Askofu Gwajima: Rais Magufuli asijaribiwe

Askofu Gwajima: Rais Magufuli asijaribiwe

Ninyi mnaosema mnashindwa kumuelewa Gwajima kwa kusema Magufuli asijaribiwe mnataka asemeje?Mnataka aseme mjaribuni rais?Kuna misimamo mingine haifai kuungwa mkono kama ile ya maandamano ya ukuta.Ni mapema sana kuanzisha mitafaruku kama hiyo wakati tunaona mh Rais anavyojitahidi kurudisha nidhamu iliyopotea kwenye utumishi wa umma na kufuta mazoea ya wizi yaliyozoeleka serikalini na kwenye chama chake cha siasa.Tunahitaji kuwa kitu kimoja na kumuunga mkono mh Rais licha ya madhaifu yake.Tunaweza kuwa na njia mbadala ya kupinga lakini si hii ya kulazimisha mapambano na vyombo vya dola kwa kukiuka amri za jeshi la polisi

kwani UKUTA ni mtafaruku mkuu?...unaielewa dhana ya ukuta...sio fujo ni maandamano ya amani au toa hiyo njia mbadala uliyoisema ili itumike.
 
Gwajima asisitiza Magufuli ni mzalendo mwenye maamuzi yenye tija. Lusekelo naye anena, asema rais apewe nafasi afanye kazi
View attachment 389025
MBONA YEYE ANATUJARIBU MARA NA ASIYE FANYA KAZI NA ASILE MARA TUMEKUSANYA PESA KUTOKA KWA MAFISADI MARA TUMEKUSANYA KODI KUTOKA KWA WAKWEPA KODI MARA KILA JUMAMOSI YA MWISHO WA MWEZI NI SIKU YA USAFI KWANINI ASILIPIE WANAOFANYA USAFI MARA TUCHANGIE MADAWATI SIJUI KODI INAYOKUSANYWA INAFANYA NINI AU NDIO MAJUBILEI YA BABA WA UBATIZO WA URAIS GWAJIMA ACHENI KUTUJARIBU SIE WATAZAMAJI WA MOVIE
 
Afanye yote,ila aachie demokrasia na mikutano ya kisiasa!cha msingi wanasiasa wafuate kanuni
Hajazuia mikutano ya siasa. Sema hamuelewi tu. Mnakuza mambo kijinga jinga. Mbona mikutano inafanyika mpaka sasa. Lakini kwa sababu mnataka kupambana na polisi. Basi matokeo ndio hayo. Polisi hawa wapo kwa ajili yetu. Kama tunakaa na kuelewana nao mbona hawana shida. Lakini kwanza ni lazima tutii sheria bila shuruti
 
kwani UKUTA ni mtafaruku mkuu?...unaielewa dhana ya ukuta...sio fujo ni maandamano ya amani au toa hiyo njia mbadala uliyoisema ili itumike.
Ukuta maana yake nini. Una faida gani kwa taifa kwa sasa. Nipe faida tano tu.hatuwezi poteza muda wetu kwa kitu kisicho na faida na tija kamwe.
 
kiongozi wa dini anasema magu asijaribiwe,ilihali ni MTU anaejua maandiko vzr kwamba nani hajaribiwi!!hlf mnafurahia hiyo kauli??jaribuni kutafakari vzr.gwajima anajua anaongea nn nyie
Hapo sasa Gwajima anaonekana ni mnafiki aliepitiliza badala aseme ukweli kuwa sheria na haki za kikatiba zifuatwe anaongea kufurahisha upande fulani, viongozi wa namna hii mhhh kazi kweli huyu ni kiongozi wa dini au msaka tonge.
 
Taratibu rangi zao zinazidi kujitokeza wanaoelewa nini kinaendelea hawasumbuki na haya matukio na kauli za sasa
 
Ukuta ni gia mpya ya chadema baada ya ile ya ufisadi kufanikiwa kututeka ili kuiondoa ccm but magufuri utendaji wake ndio kilikuwwa kilio cha wengi wakikitafuta so wanajalibu kutafuta namna ya kusikika kwani wanaweza kupotea, kumbuka sote tuliunga mkono ukawa sababu ya ufisadi ,neno ufisadi tayari limepotea chadema
 
Lumumba mnachekesha leo Gwajima amekuwa shujaa tena lol.
 
Ninyi mnaosema mnashindwa kumuelewa Gwajima kwa kusema Magufuli asijaribiwe mnataka asemeje?Mnataka aseme mjaribuni rais?Kuna misimamo mingine haifai kuungwa mkono kama ile ya maandamano ya ukuta.Ni mapema sana kuanzisha mitafaruku kama hiyo wakati tunaona mh Rais anavyojitahidi kurudisha nidhamu iliyopotea kwenye utumishi wa umma na kufuta mazoea ya wizi yaliyozoeleka serikalini na kwenye chama chake cha siasa.Tunahitaji kuwa kitu kimoja na kumuunga mkono mh Rais licha ya madhaifu yake.Tunaweza kuwa na njia mbadala ya kupinga lakini si hii ya kulazimisha mapambano na vyombo vya dola kwa kukiuka amri za jeshi la polisi
Dawa yake ni UKUTA tuu maana hakuna namna nyingine, welcome Sept 1
 
Asijaribiwe? Mbona huo upuuzi sana kutoka kinywani kwa mchungaji! Asiyejaribiwa ni Mungu pekee full stop.
 
Back
Top Bottom