Askofu Gwajima vs Cardinal Pengo: Polisi waingilia kati

Ivonya-Ngia

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
703
381
Polisi kanda maalum ya Dar es salaam wametoa wito kwa Askofu Gwajima kufika kwa RCO wa kanda kwa mahojiano kuhusiana na clip anazohusishwa nazo mitandaoni akitoa matamshi makali juu ya Cardinal Pengo.

=============


ASKOFU GWAJIMA ATAKIWA KUHOJIWA NA JESHI LA POLISI KUHUSU TUHUMA ZA KASHFA NA MATUSI DHIDI YA KALDINARI PENGO

Screen%2BShot%2B2015-03-26%2Bat%2B5.34.56%2BPM.png


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtaka Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima afike haraka katika kituo cha Polisi cha Kati ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa na matusi.

"Tumepokea malalamiko ya kukashifiwa na kutukanwa hadharani Mwadhama Kaldinari Polycarp Pengo ambaye ni kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile WhatsApp na mingineyo kuna sauti iliyorekodiwa (audio) na picha za video (Video Clip) zikimuonyesha Askofu Gwajima akimkashfu na kumtukana kwa maneno makali Kaldinari Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine".

Baada ya tukio hilo juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika hali ya kawaida ili kumpata Askofu Gwajima bila mafanikio na hivyo yeye mwenyewe sasa anatakiwa aende akaripoti haraka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam bila kukosa.

Ni muhimu sana kwa Askofu Josephat Gwajima kuripoti yeye mwenyewe badala ya Kutafutwa au kukamatwa ili ajibu tuhuma hizo kutokana na nafasi yake katika jamii.

Jalada la uchunguzi limefunguliwa na upelelezi wa shauri hili unaendelea ili sheria ichukue mkondo wake.

Imetolewa na:
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM

DAR ES SALAAM


Chanzo: MICHUZI BLOG
 
Laiti ungekuwa wewe ungejisikiaje kashfa kama ile????
Ebu tuuu tuchukulie kiubinadamu wa kawaida bila kujali katiba inasema nn.
Gwajima ana kesi ya kujibu dhidi ya maneno yake!!!
 
Kwenye uzi kama hivi ndiyo kipimo cha kujua jinsi gani vijana wetu wa taifa hili walivyojaza uozo kichwa na kuwa wepesi wa kuchotwa kisiasa na kutoa mawazo mepesi mepesi yasiyo na mashiko wala hekima.

Mwanadamu akikosa hekima anakuwa kama mwendawazimu na ndiyo taifa hili na vijana wake linapoelekea.
 
Ni nani mlalamikaji katika hili shauri?

Mbona kina Muhongo na werema walimwita kafulila tumbili na wakamwambia watamkata kichwa hadharani polisi hawakuoan umuhimu wa kuchukua hatua dhidi ya hiyo jinai iliyosemwa hadharani?

Ninafahamu shehe I..nani sijui alikuwa anahamasisha mauaji ya viongozi wa dii ya ki kristo hadharani lakini polisi hao wakiwa walinzi wa usalama hawakuhangaika hata kumhoji? (you tube: waueni).

Ni kweli inaezekana Pengo ameumia lakini si jukumu la polisi kuwa mlalamikaji. Watu wengi sana pia waliumizwa na undumila kuwili wa pengo kwamba huku ameafikiana na wenzake, halafu pembeni tena anageuka. Kama angelikuwa na nasaha alizoziona yeye zinafaa, alitakiwa kuzisema kwenye kikao walichokaa na si kufanya uzito kabwe.

Anyway, nina amini hili suala litakwisha kwa amanni kwa sababu Wakristo wamefundishwa unyenyekevu na msamaha. Ninaona polisi wanachokifanya ni reconciliation ya kawaida ambayo mara nyingi pia, hasa hapo zamani, (wakati wa nyerere akiwa hai), walifanya sana kazi ya upatanishi pale pande mbili zinazofanana zilipokuwa katika tofauti.

Heri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu.


Polisi kanda maalum ya Dar es salaam wametoa wito kwa Askofu Gwajima kufika kwa RCO wa kanda kwa mahojiano kuhusiana na clip anazohusishwa nazo mitandaoni akitoa matamshi makali juu ya Cardinal Pengo.


Chanzo; MICHUZI BLOG: NEWS ALERT: ASKOFU GWAJIMA ATAKIWA KUHOJIWA NA JESHI LA POLISI KUHUSU TUHUMA ZA KASHFA NA MATUSI DHIDI YA KALDINARI PENGO
 
Ni nani mlalamikaji katika hili shauri?

Polisi wanasema wamefungua file la uchunguzi, sheria inawaruhusu kufanya hivi juu ya mashauri ya jinai. Pia tambua katika kesi za jinai mshtaki ni Jamhuri so ikiwa kesi itaenda mahakamani hapo Polycarp Cardinal Pengo atakuwa ni shahidi tu.
 
Hilo liko dhahiri kiongozi. Why double standards?

Polisi wanasema wamefungua file la uchunguzi, sheria inawaruhusu kufanya hivi juu ya mashauri ya jinai. Pia tambua katika kesi za jinai mshtaki ni Jamhuri so ikiwa kesi itaenda mahakamani hapo Polycarp Cardinal Pengo atakuwa ni shahidi tu.
 
Back
Top Bottom