gwajima amemjibu slaa vizuri sana
swali la kuondoka cdm kwamba sio lowasa bali ni hawara a.k.a first lady a.k.a mushumbuzi
 
Mbona mnamshambulia Gwajima tu? Au ni kwa sababu ameigusa mouth piece yenu Slaa!!! Slaa au Dr hawezi kuongea tena ya UKAWA kama mlivyokusudia maana amechafuka sana,,anaongozwa na mwanamke???What the shame!!!! Inabidi ajishtukie sasa maana asipoangalia atakuja kuwa house boy wa Mshumbuzi.
 
Mchungaji Josephat Gwajima nakusalimu bwana Yesu asifiwe.....

Hii ni saa ya ufufuo na uzimaaaaaaaaa..........halafu mbioo
Mchungaji jana wakati unazungumza na waandishi wa habari pale Land Mark nilidhani utajibu hoja za Daktari wa theolojia, falsafa na sheria za kanisa Padre Wilbroad Peter Slaa lakini ukaenda kuzungumza maisha yake binafsi,
Ulisahau kwenye eneo hilo bora Dkt. Slaa kuliko wewe unayevunja ndoa za waumini wako hata kufikia hatua ya kutaka kuvunja ndoa ya muimbaji wa nyimbo za injili FLORA MBASHA. Tuhuma hizi ni doa kubwa kwako kama mchungaji.


Unadai Dkt. Slaa aliwatukana viongozi wa dini wakiwemo maaskofu na masheikh wa kiislamu mbona katika mazungumzo ya Slaa na wanahabari hayo hayakuwepo! Lakini Mch. GWAJIMA inaonekana unasahau sana kama viongozi wanaokutumia ambao ni LOWASSA na MBOWE. Umeshasahau kuwa ni wewe uliyemtukana Kadinali Polycarp Pengo hata kufikia hatua ya kumuambia Kadinali Pengo ni kama mtoto mdogo anavishwa pampers, umesahau? Kati ya wewe na SLAA nani mwenye kuwatukana maaskofu?


Maneno yako kwa Askofu PENGO yalileta taharuki kubwa miongoni mwa waumini wa Kikatoliki na watanzania waliowengi ambao utamaduni wa kutukana viongozi wa dini hawajauzoea lakini nampongeza sana Kadinali PENGO kwani alionyesha ni kiasi gani kiongozi wa kiroho anavyopaswa kuishi kwani Mungu alimpa hekima ya kukujibu kwa kusema anakusamehe kwa moyo mweupe na Mungu akupe rehema ubadilike na akawaomba wote waliokwazika kwa kauli yako ya kumtukana na kumdhalilisha waungane naye kukusamehe na kukuombea ubadilike. Nilitegemea wewe au waliokutuma mngeomba msamaha kwa kupotoka ila mlikaa kimya sababu ni hulka yako kutukana wengine!


NIRUDI KWENYE MADA KUU


Mchungaji GWAJIMA ulitakiwa kujibu hoja hizi za DKT. SLAA

1. Kuwa wewe ndiye uliyempigia simu ya kumpa taarifa ya kukatwa kwa LOWASSA na hivyo CHADEMA wakaribishe, jambo ambalo ulilikubali.

2. Ushiriki wako kwenye mazungumzo ya kamati kuu ya CHADEMA ulienda kama nani?

3. Wewe ulimueleza SLAA kuwa wamkubali LOWASSA sababu viongozi wote wa dini wanamuunga mkono wakiwemo kanisa analosali LOWASSA yaani KKKT, masheikh na maaskofu wa 30 kati ya 34 wa kikatoliki ambao kila mmoja LOWASSA alimpa katili ya Milioni 60-300. Tulitaka ukubali au ukatae au ufafanue. Hukufanya hivyo! Maadam hukujibu tujue wewe ni kiongozi wa kanisa unayeunga mkono matumizi makubwa ya fedha kuwanunua watu hasa viongozi wa kiimani ili kupata madaraka jambo ambalo anapaswa ukafanye TOBA Mchungaji!

4. Dkt. SLAA alimtuhumu LOWASSA kwa kuidanganya CHADEMA kuwa angehamia na wenyeviti wa CCM wa Mikoa 22, wa Wilaya 88, na wabunge wanaomaliza muda wao 50. Kitu ambacho hakikufanyika hivyo LOWASSA akawa LIABILITY badala ya ASSET! Wewe uliyekubali kuwa ulikuwa mshenga hukueleza hili?

5. Dkt. SLAA anasema alieleza kabla ya LOWASSA kupokelewa aitishe waandishi wa Habari ajisafishe na makandokando ya ufisadi halafu ndio ahamie CHADEMA, Kitu ambacho hakikufanyika na hivyo kuendelea kuwa mchafu yaani FISADI. Tulitaka mshenga ufafanue hili kama kweli au si kweli?


DKT. SLAA BADO NI SHUJAA NA MSHUMAA WA SIASA ZA UPINZANI HAPA TANZANIA MAANA ALIZUNGUMZIA MISINGI YA KIONGOZI WA UMMA NA USALITI UNAOFANYWA DHIDI YA
WANAMAGEUZI WALIOJENGA UPINZANI KWA JASHO NA DAMU HALAFU HARAKATI HIZO ZINASALITIWA KWA TAMAA YA FEDHA AU MADARAKA HUKU MISINGI ILIYOWEKWA IKIKIUKWA HASA YA UADILIFU.

4.kwahiyo kam angekuja na watu hao ufisadi wa lowasa ungefutika????
liability iko ndan ya assset

5.ajisafishe chadema kwan chadema imekuwa mahakama pale
aliwaeleza jins richmond ilivyokuwa na dr slaa akaridhia na makofi akapiga
dr anaend mbali zaid anasema niliweka masharti mawili,sasa unajiuliza kuna masharti ya chadema na masharti ya dr slaa,kile ni chama na lazima chama kikubaliane na sio mtu mmoja aje na masharti yake km alivyofany dr,chama kinakubali then kinapitisha maazimio

katika katiba ya chadema hakuna sheria hiyo inayosema mtu akija chadema lazima ajisafishe
 
mi nashangaa sana yeye gwajima
kama ni.mchingaji leo hii watu wamesahau kesi ya mbasha haijaisha,padre aliyekura maharage bado,juzi hapa kaangusha nguzo ya tanesco leo yuko kwenye siasa hv kweli huyu anamtumikia nani huyu.
 
Wachungaji Wachungaji acheni kuwatukana wanawake matusi ya mafumbo maana nikimsikiliza Gwajima ni kama vile anawadharau sana wanawake kwa maamuzi yao na kwamba wapo wanaume wana akili za kushikiwa na wake zao ni kosa kubwa! kama vile wanawake hawana akili. Hebu tujiulize sisi wenyewe ikiwa Kiongozi wa Chama ni mwanamke na mumewe kamshauri haya mkewe na kukataa kujiunga na UKAWA bado itasemekana huyu mwanamke ana akili za kushikiwa na mwanamme?..

Kuna akili gani ya ndoa ambayo mwanamme hutakiwi kumsikiliza mkewe! hata kama maamuzi ya Dr.Slaa yanatokana na mkewe ina maana hata katika mikutano ya Chadema mkewe alikuwepo akimpa viwiko vya kubali au kataa? Je, alipochaguliwa kugombea Urais kwa tiketi ya Chadema, hiyo kamati kuu ilikwenda mshauri mkewe kwanza! na alikubali baada ya kuongea na mkewe au?

Huyu Gwajima, Askofu mzima wa dini inakuwaje awe mshauri na msemaji mkuu wa Chadema (UKAWA) tena amefikia ku record watu kama ushahidi wake wakati sheria za kiimani, Mchungaji au Askofu anafungwa na sheria ya Usiri ( Confidentiality) na muumini wake kaitka swala lolote iweje iwe rahisi kwa Mchungaji huyu ku record mazungumzo yake na Mkewe Dr. Slaa ili kufichua siri za Dr.Slaa. Huu ndio uchungaji kweli au Utapeli?

Jamani hii UKAWA imeingiliwa vibaya sana, hawa watu wametokea wapi? Huyu Gwajima anajulikana mujini kwa kubariki kitandani wale wenye shida zao za maisha, leo amekuwa shujaa wa UKAWA! Ama kweli walisema ukistaajabu ya Mussa, Utaona ya Firaun!
unazungumzia wachungaji wepi?
unazungumzia wanawake wepi? Kama na huyo mushumbusi huyo kwa vitendovye, si kwamba tu kajitukanisha mwenyewe bali pia kamtukana, kamkwaza na kamdhalilisha sana dr slaa wetu.

Kwanza ujue daktari alishadanganya kuwa kustaafu kwake si kwa sababu ya kushinikizwa na kumsikiliza mkewe bali kwa sababu eti ya lowassa. Na tena ujue inategemea mwanamke unamsikiliza kwa yepi? kwa hiyo hata kama ni utumbo usikilizwe tu maadam ni mwanamke?!!!!

inategemea ni siri gani. siri za maovu zinazohatarisha amani ya taifa si siri. nyie ndo wale mnaosema eti wizi wa escrow au meremeta au kiwira eti ni siri za taifa!!!!! kivipi? Siri za Taifa ni zile zenye maslah kwa Taifa na si hizi za kuficha maovu yanayoliangamiza Taifa
 
mi nashangaa sana yeye gwajima
kama ni.mchingaji leo hii watu wamesahau kesi ya mbasha haijaisha,padre aliyekura maharage bado,juzi hapa kaangusha nguzo ya tanesco leo yuko kwenye siasa hv kweli huyu anamtumikia nani huyu.

Anaishi maisha yake na hajali na anajua kwanini hajali wala haogopi ukweli anao na anajiamini kwakuwa anawafahamu na kuwajua vilivyo
 
Hata mimi huyo anayejiita askofu Gwajima nimemdharau sana hana maadili ya ukristu kabisa,wafuasi wake sijui aliwapa limbwata gani

Kwenye makanisa yetu walokole hakunaga siri mapepo hukemewa hadharani, ukitenda dhambi unaungama mbele ya kanisa, kufunga ndoa hadharani, kunena kwa lugha ya kimalaika hadharani. Hakuna majungu huku. Hata hivyo askofu Gwajima na padre Dr. Slaa, wote ni viongozi wa dini ya kikristo, waacheni wataelewana wenyewe.
 
umeandika uchafu mwingi siwezi soma yote,ila nataka nikushauri kitu kimoja,ushabiki na umburura ni kitu kibaya,gwajima amemjibu slaa vizuri sana
swali la kuondoka cdm kwamba sio lowasa bali ni hawara a.k.a first lady a.k.a mushumbuzi

Kwa hiyo wewe umeyapokea maneno ya Gwajima kama kweli na kweli tupu?
 
Hili sakata la Gwajima na Slaa & Family, Lime;leta tatizo kubwa kiuaminifu, Nimeskiliza Gwajima mara kadha na kusoma mageziti yote talioandika kuhusa Press conference yake:


1. Gwajima ni Kiongozi wa dini na wafuasi wake watakuwa ni wafuasi wa vyama tofauti vya siasa, Lakini katika itikadi zao za dini watakuwa waa dini moja na ASKOFU wao ni Gwajima, sasa iwapo Gwajima ni mwana Chadema au Ukawa, wale wafuasi wake wa vyama vingine , wanalionaje hilo. what picture does this give you. Mchungaji anayevutiya upande mmoja ( BIASED )
2. Kitu Trust/Imani, ni muhumi sana na ni lazima kuheshimika na kutukuzwa, Gwajima kama Kiongozi wa kanisa hakupaswa kuwe wazi siri alizoaminiwa na Slaa & Family, ikiwa leo ka mwaga yote hayo kwa ajili ya siasa ina maana anaweza kufanya zaidi ya hiyo wakati wowote ule na kwa niaba ya manufaa yake pekee.
3. Gwajima kujisifu ya kuwa yeye ana Control Maisha ya Slaa na familiya yake , kwa sababu anajua siri zao za ndani, kwani walinzi na mfanyikazi wa ndani , wote wana ripoti kwake, hiyo inatisha sana. Jee hao waumini wanao mpa siri zao na kumuomba awaombeye ili waepuke na mabaya, hivyo kweli siri zao ziko salama???
4. Kumleta Mlinzi wa Slaa na Mchungaji aliye na siri za mkee wa slaa, kumwaga siri za hiyo familia, tena hao watu inaonyesha ya kuwa ni watu walio pewa fundisho ya nini la kusema na namna ya kuzungumzia, ni kitu cha kusikitisha.
Nimekopi hapo chini baadhi ya habari za hiyo press conference, zilizo andikwa kwenye magazeti ya leo, ningependa tutafakari bila ya kufikira mambo ya siasa, which is the cause of this circus, na tuangalie in an humanly possible way if this is a right approach to be taken by a religious leader, who is trusted by our confessions, and believing that he is above all that influences humans negatively.

With all my heart I disagree with Gwajima, and he should be rejected by all who believe that the institution of GOD should be above all these dirty and petty political fights, NA NINAJIULIZA, IKIWA GWAJIMA ANA TABIA YA KUREKODI WATU, SIJUI AMESHAWAREKODI WAUMINI WAKE WANGAPI NA KWA NIA GANI????:







HARAKATI ZA KUMWOKOA DK. SLAA
Mtanzania-Gazeti la Kiswahili la kila siku
Ili kuhakikisha anamsaidia Dk. Slaa aweze kurejea katika hali yake, Askofu Gwajima alisema alilazimika kumtafuta Josephine kwa nguvu zote ili waweze kuzungumzia na hatimaye amruhusu kuendelea na siasa.
“Nilimpigia simu na kumwomba tukutane pale Shekinah Garden, Mbezi Beach, tulifanikiwa kukutana jioni ya saa 12, nilitumia muda mwingi kumbembeleza nikimwambia tafadhali mama mruhusu huyo mtu aendelee na siasa, huku nikimrekodi, lakini alionekana kushikilia msimamo wake.
“Mama huyo aligoma kumruhusu kwa sababu eti ameandaa vitu vya biashara na ameshawaambia watu hata nje ya nchi kwamba ndiye atakuwa ‘First Lady’.
“Akahoji sasa watanionaje, nilikuwa nimepanga kuanza kufanya biashara Malaysia, mimi siwezi kukubali kabisa na sitakubali hata iweje,” alisema Askofu Gwajima huku akimnukuu Josephine.

Askofu Gwajima alisema siku iliyofuata, yaani Julai 28, mwaka huu, alimpigia tena simu Josephine ili wakutane Kibo Complex, Tegeta wakiwa na mtu mwingine mmoja ambaye hakumtaja jina ili kumshawishi ajaribu kumnusuru Dk. Slaa asiharibikiwe baada ya kutokwenda Chadema.
“Tukiwa ndani ya gari yake, tukaanza kumwomba tena, nikajua tatizo linaweza kutokea nikawa narekodi tena. Safari hii mwenzangu alikuwa na huruma, akamwomba mama tusaidie huku tukijua siku hiyo Lowassa anakabidhiwa kadi ya Chadema pale Bahari Beach Hotel.
BOMU JINGINE
Askofu Gwajima, alisema endapo Dk. Slaa ataibuka kujibu hoja zake, atatoboa siri nyingine nzito namna alivyokwenda nchini Afrika Kusini hivi karibuni.
“Nasema kama Dk. Slaa akijaribu kujibu haya, nitatoa siri nzito namna alivyokwenda Afrika Kusini akiwa na watu wanne,” alisema Askofu Gwajima.
 
Mie Gwajima simpendi kwa sababu alimtukana kiongozi wangu mkuu wa dini ninayemuheshimu sana kuliko watu wote hapa duniani.

14ikeiu.jpg


Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema kuwa, amemsamehe Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, mchungaji Josephat Gwajima ambaye hivi karibuni alimtolea maneno ya kashfa mbele ya waumini wake kutokana na kutofautiana juu ya msimamo wa viongozi wa Kikristo kuhusu Katiba inayopendekezwa.
Kardinali Pengo alitoa msamahaa huo mbele ya waumini wake katika Kanisa la St Joseph jijini Dar es Salaam jana.
Mchungaji Gwajima anadaiwa kutoa kauli za kumkashifu kiongozi huyo kwamba amewasaliti wa viongozi wenzake wa Kikristo kwa kuwataka waumini wa dini hiyo kuamua wenyewe suala la Katiba inayopendekezwa kinyume na msimamo wa waraka wa kupinga katiba hiyo uliotolewa na Jukwaa la Wakristo Tanzania (CCT).
Baada ya kutolewa kwa waraka huo ulioagiza waumini kuipigia kura ya hapana katiba hiyo, Askofu Pengo alinukuliwa akisema viongozi wa dini hawana mamlaka ya kuzuia wananchi kuikubali au kuikataa Katiba hiyo huku akisisitiza waumini waachiwe uhuru wa kuamua.
Akizungumza jana wakati wa ibada ya Jumapili, Kardinali Pengo, bila ya kutaja jina alisema: "Natumia nafasi hii kueleza juu ya maneno ambayo yalitolewa na mchungaji fulani, sikumbuki anaitwa nani.. nasema nimemsamehe kutoka ndani ya moyo wangu wote na anaweza kuwa na sababu zake ila nimemsamehe kabisa.
"Sina ghadhabu wala chuki ila kinyume chake, naomba tumwombee yeye na watu wote waliohusika ili Mungu aweze kutulinda na kutudumisha hali ya amani ya Taifa letu."
Alisema hatua kumkamata mchungaji huyo ni sehemu ya kutekeleza utaratibu wa jeshi hilo tu lakini yeye kwa nafsi yake ameshamsamehe.




 
Sijasoma upuuzi wako ulioandika hapo, ila napenda kukuuliza swali moja, uliona sawa kwa Dr Slaa kutangazia dunia kuwa maaskofu wa Tanzania, kati ya 34, 30 wamepokea rushwa kutoka kwa Lowassa?

Lowassa ana madhambi yake ikiwemo ufisadi, lakini kuhusisha maaskofu na rushwa ni jambo hatari sana. Hivyo binafsi siwezi kujifanya mwendawazimu eti nimtete Dr Slaa kwa majibu anayopewa.
 
Nimemsikiliza kwa makini jana Askofu wa Kanisa la Ufufuko na Uzima, Josephat Gwajima akitoa utetezi wake juu ya kile kilichoelezwa na Dr Slaa kuwa ni Ushenga baina ya ndoa ya Lowasa na CHADEMA. Kimsingi amekubaliana na yale yaliyoelezwa na Dr Slaa na kujitetea eti alikuwa anafanya hivyo kama wajibu wake wa msingi kwa wanasiasa. Eti kwamba wanasiasa wengi wanapotaka kugombea wanaenda kwa waganga wa kienyeji hivyo yeye alitaka kumuandaa Lowasa kiroho.


Jambo lililonishtua zaidi ni pale aliposema kuwa kama Dr Slaa ataendelea kuwatukana Maaskofu wa Kanisa Katoliki, Anglikana, Lutherani, TAG, Masheikh na Maimamu nk, hatakaa kimya bali atajitokeza kuwatetea. Kwamba Masheikh na Maaskofu wasijisumbue kumjibu Dr Slaa bali yeye ataifanya kazi hiyo.


Binafsi nimetafakari sana juu ya msimamo huu wa Gwajima. Nimejiuliza, ni wapi Dr Slaa kawatukana Masheikh na Maaskofu? Au kuwaambia kuwa baadhi yao wamepokea hongo toka kwa Lowasa jambo ambalo ni kweli ni matusi? Ni lini Gwajima amekuwa na urafiki na Maaskofu wa Kanisa Katoliki? Ni lini Gwajima amekuwa na Urafiki na Masheikh na Maimamu?


1. Gwajima aliwahi kumtukana Askofu Pengo wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam


2. Gwajima huyo huyo aliwahi kumtukana Askofu Balina wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga ambaye kwa sasa ni marehemu.


3. Gwajima pia aliwahi kumtukana Askofu Norbert Mtega wa Kanisa Katoliki, Jimbo kuu la Songea.


4. Gwajima pia aliwahi kuwatukana Masheikh na Maimamu wakati wanadai haki ya Waislam ya kuwa na Mahakama ya Kadhi ndani ya Katiba Mpya.


Kimsingi Mchungaji Gwajima katika hili hana moral authority ya kumnyooshea kidole Dr Slaa ambaye hajatukana. Yeye ndiye alipaswa kujikanya mwenyewe kwa matusi ambayo amekuwa akiporomosha kila siku kwa mahasimu wake kiroho na kisiasa.
 
Back
Top Bottom