Kipangaspecial
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 19,430
- 25,968
Miaka 59 ya UHURU tuna vyote hivi;Heshima sana wanajamvi,
Askofu Mkuu sana Dkt. Gwajima kaja na style ya aina yake katika kuomba kura jimbo la Kawe.
Mosi Dr Gwajima kaja na ahadi ya kutuletea maboat ya uvuvi vijana wa Kawe. Vijana wote wa Kawe wajiandae kuvua samaki katika Bahari kuu ya Hindi.Hii ni habari njema hasa vijana wetu wasiokuwa na ajira wajiandae kupata ajira ya kuvua samaki.
Pili kabla ahadi ya kuvua haijatulia katuletea ahadi nyingine tena ya kutupeleka USA baby kule anakoishi Nyani Ngabu yaani ni raha juu ya raha ikiwa wewe ni mkaazi au mpiga kura wa Kawe.Mimi mwenyewe nafanya mpango wa kuhamia Kawe nani asiyetaka kwenda USA !.
Ahadi za Askofu Dr Gwajima ni nyingi na tamu tamu kusikia na kusikiliza lakini napata ukakasi kama kweli ana uwezo wa kuzitekeleza.Nadhani nia yake kubwa ni kupata ubunge akishaupata mambo mengine yatajiset yenyewe.
Hii si mara ya kwanza Askofu Dr Gwajima kutoa ahadi ambazo hazina kichwa wala miguu,kuna ahadi ya tren ya umeme sijui imetekelezwa kwa kiwango gani ?.Kuna ahadi kugeuza madrasa na misikiti kuwa Sunday school sijui mpaka sasa ngapi zimeshageuzwa.Kuna ahadi ya kufufua misukule sijui kama kuna ndugu anaweza kuja hapa na kutupatia ushuhuda wa ndugu yake alinyofolewa katika minyororo ya usukule.
Ngongo safari Bukoba kwasasa nipo sokoni Katerero kwa nshomile wapo gado kweli kweli.
Mount Kilimanjaro
Serengeti National Park
Mikumi
Ziwa Victoria, Tanganyika
Makaa ya mawe Songea
Bandari ya DSM
Gesi ya Mtwara
Almasi
Tanzanite
Dhahabu
Bado CCM imeshindwa kumpa mwananchi MAJI ya kunywa safi na salama tu