Askofu Gwajima vs Cardinal Pengo: Polisi waingilia kati

Askofu Gwajima vs Cardinal Pengo: Polisi waingilia kati

Una kichwa cha gwajima, Pengo ameeleza kilichotokea na kuwa alikuwa anatoa maoni yake kwa jambo lile, unawezaje kusema aliafikiana na wenzake, ?!?,!! (;_(),()).

Hivi wewe unakubaliana na watu kakuambia kura gani ikapigwe?? We Huna brain mpaka uambiwe na gwajima cha kufanya.

Msukule wa ccm unatoa povu
 
Wenye upeo mdogo wa kufikiri ndo wanafikiri Gwajima alimtukana Pengo lakini yote yatajulikana jumatatu kuanzia saa tatu huu ushabiki wa kijinga hautosaidia chochote kwani ukweli humweka mtu wazi bila kuogopwa chochote.
 
Ndugu zangu, tuache malumbano turudi kwenye hoja. Gwajima ametumia lugha inayopingama na maadili tuliyoyategemea toka kwake. Askofu, kiongozi wa kidini, baba wa kiroho wa watu wengi, mzazi na mume wa mtu...anasimama hadharani kutoa maneno machafu, makali mabaya dhidi ya mwanaume mwenzake, kiongozi mwenzake, kwa namna ya kejeli, haoni kama badala ya kuufikisha ujumbe kwa mlengwa amejidharaurisha na kujishushia hadhi na kujipunguzia imani kwa waumini, wafuasi, marafiki na wanafamilia wake? Hakuweza kuiga mfano wa Joseph mume wa Maria, kama anavyojua historia ile ya kwenye bibila, ya kutumia busara na hekima za ajabu baada ya kugundua kuwa mambo yanaenda kombo? Je tuendelee kuwa na imani na mtu ambaye analugha ya matusi na kejeli, asiye na umahiri wa kuchagua hadhira wakati yeye mwenyewe akidai kuwa analitetea taifa letu?

Kati ya hoja za Gwajima ni kuwa Pengo anapingana na maaskofu wenzake, je taifa la Tanzania halihitaji viongozi ambao wapo makini na tayari kukosoa na kukosolewa bila kuficha ukweli kwa ajili ya kulinda itikadi mbovu?

Gwajima bila shaka unaikumbuka ile hadithi ya Yoseph mtoto wa Abrahamu aliyeuzwa na nduguze kwa waishmaeliti, na baadaye akiwa nyumbani kwa Pontifar, mama mwenye nyumba alimtaka kimapenzi naye alionyesha uadilifu wake hata bila kukubali kwa sababu tu anayemtaka kufanya hivyo ni boss wake. Je Pengo si mfano halisi wa uadilifu huo?

Gwajima angalia Yesu alivyokubali kufa msalabani na kutetea ukweli mbele ya Farao, sasa mambo haya yote Gwajima hayajui au yeye hayamhusu>?

Mimi nimeshuhudia wachungaji na makasisi wengi ambao, wanapotaka kufanya sala wanafanya tafakari na kutubu kuomba msaada na msamaha wa Mungu, laikini askofu Gwajima, baada ya kuyatamka matusi yote, anawaita watu na kusema sasa tutaomba kwa jina la Yesu...je ni kweli Yesu amevumilia matusi hayo yote na ataendelea kuisikiliza sala ya Gwajima?

Ningekuwa na uwezo wa kumshauri Gwajima, ningemwambia aende kumwomba radhi Kardinali Pengo na kisha aende Polisi akajisalimishe kama alivyotakiwa kufanya. TUSIRIPUKE NDUGU ZANGU WATANZANIA NA KUWAPIGIA MAKOFI WATU WANAOSIMAMA MAJUKWAANI NA KUUTAFUTA UMAHILI KWA KUTUMIA UDHAIFU WA WENGINE. KAMA MTU NI MAHILI, HOJA ZAKE NA MIKAKATI YAKE ITAONEKANA TU.

Umetoa matapishi tupu, hakuna cha maana
 
Ahsante Jamhuri kwa kuona huu utovu wa nizamu...Huwezi ukatukana hadharani matusi makubwa mbele ya jamii yenye mchanganyiko wa watu na watoto wadogo halafu uachwe...

Tunajenga jamii yenye maadili...Gwajima anapaswa kupewa onyo kali na ikiwezekana Kanisa lake lifungwe mara moja kwa kuwa kama kiongozi mkuu wa kanisa anaporomosha matusi ya nguoni iweje kwa waumini ambao wanamsikiliza na kumuamini...???

Ifike mahali viongozi wahuni wanajiita wachungaji kwa kujipachika wachunguzwe mara moja afya za akili zao maana ni hatari kwa Taifa.

Wewe mwanga nini?
 
Kutukana hadharani ni kosa la jinai.Hata kama ana sababu

Hivi kuna tusi gani ambalo Gwajima alitukana?
Mjinga? Asie na akili? Mpuuzi? Kazeeka? Kisheria je haya maneno yanatafsiriwaje?

Tatizo watu wana mihemko na sio fact in ussue
 
Wenye upeo mdogo wa kufikiri ndo wanafikiri Gwajima alimtukana Pengo lakini yote yatajulikana jumatatu kuanzia saa tatu huu ushabiki wa kijinga hautosaidia chochote kwani ukweli humweka mtu wazi bila kuogopwa chochote.

Mi naomba mtu aliesikia hayo matusi aorodheshe hapa tusi moja kwa jingine
 
Hili sakata la Gwajima na Pengo linazidi kudhihirisha uwezo mdogo sana wa wafuasi wa Chadema(ukawa) wa kupambanua mambo.

Kama huwezi kuelewa jambo dogo tu la Kauli ya Pengo vipi kwenye mijadala mikubwa si ndo utatoka kapa? Tatizo mihemko imewazidi uwezo wenu wa kufikiri.

Pengo hajatetea Katiba hata kidogo ila kaumia fact kupata hitimisho la kauli yake.

Ndio KATIBA ni mbovu kwa walio wengi ila si wote wanaiona mbaya. Wapo wanaoona ni nzuri.

Hajasema ipigiwe kura ya ndio wala hapana ila aliwahasa viongozi wa dini kuwa sio kazi yao kuwachagulia maamuzi wananchi bali kupiga kura ya ndio au hapana ni jukumu la wananchi wenyewe.

Kazi ya viongozi wa dini ni kuwahimiza wananchi waisome na kuielewa ili wakati wa kupiga kura ndo wafanye uhamzi sahii badala ya viongozi kuwachagulia upande. Kuwachagulia upande wananchi ni sawa na kuwadharau na kuwashusha utu wao kana kwamba wao hawana uwezo wa kuchanganua mambo yanayohusu mstakabali wa maisha yao.

Kazi ya kusema katiba ni mbaya au nzuri ni kazi ya serikali,wanaharakati na wanasiasa.

Kiongozi wa dini anayependa kufanya kazi za wanasiasa avue majoho aende kwenye majukwaa
 
Kwahyo nani yuko SAWA? Gwajima au Pengo

Kabla ya kufika huko kwa kusema nani yuko sahihi au sawa kwanza embu tujilizishe na haya machache.

Alichosema Pengo ni maoni yake binafsi ila lile tamko la maaskofu ni la wengi. Kwanza hatujui maaskofu mpaka wanaazimia kutoa tamko hatujui kuna taratibu gani huwa zinafuatwa: je! wanaitwa maaskofu wote wanapiga kura au linalosema na kiongozi basi linakuwa la wote?

Lakini kwa akili nyepesi tamko la maaskofu ni la wengi (Collectively) lakini siwezi kushangaa kama kuna maaskofu wachache wenye maoni tofauti mf: Cardinali Pengo.

Lakini kwa kiongozi wa kiroho kama Gwajima kutoa maneno kama yale, na dhambi kubwa zaidi ni pale anaposema ni "ROHO MTAKATIFU" kamtuma.

Kikubwa zaidi kuna familia pale zinakwenda na watoto wadogo unadhani anawajengea msingi gani wa maisha; kwamba kumtusi mtu ni jambo la kawaida tu kama mnapingana naye mawazo na maono?

Kuna msemo unasema Utu uzima huja na hekima lakini nasikitika kusema kwa Gwajima ni tofauti.
 
Sisi tuna akili zetu za kuchagua ndio au hapana, sio kusurutishwa na Kina gwajima tuseme hapana, nyie mliozoea kuiga fulani akisema hapana ndio watu ambao nawafananisha na mwanafunzi anayetizamia majibu ya mtihani kwa mwenzake bila kutumia akili yake A.K.A VILAZA.

mbona mnaambwia hapana kutenda dhambi, mbona Pengo hawaambi mchague ndio au hapana kutenda dhambi??
 
Hata aloangusha ndege Ufaransa ni ALSHABAB,isije ikawa una njaa unawasingizia alshabab,Mbona roho mtakatifu katajwa hapa,kinachokuumaa wewe mimi kumtaja Mtume ni nini?una mihemko kweli wewe ten isiyo na tija.

Watu kama nyie tushawazoe,mnapenda dini kuliko mungu,its okay mdogo wangu...
 
Kuna kauli zingine zita tafsiriwa tofauti na watu kutokana na misimamo yao kuhusu imani au hata kimtazamo wa maisha kutokana na kile tunacho amini au simamia.

Hawa viongozi wa dini inabidi wajue kupishana kimsimamo aimpi mwingine haki ya kumkejeli mwenzie particularly tunapo ongelea misimamo ya watu mungu.

Halikadhalika ingawa kauli azikuwa sawa hila sioni tofauti ya walichokisema baadhi ya wanasiasa wa upinzani ya kuwa raisi wetu ni dhaifu mbele ya jamii.

Sioni tofauti ya wanasiasa na vyama vyao kukejeliana hadharani; on that note polisi wanatumia sheria gani iliyopo au sehemu gani ya katiba kusema wanamtafuta Gwajima na kosa lake liko wapi kisheria. Huu utaratibu wa kufanya mambo kwa cherry picking ndio tatizo.

JK angesema Mnyika ashitakiwe kwa kumuita dhaifu CDM wangesemaje? kupishana kwa misimamo ipo. Isipokuwa kupishana kunakotokana na dini inaweza kuwa tatizo ndio maana huwa siasa na dini azichanganywi; tazama misimamo ya kisiasa badala ya kuwapelekea wanasiasa kushitakiana inawafanya watu wa dini ndio waitiane polisi wakati hao watu kazi yao ni kuhubiri habari za mungu.

Tumtafute mungu kwenye nyumba za ibada na tutafute siasa bora kupitia viongozi tunaowachagua kila mtu na kazi yake.
 
Hivi kuna tusi gani ambalo Gwajima alitukana?
Mjinga? Asie na akili? Mpuuzi? Kazeeka? Kisheria je haya maneno yanatafsiriwaje?

Tatizo watu wana mihemko na sio fact in ussue

Wewe ni mjinga. Huna akili...mpuuzi..umezeeka
 
Watu kama nyie tushawazoe,mnapenda dini kuliko mungu,its okay mdogo wangu...
wEWE UNAWASHWA WEWE,mimi kumnukuu Mtume Muhammad kumekuuma nini? ni sawa na kumnukuu msomi au mwanafalsafa yeyote,sasa wewe umekwazika na nini?mie sio muumini wa itikad za kijinga,humu JF watu mara kadhaa humnukuu Yesu na Wanafunzi wake kadhaa. Pamoja na hayo huu uzi unahusu Gwajima na Pengo na post niliyoijibu imeendana na nilichokinukuu,kama huna la kufanya kashikishwe ukuta mbulu K3NG3 w3333
 
Wenye upeo mdogo wa kufikiri ndo wanafikiri Gwajima alimtukana Pengo lakini yote yatajulikana jumatatu kuanzia saa tatu huu ushabiki wa kijinga hautosaidia chochote kwani ukweli humweka mtu wazi bila kuogopwa chochote.

Devil's advocate at work
 
it only requires to use common sense sio ushabiki tu. cha msingi sikiliza alichosema Gwajima na sikiliza alichoongea Pengo ndipo utoe maoni sio kukurupuka tu na kulopoka kama mwendawazimu. na kuhusu polisi kufanya hivyo ni wajibu wao kwakuwa ni kosa la jinai. watu wengne wanaleta hoja za ajabu ooh mbona flani alifanya ivi hakukamatwa. ishu ya kutokamatwa flani sio kigezo cha kutokumuwajibisha mwingne afanyapo kosa. tusiwe kama bendera kufuata upepo yatupasa kua na maamuzi kutoka moyoni mwako as long as you feel your right.
 
Back
Top Bottom